Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 10,448
- 8,705
Na kadai Nyerere aliwahi kusema Muhindi asiruhusiwe kuongoza Waislam. Nyerere ambae alikaribia kugombana na wenzie akitetea usawa wa wote, wahindi, wazungu, waafrika. Mada ni uislamu. Msemaji mwongo na wewe, kama wewe sio yeye, pia mwongo mkubwa
Basi usiiruke mada kuu hiyo, mada yako hapa ni Waislamu walikandamizwa. Ulitaka kujifanya mada ni wanaharakati za uhuru waliosahaulika kwa ujumla, nikakwambia mongo. Umeshindwa kujificha?Mwalimu Nyerere aliwakandamiza sana Waislam na akiwaogopa mno hasa baada ya kuona nguvu yao wakati wa kudai uhuru.
hili linaonyesha vipi kwamba Nyerere alikandamiza Waislamu? Halafu imesemwa kwenye mhadhara wa Mohamed Said kwamba nyaraka haikutaja chanzo cha waandishi au mawazo, wewe umejuaje, umehadithiwa na Skyes?Hivi unajua kuwa hata ile hotuba aliyosoma Umoja wa Mataifa 1955 ile hotuba iliandikwa na Kamati ya TAA chini ya uongozi wa Abdulwahid Sykes 1950? Hili ulikuwa unalijua?
Unajua kuwa Nyerere hakutaka Waislam wawe na Chuo Kikuu na ndiyo maana akaivunja East African Muslim Welfare Society 1968 ambayo ilikuwa katika harakati ya kukijenga? Unajua kuwa njama hiyo aliifanya akishirikiana na Kanisa Katoliki?
Mohammed Said,Ukitaka umuelewe vyema Mwalimu Nyerere inakubidi kwanza usome kitabu na kama unaona shida ya kusoma ipo DVD ilirekodiwa Msikiti wa Mtambani mwezi wa Ramadhani mwaka jana. DVD hii inapatikana Al Hazm Bookshop Msikiti wa Mtoro. Ukipenda msome pia John Sivalon, Bergen, Njozi, Mwaijage, Ghassany nk. kuna mengi ndani ya vitabu hivyo kuhusu Nyerere ambavyo havifahamiki kwa wengi. Mwalimu Nyerere aliwakandamiza sana Waislam na akiwaogopa mno hasa baada ya kuona nguvu yao wakati wa kudai uhuru.
Hivi unajua kuwa hata ile hotuba aliyosoma Umoja wa Mataifa 1955 ile hotuba iliandikwa na Kamati ya TAA chini ya uongozi wa Abdulwahid Sykes 1950? Hili ulikuwa unalijua?
Unajua kuwa Nyerere hakutaka Waislam wawe na Chuo Kikuu na ndiyo maana akaivunja East African Muslim Welfare Society 1968 ambayo ilikuwa katika harakati ya kukijenga? Unajua kuwa njama hiyo aliifanya akishirikiana na Kanisa Katoliki? Insha Allah taratibu tutaeleweshana na huenda iko siku Mungu atatuelekeza katika haki na tutashirikiana katika haki na usawa ili nchi yetu itengemae.
Ukitaka umuelewe vyema Mwalimu Nyerere inakubidi kwanza usome kitabu na kama unaona shida ya kusoma ipo DVD ilirekodiwa Msikiti wa Mtambani mwezi wa Ramadhani mwaka jana. DVD hii inapatikana Al Hazm Bookshop Msikiti wa Mtoro. Ukipenda msome pia John Sivalon, Bergen, Njozi, Mwaijage, Ghassany nk. kuna mengi ndani ya vitabu hivyo kuhusu Nyerere ambavyo havifahamiki kwa wengi. Mwalimu Nyerere aliwakandamiza sana Waislam na akiwaogopa mno hasa baada ya kuona nguvu yao wakati wa kudai uhuru.
Hivi unajua kuwa hata ile hotuba aliyosoma Umoja wa Mataifa 1955 ile hotuba iliandikwa na Kamati ya TAA chini ya uongozi wa Abdulwahid Sykes 1950? Hili ulikuwa unalijua?
Unajua kuwa Nyerere hakutaka Waislam wawe na Chuo Kikuu na ndiyo maana akaivunja East African Muslim Welfare Society 1968 ambayo ilikuwa katika harakati ya kukijenga? Unajua kuwa njama hiyo aliifanya akishirikiana na Kanisa Katoliki? Insha Allah taratibu tutaeleweshana na huenda iko siku Mungu atatuelekeza katika haki na tutashirikiana katika haki na usawa ili nchi yetu itengemae.
