Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 15,819
- 33,255
- Thread starter
-
- #141
Sio wapiga kura hawa wa leo Tanzania ambao waliopata tetesi kipindi fulani jamaa amerest in peace walianza kufurahia na kufanya shereheMzee Baba bahati mbaya sana ulivyoandika ni kinyume Cha uhalisia. Wapiga kura watamchagua tena Dr Magufuli. October 28 sio mbali.
Una uhakika gani kama ni wapiga kura??? Dr.Slaa aliwashauri nyie chadema mjenge msingi kila kijiji lakini hamkumuelewa. Leo hii hata members Register haipo kama ipo basi haiko updated. Nani atawatafutia kura?? Tundu Lissu alivyopita juzi shinyanga, mwanza tarime nk. ndiyo uhamasishaji huo hakuna juhudi zozote zinazoendelea baada ya hapo. Halafu useme utapambana na Magufuli. Sasa hivi Jiwe anawacheki tu na kujisemea hiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiKwani huko anakopita huoni wale wanampokea wako kwenye keyboard
Huko vijijini ndo wamemkataa magufuli vibaya sana. Nakupa kazi ndogo tu. Nenda Vijiji vya Iringa, Mbeya, Songwe, Katavi na Rukwa alafu nenda vijiji vya LINDI na Mtwara alafu malizia vijiji vya Kigoma, Kagera, Mara, Singida, Manyara, Arusha na Kilimanjaro. Ukipata hayo majibu then rudi hapa.Andiko lako zuri saaana kwa watu wenye stress litawasaidia, rudi shule ukasome siasa na focus yako iwe kwenye siasa za Tanzania na hasa mfumo wa ccm. Unaanzia wapi kuitoa ccm yenye mtandao kuanzia kwa balozi wa nyumba kumi, mabalozi ndiyo watafuta kura, kwa upande mwingine upinzani unategemea mafuriko. Poor analysis as u trying to compare unlikes.
Nikusaidie tu kimahesabu; tanzania bara ina jumla vijiji 12000;
Kila kijiji kina kinaweza kuwa na wastani wa idadi ya KAYA 1500 hivyo kuwa na wastani wa chini kabisa wa mabalozi 150.
Ukifanya hesabu za chini kabisa kwamba vijiji 12,000 vina mabalozi 12,000*150 = mabalozi 1,800,000. Kwa hiyo balozi akipewa jukumu la kutafuta wapiga kura wachache sana kwenye ubalozi wake mfano 10.
Kwa mahesabu ya makadirio utaona ccm ikipata kura 18,000,000
Kumbuka pia kuwa idadi ya wanaccm kwa hesabu za karibuni kulingana na ripoti ya PolePole wako 16,800,000
CCM ITASHINDA KWA 95% HUU NDIYO UKWELI MCHUNGU
ndiyo
Endeleeni na propaganda zenu ila ukweli ni kwamba kuna Landslide victory kwa Tundu Lisse kwenye uchaguzi wa mwaka huu. Historia kubwa sana inaenda kuandika Tanzania. Amini Amini maneno yanguUna uhakika gani kama ni wapiga kura??? Dr.Slaa aliwashauri nyie chadema mjenge msingi kila kijiji lakini hamkumuelewa. Leo hii hata members Register haipo kama ipo basi haiko updated. Nani atawatafutia kura?? Tundu Lissu alivyopita juzi shinyanga, mwanza tarime nk. ndiyo uhamasishaji huo hakuna juhudi zozote zinazoendelea baada ya hapo. Halafu useme utapambana na Magufuli. Sasa hivi Jiwe anawacheki tu na kujisemea hiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
Hawezi kuwa kiongozi huyu, hana hoja za maendeleo na anajipendekeza sana kwa wazungu
Mkuu usijidanganye he is going to win the battle early.Kiukweli Magufuli hana wa kumpigia kura. Kila Kona kaharibu.
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] Lissu huyhuyu Mwabudu Wakoloni na Wakenya. Akipata kura zaidi ya asilimia 7, nakuachia Nyumba Yangu iliyopo Mtaa wa Ufipa
H
Pia ujue huyo wa kijijini hajui maana ya uhuru wa kutukana, bali anajua watu lazima waheshimu viongozi,
Kwa hiyyo uhuru wenu wa kutukana haumsaidii, kwa sababu hajawahi kuzuiwa kufanya mambo yake huko kijijini,
bali alichoona ni kwamba kuna hospitali na maji umeme na elimu bure vimesogezwa kwake karibu.
Kwa hiyo atampigia mtu aliyemsogezea huduma.
Kitendo cha Lisu kumpigia kampeni fisadi Lowasa tunakiitaje ?
Au mwanaccm anayeitwa fisadi akija Chadema anatakata.
Kiukweli upinzani ukijipanga vizuri unatoboa. Kuna kundi la wafanyabiashara wanavyosumbuliwa na mfumo wa kodi , wafanyakazi wa serikali ambao kwa miaka mitano hawajui nyongeza ya mshahara au kupandishwa madaraja, kuna waliolizwa na korosho zao, wanafunzi wa vyuo mikopo haieleweki, kuna wastaafu hawajapewa pesa zao kwa miaka sasa, kuna kanda zimegabuguliwa kwa makusudi, CCM yenyewe ina mipasuko, ajira kwa vijana hakuna . Upinzani ukifanyia kazi hizi hoja, naamini zinawagusa watanzania wengi na hivyo kwenye uchaguzi kazi itakuwa ni pevu haswa. Shida ya upinzani ni kuwa hata watu wakisema wampe TL uraisi, mawaziri watakuwa ni wapi??
Nani kakwambia Tundu Lissu hana uwezo???? Unamjua vizuri au unamsikia tu Tundu Lissu????MKUU naona mnaota ndoto za mchana. Kiukweli bila hata kuhitaji Akili ya chekechea Tundulisu hana uwezo wa kuvaa viatu vya Magufuli.
Hata yeye Anajua na chadema wanajua kwamba hawawezi kuongoza nchi.
Tanzania haiitaji wapiga maneno. Inahitaji MTU kama Magufuli Ambae Anatenda na sio Hadithi.
Ni watu wavivu wasiopenda kuwajibika wanatafuta sababu kwamba chanzo cha umaskini wao ni CCM kumbe ni ujinga wakufikiri.
OCTOBER ndio mtajua Watanzania wanataka waropokai au mchapakazi.
Una uhakika gani kama ni wapiga kura??? Dr.Slaa aliwashauri nyie chadema mjenge msingi kila kijiji lakini hamkumuelewa. Leo hii hata members Register haipo kama ipo basi haiko updated. Nani atawatafutia kura?? Tundu Lissu alivyopita juzi shinyanga, mwanza tarime nk. ndiyo uhamasishaji huo hakuna juhudi zozote zinazoendelea baada ya hapo. Halafu useme utapambana na Magufuli. Sasa hivi Jiwe anawacheki tu na kujisemea hiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
Dawa ipo tayari ndugu. Hakuna namna CCM watatoka mwaka huu!!Ccm imekufa siku nyingi sana walichobakiwa nacho ni kutumia watumishi wachache wa dola wasio waaminifu kuiba kura tu. NINAWAOMBA SANA VYAMA VYA UPINZANI MWAKA HUU MTAFUTE MWAROBAINI WA KUZUIA MAKADA WACHACHE WA CHAMA WALIOCHOMEKWA SERIKALINI KUIBA KURA, Mkifanikisha hili tu ccm kwisha kabisa
Cha kuwashauri kwa sasa ni kuwa wajipange kuwa Chama pinzani makiniCcm muda wao umekwisha,wakabidhi Ikulu kuanzia muda huu!
Sio wapiga kura hawa wa leo Tanzania ambao waliopata tetesi kipindi fulani jamaa amerest in peace walianza kufurahia na kufanya sherehe
DOLA NI WATANZANIA kama ujui.Unaijua dola ya Tanzania?
Schoolboy politics at its best!
Wake up boy!
Hana uwezo was kupata hata 30%Amani iwe nanyi wadau na kwa wakazi wa Dar poleni na Tetemeko
Niende kwenye mada!
Ni ukweli ulio wazi kuwa John Pombe Magufuli hawezi shinda uchaguzi wa mwaka huu na hizi ndizo sababu
1. Kuna mgawanyiko mkubwa sana ndani ya CCM
Najua CCM sasaivi wanajaribu kuwaita makada wao nguli ambao waliumizwa na magufuli Kama Kinana, Nape na Makamba wakiamini hawa wanaweza kurudisha hali ya CCM kikampeni ila ukweli ni kuwa hapana it’s too late. Kwa CCM wengi wana amini kuwa mwenyekiti wao ni mtu wa visasi na kutumia tu watu kwa faida zake hivyo wengi wanaamini kuwa hata hawa wakirudi hawatarudi kwa moyo mweupe. CCM wengi wanevunjika moyo na hawana raha na Magufuli. Suala la Kikwete kuonekana hivi karibuni akitoa tathimini ambazo zinaonekana kabisa ni tofauti na nyimbo anazoimba magufuli limewafanya watu wengi waone dhahili kuwa CCM sio moja!
Kwenye hili maneno ya Mzee Butiku kwa vyombo vya dola kuhusu uchaguzi wa mwaka huu aliyoyatoa kwenye kikao cha NCCR yananifanya ku conclude kuwa hata class ya wazee nyeti wa nchi hii wamesha endorse mabadiliko yatakayofanyika nchini hapo October kupitia sanduku la kura.
2.Lissu kutokuwa na makandokando!
CCM wanapata shida sana kutafuta hoja ya kumpigia Lissu. Hayuko kwenye ufisadi, hayuko kwenye uzembe wala hayuko kwenye ujanja ujanja. Track record ya Lissu kuwahenyesha CCM kuanzia bungeni hadi nje ya bunge inambeba sana Lissu. Mbaya zaidi ni tukio la kujaribu kumuua. Watanzania wengi wanajua ni mwenyekiti wa CCM ndiye ambaye yuko behind jaribio la mauaji la Lissu
3. Wapiga kura wa Mwaka huu 2020!
Kiuhalisia wapiga kura wengi wa mwaka huu ni vijana wa miaka ya themanini nwishoni na tisini. Alafu kuna kundi la vijana wa 2000. Haya makundi ni makundi yenye kiu ya mabadiriko, ni makundi ya kizazi cha internet ambacho kinajua mengi na kuona mengi. Mizani hiki sio loyal kwa CCM tofauti na kizazi cha 60’s na 70’s.
4. Makosa ya wazi ya magufuli- Magufuli kafanya makosa mengi ya wazi, kubambikia watu wanaompinga kesi na kuwaonea Mf viongozi wa upinzani, msanii idris, mwandishi erick kabendera na vijana mdude nyangari na kina tito magoti.
Magufuli katoa matamko yaliyosababisha maisha ya watu kuathilika kiuchumi kama tamko la kuzuia uagizwaji wa sukari jambo lililopelekea bei ya sukari kupanda maradufu
Kwa wakulima Pia Kuna maamuzi ya serikali yaliyoharibu biashara za wakulima na kuwa let was shida Mf Korosho, mbaazi na hata mahindi bila kusahau mazao mengine ya biashara
Kwa wafanyakazi ndo usiseme. Hawa hawaongei ila wote moyoni wanasema wana jambo Lao nae na hiyo itakuwa ni October 2020
Kwa wafanyabiashara hawa ndo wengi wana amini kuwa magufuli amekuja kuwatesa. Wengi wanaona kama snawadhulumu hasa wakiona wanavyofirisiwa na kufungiwa biashara na TRA.
Mwisho kabisa ni kwa vijana graduate- hawa ni kundi kubwa lililoachwa bila ajira. Sekta binafsi iliwaajiri wengi sana kipindi cha awamu ya nne ila kwa mkwamo kwenye awamu hii ya tano wengi wamepoteza kazi na wengine ndo hawajapata kabisa kazi.
kuna mengine mengi kama mafao ya wastaafu ila itoshe tu kusema kuwa Kuna uwezekano wa asilimia 98 kuwa kuna historia itakayitikisha Ardhi ya Africa Mashariki inaenda kuandikwa October mwaka huu!!
Karibu Ikulu( Magogoni na Chamwino) Tundu Antipas Lissu!