Ukweli kuhusu uchaguzi wa mwaka 2020 Jinsi Hayati Magufuli alivyouvuruga

Huku umepotea njia bwashee, mbona thread za mambo ya uuzwaji bandari zimejaa hapa jukwaa la siasa?

Si kila mtu anataka kujiumiza nafsi muda wote, hapa unajifanya una uchungu wakati juzi tu umetoka kwenye parade la ubingwa wa Yanga, hivi kwa nini wungi ule msingeutumia kuandamana mpaka ikulu?

Mimi sipendi ujinga ujinga, na mimi na angalia namna ya kulamba asali sina muda wa kuendelea kujiumiza nafsi kwa ajili ya watu wajinga.
 
Tunaojuwa ukweli wa mambo ndio maana tumechaguwa kukaa kimya, huyu mama ametutowa jehenamu.

Haya mambo ya bandari tuweke kando kwanza lakini watu waelewe vizuri alipotutowa huyu mama.
Shindwa pepo, aliyekutuma nae ashindwe, nyie wote ni mawakala wa shetani.

Ametutoa jehanamu wakati ndio kwanza katufikisha utumwani Dubai?!
 
Wapinzani amkeni mnapotaka kupambana na Ccm muijuwe vizuri nguvu ya Ccm IPO kwa wakurugenzi na maafisa watendaji Kata, nje ya hapo Ccm ni kifo cha mende chaliii.[emoji419][emoji375]

Sent using Jamii Forums mobile app
Niliitwa na kupewa maelekezo kuwa nimpige pingamizi mgombea udiwani mwenzangu wa CHADEMA ili atolewe na kisha nibaki mimi na wa CCM, nilikataa ila walimpiga pingamizi wenyewe, Mungu ni mwema jamaa akalijibu pingamizi na jina likarudi - aligombea.

Ushetani ukafanyika wakati wa kupokea vifaa, wagombea wa vyama ni lazima tuwepo lakini hatukuitwa, vikapokelewa kinyemela, havikukaguliwa nasi.

Asubuhi mawakala wakazuiwa kuingia kwenye chumba cha kupigia kura, maboksi yakaingia na kura feki ndani. Mimi nilikuwa na wakala mmoja tu, aingie kituo 1 lakini nae alinyimwa barua.

Nilipanga kufungua kesi ya uchaguzi lakini nchi nzima ilipararaizi kwa kujua hata hukumu zitakuwaje, yaani tutapoteza muda tu mahakamani. Sheria yenyewe ya uchaguzi ni katili, inataka ili ufungue kesi uweke SECURITY ya shilingi laki 5, hii tayari ni uminyaji wa haki, kesi za uchaguzi zinatakiwa kuwa bure kabisa hata filing fee inatakiwa kuondolewa. Mgombea wa CCM alishinda uchaguzi kwa kupata kura 1500 hivi, akifuatiwa na wa CHADEMA Aliyepata kura 700 hivi mimi nilipata kura 120 hivi. Idadi wa waliojiandijisha kupiga kura ni 12,000
 
Ajabu liachwa kujadiliwa jambo present linalotuumiza wabara kwa sasa, utupeleke kwenye uchafuzi wa 2020 uliomuweka pia madarakani huyu mama yako msaliti aliyetupeleka utumwani Dubai, halafu ajabu zaidi, unasema huyu mama amekuja kututoa jehanamu?!

Wewe kumbe ni mpuuzi sana, umepelekwa utumwani Dubai juzi tu, leo unasema umetolewa jehanamu!.
 
Hapo mgombea wa Chadema alishinda.

Yani maana yake mchakato wa kupenyeza kura feki ulikuwa mgumu au Mtendaji akiamuwa kumtosa, kuna madiwani hawaivi na watendaji, Mtendaji anajuwa yuko radhi ashinde mpinzani kuliko mgombea wa Ccm.
 
Yaani wewe akili yako ndogo sana kura 3000 kata nyingine zina watu hata 1500 hawafiki unakuwaje na kura 3000. Haya basi leta evidence zinazo onyesha hayo matokeo kwasababu automatically unamaanisha kuna maeneo ambako kura zilizidi idadi ya wapiga kura wa eneo hilo. Acheni ujinga wapinzani walipigwa kipigo cha umbwa mwizi. Watanzania wana akili wanataka matokeo ya utekelezaji wa changamoto za wananchi. Na Magufuli aliweza sana kwenye hili.

Kura hazitolewi kwa wezi, walevi na wadangaji.

Sent from my Infinix X672 using JamiiForums mobile app
 
Hukumbuki hata mama yako msaliti alliwahi kusema akiwa Mbeya kwenye kampeni, hata tukipigia kura upinzani, ushindi watapewa CCM?

Huyo ndie amekuja kukutoa jehanamu?

Katafute akili ulipoziacha.
 
Tunaojuwa ukweli wa mambo ndio maana tumechaguwa kukaa kimya, huyu mama ametutowa jehenamu.

Haya mambo ya bandari tuweke kando kwanza lakini watu waelewe vizuri alipotutowa huyu mama.
HuYo bitozo baya si alikuwa mgombea, na alijua kila kitu na alishasema yeye na Magufuli ni kitu kimoja na kazi iendelee
 
Any evidence to justify your argument. Wote hapa mnaongea kwa hisia tu nothing anymore. Kama ambavyo wote wa naongea kwa hisia wote mnaongea kwa hisia hisia tu hakuna mwenye ushahidi.

Lakini kama kura ziliibwa si mngeenda mahakamani kudai na kujustify?? Wapinzani hawa hawa kweli washindwe kwenda mahakamani and they have evidences it can't be. Utapeli tu wa kisiasa mnaeneza

Sent from my Infinix X672 using JamiiForums mobile app
 
Wananchi wanatukabali hutaki Katiba Mpya, Wananchi wanatukubali hutaki Tume ya Uchaguzi iundwe upya. NONSENSE.
 
Mama Samia mitano tena, mpaka mpate akili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…