LG: Insha Allah nitakiweka kisa kizima cha AMNUT ukumbini. Nimtz kama mtafiti wa nje kapitwa na mengi sana. Sheikh Hussein Juma akikaa Mtaa wa Nyamwezi/Mafia nyumba ya bibi yangu bint Farijallah Mkubwa ilikuwa Mafia/Msimbazi pale inapopita barabara ya Msimbazi hivi sasa. Nakufahamisha haya yote ili ujue kuwa mimi si wakumsikiza mtu kutoka Canada, Augustus Nimtz kuhusu historia ya wazee wangu na jinsi walivyoyaona mambo kwa wakati ule. Sheikh Hussein Juma sijui lini alikuwa kiongozi wa AMNUT. Mwenyekiti wa AMNUT alikuwa Mashado Ramadhani Plantan na Katibu alikuwa Abdulwahid Abdulkarim. Mashado nyumba yake ilikuwa Kirk Street (sasa Lindi)/Nyamwezi na mjomba wangu Shomari Lupindo alikuwa jirani yake. Nadhani umenielewa. Insha Allah nitakiweka kisa cha AMNUT ili ukumbi ufaidike. Napoandika hivi sasa ni kama watu hawa nawaona. Tatizo ulokuwanalo wewe ndilo lilomtatiza Nyerere wakati Abdulwahid Sykes na Dr Klerruu wanaandika historia ya TANU. Mtu kutoka Musoma anataka awaeleze watu wa Dar es Salaam siasa za mji zilikuwaje na yeye mgeni kaingia mjini hata miaka kumi haijafika. Huu ni muhali mkubwa. Nimtz utafiti wake ulizama zaidi katika Tariqa Quadiriyya na alikaa sana kwa Sheikh Mohamed Ramia Bagamoyo. Tasnifu yake ipo Maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Hiyo ina mengi kuliko kitabu.
Mkuu Mohammed Said kuwafahamu hawa masheikh kufahamiana au kuwa ndugu zao haiondoi mashaka yangu juu ya maandiko yako yenye mwelekeo wa udini.
Maandiko kwa ujumla kama nimeyaelewa vema yasema hivi:
1Waislamu ndo waliopigania uhuru zaidi kuliko kundi jingine lolote hasa la Kikristo kabla
ya uhuru kupitia TAA/TANU
2 Baada ya uhuru Nyerere alihakikisha historia ya waIslamu waasisi wa kupigania uhuru
wanapuuzwa katika na kusahauliwa katika maeneo yote
3 Kwamba Mohammed Said anaandika kitabu cha kuonyesha "ukweli" wenyewe na jinsi unavyoonyesha muIslamu alivyo na anavyo kandamizwa nchini Tanzania.
4Kwamba Mohammed Said na nduguze anaowafahamu hata kwa mitaa waliyoishi na wa
Islamu wengine, hawajafaidika na uhuru tuliopata takriban miaka 50 iliyopita
Sasa kwa mtazamaji wa kawaida wa mada hii ya "Ukweli kuhusu waasisi wa TANU na harakati za kupigania uhuru" mimi nimefarijika sana kupata some details kutoka kwa Mohammed Said juu ya yaliyojiri kabla na baada tu ya uhuru.
Nadiriki kusema nimefahamu articles za Mohammed Said tokea magazeti hasa The East African.
Pamoja na ukweli kuwa sikubaliani kabisa na mada za ndugu yangu huyu kwa vile mada hizi zimekaa kuitukuza imani yake kama ndio ikliyopigania uhuru.Na kwamba imani hiyo ikatekelezwa baada ya uhuru na Mwalimu.
Mimi nimeweka maandiko ya watu wawili kukanusha kuwa waTanganyika walipigania uhuru kama mwAfrka kwanza na si kwa imani zao.
Na kupinga ukoloni haukuanza na waislamu , post za nyuma nimeonyesha juhudi za kina Mirambo, Mkwawa , Meli na Sina, na hawa wala hawakuwa waIslamu au waKristo.
Maandiko ya Prof Mhina na Mitz yote Ndugu yangu huyu anayakataa ati kwa vile yeye amekula na kuishi na hao anawaita waasisi wa kiislamu wa uhuru wetu.
Maandiko haya mawili nimeya weka ili kuonyesha kuwa WAISLAMU WALIKATAA UDINI, hata kabla ya uhuru kwa kuikataa AMNUT!!!
Maandiko yapo mengi tu ya kukanusha mwelekeo wa udini wa mwandishi Mohammed Said.
Na vile vile kabla ya uhuru vyama kama TAA vilikuwepo vingi tu mikoani, hivi ni pamoja na vyama vya ushirika vilvyojulikana sana na kuwa na nguvu kubwa.
MS, Mwalimu Nyerere ni jina kubwa kuliko unavyofikiri.
Nina uhakika kuwa leo hii mimi na wewe tusingekuwa tunaelezana haya kama isingekuwa Mwalimu kuondoa matabaka ya kabila , dini na rangi.
Nimeonyesha vile vile kuwa AMNUT, chama cha Kiislamu, kilitaka ubaguzi wa rangi uendelezwe katika Tanganyika.
Sasa unaposema tatizo langu ndilo la Nyerere mtu wa Musoma, na asingeweza kuelewa mambo ya mjini mimi nakushangaa sana.
Bado wa mjini(waIslamu) wakampa Nyerere uenyekiti wa TANU na baadaye Urais wa Tanganyika.
Umjini huo huo ndio ukaviua vyama vya kibaguzi kama AMNUT na vingine vikaishia kupigwa marufuku.
MS you are full of contradictory stories that are nice to read though!!!