Usimtetee.
Tanzania ingekua ni Muungano wa Serikali 3 malalamiko mengi tusingekua nayo , si zamani, sasa wala baadae kwa sababu kila Serikali ingekua unajua na kutenda ndani ya mipaka yake tofauti na sasa.
Unaambiwa majukumu ya. iliyokua iwe Serikali ya Tanganyika yanafanya na Serikali ya Muungano. Hapo utatofautisha vipi Muungano na Tanganyika.
Kuungana ni jambo jema~ nakubaliana wewe
Kuunganisha nguvu ndio ushindi ~ swadakta
Aliacha nchi moja na Serikali mbili hapa ndio uongo.
Kilichoonekana nchi moja ni kwa sababu ya nidhamu ya woga, alikua hataki kupingwa kwenye swala la Muungano wa Serikali 2, na ukimpinga you would face the consequence.
Case study: Aboud Jumbe Mwinyi 1983 na
G55: 1993
Kama aliacha Serikali mbili nchi moja, mpaka 1985 anang'atuka Urais a Jamhuri ya Muungano na 1991 anang'atuka Uenyekiti wa CCM, safari kati ya Bara na Zanzibar ilikua lazima Passport au kitambulisho maalum Cha Uhamiaji?
Ziara za Kiserikali kwa wageni wa Kimataifa walikua wakienda Zanzibar kupitia Tanzania Bara walikua wanafanya process zote za Uhamiaji ikiwemo visa. Wageni wa Tanzania mfano Marais wa nchi za Nje na Ujumbe wao walikua Wakija TANZANIA ni "LAZIMA" wapelekwe na Zanzibar.
Mambo haya yameondoka yeye akiwa Hana wadhiwa wowote wa Kiserikali au Kichama.