Ukweli kuhusu uwekezaji wa Mo Dewji Simba ndiyo huu

Waswahili wanataka ushindi dhidi ya Yanga basi, wanaacha masiliahi mapana ya timu yetu, wanadhani mo atakuepo milele
 
Alichofanya mo ni kama alitoa rushwa ili awekeze Simba Kwa Bei sliyotaka, kabla hata mchakato wa uwekezaji haujaanza mo alianza kuwapa Simba pesa ya usajili na matumizi mengine.
Simba walipoingia mkataba na sport pesa mo alilakamika na kudai kwanini hawakumshirikisha lakini wakati huo mchakato ulikuwa haujaanza.
Wakina Mula Ngq'mbi walioshiririki mchakato wanakiri waliofanya bila kutafuta thamani ya Simba mbaya zaidi waliohoji waliitwa wasaliti na kupewa majina ya ajabu.
Sheria inasema wawekezaji wawe si pungufu ya 3 ila yeye amekuwa peke yake.
Walioshiririki wengi wamepewa zawadi ya ujumbe wa bodi sababu hawawezi kuhoji chochote
 
Ndiyo unavyojidanganya kama haya ameyaleta MO. Kama ni hivyo mbona ameshindwa kuleta hayo akiwa Mbagala Market na Ile timu yake ya kule Singida
 
Ungeleta na uwekezaji wa yanga kama ulifuata sheria na kanuni zote ili simba waige au na wewe ushachukua bahasha ya kaki unasifia mapambio hapa na mo wakati anaichukua simba je ilikuwa na thamani hyoya billion 20 ?
 
Mara ya mwisho kwenda uwanjani ni lini au unaongea tu kwenye keyboard huna chochote unachochangia kwenye team ila una hoji billion 20 ziko wapi
 
Kama vipi Moo aturudishie tu timu yetu! Sisi mashabiki tumechoka kuitwa mbumbumbu na wapinzani wetu.
Yanga anapata elfu 3,500/= kwenye jezi inayouzwa elfu 35,000/= kweli aliyeturoga mashabiki wa simba na yanga ndo huyo hyo aliyeturoga kwenye siasa ndio maana ccm washajua wanaongoza mazezeta hawajali wanafanya wanachojisikia wao tu.
 
Mkuu hawa ni mashabiki wa yanga wanajificha kwenye kivuli cha simba kipindi team inashindia mihogo sio kigwangala wala wala hawa wanaopapatika hapa kwenye comment aliyekuwa anasaidia hela ya kuendesha team leo hii team imeamarika ndio wanakuja na hoja za billion 20 ziko wapi
 
Mo na viongozi wa simba wakitaka waitafune bila kuulizwa wafanye mambo matatu tu.

1. Kufanya vizuri sana kimataifa.
2. Kuifunga Yanga mara nyingi iwezekanavyo.
3.Kushinda ubingwa wa ndani kwa kadri itakavyowezekana.

Haya ndo malipo ya kuitafuna Simba bila kuulizwa.
 
Yanga wanavaa magodoro mkataba wake una thamani gani kutoka kwa GSM
 
Haya mambo yanatokea sana kwenye nchi yetu. Huko kwenye siasa ndio usiseme.. 10% inazima watu midomo
 
Simba na Yanga zinamilikiwa na serikali kwa 100%, hao wengine unaowaona ni waendeshaji tu wa hizi timu, hakuna mchakato wowote wa kisheria utafanyika wa timu hizo kumilikiwa na watu binafsi.

Mwenye masikio na asikie.
 
Mkuu hawa ni mashabiki wa yanga wanajificha kwenye kivuli cha simba
Sijui wewe una umri gani. Lakini mimi wakati Yanga inafungwa bao sita bila (6-0) nilishakua duniani tayari napumua na kuijua dunia.

Hoja yangu ni kwamba haya mambo ya Uwekezaji na Hisa ni mambo ya kitaalam na hayafuatwi na Klabu ya Simba. Hakuna hatua hata moja ya kitaalam iliyofanyika tokea ule mkutano ulioridhia Mo kupewa Asilimia arobaini na tisa (49%) ya Klab ya Simba.

Mimi siyo shabiki maandazi bali ni mwanasimba ambaye wakati wote natembea na akili zangu zikiwa kichwani. Kwa nini Klab yetu haithaminishwi na ijulikane thamani yake?

Kwa nini uwekezaji wa Mo hauko wazi ili ijulikane anawekeza kiasi Gani Simba? HIvi ni nani anayejua mwaka jana kwa mfano kwenye msimu uliopita, Simba ilitumia kiasi gani kwenye Usajili, mishahara ya wachezaji na wafanyakazi wa Klab, Gharama za ushiriki wa mashindano ya ndani na ya kimataifa, na mambo ya uwekezaji mwingine.

HIvi ni nani aliamua uwanja wa Bunju uitwe "Mo Arena" na kwa makubaliano gani?
 
Nakuunga mkono siku zote kwenye mkutano wa Simba wa mwaka ripoti ya fedha haijadiliwi kiundani Kuna kupelekeshana Tena wanaitisha siku ambayo Simba Ina mechi Wala hawajawahi kuiweka hadharani wakati muundo umekamilika
 
Nakuunga mkono siku zote kwenye mkutano wa Simba wa mwaka ripoti ya fedha haijadiliwi kiundani Kuna kupelekeshana Tena wanaitisha siku ambayo Simba Ina mechi Wala hawajawahi kuiweka hadharani wakati muundo umekamilika
Unajua kuna swali likiulizwa watu watanuna?

Hivi klab yetu ya Simba nani ni mmiliki wake??

Kama kuna mtu anajua anayeimiliki Simba kwa sasa atuambie!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…