Ukweli kuhusu waasisi wa TANU na harakati za kupigania uhuru

Status
Not open for further replies.
Wanaukumbi mbona mjadala unapungua kasi siyaoni mawimbi makubwa ya pale mwanzo ya kuzamisha "super tankers." Mjadala umetoka ladha au kitu gani? Prof. Mhina hajapatikana au vipi?
Waliokuelewa ni hawa:

JOKA KUU
Mohamed Said,
..unaweza ukatueleza kisa kilichosababisha Christopher Kassanga-Tumbo, na Joseph Kasella Bantu kuwekwa kizuizini?
..pia kuna Machifu kama Fundikira na Kidaha Makwaia nao walitiwa msukosuku na Mwalimu Nyerere. hawa nao tatizo lao lilikuwa ni nini?
CHAMA
.....vitabu vyako vinapatikana vipi?
 
Ngoja nikuhadithie mstuko nilopata siku niliposikia watu wanamwita Nyerere "Baba wa Kanisa." Ilikuwa mwaka 1995 tunaadhimisha mwaka mpya wa Kiislam katika Viwanja vya Mnazi Mmoja. Marehemu Prof. Malima na mimi tulipangwa kuwahutubia Waislam. Prof. Malima alieleza mengi aliyoyaona serikalini jinsi ubaguzi dhidi ya Waislam ulivyoshamiri hasa Wizara ya Elimu. Aliposhuka yeye sasa ni usiku tushaswali Isha mimi nikapanda kuzungumza. Mimi nilieleza historia ya Waislam na mchango wao katika kupigania uhuru wa Tanganyika. Mwisho nikaeleza "mgogoro" wa EAMWS na nafasi ya serikali katika kadhia ile. Sasa ikawa kuna mahali wakati namtaja Nyerere nikamwita Baba wa Taifa. Zogo likalipuka. Mimi niko juu ya jukwaa nasikia kelele lakini sisikii yale ambayo watu wanasema. Palipotulizana kidogo ndiyo nikasikia wanasema kwa sauti, "Baba wa Kanisa, Baba wa Kanisa, Baba wa Kanisa." Yaani Mwalimu kwa yale alowafanyia Waislam wao hawawezi kamwe kumuona kama Baba wa Taifa bali ni Baba wa Kanisa. Hii cassette tape ninayo hadi leo. Baada ya kusikia vile palepale nikabadili mwelekeo wa ile hotuba nikawataka Waislam wajitazame iweje leo kiongozi alopendwa na wazee wao leo aje aonekane msaliti? Siku ya pili taarifa zikanifikia kuwa cassettes za ile khutba yangu zinauzika mjini kama keki za moto.
Safi sana mkuu Mohammed Said , maana tukikuweka kwenye bahasha inayokueleza vilivyo unakuwa mkali kupindukua.
Kwa vyovyote vile unachokuhubiri ni uchochezi, unachochea vurugu za kidini kwa kutumia kalamu na mihadhara, audience yako ikiwa vijana wadogo wa kiislamu.
Kwenye mihadhara yako usisahau kuandika kuwa wasikilizaji karibu wote ni vijana wa madrassa mliowakusanya kutoka sehemu mbalimbali.
Kwa mantiki hiyohiyo sasas wewe tukuiteje ? mwandishi wa historia ya kiislamu?
Maana historia hiyo wengine haituhusu au unaonaje.
 
LG: Hili lingekuwa la maana sana kama ungemfahamisha Prof.Mhina kuwa Mohamed Said kasema kadha wa kadha sasa nakuomba uingie ukumbini umjibu. Kutumia paper ya Prof. Mhina kunijibu sidhani kama itanogesha mjadala. Natoa changamoto kwa wanaukumbi kwa ujumla tafadhalini mtafuteni Prof. Mhina popote alipo kama mnamfahamu aje Insha Allah na yeye achangie sote tunufaike.

Mkuu Mohammed Said usijiwejke juu sana katika fani ya usomi na sisi tunajua kuperuse, kutafuta na kupipata kile kunachoweza kukuweka kwenye bahasha unayostahili.
Kama waandishi wote tunaorefer wangekuja kutetea mada zao hapa jamvini , basi huu ukumbi usingekewa ulivyo.Na waliotangulia je? maandishi yao ingekuwaje?
Katika mada hii JIBU ALLEGATIONS HIZO ili uweze kuona fallacy ya argument yako.
 
1. Nyerere hakutaka kumuachia Mzee Mwinyi kwa kupenda. alitaka sana Mtu wake awe Rais baada yake. lkn wakati ule katiba ilitaka Rais atoke ZNZ, na so far wakati Ule Nyerere Nchi ilishamshinda. hali mbaya ya uchumi ilibidi lazima aachie Ngazi...Kipande hiki naachia wanahistoria kufanya utafiti kilichojiri wakati wa Mkutano wa CC wa CCM wakati Ule...Ilikuwa ni mara ya pili Nyerere kulia Ndani ya Kikao....!!!

Katiba haizungumzii mgombea wa urais atoke wapi. Inachozungumzia ni mgombea mwenza. Tutajie kifungu cha katiba kinachosema au kilichokuwa kikisema kuwa rais ni lazima atoke upande fulani wa JMT. Nyerere hakulazimika kumwachia mzanzibari urais. Hakulazimishwa na mtu kuachia ngazi maana wakati ule hakukuwa na term limits. Hayo hadithi za kwenye mikahawa ati Nyerere alilia ni upuuzi mtupu.

2. Fundi..nakutajia CHUO cha BANK- Iringa amepewa nani?

Unauliza jibu badala ya kutuambia kapewa nani? Sema, uumbuke.

