Sikubaliani na maoni ya mtoa mada katika maeno kadhaa
Maeneo hayo ni kama Ifuatavyo.
1. Suala la mke kutomheshimu mume anayetaka kumuoa.
My take : ukioa mwanamke malaya lazima akudharau,ila ukioa mwanamke aliyejitunza basi atakuheshimu.
Hivyo sio kwamba dunia ndio haimheshimu baba bora hapana,bali sisi wanaume tunashindwa kuchagua wake ambao watatufanya tuwe waume na mababa bora.
HAUWEZI KUWA MUME/BABA BORA MBELE YA MWANAMKE MALAYA ASIYEJIHESHIMU.
2. Nice guy.
mwanamke malaya pekee ndio atakayekuona nice guy pale unapotaka kumuoa,na sio mwanamke alyejitunza mwenye adabu zake.
My take : tutafute wanawake wanaojiheshimu(wapo) ili tukiwatangazia ndoa wasituone ni akina mr nice guys.
3 . mke kumpenda mwanaume anayetembea na wake za watu.
mwanamke sio kwamba anampenda mwanaume anayetembea na wake za watu hapana,mwanamke anampenda mwanaume mwenye wanawake wengi awe MKE wa mtu au asiwe mke wa mtu.
LEngo la mtoa mada ni kudhoofisha ndoa watu wasioe,lakini kiuhalisia tutafute wake wenye maadili waliostaarabika kisha tuwaoe.
Kitu cha msingi ambacho mtoa mada amekiacha ni kuueleza umma kwamba mambo yote aliyoyataja yanatokana na MALEZI ya huyo mwanamke.
Na malezi ni kila alichokiona mtoto kinamuathiri katika malezi.
Kila alichokisikia kinamuathiri katika malezi.
Kila alichokifanya kinamuathiri katika malezi.
Mwanamke ambaye amekulia huku akiona na kusikia matukio ya ajabu ya wanaume au baba yake na huku mama yake huyo akivumilia matukio hayo,basi tutarajie huyu mtoto akikua lazima ataona kwamba huyo ndio mwanaume wa kweli kwa sababu wakati anakua yeye aliona wanaume wa aina hiyo
Na ndio maana kuna wanawake wakikufuma umechepuka wanakuacha kwa sababu hawakukulia katika mazingira ya kuintertain uchepukaji.
Lakini wapo wanawake ukichepuka wataendelea kuwa na wewe kwa sababu walikulia katika mazingira hayo na kuona jambo la kawaida sasa huyu atakuachaje na kwake ni ishu ya kawaida ?
Hivyo mtoa mada alitakiwa aseme kwamba kuna aina fulani ya wanawake ndio wanafiti katika utafiti wake,na wala sio wanawake wote.
Hivyo mtoa mada alitakiwa akubali kwamba yote aliyoyasema yanatokana na aina fulani ya wanawake na sio wanawake wote.
kwa msingi hio mtoa mada alitakiwa akataze wanaume kuoa aina fulani ya wanawake na sio wanawake wote.
Hivyo basi : NDOA NI MBAYA IKIWA UTAO AINA FULANI YA WANAWAKE,NA WALA SIO KWA WANAWAKE WOTE.
mwanamke utakayemuoa ndio dunia yako,hivyo ukichagua vizuri atakuheshimu na dunia itakuheshimu,na ukochagua vibaya atakudharau na dunia itakudharau.