Son of Alaska
JF-Expert Member
- Jun 2, 2008
- 2,812
- 1,061
watoto wa mjini bana,wakibahatisha kuukimbia umande,basi inakuwa taabu-eti,"pepo mbaya naona kakatiza hapa"
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ungekuwa credible kama ungesema haya mapema. Pepo mbaya aliishaingia hapa. Na ataambiwa kuwa tumemstukia bila kificho.
Amandla.......
Hee! Fundi sasa unatukana kila mtu,mimi,Mohammed,Yaya.Hata wenzako akina Lole wakikupoza husikii tena.Mimi sikupendelea iwe hivyo lakini najuwa umeuona huu mjadala wa kutetea kudhulumiwa kwa waislamu sasa umekuwa moto kwako.Nilikushauri mapema kaa kimya.Another fool! Jazba ipi ya KIDINI? Unataka kudai kuwa nawaona wapuuzi kwa sababu ni waislamu? Upuuzi nao una dini? Basi, iko kazi.
Amandla......
Wanaukumbi tutulize na tuendeleze mjadala kwa taratibu hapana haja ya kuparurana. Haya ni mawazo na ghitilafu ni jambo la kawaida sana. Ingekuwa sote tunakubaliana kwa kilajambo dunia ingechosha na kuchusha. Hebu msomeni Mzee Mshume. Huyu Mzee akikaa Mtaa wa Tandamiti karibu na Mtaa wa Gogo ilipokuwa moja ya nyumba za baba zangu. Nyumba yetu ilikuwa Gogo namba sita na nyumba ya mwisho mtaani ilikuwa nyumba ya mama yake Abdu Mgunya mmoja wa marafiki zangu utotoni. Hapa kwao ndipo ilipokuwa club ya Kilwa Jazz katika miaka ya 1960. Nje ya nyumba hii pakichezwa bao na ni hapo ndipo nilpomjulia Abdallah Kassim Hanga. Akija pale kucheza bao takriban kila siku. Sasa turudi kwa Mzee Mshume Kiyate. Someni kwa furaha:
Napenda nianze dibaji ya kitabu hiki kwa kisa nilichoelezwa na
mmoja wa wazalendo wa nchi yetu – Ahmed Rashad Ali – kutokana
na kisa alichohadithiwa na Mwalimu Julius Nyerere mwenyewe.
Siku hiyo , Ahmed Rashad alikuwa pamoja na Dossa Aziz na Lucy
Lameck. Ilikuwa mwaka wa 1965 siku ile Ian Smith alipojitangazia
uhuru. Ahmed Rashad wakati ule alikuwa Katibu Mkuu Msaidizi
Idara ya Habari. Walimkuta Mwalimu Nyerere nyumbani kwake
Msasani anaandika. Ahmed Rashad anasema katika kutafakari mambo
yaliyokuwa yakiendelea Rhodesia Mwalimu Nyerere aliwahakikishia
kuwa Uingereza haitofanya lolote dhidi ya Ian Smith kwa kujitangazia
uhuru wa maguvu. Ahmed Rashad anasema Mwalimu Nyerere neno
alilotumia ni kuwa hawa ni mtu na mjomba wake. Inawezekana
labda Mwalimu Nyerere kwa kukumbuka historia ya kudai uhuru wa
Tanganyika aliwajua vyema Waingereza na fikra zao na kwa ajili hiyo
akakileta kisa hicho cha TANU. Mwalimu Julius Nyerere alikiita kisa
hicho ‘the TANU spirit' – yaani moyo wa TANU – vile ulivyokuwa
wakati wa harakati za kudai uhuru. Mwalimu Nyerere alisema kuwa
siku moja wakati wa kudai uhuru alikuwa anatoka nyumbani kwake
Magomeni Majumba Sita kwa miguu kuelekea Kariakoo ili kupata
mahitaji yake. Mwalimu Julius Nyerere alisema kuwa katika safari
hiyo mfukoni mwake alikuwa hana hata senti moja.
Akiwa njiani karibu na sehemu inayoitwa Mwembe Togwa,
Mwalimu alikutana na Mzee Mshume Kiyate. Mzee Mshume alikuwa
mfanyabiashara wa samaki katika soko la Kariakoo. Mzee Mshume
alikuwa mzee aliyeheshimika sana mjini Dar es Salaam na alikuwa
mmoja wa wazee katika Baraza la Wazee wa TANU. Mwalimu
Julius Nyerere akamfahamisha Mzee huyo kuwa anakwenda sokoni
Kariakoo lakini hakuwa na fedha za kununulia mahitaji yake. Mzee
Mshume Kiyate aliingiza mkono katika koti lake, akatoa shilingi mia
mbili na kumpa Mwalimu Julius Nyerere. Ukitaka kujua thamani ya
fedha hiyo kwa wakati ule, naitoshe kujua kwamba ilimgharimu mtu
shilingi mia tano tu kujenga nyumba ya vyumba sita katika eneo la
Kariakoo.
Kutokana na hali hii Mzee Mshume aliona itakuwa ni kumtwisha
Mwalimu Julius Nyerere mzigo ikiwa atakuwa anashughulika na
kuwatafutia wanawe chakula na wakati huohuo akiwa na jukumu la
kufanya kazi za TANU. Ndipo Mzee Mshume alipojitolea kuihudumia
nyumba ya Mwalimu Julius Nyerere kwa chakula. Alifanya hivyo hadi
uhuru ulipopatikana. Baada ya uhuru Mwalimu Nyerere alimwomba
Mzee Mshume aache kufanya hivyo lakini alikataa. Badala yake
akamtafadhalisha Mwalimu Nyerere aendelee kupokea chakula chake
na kile ambacho kinatolewa na serikali kwake yeye kama mkuu wa
nchi, alimwomba Mwalimu awakirimu wageni wake. Mzee Mshume
Kiyate ni mfano wa aina ya viongozi wa TANU waliokuwepo wakati
wa kudai uhuru. Mzee Mshume alifanya mengi katika kudai uhuru na
hata baada yake.
Kisa hiki kwa mara ya kwanza kabisa kilihadithiwa hadharani
na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, marehemu Ditopile
Mzuzuri Mkiwaona, kada wa Chama Cha Mapinduzi. Ditopile
alikieleza kisa hiki kama alivyokieleza Mwalimu Nyerere kwa
Ahmed Rashad kwa nia ile ile ya kuonyesha moyo wa TANU. Kwa
bahati mbaya waandishi wa magazeti wakapotosha kisa kizima.
Badala ya kutoa umuhimu kwa moyo wa ukarimu wa Mzee Mshume
na kumueleza kama mzalendo aliyejitolea katika kupigania uhuru,
magazeti yakageuza maneno ya Ditopile kuwa masimango kwa
Mwalimu Nyerere, yaani alikuwa akilishwa chakula bure. Kwa ajili
hii nafasi ambayo ingeliweza kutumiwa ili kueleza umuhimu wa Mzee
Mshume na historia ya TANU ikapotezwa.
Baada ya maasi ya wanajeshi wa KAR tarehe 20 Januari 1964
kuzimwa na Jeshi la Kiingereza, TANU ilifanya mkutano mkubwa sana
katika viwanja vya Jangwani Dar es Salaam. Mzee Mshume kwa niaba
ya wazee wa TANU alipanda jukwaani na kumvisha Nyerere kilemba
kama ishara ya kumuunga mkono. Picha ya mzee Mshume akimvisha
Nyerere kilemba ilichapishwa katika magazeti mengi. Halikadhalika,
picha nyingine mashuhuri ya Mzee Mshume na Mwalimu Nyerere ni
ile iliyopigwa Novemba 1962 wakati wa Uchaguzi Mkuu.
Picha hiyo inamuonyesha Mzee Mshume akiwa amevaa koti,
kanzu na kofia na huku amemshika Mwalimu Nyerere mkono
akimsindikiza kupiga kura. Magazeti ya Chama na Serikali – Uhuru
na Daily News yamekuwa yakiitumia picha hii kila baada ya miaka
mitano katika uchaguzi wa rais kama njia ya kuwahamasisha watu
kupiga kura na kumchagua Mwalimu Julius Nyerere. Kwa bahati
mbaya picha ile siku zote hutoka bila maelezo na kwa hiyo wengi
hawafahamu yule mzee aliyefuatana na Mwalimu Julius Nyerere
kuwa ni nani. Kadhalika, si wengi wanaoufahamu mchango wa Mzee
Mshume Kiyate katika kupigania uhuru wa Tanganyika kwa sababu
Mwaka 1995 Jiji lilipoamua kubadilisha jina la mtaa aliokuwa akiishi
Mshume Kiyate – yaani Mtaa wa Tandamti ili uitwe Mtaa wa Mshume
Kiyate kama ishara ya kumuenzi na kuthamini mchango wake katika
kupinga ukoloni, baadhi ya magazeti yalipinga kitendo hicho. Je, ni
nani wa kulaumiwa endapo wananchi wenyewe hawajui historia ya
ukombozi wa nchi yao?
SOA: Usitusimange ndugu yetu sisi tunaasili ya kusoma hata kabla Mjerumani na Muingereza hajatia mguu Tanganyika. Una khabari kuwa Krapf alipata mshangao mkubwa alipomkuta Chifu Kimweri wa Vuga yuko katika mahakama yake akiandika na kusoma hati za Kiarabu? Chifu Kimweri na wanawe wote walikuwa wanajua kusoma na kuandika. Huna khabari Chifu Mkwawa alikuwa akiandikiana barua na Sultan wa Zanzibar kwa hati za Kiarabu? Tena alikuwa hampi mtu uongozi katika himaya yake hadi amesilimu na kuwa Muislam? Mmoja wa makamanda wake akiitwa Yusuf.
Babu yangu mzaa mama Sheikh Mohamed Mvamila alikuwa maisha yake yote hadi anaondoka duniani akiandika barua kwa irabu za Kiarabu na alisomesha watu wengi sana katika madrasa yake. Mama zangu wote wamejua kusoma na kuandika bila hata kuingia darasa kama wengi wanavyolijua darasa. Na mimi alianza kunifundisha kusoma kama alivyofundishwa yeye na hayati Sheikh. Babu yangu ni Mzaramo wa Mkamba lakini baada ya Vita Kuu ya Kwanza alihamia Musoma akiwa kijana mdogo sana. Alizaa watoto wanne wote hapo Musoma na alifundisha dini huko hadi Mungu alivyomuhitimisha. Hilo suala la kuogopa umande kwetu halikuwapo. Naweka kipande hiki hapo chini kwa faida ya wanaukumbi:
Missionaries became envious of the level of civilisation and literacy advancement achieved by Muslims through the Arabic script taught in the ‘madras' system of education not only at the coast in Zanzibar, Bagamoyo, Kilwa or Mikindani but also in far way places in the interior, like Usambaa, Tabora Kigoma, Ujiji were Islam was firmly established. Missionaries in collaboration with the colonial government initiated plans to subvert whatever progress Muslims had made. The first step taken by the British when they took over the country from Germany after the First World War was to abrogate the Arabic script, which was in use for many years in favour of the Roman script. By a mere stroke of a pen people who were educated were overnight reduced to illiterates. These instant, British and missionaries made illiterates were the poets of yesterday and the ‘ulamaa' who had intellectually held their own against missionaries defeating them in debates with ease. The vacuum created by the abrogation of Muslim education system was filled with missionary education with the British colonial government as the overseer. Knowledge was now disseminated from the class room with missionaries as teachers instead of the ‘maalim' in the ‘madras'. Tanganyika was now open for evangelisation.
Mnaolalamika kuwa Fundi Mchundo ametumia matusi kumuita Ami na Ya ya kuwa wapuuzi, mlikuwa wapi huyo huyo Ami alipomuita Mkandara mpuuzi? Huyo pepo mbaya mnamuona sasa wakati mmegeuziwa kibao? Hao jamaa wawili ni wapuuzi, fools na kama nilivyosema awali, kunguni ( na hapa nilyemtukana ni kunguni) katika jamii yetu. Unafik haupendezi. Huyu Mohamed Said asiyeacha kujiita muungwana alikuwa wapi wakati huyo mpuuzi Ami akimuita Mkandara mpuuzi, kwa sababu tu ametofautiana nae? Badala yake, aanamsifia:MKANDARA
Huyu ndiye mpuuzi kabisa katika michango yake.Yeye anaonekana ana wazazi waislamu,na anajiita muislamu.Hataki kuudhi upande wowote kati ya hizo.
Usomi wake wote,kama alivyo Fundi Mchundo hataki Nyerere abebeshwe lawama za madhambi yake.Vile vile madhambi ya Christian lobyy anataka lazima lawama zake ziwaendee waislamu.
Akina Mwinyi,Kawawa na viongozi wengine waislamu walikuwa wakitumiwa na kushinikizwa,yale waliyoyafanya leo yanawatukanisha na kututukanishwa sote waislamu.Haya ni moja ya mafanikio ya wakristo kwa waislamu Tanzania,kuwafanya wasijiamini.Hata wakipewa nafasi huona ni fadhila tu,hivyo lazima wafanye kama wanavyoambiwa
Wakati huo huo leo akitokea kiongozi serikalini akitaka kitu cha halali kifanyike chenye mwelekeo wa kiislamu,basi huzushiwa mengi na kurudiwa katiba ili kishindikane kufanyika.Akiondoka tuambiwe kwa mfano "Nini kilimfanya Kikwete na Shein wote waislamu washindwe kuanzisha hiyo mahakama ya kadhi na kujiunga na OIC"
Hapo watasifiwa kuwa ni kwa vile wao ni wazalendo na walijuwa hivi vitu ni vya kibaguzi!.
Unafik kwa watu wazima haupendezi. Hawa kunguni niliacha kuwajibu lakini naona hawataki kujifunza. Watu ambao hawaogopi kusema uongo wazi wazi hawastahili heshima ya kujadiliana nao!Ami: Ahsante sana kwa uchambuzi wako. Mungu atakulipa Insha Allah.
Kama Mkristo ninachokumbuka ni kuwa kuna wakati hatukubaguana kidini kwa kuangalia majina kwani hatukujali hata majina tuliyowapa watoto wetu wa kuzaa. Nyakati hizo haikuwa taabu kwenye familia ya Kikristo kukuta watoto wanapewa majina kama Abdalla, Shakila, Hamisi, Juma, Mwajuma na mengine mengi tu ya Kiislamu na hasa kwa wale walioshi sehemu za pwani kama Dar es Salaam. Pia Wakristo wengi tu hawakuona taabu kununua nguo kama kanzu, vikoi, baragashia, buibui na katu watu hawakubaguana kwenye sherehe kama za vifo, harusi, Iddi, Krismasi na Pasaka.
Huo ulikuwa ni wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere na watu walitanguliza utaifa kwanza lakini kwenye miaka ya sabini akatokea mdudu mbaya kwa umbo la mkufunzi kutoka nchi ya Pakistani. Hawa akina Mohamed Said ni matokeo ya mbegu ya chuki iliyopandikizwa na Mpakistani huyo miongoni mwa vijana hawa wakati huo baadhi yao wakiwa tayari chuo kikuu. Kwa sababu tulikuwa na utawala thabiti mikakati hii ya kutaka kutugawa kidini na kupandikiza mbegu ya chuki iliweza kuzimwa bila kuleta madhara lakini mwaka 1985 akaingia Mzee Rukhsa and all hell broke loose !
Mohamed Said anajua hawangeweza kufanikiwa kwa namna yoyote ile Mwalimu alipokuwa hai kwani Watanzania kwa ujumla wao bila kujali dini au rangi waliutambua na kuuenzi mchango wake. Siyo tu aliongoza harakati za kupigania uhuru bali juhudi zake zilizofuatia za kupigania umoja na usawa wa Watanzania bila kujali dini, rangi,jinsia au mali. Uthibitisho ulionekana hata kwa kipofu jinsi Watanzania walivyomlilia siku mwili wake ulipopokewa uwanja wa ndege kutoka Ulaya hadi anazikwa kijijini kwake Butiama.
Najua Mohamed Said na kundi lake wamesubiri hadi watu wamesahau machungu waliyokuwa nayo wananchi kwa kupotelewa na jemadari wao na Baba wa Taifa ili waanze hizi chokochoko zao za kebehi na dharau zao. Bahati mbaya ni kuwa wingu la udini limewafunika macho na kuwaziba masikio hadi wanashindwa kutambua hatari itakaikabili Taifa wakiendelea na hizi hadithi zao za hatari. Lakini baya zaidi ni ukosefu wa utawala ulio thabiti na makini unaoruhusu wenda wazimu kama akina Mohamed wasiojua hata kile wanachokitafuta kuchezea amani na umoja wa Watanzania. Pamoja na yote nina matummaini hawatafanikiwa.
Usiwe na wasi wasi Mkuu Mwalimu aliweza ku-connect na hata waliokuletea Uislamu intellectually.Mwalimu hakuchagua rafiki kutokana na dini bali aliangalia sana msimamo wa usawa wa kibinadamu.1966 ni baada ya uhuru, tuwekee picha kabla ya uhuru, kama hutoona vibarakashia vitupu