Ajabu moja ya historia hii ni kuwa inaumiza wengi na sishangai kuwa lugha yako inakuwa kali kidogo. Lakini ukweli ndiyo huu historia ilitaka kufichwa na mimi Mungu akajaalia nikaiandika. Ikiwa hujakisoma kitabu kisome utakutana na madaktari wote waliokuwa katika siasa: Dr. Joseph Mutahangarwa, Dr Luciano Tsere, Dr Michael Lugazia, Dr Vedasto Kyaruzi. Utamsoma Chief Patrick Kunambi, Chief Kidaha Makwaia nk.
Kleist Sykes baba yake Abdulwahid ndiyo alikuwa katibu muasisi wa African Association 1929 na mwanawe akaja kuichukua nafasi hiyo ya ukatibu1950. Haya yalifichwa ikawa historia ya TANU ni Nyerere pekee yake. Hili ndilo lililokuwa likinisikitisha sana. Ikiwa katokea mtu anakasirishwa na ukweli huu hii ni bahati mbaya sana.
Hao wa kina Sykes wenyewe wamemruka huyo Saidi na uzushi wake.... Bahati nzuri na mimi nilipata bahati ya kumfahamu marehemu Wahid Kleist Sykes. Mwanae Kleist was my school mate and my best friend still up to this day. Nyerere alianza kuandika vitu akiwa Makerere na hata ile hotuba unayodai aliandikiwa na akina Sykes...
Hao wa kina Sykes wenyewe wamemruka huyo Saidi na uzushi wake.
Sikiliza hapa jinsi mayor Sykes alivyodadavua jinsi Saidi alivyojipendekeza kwa familia yao na udini wake.
Fundi Mchundo, umesikia Sykes alivyosema alimwambia nini Saidi, Saidi unataka kuandika kitabu cha uislamu, au unaandika harakati za ukombozi kwa ujumla, au wasifu wa Bw. Sykes au nini haswa?Napenda kumtaka radhi sana Mzee Kleist Sykes kwa ku"insinuate" kuwa ni disgruntled individual. Huyo Mohamed Said anatoa distorted version ya hali ilivyo. Nakushukuru sana Tindikali kwa kutuwekea hiyo video. N
Amandla........
Lakini muhimu tujadili historia ya uhuru wa Tanganyika na mashujaa wake ambao wamefutwa katika historia yab nchi yetu. Hii ndiyo mada kuu na husika katika mjadala huu.
Mkuu sielewi kama umeyaelekeza maneno yako kwangu au mtu mwingine lakini hata hivyo nitachukulia kwamba unanambia mimi kwa sababu ndiye mtu wa mwisho kuandika kabla ya majibu haya.Ahsante kwa mawazo yako. Itakuwa bora sana endapo utakisoma kitabu. Baada ya hapo unaweza kutoa hukumu. Tatizo nilionalo katika mjadala huu ni kuwa wengi wanachangia bila ya kuwa na uelewa wa historia ya kudai uhuru wa Tanganyika.
Hii inasababisha wao kutoa maneno tu ya jumla na hili nimeliona hata kwako. Ningependa kukumbusha kama Muislam kuwa Allah katufunza adabu na hili ukizingatia hata katika maingilianao kama haya hujenga tija na mapenzi baina ya watu. Hapana haja ya kushambuliana kwa lugha kali.
Muhimu ni kusoma hoja na kujibu kwa utulivu. Hii huleta raha katika mjadala si kwa wale wanaoshindana bali hata kwa wasomaji wengine. Imam Shaffi kasema yeye anaweza kusimama kwa hoja hata na watu mia yeye akiwa peke yake lakini mjinga mmoja tu yeye huwa
keshashindwa.
Insha Allah tutaendelea kujadiliana na kuheshimiana katika maingiliano yetu hasa zaidi kwa kuwa wewe kama mimi ni Waislam na wasio kuwa Waislam watatuhukumu kwa akhlak zetu.
Hiyo hotuba iliyosomwa na Mwalimu Nyerere mwaka 1955 Umoja wa Mataifa ina kisa kirefu sana na cha kupendeza. Laiti ungekijua kisa chenyewe na watu walioandika na katika mazingira gani hadi ilipomfikia Nyerere 1955 kuna mengi naamini yangepita katika akili yako. Sasa hapo ungekuwa katika hali nzuri sana ya kuchangia. Inasemekana nyaraka hii ile yenyewe ambayo ina mkono wa Abdulwahid Sykes, Sheikh Hassan bin Amir, Hamza Mwapachu, Stephen Mhando imeondolewa katika Tanzania Nationa Archive (TNA) haipatikani.