Alexander Lukashenko
JF-Expert Member
- Sep 9, 2017
- 4,140
- 9,667
Mkuu nikisema hujafuatilia, either kwa uzembe wako au kwa kuwa busy na majukumu nakosea?Sijui wewe una umri gani. Lakini mimi wakati Yanga inafungwa bao sita bila (6-0) nilishakua duniani tayari napumua na kuijua dunia.
Hoja yangu ni kwamba haya mambo ya Uwekezaji na Hisa ni mambo ya kitaalam na hayafuatwi na Klabu ya Simba. Hakuna hatua hata moja ya kitaalam iliyofanyika tokea ule mkutano ulioridhia Mo kupewa Asilimia arobaini na tisa (49%) ya Klab ya Simba.
Mimi siyo shabiki maandazi bali ni mwanasimba ambaye wakati wote natembea na akili zangu zikiwa kichwani. Kwa nini Klab yetu haithaminishwi na ijulikane thamani yake?
Kwa nini uwekezaji wa Mo hauko wazi ili ijulikane anawekeza kiasi Gani Simba? HIvi ni nani anayejua mwaka jana kwa mfano kwenye msimu uliopita, Simba ilitumia kiasi gani kwenye Usajili, mishahara ya wachezaji na wafanyakazi wa Klab, Gharama za ushiriki wa mashindano ya ndani na ya kimataifa, na mambo ya uwekezaji mwingine.
HIvi ni nani aliamua uwanja wa Bunju uitwe "Mo Arena" na kwa makubaliano gani?
mbona maswali yote uliyouliza yamejibiwa sana na MO mwenyewe hata kina magori kipindi wanazunguka Kwenye media kutoa ufafanuzi.
na si leo wala jana ni miaka zaidi ya mitatu nyuma walijibu maswali yako yote hayo?
fuatilia interviews hasa ile ya Magori na Mulamu wakiwa E.fm
unauliza thamani ya club haifahamiki kwani kipindi wanathaminisha mali za club ulikuwa wapi?
ni bora ukafuatilia kwanza.
ugomvi na kilomoni kuhusu hati ulitokea wapi?