Hoja tatanishi sana hii, kiufupi uongozi wa SIMBA SC wanashindwa kufanya maamuzi na kulitolea ufafanuzi jambo hili la uwekezaji wa bilioni 20 kwa muda mrefu sasa kwakuwa Simba Sc ipo kwenye mtego fulani wa kiufundi juu ya makubaliano yaliyofanyika kati ya uongozi wa Simba sc na Mo, Sasa huu mtego uliopo kwenye makubaliano yaliyofanyika kihuni (wakati huo) ndio unaompa MO mamlaka ya kuitawala Simba Sc na mbaya zaidi anautumia mtego huo huo kuitumia Simba sc kwa maslahi yake binafsi, biashara zake na taasisi zake.. kuutegua huo mtego ni mpaka wote walio juu watoke usingizini ila kwasasa mhindi kashawageuza misukule hawana wanachokielewa zaidi ya kuitia NDIO, SAWA, YES na kumfisia mtu bila utashi.. mtego wa kuwanasa maskini ni pesa tu..