3. Hata Hizo shule za kanisa zilizoporwa na Nyerere Kanisa hawakujenga. Shule Zilijengwa na Mkoloni zikapewa kanisha kuziendesha. as moja ya Ajenga ya Mkoloni kutumia DINI kutawala...Local Wakristo fanyeni hesabu shule ngapi mmejenga kwa Mikono yenu?...hapa Mkapa akawapa tena shule ya Magamba...muifanye Chuo Kikuuu...Shule ya Mazengo---na Chuo cha Nyegezi...!!!

Uongo mtupu. Shule hizi zilijengwa na wamisheni na sio wakoloni. Nyingine zilijengwa hata kabla ya utawala wa kiingereza kuingia sasa utasemaje kuwa walijenga wakoloni? Hizo zote unazozungumzia ni shule zilizokuwa za wamisheni na zilirudishwa kwao baada ya serikali kushindwa kuziendesha. Shule zinajengwa na makanisa kutokana na sadaka za wakristu. Sasa kuanza kuuliza ngapi wamejenga kwa mikono yao ni upuuzi mtupu. Angalia tu ni shule ngapi ziko mikononi mwa madhaehebu tofauti ndipo utajua kuwa sadaka zao zinafanya kazi.

4. Hio idadi ulotaja, sikatai, lkn wenzetu kwa kuwepo wao wachache tu Mmefanya Kikwete aitwe Mdini. mlitaka hizo nafasi zote ziende kwenu....nafasi ya BOSS wa TISS ilikuwa na mjadala mrefu hapa JF. utafute uuone. So far hatuhitaji eti waislam wangapi wamechaguliwa, tusipenda ni pale mwislam hata mmoja akichaguliwa kuongozo Idara au Shirika wenzetu mnakuja juu.,mmejizoesha Vibaya kuona Utawala wa Serikali ni Mali yenu....
.....JK teuzi zote anazofanya balaa linakuja pale ambapo kawateua waislam wawili/watatu wenzetu mnaanza kulipuka. ipo Mijadala mingi hapa JF, ambayo kila teuzi ya JK ambayo ndani yake yuko mwislam alau mmoja, mmekuja juu...teuzi zingine hata huwezi kukuta mijadala hapa JF, wala watu kuhoji CV zao...na zikihojiwa tu, mnaanza kutoa Pongezi...Tuache hii kitu.

Kwa nini tuache hili? Hao wakina Dr. Nchimbi, Dr. Mary Nagu wanaoandamwa kila siku kuwa wametoa vyeti feki ni waislamu? Nyinyi akiguswa muislamu tu mnajificha nyuma ya pazia la udini lakini wanaposakamwa wakina BEN Mkapa, EDWARD Lowasa, huo udini hamuuoni? Mimi sijawahi kusema kuwa Kikwete au Mwinyi ni wadini kwa sababu ya kuteua waislamu. Hiyo ni haki yao na wanaweza kuteua yeyote wamtakaye kama ilivyokuwa kwa Julius na Ben. Tunachokataa ni pale nyinyi mnapokazania kuona mkono wa wakatoliki hata pale ambapo serikali inaongozwa na watu ambao ni waislamu!

5. kaka neno HAKI lipo so clear. sio Upendeleo.

Kama hilo neno lipo clear unashindwa nini kuliweka wazi? Unashindwa nini kuweka wazi haki ambazo waislamu mnanyimwa kikatiba na ambazo mnadai mpewe? Au unaogopa kutaja maana mtaishiwa visingizio?

Amandla......
 
. Hata Hizo shule za kanisa zilizoporwa na Nyerere Kanisa hawakujenga. Shule Zilijengwa na Mkoloni zikapewa kanisha kuziendesha. as moja ya Ajenga ya Mkoloni kutumia DINI kutawala...Local Wakristo fanyeni hesabu shule ngapi mmejenga kwa Mikono yenu?...hapa Mkapa akawapa tena shule ya Magamba...muifanye Chuo Kikuuu...Shule ya Mazengo---na Chuo cha Nyegezi...!!!
1. Magamba Secondary School imetokana na Magamba Country Club iliyonunuliwa na Usambara-Digo Lutheran Church mwaka 1961. Kwanza iliitwa Usambara Trade School na baadae kupanuliwa kutokana na msaada wa Nation Lutheran Church ya New York na mkopo kutoka Benki Kuu ya Dunia. Shule ilitaifishwa mwaka 1969 wakati Mwalimu Gideon Chaghuza akiwa headmaster. Shule hii ilirudishwa kwa walutheri mwaka 2005.

2. Shule ya Mazengo hapo awali ilikuwa ikiitwa Alliance Secondary School na ilimilikiwa na kanisa la kianglikana Tanzania. Ilijengwa miaka ya 1940s na Passionists na wamisheni wa CMS.

3. Mwaka 1960, kutokana na ombi la Askofu Joseph Blonjous wa Mwanza, order ya kikatoliki ya White Fathers ( sasa wanajulikana kama Missionaries of Africa)walijenga chuo sehemu ya Nyegezi walichokiita Nyegezi Social Training Centre baadaeNyegezi Social Training Institute. Mwaka 1975, chuo kilikabidhiwa kwa Tanzania Episcopal Conference ambao walikiendesha mpaka mwaka 1998 walipoamua kukigeuza kuwa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine.

Amandla.......
 
Tafadhali wana JF hebu muperuzi haya yaliyotokea kabla ya uhuru.Waislamu waliazinisha chama chao kilichoitwa AMNUT(All-Muslim National Union of Tanganyika), Sasa mtu akija na kusema waislamu walionewa kabla ya uhuru ni uongo.

Tupate kutoka kitabu cha August H. Nimtz: Islam and politics in East Africa: the Sufi order in Tanzania

" Though many Muslims were active in TANU, the national leadership of the party had a disproportionate number of chrirtians, including the head,Julius Nyerere , a Roman Catholic.To some Muslims TANU seemed a party of christians that would not serve the interests of Islam.This sentiment was the prime motive in the formation in 1957 of the All-African National Union of Tanganyika(AMNUT).
This organisation was not intended to be a political party but radher a pressure group that would lobby with the government to improve the social status of Muslims. The suspicions that AMNUT supporters held about TANU increased to such a degree that, as it became clearer that Nyerere's party would inherit power from the British, the new Islamic organisation took the position that independence should be delayed until Muslims had reached parity with Christians in educational attainments.
During the year preceeding independence, when TANU shared power with the British,the AMNUT attempted to win over religious leaders in different locales to their positio, but with little success. In Kondoa ,for example fifty one shayks publicly declared oposition to the delaying strategy.
The strongest support for AMNUT was in the capital, Dar es salaam. One of its leaders, Shaykh Hussayn b. Juma, a prominent resident of the capital, was at the same time the head of the United Tanganyika Party, a government supported alternative to TANU that advocated proportional representation based on race. In Dar es salaam, nevertheless, its support began to wane as both leading and rank-and-file members began to question the wisdom of its policy on independence. TANU was able to ally the majority of the shayks to its side and opposition to the AMNUT. In late 1960, forty -three shayks gave their written support to the TANU and denounced the AMNUT. The organisation became discredited in the eyes of many and by 1963 it was moribund."

Wakuu tusidanganywe mara ooh wakoloni waliwapendelea waKristo, mara uhuru ulipatikana kwa nguvu kubwa ya waIslamu. Vitabu , kama hapo juu,vinatuambia kuwa kuna waIslamu walitaka uhuru uahirishwe sababu ikiwa udini!!
Hatushangai kuwa vyama kama AMNUT viliishia mbali kusikojulikana, kama ambavyo vitabu vya Mohammed Said vitaishia mbali na kutothaminiwa na mTanzania yoyote mwenye akili timamu.
WaTanzania wenye moyo wa Utaifa hawawezi hata kuviweka vitabu hivi nadarasani,, sana sana vitasomwa na watu wasio na muda na wenye kupendelea shari badala ya maendeleo.
 
Mkuu Mohammed Said usijiwejke juu sana katika fani ya usomi na sisi tunajua kuperuse, kutafuta na kupipata kile kunachoweza kukuweka kwenye bahasha unayostahili.
Kama waandishi wote tunaorefer wangekuja kutetea mada zao hapa jamvini , basi huu ukumbi usingekewa ulivyo.Na waliotangulia je? maandishi yao ingekuwaje?
Katika mada hii JIBU ALLEGATIONS HIZO ili uweze kuona fallacy ya argument yako.

LG. Nimejiweka vipi juu ni kwa kuomba Prof. Mhina mwenyewe aje ukumbini? Kwa nini tutayamam wakati maji yapo? Hilo ndilo lililonifanya niombe aliyeandika mada mwenyewe aingie atuelimishe. Hilo ni kawaida sana katika duru za kisomi. Naona kidogo umeghadhibika. Iweje mie sighadhibiki ilhali nyie mko wengi mnanipiga maswali, "critisism" wakati mwingine kejeli nk na ninastahamili? Au ndiyo yale yale ya Nyerere na historia ya TANU? Huu ni mnakasha tu tunaelimishana kama ndugu kwa faida ya nchi yetu. Si angalau bado tuko katika bahari tulivu tunaelezana ukweli? Nipe nikupe. Wenzetu katika hali kama hii ya jamii moja kuwa na fursa na jamii nyingine kuwa hawana kitu imewaletea vita. Nani asiyejua hii leo kisa cha Wahutu na Watusi. Hivi hali hii hapa hapa kwetu haipo? Hatutaki kwenda huko ndiyo maana tunaieleza serikali ijue Waislam tunahisi vipi. Na ndiyo maana tumeanza kwa kuandika historia yetu kuwa Waislam walikuwa mstari wa mbele kwa kuwa ilikuwa jamii ilodhulumiwa sana katika ukoloni. Katika historia hiyo tumeeleza nguvu yetu katika kuung'oa ukoloni ili waliokuwa labda hawajui wajue. Mwisho tukaeleza mbona yale tuliyoyakataa chini ya mkoloni sasa yanaendelezwa katika serikali huru ya wananchi? Mkoloni aliacha mawakala wake kupitia Kanisa? Haya yote tumeweka wazi ili serikali iamke kabla hatujachelewa. Haikustaajabishi mimi nimeweka jina langu wazi kwa kila mtu anifahamu asaa kheri wakubwa wakiwa wanataka ushahidi niwape ili warekebishe hiyo dhulma? Kwangu kuanza kuzungumza na watu kuwa kuna dhulma kadha wa kadha khasa baada ya mjadala huu wa takriban majuma mawili kwa sasa hauna tija tena.
 
Tukubaliane sote kuwa huyu jamaa anatatizo la kimsingi.
Kwanza soma vizuri kabla ya kukurupuka mantiki ndani ya ushauri wangu.My pen name is LOLE GWAKISA na si Lole Gwasika! Naweza kujifunza toka maandiko yako kuwa wewe si mtu makini katika masuala ya nchi hii.
Usipoteze muda wako kubadili mada iliyopo mbele yetu, mada ambayo imeshachukua sura mbaya ya udini, historia ya TANU na waanzilishi wake kamwe haiwezi kuchukua sura kuwa ilikuwa ni mapambano kati ya Ukristo na Uislamu.
Na hapo ndio nashangaa akili ya watu wa aina ya AMI na wateteaji wa Udini uliolemea Uislamu kutaka kuredress kitu ambacho ni cha kudhania.
Matatizo ya kimaendeleo yapo na kila mtu anakubali hili, lakini kuweka assumption kuwa Wakristo tu ndio wamefaidika na Uhuru ni ukosefu wa upeo wa kufikiri.
Dont economize your brains capacity ndugu Ami.
Kama unafikiri unaweza kuleta maendeleo kwa waislamu, bila juhudi za Taifa zima , basi you are more than welcome, ingawaje I strongly doubt your means and ways.
Tunapotetea umoja wa kitaifa, hata Mwalimu aliwahi kusema , inabidi uonekane kama mwenda wazimu vile , au kama Padri au Shekhe.Maana matunda yake huyaoni in your life time.
Ami, Mohammed Said,nimesema bila kuwabeba waTanzania wote kwenye mikakati yenu ya the future of your own selves hamfiki mbali sana, you will hoplessly get bogged down in a messy quagmire ya ubaguzi, udini zaidi na mabishano ya nani zaidi katika Uislamu.Haya tunayaona hata leo.
Nyie ndugu zetu, na pengine tunawaelewa zaidi kuliko ninyi mnavyojielewa.
Juhudi, umoja na kodi yangu na yako ndivyo vitakavyo tuwezesha.
Kukosea herufi moja ya jina lako Gwasika badala Gwakisa si dalili ya umakini wa mtu. Hebu jisome mwenyewe hapo

.560...Yeye (mohammed Said) anayojua ni kwanini waislamu wali wekwa ndani ,ati kwa sababu ya uislamu wao na sio kutofautiana as a matter of principle na Nyerere.Huu ni ishahidi wa kueneleza udini.
Historia ya waislamu wa AMNUT , imekuwa ikikwepwa na Mohammed Said na nitarudia posting ya hawa waislamu kupendekeza KUKATAA UHURU ili wawe sawa na waKristo kimasomo kwanza:
....504...Spot on Son of A
These guys are incorrigible villains scampering for A FINAL SOLUTION.
That is the alarm I have been raising all along.
This man Mohammed Said has absolutely no other remedy to the hue and cry he is raising, and that is despite several reminders from various contributors.
In that I have the opinion tat he will fail in whatever they aree scheming,with MS being the soft face of the scheme.

Mimi nafikiri kuonesha umakini wako ungejibu maswali yangu,hasa nani hayuko tayari kufaidi matunda ya uhuru?.
 
Fuatilia Mjadala ....Kipengele kimebadilishwa..so far tulikuwa tunazungumzia mambo ya baada ya Nyerere kuachia Ngazi.

Khs Shule za Kanisa(Shule zilizojengwa na Serikali ya Mkoloni).....Nimekuambia zilizotaifishwa na Nyerere ...kama unataka majina tafuta mwenyewe ktk database za Wizara ya Elimu.

Kwa Hiyo Kikwete hayuko Kikatiba Siyo? Maana kwa maelezo yako ni kwamba baada ya Mkapa alitakiwa aje Mzanzibar lakini haikuwa hivyo
 
Hivi Ingekuwaje kama Nyerere asingetaifisha Shule za misheni na kuzifanya kuwa za Uma? Ndugu zangu tupigane na adui Mjinga na tuache kutafuta mchawi matokeo yake tunataka kuchochea migogoro isiyo na Lazima. Nyerere ana madhaifu yake kama Binadamu lakini siku Zote atakumbukwa kwa kuliunganisha Taifa hili na kuwa kitu kimoja regardless ya makabila yetu Dini zetu na hata rangi zetu. Mohamed Said unaweza ukawa na pointi nzuri lakini the way unavyoipresent inatia mashaka kidogo, haiwezekani Kukosa Elimu kwa Waislamu Ukawalaumi wakristo hata Kidogo ndugu yangu
 
Tafadhali wana JF hebu muperuzi haya yaliyotokea kabla ya uhuru.Waislamu waliazinisha chama chao kilichoitwa AMNUT(All-Muslim National Union of Tanganyika), Sasa mtu akija na kusema waislamu walionewa kabla ya uhuru ni uongo.

Tupate kutoka kitabu cha August H. Nimtz: Islam and politics in East Africa: the Sufi order in Tanzania

" Though many Muslims were active in TANU, the national leadership of the party had a disproportionate number of chrirtians, including the head,Julius Nyerere , a Roman Catholic.To some Muslims TANU seemed a party of christians that would not serve the interests of Islam.This sentiment was the prime motive in the formation in 1957 of the All-African National Union of Tanganyika(AMNUT).
This organisation was not intended to be a political party but radher a pressure group that would lobby with the government to improve the social status of Muslims. The suspicions that AMNUT supporters held about TANU increased to such a degree that, as it became clearer that Nyerere's party would inherit power from the British, the new Islamic organisation took the position that independence should be delayed until Muslims had reached parity with Christians in educational attainments.
During the year preceeding independence, when TANU shared power with the British,the AMNUT attempted to win over religious leaders in different locales to their positio, but with little success. In Kondoa ,for example fifty one shayks publicly declared oposition to the delaying strategy.
The strongest support for AMNUT was in the capital, Dar es salaam. One of its leaders, Shaykh Hussayn b. Juma, a prominent resident of the capital, was at the same time the head of the United Tanganyika Party, a government supported alternative to TANU that advocated proportional representation based on race. In Dar es salaam, nevertheless, its support began to wane as both leading and rank-and-file members began to question the wisdom of its policy on independence. TANU was able to ally the majority of the shayks to its side and opposition to the AMNUT. In late 1960, forty -three shayks gave their written support to the TANU and denounced the AMNUT. The organisation became discredited in the eyes of many and by 1963 it was moribund."

Wakuu tusidanganywe mara ooh wakoloni waliwapendelea waKristo, mara uhuru ulipatikana kwa nguvu kubwa ya waIslamu. Vitabu , kama hapo juu,vinatuambia kuwa kuna waIslamu walitaka uhuru uahirishwe sababu ikiwa udini!!
Hatushangai kuwa vyama kama AMNUT viliishia mbali kusikojulikana, kama ambavyo vitabu vya Mohammed Said vitaishia mbali na kutothaminiwa na mTanzania yoyote mwenye akili timamu.
WaTanzania wenye moyo wa Utaifa hawawezi hata kuviweka vitabu hivi nadarasani,, sana sana vitasomwa na watu wasio na muda na wenye kupendelea shari badala ya maendeleo.

LG: Insha Allah nitakiweka kisa kizima cha AMNUT ukumbini. Nimtz kama mtafiti wa nje kapitwa na mengi sana. Sheikh Hussein Juma akikaa Mtaa wa Nyamwezi/Mafia nyumba ya bibi yangu bint Farijallah Mkubwa ilikuwa Mafia/Msimbazi pale inapopita barabara ya Msimbazi hivi sasa. Nakufahamisha haya yote ili ujue kuwa mimi si wakumsikiza mtu kutoka Canada, Augustus Nimtz kuhusu historia ya wazee wangu na jinsi walivyoyaona mambo kwa wakati ule. Sheikh Hussein Juma sijui lini alikuwa kiongozi wa AMNUT. Mwenyekiti wa AMNUT alikuwa Mashado Ramadhani Plantan na Katibu alikuwa Abdulwahid Abdulkarim. Mashado nyumba yake ilikuwa Kirk Street (sasa Lindi)/Nyamwezi na mjomba wangu Shomari Lupindo alikuwa jirani yake. Nadhani umenielewa. Insha Allah nitakiweka kisa cha AMNUT ili ukumbi ufaidike. Napoandika hivi sasa ni kama watu hawa nawaona. Tatizo ulokuwanalo wewe ndilo lilomtatiza Nyerere wakati Abdulwahid Sykes na Dr Klerruu wanaandika historia ya TANU. Mtu kutoka Musoma anataka awaeleze watu wa Dar es Salaam siasa za mji zilikuwaje na yeye mgeni kaingia mjini hata miaka kumi haijafika. Huu ni muhali mkubwa. Nimtz utafiti wake ulizama zaidi katika Tariqa Quadiriyya na alikaa sana kwa Sheikh Mohamed Ramia Bagamoyo. Tasnifu yake ipo Maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Hiyo ina mengi kuliko kitabu.
 
Katiba haizungumzii mgombea wa urais atoke wapi. Inachozungumzia ni mgombea mwenza. Tutajie kifungu cha katiba kinachosema au kilichokuwa kikisema kuwa rais ni lazima atoke upande fulani wa JMT. Nyerere hakulazimika kumwachia mzanzibari urais. Hakulazimishwa na mtu kuachia ngazi maana wakati ule hakukuwa na term limits. Hayo hadithi za kwenye mikahawa ati Nyerere alilia ni upuuzi mtupu. ..

....kama habari za Mikahawa endelea hivyo hivyo...alilazimishwa na Hali ya Uchumi...!!!
Am not sure na Katiba..kama nimekosea mtanisamehe...!!!ila Kimsingi Nyerere alikuwa na mtu wake ambae alishindwa kumsimika..!!!

Unauliza jibu badala ya kutuambia kapewa nani? Sema, uumbuke. ...Chuo kimepewa KANISA.

Uongo mtupu. Shule hizi zilijengwa na wamisheni na sio wakoloni. Nyingine zilijengwa hata kabla ya utawala wa kiingereza kuingia sasa utasemaje kuwa walijenga wakoloni? Hizo zote unazozungumzia ni shule zilizokuwa za wamisheni na zilirudishwa kwao baada ya serikali kushindwa kuziendesha. Shule zinajengwa na makanisa kutokana na sadaka za wakristu. Sasa kuanza kuuliza ngapi wamejenga kwa mikono yao ni upuuzi mtupu. Angalia tu ni shule ngapi ziko mikononi mwa madhaehebu tofauti ndipo utajua kuwa sadaka zao zinafanya kazi.
..Endelea kukutaa Ukweli...!!!

Kwa nini tuache hili? Hao wakina Dr. Nchimbi, Dr. Mary Nagu wanaoandamwa kila siku kuwa wametoa vyeti feki ni waislamu? Nyinyi akiguswa muislamu tu mnajificha nyuma ya pazia la udini lakini wanaposakamwa wakina BEN Mkapa, EDWARD Lowasa, huo udini hamuuoni? Mimi sijawahi kusema kuwa Kikwete au Mwinyi ni wadini kwa sababu ya kuteua waislamu. Hiyo ni haki yao na wanaweza kuteua yeyote wamtakaye kama ilivyokuwa kwa Julius na Ben. Tunachokataa ni pale nyinyi mnapokazania kuona mkono wa wakatoliki hata pale ambapo serikali inaongozwa na watu ambao ni waislamu!
..Fundi Hata kama Hukusema wewe..lkn wenzako wanalisema hili....

Hatusemi kila akiguswa muislam udini? mbona kaguswa Msabaha?, akaguswa na Karamagi? Dr. Idrissa? kuna mwislam kasema udini?..Mistakes zao za Kiuongozi huwezi kupata support ya waislam.

Serikali kuongozwa na Mwislam si Hoja kuwa Mkono wa Kanisa hauna nguvu...hao wote uliowataja wamekuwa wanakwenda kwa pressure za Wakristo.

Kama hilo neno lipo clear unashindwa nini kuliweka wazi? Unashindwa nini kuweka wazi haki ambazo waislamu mnanyimwa kikatiba na ambazo mnadai mpewe? Au unaogopa kutaja maana mtaishiwa visingizio?

Amandla......
...Ndugu yangu Katiba hatuna Ugomvi nayo. japo mara kwa mara thru katiba mmekuwa mnakuja Juu. Ugomvi wetu upo ktk Utendaji wa Serikali.

--Suala la Mihadhara ya Kiislam..japo katiba inasema kila mmoja yu huru kufuata na Kutangaza DINI yake, Wakifanya waislam inaonekana ni Tatizo....Wenzetu mnapita majumbani na barabarani kutuuzia Injili...
---Taasis za Kiislam ili zisajiliwe lazima zipitie Bakwata, kinyume chake huwezi sajiliwa...!!! na Taasisi Zingine zinafungiwa.
---Wageni wa Kiislam wanafukuzwa...wageni wenu Haki kutangaza Injili..
---Misaada ya Kiislam inakuwa blocked....yenu HAKI kuingia...

ndio maana nikakwambia HAKI ipo wazi.
 
Safi sana mkuu Mohammed Said , maana tukikuweka kwenye bahasha inayokueleza vilivyo unakuwa mkali kupindukua.
Kwa vyovyote vile unachokuhubiri ni uchochezi, unachochea vurugu za kidini kwa kutumia kalamu na mihadhara, audience yako ikiwa vijana wadogo wa kiislamu.
Kwenye mihadhara yako usisahau kuandika kuwa wasikilizaji karibu wote ni vijana wa madrassa mliowakusanya kutoka sehemu mbalimbali.
Kwa mantiki hiyohiyo sasas wewe tukuiteje ? mwandishi wa historia ya kiislamu?
Maana historia hiyo wengine haituhusu au unaonaje.

LG: Ahsante sana kwa mchango wako. Wala hujakosea hakika mimi ni mwandishi niliyejitolea kuinusuru historia ya Waislam. Wala sioni aibu kwa hilo. Ama hilo la kuchochea vurugu si kweli. Sasa karibu miaka kumi na zaidi nafanya mihadhara ya wazi na Waislam wanakuja nisikiliza hata siku moja sijapata sikia kuwa Waislam baada ya kunisikiliza wamekwendafanya fujo mahali (Mungu apishie mbali). Na si kama ninazungumza na vijana wa madrassa kwani umri wao ni mdogo mno hao tunawahimiza katika kuhifadhi Qur'an. Ninaozungumza nao ni vijana wakubwa wa sekondari na vyuo. Naalikwa kwingi hadi nchi za nje kwa kuwa kuna mantiki kwa hayo nisemayo. Insha Allah nitaweka paper nilizotoa ukumbini kwa faida ya wanaukumbi na wao watanihukumu. Kuwa historia hiyo ya Waislam na harakati za kudai uhuru kuwa wengine haiwahusu hapana ugomvi.Lakini naamini kwa wale inaowahusu vilevile haitakuwa haki kwao kukatazwa kuitukuza.
 
Ama hilo la kuwa mimi ni mkali si kweli. Nawaachia wanaofuatilia huu mnakasha waseme baina yetu ni nani amekuwa na lugha kali?
 
Chuma,
Mbona unapenda uongo? Au kwa vile mwezi mtukufu umaishapita? Hakuna taasisi inayoitwa kanisa. Sema chuo kimepewa kanisa fulani na sasa hivi kinaitwa jina hili!

Huyo mtu wa Nyerere ni nani? Mbona unashindwa kumtaja?

Nitajie sheria ambayo inamzuia muislamu kufanya mhadhara, kupita majumbani na barabarani kuuza Quran. Mbona watu wanachukia na kuwalalamikia Mashahidi wa Jehovah bila kuonekana kama wanachukia ukristu? Siku za mechi kati ya Simba na Yanga, nasikia ukikosea upande wa kukaa utapata taabu sana. Kwa hali hiyo basi hao wapenzi wa mpira watakuwa na haki ya kusema serikali haiwapendi? Nchi yetu ina watu wenye imani tofauti ambao si wote wanafurahia vitendo vya wenye dini tofauti na hata wenye imani kama yao ( kuna wamisheni ambaoi wanaona maombi ya walokole kuwa kero) lakini hii haina maana kuwa serikali inazikandamiza.

Hivi Al Muntazir na Feza ni shule za Bakwata? Niambie kifungu kipi cha sheria kinachosema kuwa taasisi zote za kiislamu ni lazima zipitie Bakwata.

Mbona mashahidi wa Yehova walipigwa marufuku kuhubiri nchini kwa muda mrefu tu? Nao ni waislamu?

Mgeni yeyote anayeonekana nia yake ni kuvuruga amani iliyopo anastahili kufukuzwa bila kujali dini yake.

Misaada ipi ya kiislamu iliyokuwa blocked?

Hapa hakuna mahali ulipoonyesha kuwa waislamu wananyimwa haki zao. Jaribu tena.

Amandla......
 
..Fundi Hata kama Hukusema wewe..lkn wenzako wanalisema hili....

Hatusemi kila akiguswa muislam udini? mbona kaguswa Msabaha?, akaguswa na Karamagi? Dr. Idrissa? kuna mwislam kasema udini?..Mistakes zao za Kiuongozi huwezi kupata support ya waislam.

Serikali kuongozwa na Mwislam si Hoja kuwa Mkono wa Kanisa hauna nguvu...hao wote uliowataja wamekuwa wanakwenda kwa pressure za Wakristo.

Uwe na msimamo. Hauwezi kusema kuwa wakina Msabaha, Karamagi na Idrissa kilichowaponza ni mistakes zao halafu ukageuka hapo hapo na kudai kanisa ndiyo lililowatoa! Huo ndio undumila kuwili tusikopenda. Bahati mbaya ni mtazamo kama huo ndio uliotawala mada hii.

Mkuu FM Chuma ni Mbabaishaji tu ni heri hata Mohamed Said kidoogo
 
LG: Insha Allah nitakiweka kisa kizima cha AMNUT ukumbini. Nimtz kama mtafiti wa nje kapitwa na mengi sana. Sheikh Hussein Juma akikaa Mtaa wa Nyamwezi/Mafia nyumba ya bibi yangu bint Farijallah Mkubwa ilikuwa Mafia/Msimbazi pale inapopita barabara ya Msimbazi hivi sasa. Nakufahamisha haya yote ili ujue kuwa mimi si wakumsikiza mtu kutoka Canada, Augustus Nimtz kuhusu historia ya wazee wangu na jinsi walivyoyaona mambo kwa wakati ule. Sheikh Hussein Juma sijui lini alikuwa kiongozi wa AMNUT. Mwenyekiti wa AMNUT alikuwa Mashado Ramadhani Plantan na Katibu alikuwa Abdulwahid Abdulkarim. Mashado nyumba yake ilikuwa Kirk Street (sasa Lindi)/Nyamwezi na mjomba wangu Shomari Lupindo alikuwa jirani yake. Nadhani umenielewa. Insha Allah nitakiweka kisa cha AMNUT ili ukumbi ufaidike. Napoandika hivi sasa ni kama watu hawa nawaona. Tatizo ulokuwanalo wewe ndilo lilomtatiza Nyerere wakati Abdulwahid Sykes na Dr Klerruu wanaandika historia ya TANU. Mtu kutoka Musoma anataka awaeleze watu wa Dar es Salaam siasa za mji zilikuwaje na yeye mgeni kaingia mjini hata miaka kumi haijafika. Huu ni muhali mkubwa. Nimtz utafiti wake ulizama zaidi katika Tariqa Quadiriyya na alikaa sana kwa Sheikh Mohamed Ramia Bagamoyo. Tasnifu yake ipo Maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Hiyo ina mengi kuliko kitabu.

Mkuu Mohammed Said kuwafahamu hawa masheikh kufahamiana au kuwa ndugu zao haiondoi mashaka yangu juu ya maandiko yako yenye mwelekeo wa udini.
Maandiko kwa ujumla kama nimeyaelewa vema yasema hivi:
1Waislamu ndo waliopigania uhuru zaidi kuliko kundi jingine lolote hasa la Kikristo kabla
ya uhuru kupitia TAA/TANU

2 Baada ya uhuru Nyerere alihakikisha historia ya waIslamu waasisi wa kupigania uhuru
wanapuuzwa katika na kusahauliwa katika maeneo yote

3 Kwamba Mohammed Said anaandika kitabu cha kuonyesha "ukweli" wenyewe na jinsi unavyoonyesha muIslamu alivyo na anavyo kandamizwa nchini Tanzania.

4Kwamba Mohammed Said na nduguze anaowafahamu hata kwa mitaa waliyoishi na wa
Islamu wengine, hawajafaidika na uhuru tuliopata takriban miaka 50 iliyopita

Sasa kwa mtazamaji wa kawaida wa mada hii ya "Ukweli kuhusu waasisi wa TANU na harakati za kupigania uhuru" mimi nimefarijika sana kupata some details kutoka kwa Mohammed Said juu ya yaliyojiri kabla na baada tu ya uhuru.
Nadiriki kusema nimefahamu articles za Mohammed Said tokea magazeti hasa The East African.
Pamoja na ukweli kuwa sikubaliani kabisa na mada za ndugu yangu huyu kwa vile mada hizi zimekaa kuitukuza imani yake kama ndio ikliyopigania uhuru.Na kwamba imani hiyo ikatekelezwa baada ya uhuru na Mwalimu.
Mimi nimeweka maandiko ya watu wawili kukanusha kuwa waTanganyika walipigania uhuru kama mwAfrka kwanza na si kwa imani zao.
Na kupinga ukoloni haukuanza na waislamu , post za nyuma nimeonyesha juhudi za kina Mirambo, Mkwawa , Meli na Sina, na hawa wala hawakuwa waIslamu au waKristo.
Maandiko ya Prof Mhina na Mitz yote Ndugu yangu huyu anayakataa ati kwa vile yeye amekula na kuishi na hao anawaita waasisi wa kiislamu wa uhuru wetu.
Maandiko haya mawili nimeya weka ili kuonyesha kuwa WAISLAMU WALIKATAA UDINI, hata kabla ya uhuru kwa kuikataa AMNUT!!!
Maandiko yapo mengi tu ya kukanusha mwelekeo wa udini wa mwandishi Mohammed Said.
Na vile vile kabla ya uhuru vyama kama TAA vilikuwepo vingi tu mikoani, hivi ni pamoja na vyama vya ushirika vilvyojulikana sana na kuwa na nguvu kubwa.

MS, Mwalimu Nyerere ni jina kubwa kuliko unavyofikiri.
Nina uhakika kuwa leo hii mimi na wewe tusingekuwa tunaelezana haya kama isingekuwa Mwalimu kuondoa matabaka ya kabila , dini na rangi.
Nimeonyesha vile vile kuwa AMNUT, chama cha Kiislamu, kilitaka ubaguzi wa rangi uendelezwe katika Tanganyika.
Sasa unaposema tatizo langu ndilo la Nyerere mtu wa Musoma, na asingeweza kuelewa mambo ya mjini mimi nakushangaa sana.
Bado wa mjini(waIslamu) wakampa Nyerere uenyekiti wa TANU na baadaye Urais wa Tanganyika.
Umjini huo huo ndio ukaviua vyama vya kibaguzi kama AMNUT na vingine vikaishia kupigwa marufuku.
MS you are full of contradictory stories that are nice to read though!!!
 
Mkuu LG na FM nawashukuru sana kwa namna mlivyochangia huu Mjadala nimejifunza mengi sana na Nasema Sidanganyiki na aina yeyote ya kunichonganisha na rafiki/Ndugu zangu waislam ambao wengi nimesoma nao, wengi nafanya nao kazi, wengi tu napanda nao hata kwenye daladala na ninakula nao, kama yeye MS haoni faida ya yote hayo basi ana lake Jambo na ninashukuru uwepo wenu maana At Least mme neutralize Upotoshwaji na uchochezi
 
1. Nyerere hakutaka kumuachia Mzee Mwinyi kwa kupenda. alitaka sana Mtu wake awe Rais baada yake. lkn wakati ule katiba ilitaka Rais atoke ZNZ, na so far wakati Ule Nyerere Nchi ilishamshinda. hali mbaya ya uchumi ilibidi lazima aachie Ngazi...Kipande hiki naachia wanahistoria kufanya utafiti kilichojiri wakati wa Mkutano wa CC wa CCM wakati Ule...Ilikuwa ni mara ya pili Nyerere kulia Ndani ya Kikao....!!!

2. Fundi..nakutajia CHUO cha BANK- Iringa amepewa nani?

3. Hata Hizo shule za kanisa zilizoporwa na Nyerere Kanisa hawakujenga. Shule Zilijengwa na Mkoloni zikapewa kanisha kuziendesha. as moja ya Ajenga ya Mkoloni kutumia DINI kutawala...Local Wakristo fanyeni hesabu shule ngapi mmejenga kwa Mikono yenu?...hapa Mkapa akawapa tena shule ya Magamba...muifanye Chuo Kikuuu...Shule ya Mazengo---na Chuo cha Nyegezi...!!!
.....
4. Hio idadi ulotaja, sikatai, lkn wenzetu kwa kuwepo wao wachache tu Mmefanya Kikwete aitwe Mdini. mlitaka hizo nafasi zote ziende kwenu....nafasi ya BOSS wa TISS ilikuwa na mjadala mrefu hapa JF. utafute uuone. So far hatuhitaji eti waislam wangapi wamechaguliwa, tusipenda ni pale mwislam hata mmoja akichaguliwa kuongozo Idara au Shirika wenzetu mnakuja juu.,mmejizoesha Vibaya kuona Utawala wa Serikali ni Mali yenu....
.....JK teuzi zote anazofanya balaa linakuja pale ambapo kawateua waislam wawili/watatu wenzetu mnaanza kulipuka. ipo Mijadala mingi hapa JF, ambayo kila teuzi ya JK ambayo ndani yake yuko mwislam alau mmoja, mmekuja juu...teuzi zingine hata huwezi kukuta mijadala hapa JF, wala watu kuhoji CV zao...na zikihojiwa tu, mnaanza kutoa Pongezi...Tuache hii kitu.

5. kaka neno HAKI lipo so clear. sio Upendeleo.
Chuma,
Usituletee uwongo hapa. Hakuna mahali katiba inasema kuwa rais anayefuata (hata wakati ule) lazima atoke Zanzibar. Kilichotokea, kama hujui, ni kwamba Mwalimu alikuwa na matarajio ya kupendekezwa kwa Salim Ahmed Salim kurithi nafasi yake. Lakini kosa alilofanya Mwalimu na akaja kushtukia baadaye, ni kwamba Wazanzibari hawakumkubali Salim kwa sababu aliwahi kuwa Hizbu. Wakati huo mimi sijui Hizbu ni mdudu gani. Na Mwalimu alishaelewana na Mwinyi kwamba Mwinyi ataendelea kuwa rais wa Zanzibar. Jina la Salim lilipotajwa pale Dodoma Wazanzibari wakaja juu kuwa hawawezi kumwuunga mkono kwa kuwa aliwahi kuwa Hizbu, na kwamba rais wa Zanzibar, Ali Hassan Mwinyi anafaa kabisa kuwa rais. Mwalimu alipatwa butwaa, akaweka miwani yake mezani. Alikuwa na choice mbili. Kuahirisha kikao au kukubali matakwa ya Wazanzibari. It had nothing to do with constitution. Na kuhusu shule za makanisa ukweli ni kwamba zilijengwa na makanisa yenyewe na wala si wakoloni. Wakoloni walijenga zao na makanisa yalijenga zao. Huo ni ukweli usiopingika. Unapopigania haki hakikisha kuwa hutumii uwongo.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom