Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 21,470
- 40,593
Kwanza suala la uwekezaji na umiliki wa hisa ni suala la kitaalamu na lina misingi yake, Simba hawaifuati. Mkutano Mkuu wa Simba uliridhia Mo kupewa 49% ya hisa za Simba. Ukototozi wa thamani ya klabu umefanyika? Bado.
Wanachama wa Simba wanamiliki 51% ya hisa za Simba, kwani simba thamani yake halisi ni shilingi ngapi? Hakuna anayejua.
Mo alisema atatoa bilioni 20 kama uwekezaji. Ni uwekezaji ama ni thamani ya hisa atakazomiliki? Hiyo haisemwi.
Wanachama ambao ndiyo wanatakiwa wawe na hisa nyingi, wameshaweka shilingi ngapi kwenye Klabu ya Simba mpaka sasa? Hakuna.
Fedha anazotumia Mo kwenye kuiendesha Simba kwa sasa zinahesabika kama uwekezaji ama kujitolea kwa Mo? Kama ni uwekezaji, ni sehemu ya hisa ama ni zile bilioni 20 alizosema atawekeza? Mbele ya safari atazidai ama anatoa sandakalawe?
Hili jambo lina mazingile mengi sana.