Ukweli kuhusu waasisi wa TANU na harakati za kupigania uhuru

Ukweli kuhusu waasisi wa TANU na harakati za kupigania uhuru

Status
Not open for further replies.
Lole Gwakisa umepatia kuhusu sehemu wanazoishi waislamu wengi kuwa duni na kukuongezea pia hudunishwa. Mimi sikulaumu kwa kufikiri waislamu ni wavivu na wacheza ngoma na wasio taka shule kwani hapo ndipo upeo wako wa kufikiri ulipofika,nani anaweza kumkatalia mtu upeo wake? Inawezekana kabisa waislamu ni wavivu na wacheza ngoma na mambo mengine yote wayafanyayo kujidunisha. Waislamu wa Pemba Kilwa, Kigoma, Tabora, Tanga, Lindi, Mtwara na kwingineko Tanzania wote wana tabia zinazofanana kwa sababu ya tamadunizao za kiislamu. Tamaduni ambazo no tofauti kabisa na zile za Indonesia, Malaysia, Falme za kiarabu na kwingineko kote duniani. Waislamu wa Tanzania labda tatizo lao la kibaiolojia zaidi, wana genes za umasikini na kuwa duni si et eeeh Gwakisa. Hii inawezekana, kama waislamu wote duniani wamezaliwa na genes za kuwa magaidi kwa nini hili lishindikane? Upeo wa kufikiri ndio mpaka wa fikra kwa kila binadamu kufikia tawala zingine za tafakuru ya juu. Hebu hakikisha theory yako ya uduni wa waislamu na kukua na kuzaliwa kwa black nation katika USA, kisha soma Galtung theory of Core and Periphery halafu uone kama mpaka wa upeo wako utaongezeka au la halafu uje uwaambie wana JF

Usiishie kulaumu tu , do something about it.
Umasikini upo tena kwa sana tu , na si kwa waislamu tu, mtu wa Kasulu atasema nini?
Umasikini wenu wa mawazo na ubinafsi wa umimi utakuangamiza kimaendeleo.Deep down dhana, nafikiri, ya Mohammed Said kuweka na kupublicise allegations zake dhidi ya Nyerere, mimi nakiona kama kilio cha mtanzania mwingine anayelilia maendelea, jambo ambalo si baya.
Jambo la kusikitisha ni kumtwika Nyerere ukosefu wako wa maendeleo ukijitambulisha kwa kundi moja tu, kama mwislamu.
Matatizo kama haya ya kukosa maendeleo jamii inayoyahitaji kila mahali nchini, nenda sehemu mbali mbali za nchi na utakuta matatizo kama haya.
Tatizo lako Domokaya na wengine ni kujilinganisha maendeleo yako katika misingi ya kidini.Hapo utashindwa, tena vibaya, siyo siri.Na sababu si za kidini bali za kihistoria.Ukae ukielewa hilo.
Matatizo haya yanaweza kutatuliwa from the root.Tujenge shule sehemu hizi zote, tulime na tufanye kazi, hakuna njia ya mkato.
 
Hilo usemalo kuwa Nyerere alikuwa na sababu nyingi ya kuivunja EAMWS ni kweli kabisa na moja ya sababu hiyo ni hofu ya Waislam kupata elimu. Ukitaka habari zaidi kuhusu hili msome Sivalon. Hiki ni kitabu maarufu sana. Ikiwa hujakisoma fika Msikiti wa Mtambani hapo ndipo kinapouzwa. Wakatoliki walipojua kuwa Sivalon katoa siri zao kuhusu njama za kuwakandamiza Waislam wakimtumia Nyerere waliacha kukiuza kitabu hicho hapo Cathedral Bookshop.

Ama kuhusu mkono wa Nyerere katika hotuba ile hilo linawezekana sana na nitastaajabu ikiwa kama hakuchangia. Uzuri ni kuwa sasa baada ya kuandika kitabu kile leo tunazungumza yale ambayo hapo awali yalikuwa siri na nyeti hayafai kuzungumzwa. Hizi ndizo faida za kuandika na kuja na kitu kipya na kufanya mijadala kama hii.

Mimi sijadai kumjua Nyerere lakini baba yangu Said Salum Abdallah amenambia kuwa yeye alimuona Nyerere kwa mara ya kwanza nyumbani kwa Abduwahid Sykes pale Mtaa wa Aggrey na Sikukuu mwaka 1952 na marehemu Bwana Abdu akamfahamisha Nyerere kwa baba yangu.

Nyumba hii ipo hadi leo na ina historia kubwa sana. Mikutano mingi ya siri ya harakati za siasa ilikuwa ikifanyika pale hata kabla Nyerere hajajiunga na TAA Makao Makuu, Dar es Salaam.
Salaam Aleykum Bw. Mohamed Said,
Kwanza hongera kutupatia hicho kitabu, jee kinapatikana wapi tukinunue tukisome?.
2. Nimefuatilia mjadala kwa muda tuu, ila posti hii inajulisha source za uandishi wako ni fasihi simulizi toka kwa baba yako ndipo wewe ukaziweka kwenye fasihi andishi, critics za fasihi simulizi zitaliandama andiko lako daimu dumu.
Nakitafuta kitabu chako nikusome, ili nilinganishe na maandiko ya wahusika wenyewe kama andiko la 'Harakati za Uhuru'- lililioandikwa na Makange na Baghdelah.

Nimebahatika kupata simulizi ndogo ya maisha ya Julius toka kwa Mjane wa Sykes, wakati ule akiishi Upanga opposite Califonia Dreamer, simulizi hiyo ilionyesha kweli Julius alisaidiwa na kina Skyes ila sio kweli ni kwa fedha zao pekee, fungu kubwa lilitoka kwa Mzee John Rupia, hivyo hao kina Skykes walikuwa ni miongoni mwa wadau na si wadau pekee.

Nasubiri kukusoma, ili nichukua ulichoandika, nijumlishe na kile nilichopata kwa wengine, tuendeleze mjadala huu.
 
Hilo usemalo kuwa Nyerere alikuwa na sababu nyingi ya kuivunja EAMWS ni kweli kabisa na moja ya sababu hiyo ni hofu ya Waislam kupata elimu. Ukitaka habari zaidi kuhusu hili msome Sivalon. Hiki ni kitabu maarufu sana. Ikiwa hujakisoma fika Msikiti wa Mtambani hapo ndipo kinapouzwa. Wakatoliki walipojua kuwa Sivalon katoa siri zao kuhusu njama za kuwakandamiza Waislam wakimtumia Nyerere waliacha kukiuza kitabu hicho hapo Cathedral Bookshop.

Ama kuhusu mkono wa Nyerere katika hotuba ile hilo linawezekana sana na nitastaajabu ikiwa kama hakuchangia. Uzuri ni kuwa sasa baada ya kuandika kitabu kile leo tunazungumza yale ambayo hapo awali yalikuwa siri na nyeti hayafai kuzungumzwa. Hizi ndizo faida za kuandika na kuja na kitu kipya na kufanya mijadala kama hii.

Mimi sijadai kumjua Nyerere lakini baba yangu Said Salum Abdallah amenambia kuwa yeye alimuona Nyerere kwa mara ya kwanza nyumbani kwa Abduwahid Sykes pale Mtaa wa Aggrey na Sikukuu mwaka 1952 na marehemu Bwana Abdu akamfahamisha Nyerere kwa baba yangu.

Nyumba hii ipo hadi leo na ina historia kubwa sana. Mikutano mingi ya siri ya harakati za siasa ilikuwa ikifanyika pale hata kabla Nyerere hajajiunga na TAA Makao Makuu, Dar es Salaam.

Hiki ndicho kitu nisichokipenda. Huyo Sivalon kaandika nini kuhusu Nyerere na EAMWS. Ulitakiwa kutupa brief halafu tuachie tukatafute wenyewe kama utakuwa umetugusa. Pote hapa hamna kipya ulichotuambia isipokuwa baba yako alikuwa akimfahamu Nyerere. Huu si uandishi makini. Kuwa Nyerere aliikuta TAA si kitu kigeni. Kuwa wakina Sykes walihusika sana katika uanzishwaji na uendeshaji wa TAA , na chenyewe si kitu kigeni. Kuwa kuna watu walishirikiana na Nyerere kuandika ile hotuba nacho si kitu kigeni. Kitu kigeni ni wewe kudai kuwa ile hotuba iliandikwa na waislamu (peke yao) na Nyerere alikuwa msomaji tu. Hiki tunakupinga bila hata kusoma huo unaou uita waraka wala kusikiliza hotuba husika kwa sababu haina mantik.

Amandla....
 
Mimi nashindwa kuwaelewa. Sasa kama hali ya waislamu wengi si duni (kudumaa katika elimu n.k.) sasa mnachowalaumu wakatoliki ni nini? Si nyie ndiyo mnaodai kuwa kanisa la katoliki na Nyerere walifanya maksudi tu kutopeleka maendeleo katika sehemu wanazoishi waislamu? Sasa kama mambo yenu ni super, hao wakatoliki mnawalaumia nini?

Wote humu tunajua hali ya maendeleo ya mikoa ya pwani, Lindi, Mtwara, Kigoma n.k. Wote tunajua kuwa wenyeji wengi wa maeneo hayo ni waislamu. Tunachojiuliza ni kwa nini sehemu hizo zibaki kuwa duni? Mohamed Said na watu kama nyinyi, mnaona mkono wa wakristu katika kudumazwa huko. Wengine wanasema kuwa ndivyo waislamu walivyo. Wengine wanasema kuwa badala ya kuangalia dini za watu waliokuwa maeneo hayo tuangalie mchango wa mila na desturi zao ambazo mara nyingi hazina uhusiano na dini zao. Wengine wanasema mbona kuna sehemu ambazo wanaishi wakristu ambazo ziko nyuma kimaendeleo? Manyara, Mara, Ruvuma,Rukwa n.k. Yote haya ni katika kuangalia namna gani tutakavyoweza kumkwamua mtanzania mwenzetu kutoka katika umasikini uliokithiri. Hapa hatuzungumzii muislamu wa Malaysia au Dubai bali mtanzania wa Ikwiriri na Mwanarumango ( ambae probability kubwa ni muislamu) ambae ni maskini. Kwani tunaposema hivi, tuna maana kuwa wakristu wote wameendelea na ni matajiri? la hasha, hata huko kuna umaskini na kudumaa wa kutisha. lakini ukweli ni kuwa ni wakristu wengi kuliko waislamu waliopata elimu dunia. Na ndicho hiki tunachojadili.

Amandla.......

Nakubaliana na wewe Mkuu FM.
Tatizo la kufikiri kuwa tatizo la umaskini wa waislamu unatokana na Nyerere ni mawazo duni kabisa na ni ya mtu aliyeishiwa mawazo.
Sehemu ulizo taja nafikiri hawa waungwana hawajafika, na kwa vyovyote vule Tanzania kwao ni ile sehemu wao wanapoishi tu.
Ufinyu wa fikra zao unweza keleweka tu na mtu mwenye kufikiri kama wao tu.
Kama wanafikiri itikadi za sehemu unayotoka haichangii katika maendeleo yako basi hebu nenda Manerumango na Kiasrawe ambako wakoloni walifika muda mrefu sana, wenyeji hapo wamekataa kupokea maendeleo, kosa la nani?
 
Usiishie kulaumu tu , do something about it.
Umasikini upo tena kwa sana tu , na si kwa waislamu tu, mtu wa Kasulu atasema nini?
Umasikini wenu wa mawazo na ubinafsi wa umimi utakuangamiza kimaendeleo.Deep down dhana, nafikiri, ya Mohammed Said kuweka na kupublicise allegations zake dhidi ya Nyerere, mimi nakiona kama kilio cha mtanzania mwingine anayelilia maendelea, jambo ambalo si baya.
Jambo la kusikitisha ni kumtwika Nyerere ukosefu wako wa maendeleo ukijitambulisha kwa kundi moja tu, kama mwislamu.
Matatizo kama haya ya kukosa maendeleo jamii inayoyahitaji kila mahali nchini, nenda sehemu mbali mbali za nchi na utakuta matatizo kama haya.
Tatizo lako Domokaya na wengine ni kujilinganisha maendeleo yako katika misingi ya kidini.Hapo utashindwa, tena vibaya, siyo siri.Na sababu si za kidini bali za kihistoria.Ukae ukielewa hilo.
Matatizo haya yanaweza kutatuliwa from the root.Tujenge shule sehemu hizi zote, tulime na tufanye kazi, hakuna njia ya mkato.

Inawezekana hilo ni tatizo langu, labda. lakini siishii kusema tu hapa ninaposema na prob kuona tatizo ni nini hasa kwa kusema ninachofikiri na kupata mawazo ya watu wengine kama ninyi. Msaada wa mawazo nauhitaji, tena nauhitaji sana. Katika mahaitaji yangu ya mawazo napokea kila wazo lakini nalifurahia zaidi lile linalonikosoa kwa kunionesha ushahidi unaoshikika na si bla bla. Kuna kipindi tunakubaliana kuwa kwa kiasi kikubwa sehemu wanazoishi waislamu wengi ni duni. Tuna prob tatizo lililopelekea hali kuwa hivyo, mtu unatoa jawabu ni ngoma na mila na tamaduni zao. Mwingine hiyo hoja haimuingii akilini anatoa mifano na kusema na hili je? na hawa je? Mtu badala ya kujibu hoja aliyoulizwa anaanza kuyashambulia mawazo yako. Mathalani mimi nafikiri tatizo la ubaguzi wa dini lipo Tanzania na lipo sehemu nyingine za dunia.
Ubaguzi wa kidini unatokana na mfumo mzima wa siasa duniani. Nitatoa mfano. Imani ya dini ya kikristo inasapoti san utekelezaji wa siasa ya ubepari na mambo yake na hii inatokana na jinsi ukristo wenyewe ulivyojijenga tangu enzi za roman empire. Imani ya kiislamu haitoi nafasi kubwa kwa ubepari kutanuka na kufanya makao hii ni kutokana na misingi yake. Dunia kwa sasa inaendeshwa kibepari kwa sehemu kubwa ukiacha zile chache za kisoshalist kule venezuela, Cuba, Korea kaskazini na hata china.Pia katika nchi zinazoendeshwa kwa imani ya kiislamu katika nchi za Iran, Syria, indonesia na nyinginezo. Ukuuaji wa ubepari baada ya kuua ujamaa na kubakiza visiki hapa na pale sasa vita vyake kamili vimeaamia kwa uislamu. Kabla ya hapo hiyo vita ilikuwepo na ilipiganwa chini kwa chini katika mataifa tofauti duniani. Nyerere akawa mmoja wa maaskari wapiganaji wa vita hivyo akitumiwa na mataifa ya magharibi katika vita vya ki-intelligensia. Nyerere alifanikiwa katika vita hivyo kama alivyofanikiwa katika mission nyingine alizozifanya kwa ajili ya waingereza na wamarekani.

Ishu ni kwamba pamoja na vita hii kufichwa na kutaka kuendeshwa chini kwa chini waislamu wa Tanzania wamegundua hilo na sasa wanalisemea kuwa tumekuwa tukigandamizwa na bado tunagandamizwa na mfumo ambao ni binamu yake na ukatoliki. Wanalilalamikia jambo hili kuwa ni baya kwa sababu linaleta tengamano na linajenga chuki kati yetu. Wanaolalamika wanataka hili lifanyiwe kazi.

Tuache kujitetea kwa uwongo kwa kusema eti pia kuna sehemu wanazoishi wakristo kwa wingi hazina maendeleo. Ukisema hivyo basi itaje japo mkoa mmoja wanaoishi waislamu kwa wingi wenye maendeleo. Na pia si vyema kusema uwongo kuhusu mikoa isiyo na maendeleo huku ukiitaja mkoa wa Ruvuma, Manyara na Rukwa. Ukiitaja hiyo mikoa pia taja mikoa ambayo waislamu wako kwa wingi ukiilinganisha nayo. Hoja ya hawa watu eti hawajafika hata mikoa hiyi ni ya kitoto sana na inakufunjia hadhi vibaya mno. Angalau basi ungefahamiana nao watu unaofanya nao mijadala hapa JF.

Tanzania nzima ni masikini lakini bado fursa chache zimeelekezwa sehemu chache kwa kuwapendelea wengine na kwa kuwasahau wengine. Bajeti ya Serikali ya kujenga mashule pia imekuwa ikifanya hivyo,Labda ndio tusema serikali yetu inaendeshwa kwa mfumo wa majimbo?

Katika mkutano uliopita huu mkutano sijui wa nini sijui uliofanyikia hapa Tanzania, pale mlimani city Dr Salim Ahmed Salim aliuliza kuna nini katika mfumo wa demokrasia wa magharibi? mbona nchi nyingi masikini zinazoushabikia na kuubeba zimeendelea kuwa masikini ukilinganisha na nchi zile ziloukataa na kuupindisha. akazitaja nchi kama Malaysia, Korea Kaskazini na Indonesia.

Kabla ya kusema chochote basi angalau tujiulize je ni kweli waislamu wanabagauliwa? Tujuulize haya kwa kuangalia matukio mbalimbali yanayojiri duniani. Je kwa nini Obama anaulizwa sana kama yeye ni muislamu au la, je kuna rais mwingine yeyiote wa Marekani aliwahi kuongelewa sana imani yake kam ilivyo kwa Obama?
Tujiulize pia kuna vita vingapi na vurugu ngapi duniani katika maeneo yenye uislamu mkali. Hivyo viya na hizo vurugu zinatokana na nini? Je zinatokana na mafundisho ya dini ya kiislamu? Uchochezi au kitu gani hasa?

Tujiulize zaidi dunia yetu tunayoishi iko fair? haina unyonyaji wala ubaguzi? kama unyonyaji upo ni nani hasa anayenyonywa? na kama ubaguzi upo na makundi gani hasa yanabaguliwa? kwa nini katika kombe la dunia Waafrika kwa kiasi kikubwa hushangilia timu zao zikiwa zinatoka moja baada ya nyingine mpaka majority hubaki na timu ya mwisho ya kiafrika inayobaki mashindanoni lakina huwezi kumkuta Mwingereza akiishangila Ujerumani hata kama ikiwa timu pekee ya ulaya iliyobaki dimbani.

Tufikiri, tusiwe misikule katiak kutafakari
 
Nakubaliana na wewe Mkuu FM.
Tatizo la kufikiri kuwa tatizo la umaskini wa waislamu unatokana na Nyerere ni mawazo duni kabisa na ni ya mtu aliyeishiwa mawazo.
Sehemu ulizo taja nafikiri hawa waungwana hawajafika, na kwa vyovyote vule Tanzania kwao ni ile sehemu wao wanapoishi tu.
Ufinyu wa fikra zao unweza keleweka tu na mtu mwenye kufikiri kama wao tu.
Kama wanafikiri itikadi za sehemu unayotoka haichangii katika maendeleo yako basi hebu nenda Manerumango na Kiasrawe ambako wakoloni walifika muda mrefu sana, wenyeji hapo wamekataa kupokea maendeleo, kosa la nani?

Katika kituko cha mwaka ni hiki cha kusema eti wakazi wa manerumango wamekataa kupokea maendeleo. hivi mkoloni alikuwa na muda wa mjadala unapokea nini au hupokei? ukiona wakoloni wameshindwa sehemu jua resistance ya watu wa huko ilikuwa kali. Kwa falsafa yako naona unasema bora kutawaliwa maendeleo yatakuja, shaurin zao waislamu (Uislamu ulikuwa wa kwanza kuingia kabala ya missionaries) ambao imani yao ilimdhibiti mkoloni hivyo hawakupata maendeleo. majimaji ilipiganwa ili watu waistawaliwe na hilo limekuwa suala la kujivunia sana mpaka leo hii. Sasa wewe unasema mkoloni alikuwa bomba tu na ni koloni pekee wa kuleta maendeleo. Duh Nimechoka. Akina Marcus Garvey na Dubois waliyaacha mataa na barabara za lami na majengo marefu ya New York kurudi Afrika kuja kusitiri utu wake, wewe leo unasema hayo? Kweli mwache mtu anene umtambue yukoje
 
Sasa Mkuu hueleweki!
Wewe mwenyewe hujiwezi,mkoloni kaja ameshindwa kukuendeleza. Nyerere naye kajaribu kichwani kwako hazipandi.
Sasa walalama nini?,ridhika basi hivyo ulivyo Inshallah
 
Wandugu, kwenye hili la maendeleo na shule za misheni, tunamlaumu Nyerere bure tuu, wazungu wa kwanza kuja barani Afrika walikuwa makundi matatu, wagunduzi, wapelelezi na wamishenari. Hawa walikuja karne ya 17 wakati Waarabu na Uislamu wao walikuja barani Afrika tangu karne ya 14.

Misheni ya kwanza kujengwa Afrika Mashariki ni Bagamoyo, then Zanzibar ndipo wakaja Dar. Waarabu na Uislamu wao, wao waliangalia biashara tuu yaani Trade, kujenga misikiti na madrasa zake. Wamishenari wao waliangalia investment potential areas ndipo wakajenga misheni kubwa kubwa, hali iliyopelekea maeneo yenye mazao ya biashara Kahawa, Chai, Pamba na Katani, kupata support kubwa ya misheni sio tuu kueneza dini, bali kutoa elimu dunia, hali iliyopelekea ndugu zetu wa Kilimanjaro na Kagera kupata dini na kupelekwa shule na pesa za kahawa, what had Nyerere got to do with this?!.

Mpaka leo ukiangalia baadhi ya makanisa makubwa, yako kwe the top prime area ya maeneo mengi ili hali Misikiti imejikita zaidi Uswazi, that was not a mare chance but long time vision.

Chelewa ufike, wenzetu Waislamu, Chuo Kikuu hicho hapo Moro, madrasa tujenge lakini na shule pia sasa ndio ndio hizo zipo. Enzi zile shule za sekondari zikiwa chache, mkoani Dar, Shule ya Sekondari ya Kinondoni ndio iliyokuwa ikiongoza kwa kuzungusha (Div=0) lakini bado makuwadi wa kilio cha kubaguliwa, wakiendelea kulia kuwa wanabaguliwa, kusoma msome wote, mwenzako apate Div=1, wewe upate Div=0 alafu unalalama unabaguliwa!.

Issue sio dini, issue ni visions, planing na strategy ya kufikia malengo. Nadhani nchi za emerging markets, Tiger nations zote ni za Kiislamu and have made it, hinyo tuache kuuhusisha uduni wa Waislamu na dini yao, dini kama dini, has nothing to do na uduni au ubora wa maisha, ila dini kama biashara, has got something to do, wenzetu walihubiri dini tuu kutafuta ahera ya milele, wenzao wakahubiri dini, huku wakijenga uwezo wa kiuchumi na matokeo ndio hii imbalance inayosababisha Nyerere kutaka kubebeshwa msalaba.

Nasubiria kusoma hicho kitabu!.
 
Nonsense!, Naamini hujawasoma hao unaowataja na hujasoma historia iliyoandikwa na Mohammed Said.
Wanaomfahamu Nyerere ni wale aliowataja Mohammed ambao ndio waliomkaribisha kwenye siasa na kumlipia chakula na usafiri,halafu akalipa shukrani za punda kwa kuwapiga mateke.Nguo za Nyerere wakati wa mwanzo wa harakati za uhuru zilikuwa zikifuliwa na mama wa mmoja wa wanaharakati huo.
Hivyo Mohammed sio aliyemjua zaidi Nyerere.Waliomjuwa ni wengi ambao yeye alihojiana nao.Historia ipi inapaswa kuitwa historia sahihi ukiondoa hii.
I may be nonsense lakini ninachosema ni kwamba Mohammed Said hana monopoly ya ukweli kuhusu historia yetu. Kitabu chake juu ya maisha ya marehemu Mzee Walid Kleist nimekisoma kwa sababu nilimfahamu huyo mzee. Lakini ukikisoma hakielezei biography ya mzee Kleist bali malalamiko jinsi Nyerere alivyowapora Waislamu usukani wa uongozi wa nchi. Wewe unaweza kumkubali Mohammed kama sole source yako ya historia ya Tanganyika, ni hiari yako.
 
Sasa Mkuu hueleweki!
Wewe mwenyewe hujiwezi,mkoloni kaja ameshindwa kukuendeleza. Nyerere naye kajaribu kichwani kwako hazipandi.
Sasa walalama nini?,ridhika basi hivyo ulivyo Inshallah

Kama nilivyosema awali nena watu wakujue jinsi unavyofikiri. Hapa ni sehemu ya mjadala halafu wewe washindwa kujibu hoja. Hapa ulitakiwa ukubali au ukatae kwa ushahidi kama una mental slave au la. Sasa sijui umesusa au umekasirika sijui. Onesha hoja zangu zinavyojichanganya. Sema hapa umesema hivi na pale umesema hivi. Inawezekana kabisa complex thoughts zisieleweke na simple minds, kama wewe uko huko sijui lakini hebu tuambie basi unamfurahia nani kati ya hawa wawili, aliyempinga mkoloni akakosa maendeleo na aliyemkubali mkoloni akapata maendeleo?

Usisuse ndugu matatizo ya nchi hii ni mengi na kila mtu ana ya present anayoyafahamu yeye na mwisho wa siku tunaweza tukapata hesabu kubwa ya matatizo yetu tukakaa kujipanga tuyafanyie kazi yepi. Kama wewe umekuja na wazo kuwa tungemkubali mkolono tungeweza kuendelea zaidi. Kutokana na mawazo hayo tunaweza tukaamua tumkabidhi tena nchi hii ili atuletee maendeleo ambayo sisi tumeshindwa kuyapata miaka takribani hamsini baada ya uhuru na tumebaki kujivunia kile alichotuletea mkoloni. Au ndugu yangu Lole Gwakisa unasemaje? Sema tukusikie bwana usisuse si vizuri hivyo
 
Mohammed Said,
Haiingii akilini kwamba Nyerere hakutaka Waislamu wapate elimu. Kama ingelikuwa hivyo basi hakuwa na sababu ya kutaifisha shule za misheni ili Watanzania wote wasome bila kujali dini zao. Nyerere angeweza kuendeleza mfumo wa ukoloni na ku "turn a blind eye" to Muslims, kama kweli hakupenda Waislamu wapate elimu. Hapo ndipo tunapotofautiana. Kitabu chako nimekisoma chote. Sivalon nimemsoma pia lakini nyote hamjibu ni kwa nini Nyerere alitaifisha shule za misheni. Ukiondoa udini wako una nafasi nzuri sana ya kuwa mwanahistoria mahiri. Vision ya Nyerere ilikuwa ni kuunda taifa moja la Watanganyika wasiojali ukabila wao na dini zao na kwa kiasi kikubwa alifanikiwa. Leo anaweza kutokea Mchagga akafanya utafiti kama ulioufanya na akijikita zaidi katika Uchagga wake akaandika Nyerere aliwabagua Wachagga kwa sababu alikuta wameendelea akawavunjia vyama vyao vya ushirika. Vivyo hivyo kwa Wahaya, Wasukuma, Wajita, n.k. Lengo la Mwalimu lilikuwa ni kuunda taifa moja lenye mshikamano bila kujali dini au makabila ya watu. Na haikuwa kazi ndogo kwa kanchi kenye makabila zaidi ya 120.
 
Sisusi ila sikuzoea kutoleana fedhuli hiyo si silka katika makuzi yangu. Kawaida yangu ninapoona lugha zinakuwa si za kiungwana basi mie hujiweka pembeni na kusema salama.

Ama hilo la kusema kuna kubwa kuliko kuandika kitabu kikachapwa na kikawa kitabu cha rejea katika vyuo vikuu duniani?

Au kuna kubwa kuzidi ya kualikwa katika midahalo ya kimataifa na kuzungumza kuhusu Uislam na Siasa katika Tanzania?

Au kuna kubwa kuliko kuwa mmoja kati ya waandishi wa Afrika wanaoandika Dictionary of African Biographies?

Au kuna mafanikio katika kuandika kuliko kitabu chako kikatiwa ndani ya Cambridge Journal of African History na kikatiwa katika catalogue ya Library of Congress, Washington?

Nimeingia JF kwa kuwa niliamini hii ni "forum ya great thinkers" na napenda nitoke humu nikiamini hivyo.
 
Wandugu, kwenye hili la maendeleo na shule za misheni, tunamlaumu Nyerere bure tuu, wazungu wa kwanza kuja barani Afrika walikuwa makundi matatu, wagunduzi, wapelelezi na wamishenari. Hawa walikuja karne ya 17 wakati Waarabu na Uislamu wao walikuja barani Afrika tangu karne ya 14.

Misheni ya kwanza kujengwa Afrika Mashariki ni Bagamoyo, then Zanzibar ndipo wakaja Dar. Waarabu na Uislamu wao, wao waliangalia biashara tuu yaani Trade, kujenga misikiti na madrasa zake. Wamishenari wao waliangalia investment potential areas ndipo wakajenga misheni kubwa kubwa, hali iliyopelekea maeneo yenye mazao ya biashara Kahawa, Chai, Pamba na Katani, kupata support kubwa ya misheni sio tuu kueneza dini, bali kutoa elimu dunia, hali iliyopelekea ndugu zetu wa Kilimanjaro na Kagera kupata dini na kupelekwa shule na pesa za kahawa, what had Nyerere got to do with this?!.

Mpaka leo ukiangalia baadhi ya makanisa makubwa, yako kwe the top prime area ya maeneo mengi ili hali Misikiti imejikita zaidi Uswazi, that was not a mare chance but long time vision.

Chelewa ufike, wenzetu Waislamu, Chuo Kikuu hicho hapo Moro, madrasa tujenge lakini na shule pia sasa ndio ndio hizo zipo. Enzi zile shule za sekondari zikiwa chache, mkoani Dar, Shule ya Sekondari ya Kinondoni ndio iliyokuwa ikiongoza kwa kuzungusha (Div=0) lakini bado makuwadi wa kilio cha kubaguliwa, wakiendelea kulia kuwa wanabaguliwa, kusoma msome wote, mwenzako apate Div=1, wewe upate Div=0 alafu unalalama unabaguliwa!.

Issue sio dini, issue ni visions, planing na strategy ya kufikia malengo. Nadhani nchi za emerging markets, Tiger nations zote ni za Kiislamu and have made it, hinyo tuache kuuhusisha uduni wa Waislamu na dini yao, dini kama dini, has nothing to do na uduni au ubora wa maisha, ila dini kama biashara, has got something to do, wenzetu walihubiri dini tuu kutafuta ahera ya milele, wenzao wakahubiri dini, huku wakijenga uwezo wa kiuchumi na matokeo ndio hii imbalance inayosababisha Nyerere kutaka kubebeshwa msalaba.

Nasubiria kusoma hicho kitabu!.

Sina hakika kama ndugu yangu Pasco umekuwa ukifuatilia mjadala huu tangu mwanzo. Kuhusu suala la shule za waislamu kuwepo zilikuwepo, kama utakuwa unajuaa taasisi ya Aga Khan na shule zake na hospital zake utajua ni lini waislamu walikuwa na mwamko amboa leo wewe unadai hawakuwa nao. Waislamu wanasema si tu wanabaguliwa waligandamizwa kwa siasa chafu za kuwapandikiza watu wenye njaa zao kujinadi kuwa viongozi wa waislamu ili kuvunja nguvu za waislamu zilizoibuka kwa nguvu kipindi kicho ikiwa na lengo na nia na matayarisho ya kujenga chuo kikuu cha waislamu hata kabla ya UDSM. Nguvu hizo zilifishwa na watu waliofahamu nguvu za waislamu amba walikuwa madarakani kwa wakati huo. Waislamu wana nguvu na wana uwezo mpaka hii leo ili jitihada zao zimekuwa zikigandamizwa mara kwa mara. Ngoja nikwambie kitu je unajua ni akina nani wanaweza kuwa kati ya walipa kodi kubwa wazuri katika nchi hii?
 
Pasco,
Ndio maana katika mojawapo ya mabandiko yangu huko nyuma nimeuliza tufanye nini hivi sasa, karibia miaka 50 tangu tupate uhuru, ili tuweze kuwasaidia ndugu zetu Waislamu? Nyerere kishatangulia mbele ya haki, na Domokaya, kuendelea kulalamikia kanisa Katoliki kama ni adui haileti tija. Wenzenu wanaendelea kusonga mbele. What needs to be done, here and now, to rectify the situation? Sijapata jibu. I am more interested in solutions for tomorrow than complaints from yesterday.
 
Waleikum Salaam Pasco,

Ahsante kwa mchango wako.

Ukishanyanyua kalamu kuandika basi usiogope criticism wala usiwafanyie uadui critics kwani huo ndiyo khasa usomi. Kuwa mengi nimeyajua kwa kuwa niliishi kipindi kile na wazazi wangu walikuwa kati ya wanachama wa mwanzo wa harakati za TANU hili kwangu ni jambo la kujivunia sana na ndiyo silaha yangu kubwa.Ni silaha yangu kwa kuwa kuna baadhi ya wenzetu Mungu hakuwajaalia kuwa na historia yoyote ambayo wanaweza wakaihadithia.

Umemtaja marehemu Rashid Kheri Baghdelleh yeye alikuwa rafiki ya baba yangu na akija hadi kwetu. Alhamdulilah. Mungu awarehemu hawa wazee kwani wote wametangulia mbele ya haki.

Narudi katika mchango wako. Insha Allah ukisoma kitabu utaona hayo ulosema wewe katika mchango wako mie nilikutangulia kueleza. Wafadhili wa TANU walikuwa John Rupia, Dossa Aziz, Abdulwahid na Ally Sykes, Mwinjuma Mwinyikambi na Mshume Kiyate. Hawa ndiyo waliokuwa watoa fedha wakubwa.

Hivi unajua Kitwana Kondo akiwa Meya wa Dar es Salaam alimpa Mzee Mshume mtaa kwa ajili ya mchango wake katika kuikomboa Tanganyika lakini hadi leo wahusika wamekataa kubadilisha kile kibao cha mtaa alokuwa akikaa?

Kitabu kinapatikana Ibh Hazim Bookshop Mtoro Mosque lakini hiki ni tafasiri ya Kiswahili.
 
Pasco ahsante kwa msimamo huo wako. Tatizo ni kuwa serikali yetu haina ujasiri wa kukabiliana na yale ambayo mimi nimeyaeleza katika kitabu changu na Prof. Njozi akaeleza katika Mwembechai Killings.
 
Ukiacha kujadiliana nami kamwe hamna tatizo. Hapa halizimishwi mtu.

Haiwezekani kuwa kila ukiulizwa swali unasema tusome kitabu chako bila kutuambia wapi katika hicho kitabu majibu yatapatikana. Hii kwangu mimi haiingii akilini. Wewe umeandika kitabu, basi tumia yale uliyoyaandika kujibu hoja. Kwa kuacha kufanya hivyo kunapunguza uzito wa hoja zako. Adabu ya majadiliano ni kumheshimu mwenzio kwa kujibu maswali yake na si kukwepa kwa kisingizio kuwa majibu yamo kwenye kitabu ambacho hakipo mbele yetu na wala hautaki kukitumia kujenga hoja yako. Na vile vile heshima ya mjadala inasema kuendelea kutumia jina ambalo mhusika ameishasema sio lake ni dalili ya kutomheshimu. Badala ya kukimbilia hamaki, tuthibitishe authorship yako kwa kutuambia ni wapi katika hicho kitabu chako tutapata majibu sio kutupa blanket answers. Hii haikubaliki na wewe unajua.

Amandla.........

Wewe Fundi unashangaza sana!.Huyu bwana kafanya utafiti na kusafiri maeneo mbali mbali kujenga hoja zake mpaka akaridhika nazo na kuziweka kwenye uandishi.

Leo umemshika atumie maandishi yake kukushawishi wewe hapa kwa yale aliyoyaandika, na bado unakaidi ushauri wa kusoma vitabu vyake.Hivi wewe hujui kuwa baadhi ya fikra haziingii akilini papo kwa papo,unahitaji kulala nazo na kujiuliza ndipo uzikubali.Hivyo umuhimu wa wewe kusoma maandishi ya Muhammed Said upo badala kumshinikiza akujibu kila kitu hapa jukwaani.
Wewe na wenzako ndio ambao muna jukumu la kuandika vya kwenu kupinga yale aliyoaandika na watu watapima.Ikiwa hamuwezi hakuna mantiki kupinga.
Iwapo mutakachoandika ni porojo na fitina tu wasomaji wanaweza wakavichoma moto kama walivyofanya kwa uongo wa waziri fulani kule Zanzibar.
 
Pasco,
Ndio maana katika mojawapo ya mabandiko yangu huko nyuma nimeuliza tufanye nini hivi sasa, karibia miaka 50 tangu tupate uhuru, ili tuweze kuwasaidia ndugu zetu Waislamu? Nyerere kishatangulia mbele ya haki, na Domokaya, kuendelea kulalamikia kanisa Katoliki kama ni adui haileti tija. Wenzenu wanaendelea kusonga mbele. What needs to be done, here and now, to rectify the situation? Sijapata jibu. I am more interested in solutions for tomorrow than complaints from yesterday.
Kwani wewe Jasusi unazungumza kama nani serikalini?.Haya YA yapi ya kufanywa yametajwa zamani na hakuna aliyejali huko serikalini.Wako waliojaribu kuonesha mfano ikawa hadithi.Unamkumbuka profesa Kighoma Ali Malima?.Mengine ni kama yale yaliyoanzishwa na waasisi wenyewe wa TANU.
 
Ndugu yangu mimi nazungumza kama Mtanzania wa kawaida tu ambaye anajali mustakabali wa nchi yetu. Si lazima niwe serikalini. Nimesema usinirudishe nyuma. Taja sasa hivi 2010 tufanyeje sisi kama Watanzania ili tuweze kusonga mbele sote pamoja kwa mshikamano na amani.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom