Ukweli kuhusu Wakatoliki kutokuabudu sanamu zilizopo makanisani

Ukweli kuhusu Wakatoliki kutokuabudu sanamu zilizopo makanisani

Umeelewa alichokiandika..??
Hakuna cha maan zaidi ya kujichanganya.Roman Catholic limejaza sanamu kanisani na wanazisujudia wazi bila kificho na zingine mnatembeza majumbani na mitaani halafu manleta hoja dhaifu eti hatuziabudu! enyi wanafiki wakubwa kusujudia sanamu sio kuziabudu?
 
Kaka kuna shida kubwa ya Elimu ya Dini ya Ukatoliki kwa wasio wakatoliki,
Huwezi kuamini hili-hakuna Dhehebu linalofata misingi ya ibada iliyomo ndani ya Biblia kama Wakatoliki nasema tena Huwezi amini hilo

Maada ya issue ya Sanamu imeongelewa sana humu,
Kwa kifupi Wakatoliki hawaabudu sanamu, na kama umewahi kumuona Mkatoliki anaabudu na kuitumikia sanamu basi huyo amekufuru na amefanya shiriki kubwa kwa Mungu wetu mwenye wivu,

Kuabudu sanamu ni kuitumainia kuwa inaweza kufanya lolote unaloliomba, hivyo unaitolea Sadaka na kuitumainia, je kweli kazi ya mikono ya binadamu inaweza kutoa msaada, haisikii, haioni, haisemi nk

Sanamu ziko kwenye makanisa ya Kikatoliki kama kumbukumbu ya uwepo wa watakatifu na wafia dini mbalimbali, hivyo ni sanamu za kuangalia na kukumbuka uwepo wao (Bikira Maria, Yesu, Joseph nk )na Sanamu zote zilizopo ni za watu waliowahi kuwepo hapa Duniani, HAKUNA KANISA LA KIKATOLIKI LENYE SANAMU YA MUNGU BABA, kwa sababu hakuna aliyemuona

Stay blessed na uwe na Amani, hakuna muabudu sanamu ndani ya Ukatoliki
Saf sana kwa ufafanuz mzuri
 
Hakuna cha maan zaidi ya kujichanganya.Roman Catholic limejaza sanamu kanisani na wanazisujudia wazi bila kificho na zingine mnatembeza majumbani na mitaani halafu manleta hoja dhaifu eti hatuziabudu! enyi wanafiki wakubwa kusujudia sanamu sio kuziabudu?
Ok! Sawa..
 
Nilikuwa naomba uongozi wa jf watuwekee kitufe cha ku translate. Maana hii lugha ya malkia wengine ni shida kidogo. Mada kama hii ina post zaidi ya miambili na views kibao inaonekana ni nzuri ila lugha iliyotumika ni ngumu kwa baadhi yetu.
 
Sijui nani kawaambia katoliki ndio kanisa aliloanzisha Yesu?!! Hata andiko husika hamkulielewa,mkikomaa na mafunisho ya mwaka A,B,C ya kanisa kila leo. Ibada ya pili ya mwaka C wa kanisa mwaka 2026 ni sawa na ibada ya pili ya mwaka C wa kanisa ya mwaka 2017. Neno la kwanza na la pili litakuwa lile lile. Bado katoliki kuna vingi sana vya kuhoji.
La msingi toeni majibu,mamlaka ya kutengeneza sanamu za bikira maria nani kawapa?! Kuzibusu sanamu nini maana yake?!
 
Kujipa moyo tu. Haina maana kbs kusema ipo lakini haimaanishi kuabudiwa. Sasa ya nin mle ndani?!! Kubusu,kupiga ishara ya msalaba huku unaiangalia sanamu au picha nini maana yeke km sio kuabudu?! Heshima,mazoea,taratibu?!!
Mambo ya imani yana mengi ya kuhoji ila majibu yapo kwenye biblia
Vipi kuhusu alama za misalaba au nyota na mwezi katika kanisa na misikiti? Je waelweza kuhitimisha kwamba hizo ni sanamu za kuabudiwa?
 
hakuna dhehebu nnalolichukia kama waroma...na hayo madude wanayaabudu na kwenda kinyume na amri za Mungu.
imeandikwa usijifanyie sanamu ya kuchonga wala kitu chochote kilicho mfano mbinguni,baharini,nchi kavu etc...na kukiabudu.
lakini hawa ndo kwanza ukiingia unakuta kila kona wamechonga masanamu ya maria mtakatifu...masanamu ya yesu..hivi mliwah kuwaona? nyie ndo kwanza mmekazana na rozari mnabusu na zina sanamu ya yesu..ni wazima nyie?
mnachefua.
Mbona mafundisho ya Roma ni Yale yanayofundishwa katika madhehebu mengine. Roma wanafundisha mapendo kama Amri kuu ya bw. wetu Yesu Kristu..sijawahi kusikia wanafundisha watu kinyume na mapenzi ya Mungu wala kufundisha waamini wake kukebehi ama kudharau dhehebu wala dini nyingine yoyote. Binafsi nafikiri ni chuki tu vinawasukuma kulisakama kanisa pendwa la popote ulimwenguni, Ila nafikiri kwa uimara wa kanisa hili hapa duniani na kwa msaada wa M/Mungu kamwe hamtafanikiwa kwa lolote lile ovu
 
Sijui nani kawaambia katoliki ndio kanisa aliloanzisha Yesu?!! Hata andiko husika hamkulielewa,mkikomaa na mafunisho ya mwaka A,B,C ya kanisa kila leo. Ibada ya pili ya mwaka C wa kanisa mwaka 2026 ni sawa na ibada ya pili ya mwaka C wa kanisa ya mwaka 2017. Neno la kwanza na la pili litakuwa lile lile. Bado katoliki kuna vingi sana vya kuhoji.
La msingi toeni majibu,mamlaka ya kutengeneza sanamu za bikira maria nani kawapa?! Kuzibusu sanamu nini maana yake?!

Mimi sioni shida yoyote ya kufanana kwa mafundisho ilimradi ni maandiko matakatifu. Wanadamu tuna tabia ya kusahau hivyo kanisa linachukua jukumu lake kuwaonya na kuwakumbusha kuhusu maagizo ya M/ Mungu.
 
Kweli kabisa,umesema wewe. Vipi kuhusu biblia inavyosema??
 
Mimi ni mkatoliki nisiyeunga mkono uwepo wa masanamu kanisani... Na ijumaa kuu huwa sijiangaishi kubusu msalaba. Sisali rozari kwakuwa naamini bikira Maria hawezi kusikia sala zangu...

Ntabakia mkatoliki kwa msimamo wangu.
Ni kwa sababu ya kutoelewa vitu viwili
i. Sanamu
ii. Kuabudu
Pia haujui kila kitu cha kiimani huendana na dhamira ya kukitenda. Sikulaumu, ila nakushauri ufuate mafundisho ya Wakatukumeni
 
Nilikuwa naomba uongozi wa jf watuwekee kitufe cha ku translate. Maana hii lugha ya malkia wengine ni shida kidogo. Mada kama hii ina post zaidi ya miambili na views kibao inaonekana ni nzuri ila lugha iliyotumika ni ngumu kwa baadhi yetu.
ikopi ukaitafsili katika Google ili upate madini mkuu.
 
Mimi ni mkatoliki nisiyeunga mkono uwepo wa masanamu kanisani... Na ijumaa kuu huwa sijiangaishi kubusu msalaba. Sisali rozari kwakuwa naamini bikira Maria hawezi kusikia sala zangu...

Ntabakia mkatoliki kwa msimamo wangu.
Ijumaa Kuu hutumika kwa maadhimisho ya mambo mengi sana ambayo wakristo wanayafanya katika siku hii pamoja na kufunga na kubusu msalaba ila Ijumaa Kuu hii tutakaloliangalia ni kuhusu msalaba kitendo cha kuubusu ni kuuabudu au kuuheshimu.

Ili tuweze kuelewa vizuri lazima tujue ibada ni nini na kuna mambo gani yanahitajika katika ibada na kinachotusumbua wengi ni kushindwa kutofautisha kati ya kuheshimu na kuabudu.

Kwa maana hiyo maana ya Ibada ni utaratibu uliowekwa na kundi la watu kwa ajili ya kufanya sala na maombi kwa ajili ya kuabudu mbele ya yule anayeabudiwa na watu husika na huyo ndiye Mungu wa kweli mbele yao.

Utashangaa nikisema kuwa Mungu huyo anaweza kuwa jua, jiwe, mti au chochote kile kilichoandaliwa na watu husika jambo kubwa nikuhakikisha shida zao zinapokelewa na kufanyiwa kazi na kujibiwa kama walivyotarajia.

Kwa hiyo penye ibada pana mungu yaani kile kinachoabudiwa na ili ikamilike na kuitwa ibada kuna mambo saba yanahitajika navyo ni Kuheshimu, kutukuza, kuabudu, kutoa sadaka, kusujudu, kusifu na kushukuru.

Kubusu

Neno Kubusu lina maana nyingi tofauti kutokana na kila Taifa likiwa na tafsiri yake lakini kuabudu ni ishara au dalili ya upendo, Heshima na Furaha.

Biblia inatuambia kuwa hata wakristo wameagizwa wasalimiane kwa busu takatifu (2 Wakorintho 13:12) na tunaona viongozi mbalimbali wanapokutana wanakumbatiana na kubusiana kadhalika hata wazazi huwabusu watoto wao wachanga ili kuwafurahisha.

Kuabudu

Neno kuabudu maana yake kuwa mtu au watu wanakisujudia au kukitukuza kitu fulani na kupeleka shida zao na kwa madai kuwa watapona au kupata faraja kutoka pale wanapozipeleka shida zao kwa yule wanayemuabudu na kutegemea kuwa matatizo yao yataisha kupitia kwake.

Mfano kila mmoja duniani anamuabudu yule anayedhani ni Mungu na Mitume wake kutokana na imani za kila mtu kwa kupelekea shida zake kwa njia mbalimbali na kujua yeye pekee ndiye atakayemsaidia katika matatizo yake.

Kuheshimu
Heshima inayozungumzwa katika mada hii ni ile ya kujishusha na kumwinua Mungu. si heshima ya juu juu tu, bali ni heshima yaenye 'ADHAMA'. Ndani yake kuna adhimisho. Adhama maana yake ni ukuu na enzi. Tunapomwadhimisha Mungu, tunaweka juu yake heshima, ukuu, mamlaka na utukufu kuwa ni yeye tu anayestahili kuwa navyo. (1 Nyakati 16:27, Mithali 8:18).

Je Kubusu Msalaba ni Ibada ya sanamu?

Inaonesha kuwa Mungu ndiye aliyekataza ibada ya sanamu na wakati huo huo Mungu alimuagiza Musa atengeneze sanamu ya nyoka wa shaba kule jangwani.

"Bwana akamwambia Musa, jifanyie nyoka wa shaba ukaiweke juu ya mti, na itakuwa kila mtu aliyeumwa, aitazamapo ataishi. Musa akafanya nyoka ya shaba, akaiweka juu ya mti. (Hesabu 21: 4-9)

Baada ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo inawafanya wakristo kujua kuwa Yesu ndiye nyoka wao wa shaba. Na ukimtazama yesu juu ya mti wa msalaba, utapona majeraha yako yote uliyotiwa na shetani. Yeye anakualika akisema;

"Niangalie mimi mkaokolewe, enyi nchi zote za dunia, maana mimi ni Mungu, hapana mwingine." (Isaya 45:22).

Pia Mtume Paulo naye anawaambia wakolosai kuwa,

"Basi vivifisheni viungo vyenu vilivyo katika nchi, uuasharati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu." (Wakolosai 3:5).

Kumbe, matendo maovu ndiyo namna ya kisasa ya ibada ya sanamu. Ni bure kuendelea kufikiri kuwa kubusu msalaba ni kuabudu sanamu. Wakristo lazima waelewe kinachosema.
Siku zote maadui wa ukristo wamekuwa wakijaribu kupotosha imani ya asili na kuleta mafundisho yenye kutia mashaka mioyoni mwa waumini. Wasipotambua hayo, watakuwa watu wa kuyumbishwa siku zote katika imani.

Ibada ya sanamu
Tangu mwanzo Mungu alichukia sana ibada ya sanamu. wapinzani wa imani ya makanisa ya Kikatoliki na Kiapotoliki wanaitumia sababu hii kupinga taswira ya msalaba.

Amri ya pili inasema hivi.

'Usijifanyie sanamu ya kuchonga wala mfano wa kitu chochote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini majani chini ya dunia, usivisujudie wala kuvitumikia....'(Kutoka 20:4-5).

Neno la mwisho

Tumekwishaona jinsi msalaba ulivyo mti wa muhimu katika maisha ya wakristo, mengi tumezungumza juu ya mti huo, wengine wamefundisha juu ya kufanya ishara ya msalaba katika vipaji vya nyuso zao. Hiyo yote ni kutaka kuonesha kuwa msalaba siyo kitu cha kawaida.

Kama ni mfuasi wa Kristo unacho cha kujivunia nao ni msalaba wa Yesu....! Waambie watu juu ya mti huo uzaao matunda yake kila siku usiojua kiangazi wala masika hata usiku wala mchanani wa ajabu sana unaookoa siku zote.

Basi wanapoutazama au kuubusu msalaba si kama wanauabudu bali ni kuonesha heshima na upendo wao juu ya mti ambao ni kielelezo cha mti uliotumika kuwakomboa watu wengi.

Kwa maana hiyo tulichojifunza kutoka katika makala hii kuwa wakristo hawaiabudu sanamu ya Yesu ila wanaiheshimu kwa kuwa ndani ya mioyo yao wanajua hakika ya kuwa hawaiabudu ile sanamu bali sanamu ile inabaki kuwa kielelezo tu.

Wao wanamwabudu Mungu tu na Yesu kristo mwana pekee wa mungu na Roho Mtakatifu katika umoja usiogawanyika wenye nafsi tatu.

Wakristo waliojaaliwa kuijua siri ya thamani iliyomo katika msalaba, waoneshe kwa vitendo heshima na upendo wao kwa kuubusu ni tendo la furaha, upendo na uondoe tashwishwi, hofu kwa kuwa tendo hilo ni safi tena ni takatifu na lenye heshima mbele za Mungu.

MUNGU AKUTIE NGUVU ILI USIMAME KATIKA IMANI ILE ILE.
 
Huu ndio ukweli ambao Roman imeamua kuuachia katika kipindi hichi cha mfungo wa kwalezima

And the LORD said to Moses, "Make a fiery serpent, and set it on a pole; and every one who is bitten, when he sees it, shall live." So Moses made a bronze serpent...

Numbers 21:8-9
Recently we received an 80-page booklet entitled "What's Behind The New World Order?" It can be traced back to the writings of Ellen G. White, foundress of the Seventh Day Adventist Church. According to this booklet, the Catholic Church is behind the New World Order. The booklet claims that this is true, since the Church is the beast of Revelation (Rev. 17). It attempts to prove this claim by exposing the "marks of the beast." Due to limited space, only one charge will be considered. This is a common charge used against the Catholic Church.

According to this booklet, one "mark of the beast" is the alteration of God's Commandments. The booklet claims that the Catholic Church dropped the "Second Commandment" which forbids "graven images", i.e. statues. Allegedly the Catholic Church condones statue worship.

Now one version of the Ten Commandments can be found in the fifth chapter of the Book of Deuteronomy (also Exodus 20). Comparing Deut. 5:6-21 in a Catholic Bible with that found in a Protestant Bible reveals no essential differences. A few words may differ but that is due to differing translations. The major difference is not content but how Catholics and Protestants traditionally divide up and number these Commandments. Unfortunately the Bible lumps the Ten Commandments all together without division or numbering. (The verse numbers are no help since they were added by Bible scholars many centuries after Christ.)

Traditionally Catholics consider Deut. 5:6-10 as the First Commandment, verse 11 as the Second Commandment, verses 12-15 as the Third Commandment and so on. Verse 21 is split up into the Ninth and Tenth Commandments - distinguishing the desire (lust) to commit adultery from the desire (greed) to steal. This division scheme was advocated by St. Augustine in his writings on Exodus. Traditionally Protestants consider Deut. 5:6-7 as the First Commandment, verses 8-10 as the Second Commandment, verse 11 as the Third Commandment and so on. Verse 21 is kept together as the Tenth Commandment.

According to the RSV Bible and Catholic Tradition, the First Commandment is:
(6)I am the LORD your God,...(7)You shall have no other gods before me. (8)You shall not make for yourself a graven image, or any likeness of anything that is in heaven above, or that is in the earth beneath, or that is in the water under the earth; (9)you shall not bow down to them or serve them; for I the Lord your God am a jealous God, visiting the iniquity of the fathers upon the children to the third and fourth generation of those who hate me, (10)but showing steadfast love to thousands of those who love me and keep my commandments. [Deut. 5:6-10; RSV]

Verse 7 forbids the worship of other gods, while verses 8-9 forbid the making of graven (carved) images that would be worshipped as gods, i.e. idols. Now worshipping statues with divine honor is one way of worshipping other gods. Verse 7 is a general statement of the First Commandment, while verses 8-9 give a specific case of this Commandment. Verses 9-10 present the punishments and rewards that are associated with these Commandments.
By combining together Deut. 5:6-10 into one Commandment, the Catholic Church is accused of altering the Commandments and covering up God's command forbidding graven images. Suspicions are further fueled when Catholic books only present the general form of the Commandment, Deut.

5:7, in order to expedite memorization. Now one must ask the question: "Does God forbid the making of statues, or does He condemn the worship of statues?" If God condemns the divine worship of statues, then the Catholic division scheme is justified since these images would be "other gods before" Him. A separate Commandment based on Deut. 5:8-10 would be redundant.
Now if God simply forbids the making of graven images, then there are problems elsewhere in the Bible. First, in Exodus 25:18-21, God commands Moses to make two statues of angels (cherubim) for the top of the Ark of the Covenant. Later in Numbers 21:8-9, God commands Moses to make a bronze serpent, so that the people who were bitten by snakes could look upon it and be healed.

Now it is true that centuries later King Hezekiah destroyed it; however, this action was done because the people worshipped it as a god (2 Kings 18:4). In the Gospel, Jesus compared Himself to the bronze serpent (John 3:14). Continuing in the Old Testament, the inner sanctuary of the Temple contained two large statues of angels according to 1 Kings 6:23-28. In the following verses, Solomon also had the walls of the Temple decorated with carved images of angels, palm trees and flowers (1 Kings 6:29ff). During the Babylonian Captivity, Ezekiel had a vision from God about the design of the new Temple. According to Ezekiel 41:17-25, this new Temple contained graven images of angels and palm trees. These passages in the Bible indicate that God does not forbid the making of statues. If God truly condemned the making of graven images in the "Second Commandment", then He must have changed His mind later in the Old Testament.

The Catholic Church during the Council of Trent (1545-1563) issued a clear statement concerning images and statues. According to the 25th Session of this General Council:
The images of Christ and of the Virgin Mother of God, and of the saints are to be had and retained particularly in churches, and due honor and veneration are to be given them; not that any divinity or virtue is believed to be in them on account of which they are to be worshipped, or that anything is to be asked of them, or that trust is to be reposed in images, as was of old by the Gentiles, who placed their hopes in idols; but because the honor which is shown them is referred to the prototypes which these images represent; so that we through the images which we kiss...or bend the knee, adore Christ and venerate the saints, whom they represent. [The Canons & Decrees of the Council of Trent (TAN Books, 1978) p. 215-6]

The Church does NOT compel her members to kneel or pray before images. No one is allowed by the Church to pray to images since they have no ears to hear or power to help us. The Church allows for the veneration of images as long as the honor is directed towards Christ and His saints.

On a related issue, some Christians may object to the veneration of images of the saints since they believe that honor should be directed towards God alone and not towards Mary or the saints (1 Tim. 1:17). This objection arises from a confusion between divine honor (adoration - supreme honor proper only for God) and respectful honor proper for men. According to the Bible, the people of God bowed down before King David to show him honor (2 Sam. 24:20; 1 Chron. 29:20; 21:21). Obadiah in 1 Kings 18:7 fell prostrate before Elijah showing him reverence for being a prophet of God. In the Ten Commandments, we are told to honor our mother and father (Deut. 5:16).

Even Jesus defended and obeyed this Commandment (Mark 7:9-13; Luke 2:51). At least for Mary, our honor to her is in imitation of Jesus, her Son (1 Cor. 11:1). The Church allows for the veneration of the saints and their images as long as it remains honor proper for men. It is good to honor the saints for their love and trust in God (Matt. 22:31-32; Heb. 11:1-12:1).
The Catholic Church has not altered the Ten Commandments of God. The Church has not dropped the "Second Commandment" as the booklet alleges. The Catholic numbering scheme may differ with the Protestant numbering scheme, but this is due to a difference in tradition and not an alteration of God's Commandments. Unfortunately the Bible is not clear on how to divide or number the Ten Commandments. If this difference is scandalous, it would be interesting to know what the author of the booklet thought of Jesus Christ when He reduced God's Commandments to the Two Great Commandments in Matt. 22:36-40.

Finally the Church strictly condemns the adoration (divine worship) of statues, images or even the saints, since this is idolatry and in direct violation of the First Commandment. For Christians a crucifix should not be considered merely as a statue of Jesus hanging on a cross, but as a reminder of the high cost of our salvation as well as His words to us:
"If any man would come after me, let him deny himself and take up his cross and follow me." [Mark 8:34]

Printed with permission from A Catholic
NAFIKILI KUFIKIA LEO UBISHI UTAKUWA UMEFIKIA MWISHO.
Dini za ulaya hizi ni shiiddaaaa. Hata kama tumeshindwa kuelewa sheria vitabuni au kama vinachanganya basi tusome historia tu. Yesu alishawahi fika Vatican? Au kuna nabii ambaye alipelekwa nchi za magharibi?
Kisha tuangalie walioshushiwa mitume ni bara gani, nchi gani na wana dini gani?
Utaona ni Asia, Israeli na wana dini yao na nchi za Kiarabu ambapo asilimia kubwa ni Waislam tu. Bora ifuatwe dini ya Kondoo . Lakini hata hivyo kondoo hawakumtaka yesu...sasa ukishaona hivyo tayari hyo ni kasoro maana hawakumuelewa na dini yao wameifanya kuwa dini ya kabila (Racial Religion) ingawa Mungu wao ni yuleyule wanayemwabudu waislam(Mungu wa Mussa). Tuje kwa Mohammed...yeye kawatukuza mitume wote mpaka wengine wasiotajwa kwenye vitabu.
Ushauri: Kuna haja ya kuchunguza kati ya dini hizi mbili kiundani naamini mojawapo yawezekana ikawa ndio dini sahihi iliyoletwa na Mungu, kuliko kulichukua jina la yesu kulipeleka vatican kulifanya ndio dini...Historia inagoma labda itengenezwe.
N.B: USHAURI HALAZIMISHWI MTU KUUFUATA. UKIONA UNAKUFAA CHUKUA, HAUKUFAI UACHE.
 
Kaka kuna shida kubwa ya Elimu ya Dini ya Ukatoliki kwa wasio wakatoliki,
Huwezi kuamini hili-hakuna Dhehebu linalofata misingi ya ibada iliyomo ndani ya Biblia kama Wakatoliki nasema tena Huwezi amini hilo

Maada ya issue ya Sanamu imeongelewa sana humu,
Kwa kifupi Wakatoliki hawaabudu sanamu, na kama umewahi kumuona Mkatoliki anaabudu na kuitumikia sanamu basi huyo amekufuru na amefanya shiriki kubwa kwa Mungu wetu mwenye wivu,

Kuabudu sanamu ni kuitumainia kuwa inaweza kufanya lolote unaloliomba, hivyo unaitolea Sadaka na kuitumainia, je kweli kazi ya mikono ya binadamu inaweza kutoa msaada, haisikii, haioni, haisemi nk

Sanamu ziko kwenye makanisa ya Kikatoliki kama kumbukumbu ya uwepo wa watakatifu na wafia dini mbalimbali, hivyo ni sanamu za kuangalia na kukumbuka uwepo wao (Bikira Maria, Yesu, Joseph nk )na Sanamu zote zilizopo ni za watu waliowahi kuwepo hapa Duniani, HAKUNA KANISA LA KIKATOLIKI LENYE SANAMU YA MUNGU BABA, kwa sababu hakuna aliyemuona

Stay blessed na uwe na Amani, hakuna muabudu sanamu ndani ya Ukatoliki
Amri kumi za Mungu...KUTOKA SURA YA 20 MSTARI WA 1 MPAKA WA 20 Mwenyezi-Mungu alizungumza maneno haya yote, akasema, “Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, niliyekutoa nchini Misri, ambako ulikuwa mtumwa. “Usiwe na miungu mingine ila mimi. “Usijifanyie sanamu ya miungu wa uongo, au kinyago cha kitu chochote kilicho mbinguni, katika nchi au majini chini ya dunia. Usikisujudie wala kuitumikia; kwa kuwa mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu. Nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha hao wanichukiao. Lakini nawafadhili maelfu ya wale wanipendao na kuzishika amri zangu. “Usilitaje bure jina langu mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako. Maana mimi Mwenyezi-Mungu sitaacha kumwadhibu anayetumia jina langu vibaya. “Usisahau kuiweka takatifu siku ya Sabato. Siku sita fanya kazi na tenda mambo yako yote. Lakini siku ya saba ni Sabato ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wako. Siku hiyo usifanye kazi yoyote, wewe, wala mwanao, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala watumishi wako wa kike, wala mnyama wako wa kufugwa, wala mgeni aliye nyumbani mwako. Maana kwa siku sita mimi Mwenyezi-Mungu niliziumba mbingu na dunia, bahari na vyote vilivyomo, kisha nikapumzika siku ya saba. Kwa hiyo mimi Mwenyezi-Mungu niliibariki siku ya Sabato, nikaitakasa. “Waheshimu baba yako na mama yako, ili uishi maisha marefu katika nchi ninayokupa mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako. “Usiue. “Usizini. “Usiibe. “Usimshuhudie jirani yako uongo. “Usiitamani nyumba ya jirani yako, wala mke wake, wala mtumwa wake wa kiume au wa kike, wala ng'ombe wake, wala punda wake, wala chochote kilicho mali ya jirani yako.”
Kutoka 20:1‭-‬17

Ukisoma Katekisimu ya kanisa la Katoliki Amri ya pili ambayo inakataza kuchonga sanamu ya kitu chochote kile kilicho Mbinguni majini juu au chini ya ardhi....kumbuka hairuhusiwi kuchonga Sanamu....Amri hii wameifuta na hawaitii kamwe...Ushahidi uko Makanisa yote ya Katoliki yote yana masanamu!!!
Matokeo yake Amri ya tatu ndiyo imekuwa ya pili yanne imekuwa ya tatu
Wamezivuruga vuruga zote!!

MASWALI
Ni nani aliyewapa mamlaka ya kumrekebisha Mwenyezi Mungu katika Amri zake jinsi mtakavyo nyinyi??
Nani amewapa mamlaka ya kutotii amri ya pili ya Mwenyezi Mungu??
 
Amri ya kukataza ibada kwa sanamu imewekwa wazi katika Biblia Takatifu, Kutoka 20:4-5, “Usijifanyie sanamu ya miungu wa uongo, au kinyago chochote kilicho mbinguni, katika nchi au majini chini ya dunia. Usiisujudie wala kuitumikia; kwa kuwa mimi Mwenyezi Mungu, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu.”

Sheria hiyo inapatikana pia katika Kitabu cha Kumbukumbu la Torati 5:8-9: “Usijifanyie sanamu za miungu za kuchonga, wala mfano wa kitu chochote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia. Isivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi Mwenyezi Mungu, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu.”

Ni kutokana na vifungu hivyo vya Maandiko Matakatifu, Waamini wa Kikatoliki wamekuwa wakituhumiwa, kushtakiwa na kushambuliwa na baadhi ya waamini wa madhehebu mengine kwamba wanapingana na maagizo ya Mwenyezi Mungu, yanayokataza ibada kwa sanamu. Tuhuma hizo zinakuwa nzito zaidi, hasa zinapohusishwa na Ibada inayofanywa na Waamini Wakatoliki siku ya Ijumaa Kuu kila mwaka.

KUNA TOFAUTI KATI YA KUABUDU NA KUHESHIMU

Kuna tofauti kubwa kati ya kuabudu na kuheshimu. Kamusi ya Kiswahili ya Maana na Matumizi, ya mwaka 1993, iliyoandikwa na SALIM K. BAKHRESSA, na kuchapishwa na OXFORD UNIVERSITY PRESS, DAR ES SALAAM, inaeleza kuwa neno “kuabudu” maana yake ni “kuomba au kufanya ibada”; na neno “kuheshimu” maana yake ni “kutukuza, kustahi au kuogopa.”

Katika maana yake ya ndani, anayeabudiwa na mwenye haki ya kuabudiwa ni Mungu peke yake. Hakuna mtu, kiumbe wala kitu chochote kinachopaswa kuabuduiwa na chenye haki ya kuabudiwa. Mtu, kiumbe au kitu hupewa heshima tu, tena ya kiwango maalum. Kwa mfano, Bikira Maria, kwa sababu ya nafasi yake katika kazi ya ukombozi, anapewa heshima ya juu kuliko watakatifu wengine. Watakatifu hao wengine hupewa heshima ya kadiri tu, chini ya heshima ile anayopewa Bikira Maria.

KWA NINI MUNGU PEKE YAKE ANASTAHILI KUABUDIWA?

Tumesema ni Mungu pekee yake, ndiye anayestahili kuabudiwa, kwa sababu ndiye MUUMBA wa vitu vyote, vinavyoonekana na visivyoonekana; ndiye anayevitawala na kuviongoza vitu vyote; ndiye mwenye uwezo juu yetu sisi wanadamu na viumbe vingine vyote; ndiye anayejua yote; ndiye aliye pote kwa ajili yetu; ndiye mwanzo na mwisho wa kila kitu; ndiye mkuu na Bwana wa wote.

Aidha, tunapomwabudu Mungu, tunakiri kwamba ndiye aliyetuumba na “ndani yake yeye sisi tunaishi, tunajimudu na tuko!” (Mdo.17:28). Kwa kufahamu hilo, Wakatoliki hawawezi kumwabudu mtu, kiumbe au kitu chochote, isipokuwa Mungu tu.

MAMBO MAKUU NA MUHIMU KATIKA IBADA YA SANAMU

Ili kufahamu vema kinachofanywa na Wakatoliki ni vema kufuatilia na kutafakari yale wanayoyafundisha na kuyasadiki wao wenyewe, badala ya kuwahukumu kadiri watu wengine wanavyofikiri na kusema. Ukweli ni kwamba hakuna Ibada yoyote ya sanamu katika Kanisa Katoliki. Hilo ni dhahiri kwa sababu ili ibada ya sanamu iwe kweli kuabudu sanamu lazima yawepo mambo makuu na muhimu mawili: Kwanza, NIA KAMILI YA KUABUDU SANAMU INAYOHUSIKA;

Pili, KUWEPO NA IBADA YA DHATI YA KUABUDU SANAMU. Ikitazamwa kwa makini, hayo mambo mawili yanakosekana katika Kanisa Katoliki linapokuja suala la picha na sanamu. Kwa hiyo, Wakatoliki hawaabudu sanamu wala picha. Kama ni hivyo, wakatoliki wanafanya nini na hizo sanamu au picha? Wanaziheshimu tu! Tukumbuke kuwa anayemwabudu mtu, kiumbe au kitu, ni sharti akihesabu na kukisadiki kuwa ndicho kinachomwezesha kuishi, kujimudu na kuwa na uhai wake (Rej. Mdo.17:28).
Ubarikiwe
 
Kaka mbona unaandika kwa povu sana?, umejaribu kusomamkwa utaratibu na kujua kilichoandikwa? Sanamu ilikatazwa kwa malengo na sababu gani basi?

Hilo andiko lako la kutoka 20: 3-6, iko wazi kabisa kuwa USICHONGE SANAMU NA KUZIABUDIA, USIFANYE SANAMU KUWA MUNGU WAKO NA UKAIFANYIA IBADA YA KUITOLEA MAOMBI PAMOJA NA DHABIHU, na Mungu alikataza hilo kwa kusisitiza kuwa MIMI NI MUNGU WAKO MWENYE WIVU,
Shida yenu nyie mnasoma nusu ya hiyo amri, na mnazitenga as if ziko mbili, hiyo Amri ya kuchonga sanamu haiishii hapo kwenye kuchonga bali kwenye kuziabudu pia

Sasa Iweje Mungu akataze Sanamu hapo kwenye hiyo Kut 20: 3-6, lakini alimwambia Musa atengeneze sanamu na kuziweka juu ya Sanduku la agano? ( ....NAWE FANYA (sanamu) za MAKERUBI WAWILI... Kutoka 25:16-22) iweje Amri zile kumi za Mungu zilikuwa zinawekwa kwenye SANDUKU LA AGANO, ambalo pia lilikuwa limepambwa na Masanamu ya Malaika (Makerubi) wawili?
Kut 26: 1-31 pia inaonyesha Mungu alipokuwa anamwambia Musa aweke Sanamu za Makerubi Hekaluni "pamoja na Makerubi, kazi ya fundi stadi" na tekelezo lilifanyika katika Kut 37:7-9.

Ukisoma Wafalme 6: 23-35, Solomoni alilipamba hekalu kwa Masanamu mbalimbali ya Makerubi na wenye uhai,
So unaposema makanisa ya Kikatoliki yamejaa sanamu, basi wewe hujasoma habari za Hekalu la Mungu pamoja na Sanduku la Agano lilivyosheheni Sanamu za kila aina

Shida ya Sanamu ipo kwenye kuziabudu, Sanduku la agano lilipokuwa linapita watu walikuwa wanaanguka kusujudu, JE WALIKUWA WANAWASUJUDIA WALE MAKERUBI WAWILI WALIOKUWA JUU YA SANDUKU LA AGANO? Jibu hapana wale makerubi ni mfano tu wa viumbe vitakatifu lakini havikuabuduwa kamwe.

Mat. 22: 20 na Lk 16:13, yasu alipewa sarafu akauliza NI YA NANI SANAMU HII NA ANWANI HII, wakamwambia ni ya Kaisari, akawaambia ya Kaisari apewe kaisari na Mungu apewe vyake, kisha hiyo Lk. Akasema mtu hawezi kutumikia mabwana wawili, MUNGU na MALI (SANAMU)

Ukimsoma Mtume Paulo amefafanua vizuri sana Ibada ya Sanamu, nenda Kasome Efe 5:5, Kol 3:5, Tim 6: 6-10 na Sura nyingi sana zinazoelezea Ibada ya sanamu

So Hakuna Mkatoliki anayeabudu Sanamu na Biblia na Amri za Mungu zinakataza hilo, so ukimuona Mkatoliki anazitolea Sadaka, na kuziomba msaada Sanamu zimsaidie basi huyo sio Mkatoliki ni mtu aliyekufuru kwa njia zake na mafundisho yake mwenyewe,
 
Amri ya kukataza ibada kwa sanamu imewekwa wazi katika Biblia Takatifu, Kutoka 20:4-5, “Usijifanyie sanamu ya miungu wa uongo, au kinyago chochote kilicho mbinguni, katika nchi au majini chini ya dunia. Usiisujudie wala kuitumikia; kwa kuwa mimi Mwenyezi Mungu, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu.”

Sheria hiyo inapatikana pia katika Kitabu cha Kumbukumbu la Torati 5:8-9: “Usijifanyie sanamu za miungu za kuchonga, wala mfano wa kitu chochote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia. Isivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi Mwenyezi Mungu, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu.”

Ni kutokana na vifungu hivyo vya Maandiko Matakatifu, Waamini wa Kikatoliki wamekuwa wakituhumiwa, kushtakiwa na kushambuliwa na baadhi ya waamini wa madhehebu mengine kwamba wanapingana na maagizo ya Mwenyezi Mungu, yanayokataza ibada kwa sanamu. Tuhuma hizo zinakuwa nzito zaidi, hasa zinapohusishwa na Ibada inayofanywa na Waamini Wakatoliki siku ya Ijumaa Kuu kila mwaka.

KUNA TOFAUTI KATI YA KUABUDU NA KUHESHIMU

Kuna tofauti kubwa kati ya kuabudu na kuheshimu. Kamusi ya Kiswahili ya Maana na Matumizi, ya mwaka 1993, iliyoandikwa na SALIM K. BAKHRESSA, na kuchapishwa na OXFORD UNIVERSITY PRESS, DAR ES SALAAM, inaeleza kuwa neno “kuabudu” maana yake ni “kuomba au kufanya ibada”; na neno “kuheshimu” maana yake ni “kutukuza, kustahi au kuogopa.”

Katika maana yake ya ndani, anayeabudiwa na mwenye haki ya kuabudiwa ni Mungu peke yake. Hakuna mtu, kiumbe wala kitu chochote kinachopaswa kuabuduiwa na chenye haki ya kuabudiwa. Mtu, kiumbe au kitu hupewa heshima tu, tena ya kiwango maalum. Kwa mfano, Bikira Maria, kwa sababu ya nafasi yake katika kazi ya ukombozi, anapewa heshima ya juu kuliko watakatifu wengine. Watakatifu hao wengine hupewa heshima ya kadiri tu, chini ya heshima ile anayopewa Bikira Maria.

KWA NINI MUNGU PEKE YAKE ANASTAHILI KUABUDIWA?

Tumesema ni Mungu pekee yake, ndiye anayestahili kuabudiwa, kwa sababu ndiye MUUMBA wa vitu vyote, vinavyoonekana na visivyoonekana; ndiye anayevitawala na kuviongoza vitu vyote; ndiye mwenye uwezo juu yetu sisi wanadamu na viumbe vingine vyote; ndiye anayejua yote; ndiye aliye pote kwa ajili yetu; ndiye mwanzo na mwisho wa kila kitu; ndiye mkuu na Bwana wa wote.

Aidha, tunapomwabudu Mungu, tunakiri kwamba ndiye aliyetuumba na “ndani yake yeye sisi tunaishi, tunajimudu na tuko!” (Mdo.17:28). Kwa kufahamu hilo, Wakatoliki hawawezi kumwabudu mtu, kiumbe au kitu chochote, isipokuwa Mungu tu.

MAMBO MAKUU NA MUHIMU KATIKA IBADA YA SANAMU

Ili kufahamu vema kinachofanywa na Wakatoliki ni vema kufuatilia na kutafakari yale wanayoyafundisha na kuyasadiki wao wenyewe, badala ya kuwahukumu kadiri watu wengine wanavyofikiri na kusema. Ukweli ni kwamba hakuna Ibada yoyote ya sanamu katika Kanisa Katoliki. Hilo ni dhahiri kwa sababu ili ibada ya sanamu iwe kweli kuabudu sanamu lazima yawepo mambo makuu na muhimu mawili: Kwanza, NIA KAMILI YA KUABUDU SANAMU INAYOHUSIKA;

Pili, KUWEPO NA IBADA YA DHATI YA KUABUDU SANAMU. Ikitazamwa kwa makini, hayo mambo mawili yanakosekana katika Kanisa Katoliki linapokuja suala la picha na sanamu. Kwa hiyo, Wakatoliki hawaabudu sanamu wala picha. Kama ni hivyo, wakatoliki wanafanya nini na hizo sanamu au picha? Wanaziheshimu tu! Tukumbuke kuwa anayemwabudu mtu, kiumbe au kitu, ni sharti akihesabu na kukisadiki kuwa ndicho kinachomwezesha kuishi, kujimudu na kuwa na uhai wake (Rej. Mdo.17:28).
Ubarikiwe
Nitajaribu kufupisha tu maelezo yangu.. ...
Hebu tuende kwenye mada kuu ambayo iko wazi kabisa haya ktk bandiko lako umekubaliana na maandiko kwamba tumeamriwa kuto kujifanyia sanamu ya miungu ya uwongo au kinyago chochote kilicho Mbinguni ardhini au majini ...pili tumekatazwa kuabudu hivi vinyago....
KWANZA
Wakatoliki wamechonga hayo masanamu...
PILI
Tuangalie je wanayaabudu? ...

Kuna mambo kama tisa hivi ambayo mmoja anaweza kuyafanya akiwa katika ibada ya sanamu. Mambo hayo yametajwa katika Biblia Takatifu.
1. Utoe sadaka Hos 4:13
2. Uitolee sanamu yako ubani 1 Fal 11:8
3. Ufanye tambiko mbele ya sanamu yako Isa 57:6
4. Uitolee zaka Hes 2:8
5. Uweke sanamu yako juu ya meza au tuseme iwepo meza Isa 65:11
6. Usujudie sanamu yako 1Fal 19:18
7. Uiinulie mikono sanamu yako Isa 44:20
8. Uichezee ngoma sanamu yako 1Fal 18:26
9. Ulale kifudifudi na kuipigia makofi sanamu yako (1Fal. 18:26).

Je Wakatoliki hamyafanyi hayo??
Usiendelee kubisha na kudanganya watu zama hizi.....
 
Back
Top Bottom