Ukweli kuhusu waasisi wa TANU na harakati za kupigania uhuru

Ukweli kuhusu waasisi wa TANU na harakati za kupigania uhuru

Status
Not open for further replies.
Ahsante Lole. Hilo la kujenga shule ndilo chanzo cha Waislam kupambana na Nyerere vita iliyoanza chinichini kuanzia 1963. Hili la ujenzi wa shule na Chuo Kikuu nimelieleza kwa kirefu sana katika kitabu. Nakushauri usome kitabu. Majibu yako yamo mle.
 
Mohammed Said pamoja na kutokubaliana na wewe juu ya lawama zako kwa Nyerere,at least wewe na wengine have come out of the closet,na kukubali kuwa andiko lako ni ya kimsingi kutetea uislamu.
Huna haja ya kusubiri muda mrefu maana vitatoka vitabu vingi tu kupinga hilo.Hata kwa thread hii na thesis yako nadhani kuna material ya kutosha kurebute propagation zako.
Sasa ukweli utabakia palepale,elimu na maendeleo sehemu nyingi walizokaa waislamu ni duni. Ungeandika kitabu kingine kualleviate hali hiyo. La sivyo rudi kwa ushauri wa Nyerere, jengeni shule za msingi na sekondari maeneo yenu.Halafu watu waache uvivu,walime waache kucheza ngoma zisizo na tija. Maendeleo ni from within, huletewi on a silver platter.
Mkuu haya matusi sasa, na hakika wewe hukusoma kuliko Waislaam hilo nakuhakikishia. Kukariri vitu sio kuelimika...
 
Ahsante Mkandara,

Nami nasoma kutoka kwako.
Nafaidika.

Ahsante ndugu yangu.
 
Niwie radhi ndugu yangu.
Sijapata kuandika matusi hata siku moja.

Kama unahisi nimekutusi nisamehe sana ndugu yangu haikuwa nia yangu.
 
Ikiwa uatasoma kitabu utakuta ndani yake kamati aliyounda Abdulwahid Sykes mwaka 1950 mmoja wa wanakamati alikuwa Sheikh Hassan bin Amir aliekuwa Mufti wa Tanganyika. Kamati hii ilijulikana kama TAA Political Sub- Committee. Hii ndiyo iliyoandika huo waraka ambao unaweza kupata habari zake katika kitabu changu na cha Cranford Pratt "Critical Phase in Tanzania."
 
By BROTHER MOHAMMED SAEED
Muslim Writer's Organization
Dar es Salaam, Tanzania. INTRODUCTION
Islam has been in existence in East Africa since the eighth century. With Islam, emerged the lingua franca, Kiswahili, spoken throughout East and Central Africa and the Swahili culture which is mostly associated with Muslims. About two-thirds of East Africa's Muslims reside in Tanzania which is the most populous of the East African countries i.e. Kenya, Uganda and Tanzania. According to the 1957 population census, Muslims outnumbered Christians at a ratio of three to two. This means Tanzania is a leading Muslim nation in the region. But the 1967 census the total figures for Tanzania Mainland are 32% Christian, 30% Muslim and 37% local belief. This shows Pagans as a leading majority. The 1967 census has not been able to show the reasons for the sudden decrease of Muslim population nor the growth of Paganism. This was the last population census showing religious distribution. It is widely believed that the figures for the 1967 census were doctored for political reasons to show Muslims were trailing behind Christians in numerical strength. This paper "lnsha Allah", will try to show the reasons behind such a move and many others.
Christianity is a relatively new religion in Tanzania having introduced into the country during the 18th Century by professional missionaries. Christianity was resisted by Muslims right from the beginning. In any uprising against the colonial state Muslims took that opportunity to attack missionaries and Christian establishments.2 Muslims perceived both missionaries and the colonial state as fellow collaborators and therefore enemies to Islam. Islamic radicalism has therefore a long history in the struggle against colonial rule and Christianity. Christianity meanwhile became a reactionary force siding with the colonial state. In the Maji Maji War of 1905 some Christians fought alongside the German army against the people to safeguard Christianity.3 In this war some Muslims were hanged particularly for killing missionaries and for waging a war against German rule.
The British took over Tanganyika (as Tanzania was then known) from the Germans after the First World War, by then the Germans had done more than their fair share in opening up Tanganyika for Christian influence through various Christian establishments. Tanganyika was divided among different Christian organizations originating from various European countries. The White Fathers were in Tabora, Karema, Kigoma, Mbeya, Mwanza and Bukoba; Holy Ghost Fathers - Morogoro and Kilimanjaro; Benedictine Fathers Peramiho and Ndanda; Capuchin Fathers - Dar es Salaam; Consolata Fathers - Iringa and Meru; Passionists Fathers - Dodoma; Pallotine Fathers - Mbulu; Maryknoll Fathers Musoma; and Rosmillian Fathers -lringa.4 When the People started to organize themselves in political entities during the British rule through various associations, Muslims in Dar es Salaam formed the African Association in 1929 and Jamiatul lslamiyya fi Tanganyika in 1933. Missionaries sensing these African organisations as organised African resistance against the colonial state warned Christians not to get themselves involved in any movements that were challenging the government.5 The church and state provided education to African Christians and denied it to majority Muslims. The two worked hand in hand to mould loyal subjects out of the educated Christians alienating them from the main stream of the struggle against British rule. Resistance against British colonialism was therefore left to Muslims and the struggle for independence and nationalist politics in Tan9anyika assumed strong Muslim characteristics.

http://www.igs.net/~kassim/nyaraka/islam_and_politics_in_tz.html

Mkuu Mohamed Said Abdallah, hivi wewe ndiye uliyeandika article hii?

C.V. yako, ukaribu wako na wakina Sykes humu ndani vyote havina maana kwa sababu hatukujui. Kilicho mbele yetu ni maandiko yako ambayo yamejaa inconsistencies. Msomi anatambuliwa na anachoandika na si wasifu wake. Einstein alikuwa mtu wa kawaida tu wakati anaandika relativity theory yake. CV yake ilikuwa nyepesi lakini kile alichoandika kikatikisa ulimwengu. Lakini ndugu yetu wewe usomi wako una walakin. Unataka kuandika upya historia nzima ya nchi yetu kwa kutumia source moja tu? Hauoni hata huyo kijana aliyekuhoji alienda kwa huyo unayedai kuwa ndiye source yako kwa uthibitisho. Kwa vile Kleist katofautiana na wewe, unamuita mnafik maana angekuwa muungwana basi angesimamia yale unayodai alikueleza bila kujali siasa.

Mkuu, hapa ulipoingia ni pabaya. Jukwaa hili lina watu wa kila aina kama ulivyoona. Wako wengi ambao nao waliishi wakati huo unaosimulia, wengine walisoma na huyo unayemtaja na wana uwezo wa kumpigia simu na kumuuliza na wengine ni hao hao unaowazungumzia! Kibaya kingine ni kuwa huu ni wakati wa mtandao, kila unachosema kinaweza kuwa fact-checked mara moja maana tofauti na unavyodhani, wengi tu wameandika kuhusu matokeo haya katika nyanja tofauti. Kutuambia kuwa wewe pekee ndiye oracle wa historia yetu ni kututusi sisi, wazazi wetu na waliotutangulia.

Hauwezi ukadai kuwa waislamu ndio waliomwandikia hotuba Nyerere halafu katika kamati unayodai ndiyo wahusika wakuu, nusu yake ni wakristu ( John Rupia, Vedasto Kyaruzi na Stephen Mhando). Hauwezi kutuambia bila aibu kuwa Mwalimu alichukua risala iliyoandikwa miaka mitano kabla na kuenda kuisoma bila kuifanyia marekebisho. Mtu yeyote anayejiandaa kutoa hotuba muhimu anafanya background studies na anatumia yaliyotangulia kujenga hoja ya kila atakachoenda kuhutubia. Bila shaka kama palikuwepo na draft ya hotuba/ article iliyohusu kitu atakachoenda kuhutubia, alisoma na ilimsaidia. Lakini kudai kuwa aliichukua jumla haiingii kichwani kwa yeyote aliyewahi kufanya presentation ya aina yeyote. Hotuba yake ilitakiwa iwe current kwa hiyo isingeweza kutumia matukio ya miaka mitano na zaidi kabla bila kuweka yale yaliyotokea karibu zaidi.

Hapa hapakufai, Mkuu. False prophets hawavumiliwi humu.

Amandla......
 
Ikiwa uatasoma kitabu utakuta ndani yake kamati aliyounda Abdulwahid Sykes mwaka 1950 mmoja wa wanakamati alikuwa Sheikh Hassan bin Amir aliekuwa Mufti wa Tanganyika. Kamati hii ilijulikana kama TAA Political Sub- Committee. Hii ndiyo iliyoandika huo waraka ambao unaweza kupata habari zake katika kitabu changu na cha Cranford Pratt "Critical Phase in Tanzania."
Mkuu sawa uliandikwa na hao ulowataja. Sasa ni kipi kikubwa haswa hapa kwa sababu kila rais duniani anaye mtu au watu wanaoandika waraka..Hii inathibitisha kitu gani haswa!
 
Kuna wakili mmoja hivi karibuni alisema: Unamshtaki mtu kwa kukuibia kuku lakini unapoambiwa ulete ushahidi wa alichoiba, unaleta bata!

Mpaka sasa haujatoa ushahidi wowte wa central thesisi yako kuwa palikuwa na bado pana structural discrimination na marginalization ya wsislamu ( ikiongozwa na wakristu hususan wakatoliki) zaidi ya kutuambia tusome kitabu chako. Jibu maswali, Mkuu, badala ya kujificha nyuma ya fig leaf. Ukali na matusi ya wanaokupinga wala yasikubabaishe. Kama ni msomi kweli basi unajua kuwa akademia hayo ni par for the course!

Amandla........
 
Ubaya wa mtandao ni huu:

http://assets.cambridge.org/97805211/10723/excerpt/9780521110723_excerpt.pdf

Craford Pratt anazungumzia kuhusu uzalendo, nationalism na si islamization kama unavyodai. Kama alivyosema Mkandara wengi wa hao unaowaita waislamu hawakuwa aina ya waislamu unaotaka kuwafanya. Walikuwa ni watu wa starehe na hawakuona tatizo kuchanganyikana na wakristu. Kwenye suala la uhuru wa Tanganyika, walikuwa Nationalists kwanza na waislamu baadae. Walijitambua kama wenye nchi hasa kwa misingi ya rangi yao. TANU haikuitwa Tanganyika AFRICAN National Union bila sababu. Kwa lugha ya siku hizi waliweka uzawa mbele na sio dini kwenye suala hili. Ndiyo maana wakina Kleist wanakumbushia mchango wa watu kama Chief Patrick Kunambi na wengine wasio waislamu. Ndiyo maana anasita unapotaka kusema kuwa uhuru huu uliletwa na waislamu wakiongozwa na wakina Sykes. Anajua sii kweli maana hawezi kuwakana wakina Rupia, Mhando, Kyaruzi, Pombeah na wengine. Anajua kuwa pamoja na Dar kuwa ndiyo kitivo lakini bila kuungwa mkono na sehemu nyingine za nchi, huo uhuru usingepatikana. Kutuambia leo kuwa uhuru umepatikana Mission Quarter si kuwaaaatendea haki wale wote waliojitoa mhanga (kwa damu na mali) katika harakati za uhuru bila kujali dini ya wenzao. Wengi wa hawa wamesahauliwa. Hicho ndicho cha kulilia.

Amandla......
 
Mkuu haya matusi sasa, na hakika wewe hukusoma kuliko Waislaam hilo nakuhakikishia. Kukariri vitu sio kuelimika...
Mkuu Mkandara wanishangaza, sisi wengine ingawaje ni "watu wa kuja" hapa Dar es salaam, lakini tunaifahamu hii Dar kuliko wazaramo wenyewe.
Na nikisema watu wanacheza ngoma huna haja ya kwenda mbali, nanda tu nje ya Dar na ujionee hali ya kilimo na maendeleo kwa ujumla.
Halafu Mohammed Said aliandika kitabu hiki kwa ajili gani?
Ili tumwonee huruma au aipindue status quo?
Mimi si msomi lakini ni muelewa, kuwa sehemu nyingi walizo wenzetu waislamu,nyingi zina maendeleo duni hili halihitaji ubishi, lakini wote ni waTanzania lazima waendelee.
Cha msingi hawataletewa maendeleo kama mvua , lazima wayaanze wenyewe, na hili waliona tusi?
Ukweli unauma ndugu yangu, lakini mimi niko tayari kuchangia shule za sehemu hizo lakini sishule za kidini, kwa maan wote ni watanzania na maendeleo tunayahitaji wote.
 
http://www.igs.net/~kassim/nyaraka/islam_and_politics_in_tz.html

Mkuu Mohamed Said Abdallah, hivi wewe ndiye uliyeandika article hii?

C.V. yako, ukaribu wako na wakina Sykes humu ndani vyote havina maana kwa sababu hatukujui. Kilicho mbele yetu ni maandiko yako ambayo yamejaa inconsistencies. Msomi anatambuliwa na anachoandika na si wasifu wake. Einstein alikuwa mtu wa kawaida tu wakati anaandika relativity theory yake. CV yake ilikuwa nyepesi lakini kile alichoandika kikatikisa ulimwengu. Lakini ndugu yetu wewe usomi wako una walakin. Unataka kuandika upya historia nzima ya nchi yetu kwa kutumia source moja tu? Hauoni hata huyo kijana aliyekuhoji alienda kwa huyo unayedai kuwa ndiye source yako kwa uthibitisho. Kwa vile Kleist katofautiana na wewe, unamuita mnafik maana angekuwa muungwana basi angesimamia yale unayodai alikueleza bila kujali siasa.

Mkuu, hapa ulipoingia ni pabaya. Jukwaa hili lina watu wa kila aina kama ulivyoona. Wako wengi ambao nao waliishi wakati huo unaosimulia, wengine walisoma na huyo unayemtaja na wana uwezo wa kumpigia simu na kumuuliza na wengine ni hao hao unaowazungumzia! Kibaya kingine ni kuwa huu ni wakati wa mtandao, kila unachosema kinaweza kuwa fact-checked mara moja maana tofauti na unavyodhani, wengi tu wameandika kuhusu matokeo haya katika nyanja tofauti. Kutuambia kuwa wewe pekee ndiye oracle wa historia yetu ni kututusi sisi, wazazi wetu na waliotutangulia.

Hauwezi ukadai kuwa waislamu ndio waliomwandikia hotuba Nyerere halafu katika kamati unayodai ndiyo wahusika wakuu, nusu yake ni wakristu ( John Rupia, Vedasto Kyaruzi na Stephen Mhando). Hauwezi kutuambia bila aibu kuwa Mwalimu alichukua risala iliyoandikwa miaka mitano kabla na kuenda kuisoma bila kuifanyia marekebisho. Mtu yeyote anayejiandaa kutoa hotuba muhimu anafanya background studies na anatumia yaliyotangulia kujenga hoja ya kila atakachoenda kuhutubia. Bila shaka kama palikuwepo na draft ya hotuba/ article iliyohusu kitu atakachoenda kuhutubia, alisoma na ilimsaidia. Lakini kudai kuwa aliichukua jumla haiingii kichwani kwa yeyote aliyewahi kufanya presentation ya aina yeyote. Hotuba yake ilitakiwa iwe current kwa hiyo isingeweza kutumia matukio ya miaka mitano na zaidi kabla bila kuweka yale yaliyotokea karibu zaidi.

Hapa hapakufai, Mkuu. False prophets hawavumiliwi humu.

Amandla......
Wewe wacha kumtisha Mohammed Said na Jukwa lako!.Hili jukwaa linajulikana zaidi na watu kama wewe,walio wengi wameisoma historia aliyoiandika na kwa ushahidi wa matukio wakakubaliana nayo.
Mohammed anatambuliwa na vyuo vingi vya kimataifa na kazi zake ziko huko,sasa wewe na jukwaa lako mutaathiri nini?.
Mohammed Said ndiye anayefaa kuandika aliclhoandika kwa sababu anatokana na familia iliyohusika na harakati za kuleta uhuru,ana nyaraka nyingi halisi na amehojiana na wahusika wenyewe sio akina hao unaosema wamesoma nao.ambao wanaweza kutoa ushahidi wa uongo makusudi kupotosha.
Ni tabia ya ukweli na haki kuibuka muda wowote na watu wa aina yako wala hawana uwezo wa kuukandamiza.
 
Mohammed Said,
You do not have the monopoly of knowing Julius Nyerere. Wewe peke yako si source ya hulka na tabia za Julius Nyerere kwa hiyo hii ya kutuambia kwamba tusome kitabu chako ndipo tutamjua Julius Nyerere ni kutaka kutusokomezea ideolgy zako na dhana. Nimewasoma wote Sivalon, Bergen, Njozi, Rasheed, Mwaijage(huyu aliwekwa detention kwa kuhusika na njama za kupindua serikali) Wote hao uliowachagua wana theme moja na wewe na kwa hivi nawaweka kundi moja. Bahati nzuri na mimi nilipata bahati ya kumfahamu marehemu Wahid Kleist Sykes. Mwanae Kleist was my school mate and my best friend still up to this day. Nyerere alianza kuandika vitu akiwa Makerere na hata ile hotuba unayodai aliandikiwa na akina Sykes nina hakika 99% Nyerere aliweka mkono wake na mawazo yake pale. Hakuwa mbumbumbu kama unavyotaka watu waamini kwamba alienda UN kusoma kitu kama kasuku. Kama ungefanya utafiki makini ungegundua kwamba kulikuwa na sababu nyingi za Nyerere kuvunja EAMWS na si kwa sababu tu ya harakati za kujenga chuo cha waislamu.
Nonsense!, Naamini hujawasoma hao unaowataja na hujasoma historia iliyoandikwa na Mohammed Said.
Wanaomfahamu Nyerere ni wale aliowataja Mohammed ambao ndio waliomkaribisha kwenye siasa na kumlipia chakula na usafiri,halafu akalipa shukrani za punda kwa kuwapiga mateke.Nguo za Nyerere wakati wa mwanzo wa harakati za uhuru zilikuwa zikifuliwa na mama wa mmoja wa wanaharakati huo.
Hivyo Mohammed sio aliyemjua zaidi Nyerere.Waliomjuwa ni wengi ambao yeye alihojiana nao.Historia ipi inapaswa kuitwa historia sahihi ukiondoa hii.
 
Amandla angalia katika footnotes utakuta majina ya walioandika waraka ule na jinsi Pratt alivyousifia. Halikadhalika utapata kuelewa kutoka kwake hali ya siasa kama ilivyokuwa wakati ule.

Bado nasisitiza kuwa ungekisoma kitabu changu ungefaidika na mengi na hata labda mrengo wa uandishi na mawazo yako katika somo hili ungelibadilika. Nasema hivyo kwa kuwa katika hii post ya sasa hivi cha ajabu nilichokiona ni kuwa umesema yale ambayo mimi nimeyaeleza katika kitabu tena kwa urefu sana. Ikiwa tutaendelea na mjadala huu wakati ukiwa wewe hujui nilichosema katika kitabu tutakuwa tunarudiarudia hoja zilezile na hili litatoa ladha ya mnakasha na hata watusomao watopoteza hamu.
 
Mohammed Said pamoja na kutokubaliana na wewe juu ya lawama zako kwa Nyerere,at least wewe na wengine have come out of the closet,na kukubali kuwa andiko lako ni ya kimsingi kutetea uislamu.
Huna haja ya kusubiri muda mrefu maana vitatoka vitabu vingi tu kupinga hilo.Hata kwa thread hii na thesis yako nadhani kuna material ya kutosha kurebute propagation zako.
Sasa ukweli utabakia palepale,elimu na maendeleo sehemu nyingi walizokaa waislamu ni duni. Ungeandika kitabu kingine kualleviate hali hiyo. La sivyo rudi kwa ushauri wa Nyerere, jengeni shule za msingi na sekondari maeneo yenu.Halafu watu waache uvivu,walime waache kucheza ngoma zisizo na tija. Maendeleo ni from within, huletewi on a silver platter.

Lole Gwakisa umepatia kuhusu sehemu wanazoishi waislamu wengi kuwa duni na kukuongezea pia hudunishwa. Mimi sikulaumu kwa kufikiri waislamu ni wavivu na wacheza ngoma na wasio taka shule kwani hapo ndipo upeo wako wa kufikiri ulipofika,nani anaweza kumkatalia mtu upeo wake? Inawezekana kabisa waislamu ni wavivu na wacheza ngoma na mambo mengine yote wayafanyayo kujidunisha. Waislamu wa Pemba Kilwa, Kigoma, Tabora, Tanga, Lindi, Mtwara na kwingineko Tanzania wote wana tabia zinazofanana kwa sababu ya tamadunizao za kiislamu. Tamaduni ambazo no tofauti kabisa na zile za Indonesia, Malaysia, Falme za kiarabu na kwingineko kote duniani. Waislamu wa Tanzania labda tatizo lao la kibaiolojia zaidi, wana genes za umasikini na kuwa duni si et eeeh Gwakisa. Hii inawezekana, kama waislamu wote duniani wamezaliwa na genes za kuwa magaidi kwa nini hili lishindikane? Upeo wa kufikiri ndio mpaka wa fikra kwa kila binadamu kufikia tawala zingine za tafakuru ya juu. Hebu hakikisha theory yako ya uduni wa waislamu na kukua na kuzaliwa kwa black nation katika USA, kisha soma Galtung theory of Core and Periphery halafu uone kama mpaka wa upeo wako utaongezeka au la halafu uje uwaambie wana JF
 
Wewe wacha kumtisha Mohammed Said na Jukwa lako!.Hili jukwaa linajulikana zaidi na watu kama wewe,walio wengi wameisoma historia aliyoiandika na kwa ushahidi wa matukio wakakubaliana nayo.
Mohammed anatambuliwa na vyuo vingi vya kimataifa na kazi zake ziko huko,sasa wewe na jukwaa lako mutaathiri nini?.
Mohammed Said ndiye anayefaa kuandika aliclhoandika kwa sababu anatokana na familia iliyohusika na harakati za kuleta uhuru,ana nyaraka nyingi halisi na amehojiana na wahusika wenyewe sio akina hao unaosema wamesoma nao.ambao wanaweza kutoa ushahidi wa uongo makusudi kupotosha.
Ni tabia ya ukweli na haki kuibuka muda wowote na watu wa aina yako wala hawana uwezo wa kuukandamiza.

Sasa mmefuata nini huku kama hili jukwaa ni la watu kama mimi? Wahusika wenyewe wamemkana huyu Mohamed Said sasa unataka ushahidi gani kwani anatumia facts kujenga uongo?

Amandla........
 
Amandla angalia katika footnotes utakuta majina ya walioandika waraka ule na jinsi Pratt alivyousifia. Halikadhalika utapata kuelewa kutoka kwake hali ya siasa kama ilivyokuwa wakati ule.

Bado nasisitiza kuwa ungekisoma kitabu changu ungefaidika na mengi na hata labda mrengo wa uandishi na mawazo yako katika somo hili ungelibadilika. Nasema hivyo kwa kuwa katika hii post ya sasa hivi cha ajabu nilichokiona ni kuwa umesema yale ambayo mimi nimeyaeleza katika kitabu tena kwa urefu sana. Ikiwa tutaendelea na mjadala huu wakati ukiwa wewe hujui nilichosema katika kitabu tutakuwa tunarudiarudia hoja zilezile na hili litatoa ladha ya mnakasha na hata watusomao watopoteza hamu.

Hapa si mahala pa biashara. Ulieandika hicho kitabu si wewe? Basi kwa nini usitumie yale uliyoandika kupinga hoja zetu badala ya kukazania kuwa tukisome? Au uiliandikiwa, Mkuu, kwa hiyo hauwezi kukumbuka kilichoandikwa?

Amandla....
..
 
Lole Gwakisa umepatia kuhusu sehemu wanazoishi waislamu wengi kuwa duni na kukuongezea pia hudunishwa. Mimi sikulaumu kwa kufikiri waislamu ni wavivu na wacheza ngoma na wasio taka shule kwani hapo ndipo upeo wako wa kufikiri ulipofika,nani anaweza kumkatalia mtu upeo wake? Inawezekana kabisa waislamu ni wavivu na wacheza ngoma na mambo mengine yote wayafanyayo kujidunisha. Waislamu wa Pemba Kilwa, Kigoma, Tabora, Tanga, Lindi, Mtwara na kwingineko Tanzania wote wana tabia zinazofanana kwa sababu ya tamadunizao za kiislamu. Tamaduni ambazo no tofauti kabisa na zile za Indonesia, Malaysia, Falme za kiarabu na kwingineko kote duniani. Waislamu wa Tanzania labda tatizo lao la kibaiolojia zaidi, wana genes za umasikini na kuwa duni si et eeeh Gwakisa. Hii inawezekana, kama waislamu wote duniani wamezaliwa na genes za kuwa magaidi kwa nini hili lishindikane? Upeo wa kufikiri ndio mpaka wa fikra kwa kila binadamu kufikia tawala zingine za tafakuru ya juu. Hebu hakikisha theory yako ya uduni wa waislamu na kukua na kuzaliwa kwa black nation katika USA, kisha soma Galtung theory of Core and Periphery halafu uone kama mpaka wa upeo wako utaongezeka au la halafu uje uwaambie wana JF

Mimi nashindwa kuwaelewa. Sasa kama hali ya waislamu wengi si duni (kudumaa katika elimu n.k.) sasa mnachowalaumu wakatoliki ni nini? Si nyie ndiyo mnaodai kuwa kanisa la katoliki na Nyerere walifanya maksudi tu kutopeleka maendeleo katika sehemu wanazoishi waislamu? Sasa kama mambo yenu ni super, hao wakatoliki mnawalaumia nini?

Wote humu tunajua hali ya maendeleo ya mikoa ya pwani, Lindi, Mtwara, Kigoma n.k. Wote tunajua kuwa wenyeji wengi wa maeneo hayo ni waislamu. Tunachojiuliza ni kwa nini sehemu hizo zibaki kuwa duni? Mohamed Said na watu kama nyinyi, mnaona mkono wa wakristu katika kudumazwa huko. Wengine wanasema kuwa ndivyo waislamu walivyo. Wengine wanasema kuwa badala ya kuangalia dini za watu waliokuwa maeneo hayo tuangalie mchango wa mila na desturi zao ambazo mara nyingi hazina uhusiano na dini zao. Wengine wanasema mbona kuna sehemu ambazo wanaishi wakristu ambazo ziko nyuma kimaendeleo? Manyara, Mara, Ruvuma,Rukwa n.k. Yote haya ni katika kuangalia namna gani tutakavyoweza kumkwamua mtanzania mwenzetu kutoka katika umasikini uliokithiri. Hapa hatuzungumzii muislamu wa Malaysia au Dubai bali mtanzania wa Ikwiriri na Mwanarumango ( ambae probability kubwa ni muislamu) ambae ni maskini. Kwani tunaposema hivi, tuna maana kuwa wakristu wote wameendelea na ni matajiri? la hasha, hata huko kuna umaskini na kudumaa wa kutisha. lakini ukweli ni kuwa ni wakristu wengi kuliko waislamu waliopata elimu dunia. Na ndicho hiki tunachojadili.

Amandla.......
 
Hilo usemalo kuwa Nyerere alikuwa na sababu nyingi ya kuivunja EAMWS ni kweli kabisa na moja ya sababu hiyo ni hofu ya Waislam kupata elimu. Ukitaka habari zaidi kuhusu hili msome Sivalon. Hiki ni kitabu maarufu sana. Ikiwa hujakisoma fika Msikiti wa Mtambani hapo ndipo kinapouzwa. Wakatoliki walipojua kuwa Sivalon katoa siri zao kuhusu njama za kuwakandamiza Waislam wakimtumia Nyerere waliacha kukiuza kitabu hicho hapo Cathedral Bookshop.

Ama kuhusu mkono wa Nyerere katika hotuba ile hilo linawezekana sana na nitastaajabu ikiwa kama hakuchangia. Uzuri ni kuwa sasa baada ya kuandika kitabu kile leo tunazungumza yale ambayo hapo awali yalikuwa siri na nyeti hayafai kuzungumzwa. Hizi ndizo faida za kuandika na kuja na kitu kipya na kufanya mijadala kama hii.

Mimi sijadai kumjua Nyerere lakini baba yangu Said Salum Abdallah amenambia kuwa yeye alimuona Nyerere kwa mara ya kwanza nyumbani kwa Abduwahid Sykes pale Mtaa wa Aggrey na Sikukuu mwaka 1952 na marehemu Bwana Abdu akamfahamisha Nyerere kwa baba yangu.

Nyumba hii ipo hadi leo na ina historia kubwa sana. Mikutano mingi ya siri ya harakati za siasa ilikuwa ikifanyika pale hata kabla Nyerere hajajiunga na TAA Makao Makuu, Dar es Salaam.
 
Amandla kuna wakati unatumia lugha safi na kuna wakati unatoka katika mstari, hamaki inatangulia fikra yako. Sisemi usome kwa kuwa nataka kufanya biashara. Ukitumia lugha hiyo utanifanya niache mjadala na wewe kwani mimi si mtu wa hulka za kukashifiana sikulelewa hivyo. Nimefunzwa na walimu wangu toka chuoni (madras) hadi shule adabu ya majadiliano. Hata wale wasionipenda kabisa hawajapata kusema kuwa mimi nimeandikiwa vitabu nilivyopata kuandika. Amandla wewe umefurtu ada. Kwa hiyo kuanzia sasa usishangae utakapoona sijadiliani na wewe kamwe.
 
Ukiacha kujadiliana nami kamwe hamna tatizo. Hapa halizimishwi mtu.

Haiwezekani kuwa kila ukiulizwa swali unasema tusome kitabu chako bila kutuambia wapi katika hicho kitabu majibu yatapatikana. Hii kwangu mimi haiingii akilini. Wewe umeandika kitabu, basi tumia yale uliyoyaandika kujibu hoja. Kwa kuacha kufanya hivyo kunapunguza uzito wa hoja zako. Adabu ya majadiliano ni kumheshimu mwenzio kwa kujibu maswali yake na si kukwepa kwa kisingizio kuwa majibu yamo kwenye kitabu ambacho hakipo mbele yetu na wala hautaki kukitumia kujenga hoja yako. Na vile vile heshima ya mjadala inasema kuendelea kutumia jina ambalo mhusika ameishasema sio lake ni dalili ya kutomheshimu. Badala ya kukimbilia hamaki, tuthibitishe authorship yako kwa kutuambia ni wapi katika hicho kitabu chako tutapata majibu sio kutupa blanket answers. Hii haikubaliki na wewe unajua.

Amandla.........
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom