Ukweli kuhusu waasisi wa TANU na harakati za kupigania uhuru

Ukweli kuhusu waasisi wa TANU na harakati za kupigania uhuru

Status
Not open for further replies.
Gole Gwasika,
Mkuu hapa ndipo nisipokuwbaliana na wewe na watu kama wewe ndio Mohamed Said anawafananisha na Nyerere - Utanisamehe pia.

Ni lazima kwanza usome habari kisha fanya utafiti kujua kilichotokea na sio ku copy na ku paste hali hujui historia ya nchi. Kupingana na TANU wakati wowote au chama chochote haina maana unatokana na ubishi wa Waislaam bali ndio demokrasia ya kweli mtu kuchagua viongozi wako, kukubaliana na malengo ya chama na hata kuweza kuweka Upinzani kwani hakuna binadamu aliye kamili.
Sasa kama wewe unaamini wapo Miungu Watu ambao wanatakiwa kufuatwa tu kama sisi ni kondoo, hii haiwezi kuwa hoja kwa waumini wengine ambao wanaamini hakuna tena kondoo ila sote ni Umma mmoja.

Na Imani yako wewe haiwezi kuwa sifa kwa waumini wengine, la muhimu kwako amini unachoamini wewe kwa tafsiri yako na kaa pembeni kunywa maji ukisikia kiu. Hii habari ya WAO hivi na SISI ni hivi kisha unadai watu kupendana ndio Unafiki huu mkuu wangu. Na hakuna msikiti ambao Muislaam anakatazwa kuingia - HAKUNA kitu hiyo..samahani tena.


Haswaa Mkuu Mkandara, dhamira yangu ya kurebute maandishi ya muheshimiwa Mohammed Said si kuwa anaandika mambo ambayo hayakuwapo, la hasha yalikuwapo.Lakini pamoja na aliyoandika yalikuwepo mengine asiyopenda kuyaelezea.Yeye anatoa conclusion kutokana na msimao wake wa udini na yale aliyohadithiwa na kusikia na kuwauliza wengine wa dini yake.

Na ndio maana ya kusoma , kuna maandishi mengi tu ya kuonyesha kuwa kile anachokidhamiria ni potofu na pamoja na maandishi yake , yapo mengi tu ya kumpinga.
Na mimi sikuanza na kuongea u MIMI, lakini muheshimiwa huyu ndo kaadika kitabu cha WAO, kitu ambacho ni msingi mkubwa wa ubaguzi Tanzaia ya leo.
Kama kuna WAO basi kuna SISI, hilo halijipingi.
Katika moja ya sheria za fizikia kuna ambayo isemayo , nairudia FOR EVERY ACTION THERE IS AN EQEAL AND OPPOSITE REACTION.
Hatuishi kwenye ombwe.
Mkuu Mkandara mimi naheshimu sana msimamo wako wa kuwa pro-active ,liberal na ambao ni endelevu na hauko subjective.
Sasa katika post no2 tu mchangiaji mmoja kapost:

History should be used to build a better future!!!!! but Sheikh Mohamed Said's motive is to destroy the national unit(y).

Mwalimu hakuwa malaika na alifanya makosa mengi tu tena ya kibinadamu, lakini leo waTanzania hatuchinjani wala kubaguana, and this his major acheivement.

Simpingi Ndugu Mohammed Said kwa sababu ni muislamu , hapana , nampinga kwa sababu ya kuanzisha dhana ya kutazama kila kitu katika miwani yake ya udini na jinsi walivoonewa na wakristo.
Naleta hizi postings vile vile kurefresh your view of the other side.
Narudia tena , kueleza matatizo kila mtu anaweza lakini si mtoa mada wala wanao msaidia katika udini wanao toa solution kwa matatizo yalipyopo.
Mwezi mmoja baada ya mjadala kuanza na hii ni post ya 443 hakuna fununu ya jibu wala uelekeo.
Lazima vile vile tujue kiini cha mjadala wenyewe, kiini kinachotokana na mihadhara ya Mohammed Said kwa vijana wadogo ambao hawakuwapo wakati wa ukoloni.
Wrong conclusions zikirudiwa rudiwa , kijana wa leo anaweza kufikiri ndio ukweli.
Worse still,udini unapochukua umuhimu zaidi katika mambo yote ya kijamii basi hatuna Taifa moja, na huo ndio UMIMI na WAO on a national scale.
Sasa ni juu ya mtoa mada ambaye ni responsible awabebe watanzania wote au awabwage kwa yale anyoyatumikia.
 
Mzozaji: Ahsante sana na nakushukuru sana kwa kuhoji mambo ya msingi kabisa katika utafiti kama ulivyoita wewe mwenyewe "documentation." Nimekuelewa. Rejea zipo nyingi na nimezipitia na kuzionyesha katika kitabu changu. Ukisoma kitabu hizo nyaraka utaziona humo pamoja na vitabu nilivyorejea. Tafadhali soma kipande hiki kutoka katika kitabu na Insha Allah utapata mwanga:

Kazi hii isingewezekana kama isingekuwa kwa msaada wa hali na mali nilioupata toka kwa Ally Sykes. Ally Sykes alinipa wasaa wa kuzungumzanae kila nilipotaka, akanieleza madhila ya ukoloni pamoja na kuwa ni mtu wa shughuli nyingi. Yeye hivi sasa anaendesha biashara yake toka ofisi yake iliyoko katikakati ya mji wa Dar es Salaam. Aliniruhusu nisome majalada yake binafsi, barua zake, shajara na kumbukumbu nyinginezo za ukoo wa Sykes. Ally Sykes alinifahamisha kuwa kumbukumbu hizi zilikuwa ndani ya sefu ambayo haikupatwa kufunguliwa kwa zaidi ya miaka thelathini. Nikiyapitia majalada yake nilishangazwa na utaratibu wa Ally Sykes wa kupanga kila kitu na kila kipande cha habari mahali pake hata kingekuwa kidogo namna gani wakati ule wa harakati. Ally Sykes ana barua ya mwaka 1954 iliyoandikwa kwa penseli toka kwa Zuberi Mtemvu kwenda kwake akimtaarifu juu ya mazungumzo aliyokuwanayo (Mtemvu) na Nyerere kuhusu yeye na TANU; stakabadhi ya hundi ya posta toka kwa Ally Sykes kwenda kwa Japhet Kirilo wakati wa Mgogoro wa Ardhi ya Wameru; nakala ya barua isiyokuwa na tarehe kutoka TAA kwenda kwa Malkia Elizabeth iliyotiwa saini na viongozi wote wa TAA: Rais Julius Nyerere, Makamu wa Rais Abdulwahid Sykes, Katibu Mkuu Dome Okochi, Naibu Katibu Dossa Aziz, Mweka Hazina John Rupia, Naibu Mweka Hazina Ally Sykes ikimpongeza Malkia kwa kutawazwa; barua ya mwaka 1952 toka kwa Rashid Mfaume Kawawa kutoka Bukoba kwenda kwa Ally Sykes ikimfahamisha juu ya hali ya siasa katika Kanda ya Ziwa; barua ya mwaka 1963 toka kwa Lady Judith Listowel, Kenneth Kaunda, Julius Nyerere, Kasela Bantu, Chifu Thomas Marealle ...orodha haina mwisho. Baadaye nilipofanya utafiti kuhusu maisha ya baba yake, Kleist Sykes, nilikuja kufahamu kwamba tabia hii ilirithiwa kutoka kwa baba yake ambae alikuwa akiweka ndani ya jalada kila kipande cha karatasi kilichokuwa na habari iliyostahili kukumbukwa. Ni jambo la kuhuzunisha kwamba sikuweza kupewa shajara za Abdulwahid ambazo nilielezwa kwamba baadhi ziko katika hati-mkato na hadi leo hazijafasiriwa. Shajara hizi nimezioana kwa macho yangu lakini kwa kukosa idhini sikuweza kuzifungua na kuzisoma. Vilevile sikuweza kupata kumbukumbu halisi za Vita Kuu ya Kwanza zilizoandikwa na Kleist Sykes kwa mkono wake mwenyewe. Hapana shaka yoyote kwamba nyaraka hizi ni hazina zenye thamani isiyo na mfano wake. Ni matumaini yangu kwamba siku moja nchi yetu itakubali na kuthamini mchango wa Abdulwahid katika taifa la Tanzania na nyaraka hizi kama kielelezo cha harakati dhidi ya ukoloni, zitakubalika na zitawekwa chini ya hifadhi ya Nyaraka za Taifa kwa faida ya vizazi vijavyo.
 
LG: Ahsante kwa kutuwekea mada ya Dr Mhina lakini sidhani kama paper hiyo inaweza kujibu kitabu changu. Hujamtendea haki kabisa Dr Mhina. Kitabu hujibiwa na kitabu siyo na mada. Niliposoma "Historia ya TANU 1954 -1977" kilichondikwa na jopo la waandishi wa CCM ndipo nami nikaamua kuandika kitabu kueleza upande wetu wa historia ya TANU. Laiti ningeandika mada hakuna mtu yeyote ambae angelijali. Leo tunajadili kwa kuwa kitabu changu kimeibua mambo mengi ambayo hayakuwa hadhir kabla ya hapo. Kama ni paper ninazo nyingi nilizoandika kuhusu somo hili "Uislam na Siasa Katika Tanganyika" wala sikumbuki hesabu yake. Zipo nilizotoa humu humu nchini na zipo nilizotoa nje ya nchi wachilia mbali makala katika magazeti ya humu nchini na nje ya nchi. Mimi sifanyi mjadala kwa kutaka ugomvi wala sithubutu kufanya hivyo. Nia na madhumuni yangu khasa ni kuihifadhi historia ya kweli ya kupigania uhuru wa Tanganyika. Hii nimechukua kama wajibu wangu na njia pekee ya kuwaenzi wazee wangu. Kuziweka kumbukumbu zao hai kwa ajili ya kizazi kijacho.
 
Mohamed Said,
Mkuu wangu hata sielewi unachotarajia kupata hapa. labda nikujibu wewe kwa kila hoja unayoanzisha ili tupate kuwa mstari mmoja maanake kila nayoandika toka nimeingia hapa hujanijibu hata moja isipokuwa kuchagua yale yaliyokuwa mepesi kwao kuyajibu.

Sasa ikiwa kweli Kleist anayo diary ya Baba yake ambayo amekataa kuitoa kwa mtu yeyote kiasi kwamba imebakia kuwa - INASEMEKANA, huoni kama yote uyasemayo ni udhanifu wa hoja yako mwenyewe kwani Kleist hajakwambia kilcihoandikwa!. Pili kama Kleist kafikia kukataa ku transcribe hizo nyaraka wala kufanyiwa Utafiti imekuwaje wewe upate habari kuwa zina mikutano ya siri ktk juhudi zake za kuanzisha TANU hali chama hicho kilianzishwa mwaka 1954 wakati Kenyatta akiwa jela toka mwaka 1952 na akatumika kifungo cha miaka saba 'til 1959. Ni wakati gani unapowaweka Abdul Wahid na Kenyatta meza moja na kwa maswala yapi muhimu kwetu?

Na kibaya zaidi ni kwamba umeshindwa kutuambia ni kitu gani walichokuwa wakijadiliana baina ya Abdul Wahid na Kenyatta hadi iwe siri kubwa na ya ukoo wa Skyes hali tunazungumzia nyaraka za chama na sii za maisha ya AbdulWahid na siri zake ambazo aliziweka ktk diary zisiwe mali ya Taifa ila yake binafsi.

Mkuu wangu nachojaribu kukuambia hapa ni kwamba yaliyokwisha tokea yametokea, unataka kuandika Historia ya Tanzania andika kama ni historia ya Tanzania lakini haya ya mchango wa Waislaam hali kila mtu anajua fika kwamba wapo wananchi wenye imani ya kiislaam walichangia sana Uhuru wetu ni kutaka kuonyesha tofauti baina ya dini hizi mbili. Ndio matatizo yanayowapata Kenya ambako Kenyatta amesifiwa sana hali wapo waasisi wa chama hicho kina Joseph Kang'ethe ambaye nina hakika Wakenya wengi hawamjui.

Na haikuwa swala la Ukabila isipokuwa Kenyatta ambaye muda mwingi wa harakati za Uhuru alikuwa jela ndiye akaja lamba dume na huyo tukamwona akiushamirisha Ukabila Kenya bila kificho. Sifa zote kapewa Kenyatta, na hata ukienda Zambia kwa Kaunda, South Africa kwa Mandela yaani kote historia ya nchi hizi imeandikwa na mwaandishi wetu waliochukua tu yale waliyoyaona mazuri kwao na kuyaandika wengine wakifikiria uandishi ni fedha hivyo waliweka chunvi za uuzaji.

Kasome historia ya Marekani, Canada au Uingereza kote utakuta wapo watu wengi sana wameachwa na sii kwa sababu ya dini. jinsia au rangi zao isipokuwa pengine michango yao haikuwa interest ya mwandishi ambaye somo kubwa kwake lilikuwa mhusika fulani na harakati za Uhuru wa nchi hiyo. Na kwa ujumla wa nchi ziku zote huwa haikusanyi kila mtu hata kidogo zaidi ya Utaifa wa wahusika ndani chombo chao kimoja yaani Chama. Hivyo ni historia ya chama ndiyo huvuta majina ya wahusika ktk kila tendo walofanya kukijenga chama au harakati zenyewe.

Nakuhakikishia kwamba hakuna mtu hapa JF wala Tanzania ambaye anasema Kina Sykes hawakuwa na mchango mkubwa ktk Uhuru wetu..Hawa watakuwa wendawazimu lakini haitokani na Uislaam wao ndio ulowasukuma kuunda chama kuutafuta Uhuru wa nchi yetu isipokuwa ni Uzalendo wao kwa nchi hii. Yawezekana pia wao walikuwa na mwamko wa harakati za Uhuru kabla ya Watanzania wengi kwani ukitazama list kubwa ya viongozi wa chama TANU waliokuwa juu ni wahamiaji zaidi ya makabila ya wazawa. Sasa hatuwezi kusema au kuandika Historia ya Tanzania kwa kuanza na mchango wa wahamiaji ktk Uhuru wa Tanzania iwe ndio historia inayokubalika hali wapo wazawa wengi tu pia walishiriki ktk kuundwa kwa harakati hizo.

We all played our part, dini makabila na hata race tofauti zilishiriki kwa njia moja ama nyingine na kwa vile sifa za ushindi wa Vita humfuata Jenerali sioni ubaya wowote Nyerere akibebeshwa joho la Baba wa Taifa kwa sababu tu askari wengi walikuwa mstari wa mbele wakipigana vita hiyo. Ila kama kweli wataka kuandika Biography ya AbdulWakil nadhani watu uliowafuata walikuwa tosha kabisa ya kukupa hadithi za maisha yake hata pasipo kuzipata zile nyaraka za siri. Unapozungumzia mchango wa Waislaam ktk Uhuru wa Tanzania ni kuanzisha tabaka za kimtazamo ktk harakati hizo kama wanavyodai Wakikuyu huko Kenya au kesho Wazuru waanzishe vagi la kusema ni wao waliokuwa wameanza harakati za Uhuru kabla ya kina Mandela na kabila la Nkosa..Na hapo ndipo vurugu itakapo anzia.

