Ukweli mchungu na ambao Wana Simba wengi hawatotaka ku usikia nikua Kuna baadhi ya fedha MO alizitoa Bure kabisa kama Mpenzi na Mwanachama wa Simba, namaanisha katika fedha izo MO ametoa Kwa mapenzi yake.
Kuna baadhi ya fedha ambazo ni Nyingi zinafika (billions) MO alikua akizitoa kulingana na hitaji la Simba Kwa wakati uo wakati klabu ilizihitaji na haikuanazo, Pesa izo alizitoa kwa mafungu si Kwa mkupuo mmoja lakini Kwa makubaliano ya yeye Kuja kurudishiwa hizo fedha Kwa maana hajazitoa kama msaaada.
Mkanganyiko uliopo je! Izi bilioni 20 alizosema ameweka itakua amejumuisha na madeni yake ya nyuma ya makubaliano maalumu ya kulipwa.
Au utakua mzigo mpya kabisa ambao au husiani na fedha anazo zidai Kwa klabu?
Kwa Wale Wana Simba wa ndaaaani Wanafahamu ata wenye uwelewa mpana Wanafahamu ila sioni dhambi yoyote Kwa MO kwakula Matunda ya kazi za mikono yake.
Mla huliwa, kwasasa tumwache MO afaidi matunda ya uwekezaji wake, pesa alizo jitolea, alizo kopesha na alizo wekeza ni Nyingi sana.
Kwasasa tumwache afaidi fedha zilizo ingia Kwa Mikataba mipya ya klabu, na klabu kufuzu Makundi.