Ni muhimu sana kwako kuelewa kwamba leo hii tuna matatizo chungu nzima, iwe Waislaam au Watanzania na hakika utakuwa umewasaidia sana Watanzania kama utaweza kuandika habari zinazohusiana na dhulma inayofanyika leo hii. Na kama ni historia ni vizuri sana ukiandika watu wote wenye mchango mkubwa ktk harakati hizo badala ya kutumia majina yao na dini zao kama ndio mchango.

Kwa mfano Ukimzungumzia Mwapachu andika mchango wake, John Rupia, Dosa, Thomas Plantan na Kyaruzi ambao pia walikuwa muhimu sana sijawasoma wakiandikwa michango yao hali aalikuwa watu muhimu sana ndani ya chama. Ila kila naposoma ni jinsi gani hawa watu walimwezesha Nyerere kufikia pale alipofikia. It's all about Adaku, yaani kama vile mtu anakupa fadhila kisha inakuwa hadithi dunia nzima wajue umemsaidia vipi. Kama sii mimi huyu mtu asingekuwa chochote!...

Aaaah mkuu wangu huu Uislaam kweli au ni unafiki mtupu usiofaa ndani ya Uislaam. Ati Nyerere alimsahau Sharrif Attas ndio kimlize Kleist kana kwamba watu hawa sahauliani..Mimi kila naporudi Nyumbani hukutana na watu niliwasahau na wao hunikumbusha na isiwe jambo la kutoka machozi wala sababu kubwa ya kushangaa hata kama tulikuwa pamoja miaka ya nyuma. Sasa unapoona watu kama Kleist wanapoitazama DVD yako na kulia machozi kisha ukashindwa kutueleza kilichomliza hapo ndipo tunaposhindwa kuchukua mahitimisho yako. Nasema hivi kwa sababu hata mimi husimuliwa mambo ya marehemu baba yangu na hutokwa na machozi aidha kwa furaha ya kile alichoweza ku accomplish ama pasipo sababu maadam anayezungumziwa ni mzazi wangu..

Mkuu nimemaliza na sijui kama umeweza kuona upande wetu tunaitazama picha hii vipi kama wasomaji. Na hakuna kitu kibaya kwa mwandishi yeyote ambaye anataka kubishana na customers wake akifikiria yeye anajua zaidi yao. Sisi ndio wanunuzi na wapenzi wa historia ya nchi yetu na tuna haki ya kukwambia makosa yako kama mwandishi. Ukiweza kuwasikiliza wateja na ukaweza kuandika Historia ya Tanzania ikiwa na Mtazamo wa Uzalendo kwa nchi yetu utapata sifa na mauzo bora zaidi ya kutumia dini za wahusika kwa sababu HAIHUSU!.

Bob Mkuu..............Heshima mbele......duuhh kama mtu anasoma na kuelwa ulichoandika hapo juu..............basi haina haja tena ya kuendeleza mjadala............

Ndg M'med.........vitabu ulivyonitaji hapo juu nimevisoma.......walioandika ni waandishi kama wewe.............historia HAIJAFUNGWA KUREKEBISHWA.........and especially kwenye VITABU.................lakin lengo lako kupitia kwa NDUG YAKO KLEISTna dini ya Kiislamu.............there is a lot to be desired...............
hebu jaribu kuuweka udini pembeni.........halafu ungekuja na mawazo kuwa historia yetu ilivyoandikwa kwenye vitabu hivi na vile inabidi irekebishwe kwnai kuna mambo muhimu yaliyoachwa.............watu wange/tune-evaluate............hizo facts na kurekebisha......lakini kutueleza Kleist (Nduguyako) alilia alipoona DVD yako............surely it does not mean anything..........

Halafu kitu kingine kwneye uandishi wako...............una kasoro moja niliyoiona...............i.e. KUHISI MTU MWINGINE ANAFIKIRIA NINI...........unless wewe una nguvu za Mola wetu..............sidhani kama ni sahihi kusema hivi
Chanzo cha mnakasha huu ni DVD niliyozungumza kuiweka historia ya TANU katika mstari ambao mimi niliona unafaa. Nikiamini kuwa ninayoeleza yamekuwa yakiwatia hofu baadhi ya watu fulani kwa miaka mingi sana. Hofu hiyo ilikuwa inatokana na ukweli kuwa Nyerere hakuanzisha harakati za kujigomboa ingawa yeye mwenyewe alitaka sana historia ya TANU ianze na yeye.
 
LG Ahsante sana kwa mchango wako tafadhali soma hii:


Prof. Malima found out that professionalism and objective decision making had long been forgotten in the ministry. Examinations were marked using candidate’s actual names instead of numbers as is the norm the world over. This created an environment in which it was easy for Christian candidates to be favoured. Prof. Malima also found that Muslim functionaries were barred from promotions. Prof. Malima had to rectify the discrepancies at the ministry. First he promoted three Muslims whose promotions were long overdue after retiring three Christians whose retirement was long overdue. Prof. Malima also promoted a Muslim to the post of commissioner. This change made the balance of distribution of top post at the ministry between Muslims and Christians to stand at 30% to 70% scales still tipping in favour of Christians.
Yet inspite of this imbalance Christians in the ministry complained that Prof. Malima’s promotions were religiously motivated. Prof. Malima found out that the population of Muslim students in primary school was more than 50% but they were few in secondary schools. He realised something must be seriously wrong and he therefore directed that examinations numbers should be used in marking examinations. After these change the number of Muslims students admitted to secondary schools increased by forty percent. Prof. Malima fears were confirmed that there was cheating in the ministry. And that kind of cheating was worse than ordinary cheating. Those who were playing that kind of game were poising to put the country in a dangerous path which could in the future cost the nation dearly.

Prof. Malima wrote a confidential report to the President on the state of affairs he had found in the ministry. In that report Prof. Malima mentioned the stagnation of Muslims and women in education. Prof. Malima warned that if this problem was not solved it was going to create problems to the country in the future. Prof. Malima's report leaked to the press. This letter by Prof. Malima made him a hero to his own people and a villain to the establishment and to the most fervent enemies of Islam in Tanzania. There was panic in the ministry and the government as a whole.

It is said that among those who received the report was the former Vice-President and Prime Minister Joseph Warioba. It was obvious that Nyerere was monitoring President Mwinyi in everything he did. To be able to do what he did Nyerere had to have people deep inside President Mwinyi’s establishment. Nyerere and Warioba were outraged by the letter and tried to have him sacked from the government and party in the same style which ousted Jumbe four years earlier. But this time the issue on the agenda was more sensitive and transparent then was the case with Aboud Jumbe which was covered by political intrigues. Muslims were following closely Prof. Malima’s fight against the Christian bastion with great interest. Muslims had found a leader they could believe in and support.

........hizi habari za Prof. Kighoma Malima kuwa Waislamu wa/tulikuwa wa/tunaonewa sijui ushahidi wake uko wapi............au ndio yale yale Diary za akina Kleist..............
 
LG: Ahsante kwa kutuwekea mada ya Dr Mhina lakini sidhani kama paper hiyo inaweza kujibu kitabu changu. Hujamtendea haki kabisa Dr Mhina. Kitabu hujibiwa na kitabu siyo na mada. Niliposoma "Historia ya TANU 1954 -1977" kilichondikwa na jopo la waandishi wa CCM ndipo nami nikaamua kuandika kitabu kueleza upande wetu wa historia ya TANU. Laiti ningeandika mada hakuna mtu yeyote ambae angelijali. Leo tunajadili kwa kuwa kitabu changu kimeibua mambo mengi ambayo hayakuwa hadhir kabla ya hapo. Kama ni paper ninazo nyingi nilizoandika kuhusu somo hili "Uislam na Siasa Katika Tanganyika" wala sikumbuki hesabu yake. Zipo nilizotoa humu humu nchini na zipo nilizotoa nje ya nchi wachilia mbali makala katika magazeti ya humu nchini na nje ya nchi. Mimi sifanyi mjadala kwa kutaka ugomvi wala sithubutu kufanya hivyo. Nia na madhumuni yangu khasa ni kuihifadhi historia ya kweli ya kupigania uhuru wa Tanganyika. Hii nimechukua kama wajibu wangu na njia pekee ya kuwaenzi wazee wangu. Kuziweka kumbukumbu zao hai kwa ajili ya kizazi kijacho.

....Hiyo kanuni umeitoa wapi.........?
 
Ogah: Ahsante kwa swali lako: Ndivyo nilivyosomeshwa na waalimu wangu.
 
Ogah: Ahsante kwa swali lako. Wajibu wangu mimi ni kueleza yale ninayoyajua. Kama mtu ataamini au ataona ni uongo hilo mimi halinishughulishi sana. Natoa habari hizi nikiamini kwa yakini kabisa kuwa iko siku zitakujatusaidia kuweka mustakbali wa nchi yetu sawa ama iwe katika wakati wa kheri au wa shari. Hao watakaokuwepo hawataulizana: "Mbona hamkusema?"

Kuhusu dairy za marehemu Abdulwahid Sykes na nyaraka za ukoo wao kwa hakika wala si jambo la kubeza ni kitu ambacho mimi kilistaajabisha sana. Ukisoma kitabu changu utaona yalokuwa humo. Hapo tena unaweza ukatoa hukumu. Usitoe hukumu kabla hujafanya utafiti.
 
Mkandara: Ahsante kwa mchango wako mzuri. Napenda kukueleza kuwa shajara (diary) za marehemu Abdulwahid Sykes si moja ni nyingi. Kwa kuwa sikupata kuzisoma hakuna chochote katika kitabu changu kutoka shajara hizo. Hili nimelieleza kwa masikitiko katika kitabu. Tuendelee kutofautiana na tuendelee na mjadala. Naamini kuna manufaa makubwa yanapatika katika mjadala huu.

Ukisoma kitabu nimeeleza kuhusu mkutano wa Abdulwahid Sykes na Jomo Kenyatta kwa urefu na hali ilivyokuwa wakati ule. Kulikuwa na wanachama na viongozi wa TAA ambao walikuwa raia wa Kenya kama Dome Budohi. Hawa ndiyo walikuwa waunganishi wa harakati za TAA na KAU. Dome Budohi nikimfahamu vizuri sana na nilimtembelea Nairobi mara kadhaa kabla hajafariki dunia. Ndani ya kitabu kuna picha tumepiga pamoja. Budohi alinipa mengi sana.
 
ogah: Ahsante kwa swali lako: Ndivyo nilivyosomeshwa na waalimu wangu.

...........something must be extremely wrong kwa hao walimu na mwanafunzi wao anayeamini hivyo..................

Kama facts zinajulikana kuna haja gani ya kujaza kurasa kwa hadithi...........kisa eti lazima ujibu kitabu kwa kitabu!!...........duhh
 
Ogah: Ahsante kwa swali lako. Wajibu wangu mimi ni kueleza yale ninayoyajua. Kama mtu ataamini au ataona ni uongo hilo mimi halinishughulishi sana. Natoa habari hizi nikiamini kwa yakini kabisa kuwa iko siku zitakujatusaidia kuweka mustakbali wa nchi yetu sawa ama iwe katika wakati wa kheri au wa shari. Hao watakaokuwepo hawataulizana: "Mbona hamkusema?"

Kuhusu dairy za marehemu Abdulwahid Sykes na nyaraka za ukoo wao kwa hakika wala si jambo la kubeza ni kitu ambacho mimi kilistaajabisha sana. Ukisoma kitabu changu utaona yalokuwa humo. Hapo tena unaweza ukatoa hukumu. Usitoe hukumu kabla hujafanya utafiti.

...............MUSTAKBALI KWA KUWA MICHANGO YA AKINA KLEIST HAIJAANDIKWA?.........................waandishi ni wengi waliokuwepo na waliopo na mmoja wao ni wewe mwenyewe na wangeweza andika ili kurekebisha yaliyoachwa na waandishi wengine..............am I missing something here
 
Hivi Mohamed Said, huko unakoenda kutoa lekcha kama unavyoonekana kwenye hizo video hapo juu, huwa unawaambia wasome kwanza kitabu chako kabla haujaenda kuwahutubia? Hao vijana wanao sinzia kweli una hakika walisoma kitabu chako? Tofauti na unavyotaka kutuaminisha, vitabu vinajibiwa na mada. Ni kwenye mada ndipo watu wanapopata kukosoa au kukubaliana na kilichoandikwa. Na ni jukumu la mwandishi kuwafahamisha hata wale wasiosoma kitabu chake, jinsi kitabu chake kinavyojibu hoja zao. Kung'ang'ania kuwa lazima tusome kitabu chako kwanza ni jibu la mtu ambaye hana uhakika na hicho anachodai aliandika.

Tumekutolea mifano ya watu kibao humu ambao haukuwataja kwenye hizo lekcha zako na umekiri kuwa wapo kwenye kitabu chako. Sasa kama si mptoshaji na mchochezi kwa nini unapohutubia kadamnasi huwaweki wazi?

Amandla......
 
FM: Ahsante kwa msisitizo. Wallahi sina zaidi katika kukunasihi. Juu ya hivyo nimeweka vipande vingi kutokana na kitabu na mswada wa vitabu ambavyo bado havijachapishwa (Mufti Hassan bin Ameir na Prof. Kighoma Ali Malima). Nadhani ikiwa umesoma bila shaka utakuwa umepata kitu. Kusudi langu si lazima mtu akubaliane na msimamo wangu au jinsi ninavyochambua mambo kama niyaonavyo. Kusudi langu kuu ni kueleza yale ambayo hamkuwa mkiyajua. Sikutegemea kuwa wote watakubaliana na mimi. Ila ningependa nikudokolee kidogo Mwalimu Nyerere alisema nini baada ya kusoma kitabu. Yeye alikubali kuwa yote nilyoeleza ni sawa lakini akamaliza kwa kusema kuwa haamini kama watu wataniamini.
 
Ogah: Ahsante kwa mchango wako. Sijaweza kufahamu vizuri mchango wako. Tafadhali hebu andika tena kwa lugha nyepesi ili niweze kuelewa unataka kunipa ujumbe gani. Nakushukuru kwa kuwa nami katika mjadala huu. Hakika unanielimisha wewe pamoja na wote wanaochangia.
 
Ogah: Jitulize na fanya fikra. Usiuachie moyo ukakutawala toa nafasi kwa kichwa chako. Kuna mengi utanufaikanayo katika kufanya hivyo. Kwa kuanzia rejea katika michango yako kisha fananisha na majibu ninayotoa. Mjadala utadorora kwa matumizi ya lugha zisizo za kiungwana. Mjadala utastawi kwa kushindanisha hoja kwa hoja. Nimesomeshwa na walimu wazuri sana (madras na shule) na nawashukuru kwa elimu na maarifa waliyonipa ndiyo maana leo unanisoma humu. Haipendezi kuwatusi. Kwa kumaliza napenda nikufahamishe kuwa tafsiri ya Qur'an nilisoma kwa Sheikh Abdallah Iddi Chaurembo mwanafunzi wa Mufti Sheikh Hassan bin Ameir (hawa wote walikuwa mstari wa mbele katika TANU). Uongozi nimesomeshwa na Sheikh Hussein Malik (muasisi wa Warsha). Historia nimesomeshwa na Prof. Kaijage Dar es Salaam University na nilikuwa mmoja wa wanafunzi wake alowapenda sana.
 
FM: Uchochezi si moja ya sifa zangu. Nakuwekea kiapnde hiki uone ukoloni ulivyokuwa ukitazamwa na Waislam na uone vipi dini hizi mbili zilivyoathiriwa na utawala wa Waingereza. Huu ni muhtasari tu:

Mwaka 1951 mgogoro wa ardhi ya Wameru ulipoanza tawi la TAA mjini Tabora lilikabili changamoto hiyo kupitia juhudi binafsi za Saadan Abdu Kandoro. Kandoro aliitisha mkutano wa matawi ya TAA ya Mwanza, Kigoma na Tabora kujadili suala hilo. Uongozi wa TAA Tabora, kwa kujihusisha katika mgogoro kama huu, ilikuja kuwa ngome ya upinzani dhidi ya ukoloni. Germano Pacha, katibu wa TAA katika Jimbo la Magharibi, alikuwa miongoni mwa wale wajumbe ambao tarehe 29 Oktoba, 1953 walikwenda Government House kuonana na Gavana Edward Twining ili kujadili ule waraka wa serikali, yaani Government Circular No. 5 uliopiga marufuku wafanyakazi serikalini kujishughulisha na siasa. Mwaka uliofuata TAA ilibadilishwa kuwa TANU na Pacha alikuwa miongoni mwa wanachama waasisi. Pacha alianza kuifanyia kampeni TANU mara tu aliporudi kutoka mkutano wa TAA ulioasisi TANU. Akiwa mhitimu wa Seminari ya Kipalapala ilikuwa rahisi sana kwake kupata kumbi za kanisani, Tabora vijijijni ambamo alifanya baadhi ya mikutano yake ya mwanzoni ya kampeni za TANU. Jambo hili lilizusha ugomvi dhidi ya Pacha. Jambo lile liliwaudhi viongozi Waislam katika TANU mjini Tabora. Wamishonari walijulikana kuwa makachero wa wakoloni na wapinzani wa Uislamu. Kwa hiyo uongozi wa Waislam mjini Tabora ukamsusa Pacha na kwa muda kwa ajili ya kufanya baadhi ya mikutano ya TANU katika kumbi za makanisa. Ususiaji huu ukaifanya TANU katika Jimbo la Magharibi kuzorota. TANU haikuweza kupamba moto Tabora kama ilivyotarajiwa. Moto wa siasa uliokuwa Tabora tangu mwaka 1945 ulionekana kufifia kwa kuzuka chama kipya cha siasa.

Juhudi za kuihuisha TANU zilikuja mwaka 1955 mwaka mmoja baadae kupitia Young New Strong Football Club -kilabu ya kandanda iliyoanzishwa miaka mingi nyuma ambayo ilikuwa maarufu pale mjini. Wanachama wa kilabu hiyo baadhi yao ndiyo walikuwa waasisi wa African Association, mashuhuri miongoni mwao walikuwa Fundi Mhindi na Maulidi Kivuruga. Mwenyekiti wa kilabu hiyo alikuwa Juma Mrisho, mcheza kandanda mashuhuri kwa siku zile. Shaaban Mohamed Silabu na Bilali Rehani Waikela walikuwa katibu na naibu katibu. Uongozi huu wa klabu hiyo ya kandanda ulikutana katika nyumba ya Abeid Kazimoto aliyekuwa akifanya kazi Medical Department, kujadili jinsi ya kuifufua TANU. Sasa ilikuwa wazi kuwa Pacha, kama Mkristo na kabila yake Mlulwa kutoka Mpanda, hawezi kukubalika na Wamanyema wa Tabora. Wamanyema walikuwa wanajulikana kwa tabia yao ya ukaidi. Wakati huo TANU ilibidi ikubaliwe na Waislam wakazi wa mijini kabla ya kusambaa kwenye sehemu nyinginezo. Wamanyema kama Waislam wa mijini walikuwa nguvu thabiti ya kisiasa ambayo haikuwa raihisi kupuuzwa. Alichokuwa akikabiliana nacho Pacha kilikuwa sawasa na kile Nyerere kilimkabili baada ya kumshinda Abdulwahid Sykes katika ule uchaguzi wa TAA wa mwaka 1953. Waislam waliacha kuiunga mkono TANU kwa sababu zile zile zilizomsibu Nyerere. Uongozi wa kilabu uliamua kumualika Julius Nyerere na Bibi Titi Mohammed kuja Tabora ili kujadili tatizo hilo na kulitafutia jawabu.

Mwaka 1955 Bibi Titi Mohamed na Julius Nyerere waliitika mwaliko na kuja Tabora. Mkutano ulifanyika katika ile kilabu ya kandanda. Waliohudhuria mkutano ule walikuwa Germano Pacha, Juma Mrisho, Shaaban Mohamed Silabu, Bilali Rehani Waikela, Mohamed Mataka wakati ule akiwa muadhin wa Masjid Nur - msikiti wa Wamanyema pale Tabora, Hassan Mohamed Ikunji, Ramadhani Mussa Wajaku, Swedi Mambosasa, Said Ali Kiruwi na Hamis Khalfan. Uongozi wa kilabu ulimwambia Nyerere na Bibi Titi kuwa kilabu hiyo ya kandanda ilikuwa ikitaka udugu na TANU ili ifanye kampeni ya kuipatia TANU wanachama wengi. Uongozi huo wa TANU kutoka makao makuu Dar es Salaam uliambiwa kuwa maadam kilabu hiyo ilikuwa ikipendwa na kuungwa mkono na watu wa Tabora na ilikuwa maarufu sana, sifa hizo zingeweza kutumiwa kwa manufaa ya TANU. Vilevile Nyerere alifahamishwa kuwa kilabu hiyo ingependa kuvijumuisha vyama vitatu vya lelemama na vikundi vya taarabu, Nujum ul Azhar, Waridatil Hubb na Egyptian Club. Nyerere na Titi waliyakubali mapendekezo haya na usiku ule akifuatana na uongozi wa kilabu Nyerere alizungumza na kikundi cha watu waliyokusanyika nje ya nyumba ya kilabu juu ya hali ya Tanganyika katika siku zijazo. Nyerere alikuwa amerudi Tabora ambapo alianza siasa kiasi cha miaka minane nyuma. Jambo muhimu katika kipindi hiki pale Tabora ni kuwa wasomi wa Makerere waliokuwa St. Maryís School hawakuwapo katika harakati hizi na katika mikakati iliyokuwa ikipangwa.

Bibi mmoja wa Kiganda, Nyange bint Chande, mwanachama wa moja ya vikundi vya lelemama mjini Tabora alijitolea nyumba yake kama ofisi ya kwanza ya TANU katika Jimbo la Magharibi. Uchaguzi ulifanyika na Shaabani Marijani alichaguliwa Mwenyekiti wa Wilaya na Idd Said Ludete Katibu wa TANU. Bilali Waikela akawa mjumbe wa kamati. Kadi za kwanza za uanachama wa TANU ziliuzwa ndani ya soko la Tabora na Amani Idd na Pacha, Katibu wa Jimbo wa TANU. Pacha alikuwa na lingo la kuni pale sokoni kama biashara yake. Baadae Amani Idd alisaidiwa kazi hiyo ya kuuza kadi za TANU na Dharura bint Abdulrahman.
 
LG: Ahsante kwa kutuwekea mada ya Dr Mhina lakini sidhani kama paper hiyo inaweza kujibu kitabu changu. Hujamtendea haki kabisa Dr Mhina. Kitabu hujibiwa na kitabu siyo na mada. Niliposoma "Historia ya TANU 1954 -1977" kilichondikwa na jopo la waandishi wa CCM ndipo nami nikaamua kuandika kitabu kueleza upande wetu wa historia ya TANU.
Mkuu Mohammed Said hapo ndo wanishangaza.
Nafikiri sasa uko kwenye kona na huna mahala pa kukimbilia.
Muda wote huu wachangiaji wengi wamejaribu kukuelewesha kuwa misingi ya kitabu chako ina walakin, nawe umeshikilia msimamo wako ule ule.
Mbaya zaidi ni wewe mwenyewe kukosa ujasiri wa kuelezea yaliyoya mbele , siamini kama huna fikra za kujua kile unacho kidhamiria.
Statements kama uliyoitoa kuwa kitabu hujibiwa na kitabu kingine ni escapism. Unaanza kulemewa na kujibu hoja zilizoenda shule.Historia si ya mtu mmoja au kundi moja kuihodhi.
Na hapa JF nashukuru kuwa wachangiaji wamekuchambua vilivyo.
Katika mada zako dunia ya TANU ilikuwa ni ya waislamu tu, watu wengine mchango wao ulikuwa duni sana kulingana na wewe.Waislamu walizunguka Pwani ,Tabora,Mwanza na kwingineko wakihubiri uhuru!Nyerere alikuwepo kuwepo tu, halafu waislamu hao hao wakampa Nyerere uongozi! pana wa walakin hapa.It doesn't make sense!

Kuna vitabu vingi sana vya kichochezi ambavyo vilijibiwa na vita na kumwaga damu za watu wasio na hatia.
Kwa vile MS ni msomi wa historia basi atakuwa anakifahamu kitabu chenye utambulisho wa Mein Kampf, kitabu cha Adolf Hitler.
Misingi ya kitabu hicho nazifananisha na cha MS.Mapitio ya kitabu hiki kimsingi ni kuweka maangamizo kwa kizazi kingine kisicho cha kwake Hitler, akitoa sababu ya kukosa maendeleo kwa wajerumani ati tatizo likiwa wayahudi.

Sababu kubwa ya kuweka mada kama za Prof Mhina ni kukanusha yale mengi ambayo Ndg Mohammed Said amekuwa akihubiri kama ukweli usiopingika.Kuna maadiko mengi tu yanayo yanayoweza kumsahihisha ndugu yetu huyu kutoka katika kinjia cha fikra zielekeazo katika machafuko ya kidini.

Mada za Mkuu MS ni kwa ajili ya wanafunzi waliokulia katika misingi ya madrassa, wenye kuelemewa na hisia za udini. Mimi nafarijika sana na nashukuru uchambuzi uliotolewa na wachangiaji wengine, hasa wenye mwelekeo wa kijenga utaifa wetu.
In short what Mohammed Said is proposing for the future is religious apartheid, seperate and segregated development for separate religious and social groups in Tanzania.
Mohammed Said you will fail in your endeavours.
 
Simba na Yanga zilianzishwa na makuli wengi wao wakiwa Waislamu.....sasa na itafika wakati itadaiwa hizi ni klabu za waislamu pia :confused2:
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom