Ukweli mchungu kuhusu KINANA

Ukweli mchungu kuhusu KINANA

Naamini JK amewa-outsmart Kinana na Mangula kwa kuwateua kusimamia ccm ktk siku hizi za mwisho wa uhai chama hichi kwa maana ccm kiwafie mikononi mwao.

CCM haiponi hata ikikabidhiwa kwenye mikono ya Barack Hussein Obama.
Yani huu ni muda m'bovu sana kwa ccm hakuna jinsi na JK anajua hilo.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
Leo umekosa hoja hata moja umeamua kuandika utoto sasa,lini utatoa ushauri ambao utawanufaisha watanzania na kujenga jamii thabiti.
 
Kinana ni mwanajeshi amelitumikia jeshi kwa kipindi kirefu kwa cheo cha kanali...si mtu wa kupuuzwa

Ni kweli mkuu bungeni hapaswi kupuuzwa, na hata anavomaliza tembo wetu katu asipuuzwe! Make akipuuzwa huyu kwa jinsi inavo onekana alivo makini kusimamia kazi anayo ifanya tembo wetu watabaki historia.
 
Mkuu naloliga hurita hivi kuna Kinana mwingine tofauti na ajenti wa meli zinazo safirisha meno ya Tembo kutoka A. Mashariki?.

Huu sio ukweli mchungu kuhusu Kinana.
 
Last edited by a moderator:
Ni mtu asiyejali au mpuuzi asiyezijua vyema siasa za Tanzania anayeweza akasimama na kuudharau uteuzi uliofanywa na Rais Kikwete ambaye baada ya kushindwa mara kadhaa hatimaye amefanikiwa kumshawishi, mmoja wa wanasiasa makini na wakongwe, mtumishi wa umma wa muda mrefu, mwanadiplomasia na Kanali Mstaafu wa Jeshi, Abdulrahaman Kinana kuwa Katibu Mkuu wa CCM.

Kwa muktadha huo na kwa kuzingatia nafasi kuu ya utendaji aliyopewa, nitazungumzia kwa sehemu tu wasifu wa Kinana, mtu ambaye naamini anapaswa kuangaliwa kwa jicho la karibu na wakati mwingine kudhibitiwa ili kasi yake ya kukijenga chama alichopewa dhamana ya kukinusuru isije ikasababisha kuyumba kama si mauti ya kisiasa kwa baadhi ya vyama vya upinzani.

Ni wazi kwamba, kuteuliwa kwa Kinana kuwa Mtendaji Mkuu wa CCM Taifa, akirithi mikoba iliyomshinda, Wilson Mukama, kumetutia ganzi baadhi yetu ambao kwa muda mrefu tumekuwa ‘mashabiki’ au waumini wa kuchagiza kwa njia ya kalamu na wakati mwingine katika mijadala ya wazi kwamba, taifa lilikuwa na haja ya kutafuta mabadiliko ya uongozi kutoka nje ya chama tawala.

Sitaki kuwa miongoni mwa wapenda mabadiliko ambao kwa njia za kujifariji au za kujipa matumaini hewa wameingia katika mkumbo wa jumla jumla wa kumbeza Kinana kwa namna wanayotaka kuuaminisha umma wa Watanzania kwamba, mtu huyo anaweza akasukumwa kirahisi kwa namna ile ile ilivyopata kuwa kwa watangulizi wake kadhaa waliopata kushika wadhifa huo.

siku zote nilikuwa nikiamini kwamba, ukatibu mkuu kwa Kinana ilikuwa ni silaha moja ya maangamizi kwa vyama vya upinzani ambavyo naamini vinapaswa kuendelea kupewa fursa ya kuaminiwa na kukomaa.

Kinana anaendelea kubakia kuwa tishio kubwa kwa ustawi wa upinzani ambao ni rutuba muhimu kwa maendeleo ya demokrasia na misingi ya utawala bora.

Hili ndilo ambalo naamini wapinzani wanapaswa kulitazama na kulitafakari nyakati hizi wanapoendesha harakati zao za kukabiliana na maguvu ya dola na haya mapya ya hoja ambazo aghalab zitaongozwa na Kinana nyakati hizi taifa linapojiandaa kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa miaka mitatu ijayo.

Haitoshi kwa kina Freeman Mbowe, Profesa Ibrahim Lipumba, James Mbatia, Dk. Willibrod Slaa na Zitto Kabwe kumbeza Kinana na timu ya watendaji wake eti kwa hoja nyepesi na zisizo na mashiko za ufisadi au uchafu wa jumla jumla wa CCM.

Wapinzani na wachambuzi wa mambo wanapaswa kujua na kutambua kwamba, Kinana ni mwanasiasa wa vitendo, msomaji mzuri wa vitabu, ripoti, taarifa, magazeti, msikilizaji na msikivu mzuri wa mambo mepesi na mazito kuliko alivyokuwa ‘utopia’ Mukama anayeamini na kuzitetea nadharia zisizotekelezeka.

Si hilo tu, wapinzani wanapaswa kutambua kwamba, historia yake ya uaskari alioutumikia miaka 20 hadi mwaka 1972 akifikia cheo halisi cha jeshi cha Kanali ikimhusisha na mafunzo mahususi ya kimkakati ni sehemu ya mambo ambayo yanatawala nidhamu ya kazi ya aina ya kipekee iliyomfanya Kinana akawa jemedari wa mapambano ya CCM tangu mwaka 1995 hadi leo.

Wachambuzi wa mambo, nikiwamo mimi mwenyewe ambao siku zote tumekuwa tukiiona CCM kuwa chama kinachokufa kwa maana ya kuchungulia kaburi, tunapaswa kuanza kutafakari upya mawazo yetu hayo, nyakati hizi Kinana alipopewa dhamana ya kuwa mtendaji wake mkuu.

Tutakuwa wendawazimu iwapo tutamlinganisha Kinana na Mukama na kusahau kwamba huyu aliye kilingeni leo ndiye aliyemuongoza Benjamin Mkapa katika mapambano makali ya kisiasa mwaka 1995, zama Augustine Mrema alipokuwa tishio la kwanza la kweli dhidi ya CCM katika Uchaguzi Mkuu.

Alikuwa ni Kinana aliyefanya kazi kubwa katika kipindi chote cha kampeni akiratibu na kuongoza kampeni zote za Mkapa zilizomjumuisha pia Mwalimu Nyerere katika mazingira ambayo wengi walikuwa wakiamini CCM ilikuwa katika mwelekeo wa anguko la kihistoria.

Kinana ambaye kabla ya mwaka 1995 alikuwa tayari amepata kuwa Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Waziri wa Ulinzi alitumia vyema mbinu za medani na zile za kidemokrasia na kidiplomasia kumjengea uhalali Mkapa ambaye wakati huo alikuwa mwanasiasa ambaye hakuwa akijulikana sana.

Ni jambo la bahati mbaya sana kwamba, siku chache tu baada ya kuingia Ikulu kwa mara ya kwanza mwaka 1995, kwa sababu ama ya ulevi wa madaraka au kwa kutingwa na kazi za kimamlaka, Mkapa alisahau kazi kubwa aliyofanyiwa na Kinana.

Ni katika kipindi hicho cha kati ya mwaka 1995 na 2000 ndipo nilipokutana kwa mara ya kwanza na mara kadhaa na Kinana nyumbani kwake Masaki, jijini Dar es Salaam ambako nilipata fursa ya kumsikiliza na kuufahamu upeo mkubwa wa kuona mambo aliokuwa nao mwanasiasa huyo.

Tangu wakati huo hadi wakati wa kampeni za mwisho za mwaka 2010, niliendelea kukutana kwa nyakati fupi fupi na Kinana na mara kadhaa nikawa mtu wa kufuatilia na kuzisikiliza kwa makini, habari zake kutoka ama kwa marafiki au maadui zake wa kisiasa.

Sikushangazwa hata kidogo niliposikia tena kwamba, Mkapa alilazimika kumuangukia tena Kinana na kumuomba aongoze tena kampeni zake mwaka 2000 kabla ya Kikwete naye hajafanya kile alichofanya mtangulizi wake alipomuomba mwanasiasa huyo adhibiti joto la kiti cha urais mwaka 2010.

Uwezo wake mkubwa wa kisiasa, umakini wake na upeo mkubwa alionao katika kuona na kuchambua masuala ya siasa, uchumi na jamii ndivyo vitu ambavyo kwanza kwa nyakati tofauti vimepata kumfanya Kinana awe Mbunge wa Jimbo la Arusha kwa miaka 10, Mbunge wa Afrika Mashariki na Spika wa Bunge hilo.

Si ajabu hata kidogo kwamba, hata kabla ya kufikia huko, ni Kinana huyo huyo ambaye alipata kuwa Mwakilishi wa Kidiplomasia wa Rais wa Tanzania katika eneo la Maziwa Makuu na kabla ya hapo akiwa Mwenyekiti wa Mawaziri wa Ulinzi wa Nchi za Kusini Mwa Afrika (SADC) zama akiwa Waziri wa Ulinzi katika Serikali ya Awamu ya Pili iliyokuwa ikiongozwa Rais Ali Hassan Mwinyi.

Uzoefu wake katika siasa za kiraia unaanzia mwaka 1972 wakati alipostaafu jeshi akiwa Kanali baada ya kulitumikia kwa miaka 20 ndiyo ambao amekuwa akiutumia kama silaha kubwa ya kukijua chama chake na pengine kumfanya awe mmoja kati ya watu wachache ambao wamepata kuwafanyia kazi marais wote wane wa Tanzania.

Anarithi mikoba ya Mukama akiwa mmoja wa wanasiasa wachache wa CCM wa rika ile ile la kina Kikwete ambaye alilikimbia na kulikana kundi la mtandao mwaka 2005 ambalo baadhi yetu tunaamini kuwa, ndilo lilisababisha kuzaliwa kwa siasa mpya za kupakana matope, kuzushiana na kuhujumiana ndani na nje ya CCM.

Lakini pengine kubwa katika yote hayo anaingia madarakani huku akiwa na hazina ya uzoefu mkubwa wa kuongoza mapambano dhidi ya vyama vya upinzani na kushinda katika mazingira ambayo aghalab yamekuwa yakiacha vidonda visivyopona kwa wapinzani tangu mwaka 1995. Huyu si mtu wa kumpuuza au kumbeza hata kidogo.


Sawa umeongea vizuri, jaribu kupitia archives za miaka ya tisini kuhusu swala la uraia wake utagundua kwamba huyu mwanasiasa ana maficho mengi na hivyo lolote lawezekana
 
Uwezo wake mkubwa wa kisiasa, umakini wake na upeo mkubwa alionao katika kuona na kuchambua masuala ya siasa, uchumi na jamii ndivyo vitu ambavyo kwanza kwa nyakati tofauti vimepata kumfanya Kinana awe Mbunge wa Jimbo la Arusha kwa miaka 10, Mbunge wa Afrika Mashariki na Spika wa Bunge hilo.

Pole sana, You have been too long on words BUT too short on substance!!

Reason: You are still too green (*Rookie) to understand the depth and girth of such issues.

Advise: No research; no right to open you mouth; fanya home work yako vizuri urudi.
 
CV yake nzuri haijamsaidia kuwa mzalendo kwa nchi yake ametumia uzoefu wake,nafasi yake na ukaribu wake na Kikwete kuendeleza mtandao wa ujangiri nchini na biashara haramu za kusafirisha binadamu
 
I will never believe that Kikwete has any brain to simply outsmart anyone let alone his own appointees.
 
Endeleeni kuota tuu...hata list of shame mlisema maneno hayo hayo...then damage mliokuja kuipata inawagharimu mpaka leo..kwa hio endeleeni kujifariji lakini damage mtakayoipata itakuwa kubwa kuliko ile ya list of shame.
 
Alistaafu 1972? Au aliacha?

Mkuu hajastaafu 1972, historia yake hii hapa:

Born in the Arusha region in October 1951, Kinana did his primary and secondary studies in that city, before attending the Old Moshi Secondary School.

He was one of those responsible for the TANU party youth organization in the Korogwe district between 1971 and 1972, before following the teachings of the Kivukoni Ideological College in 1973.

From 1974 to 1985, he undertook a long career as a political commissar in several military schools, and from 1984 to 1985, at the 20th division of the Tanzania Peoples Defence Force (TPDF).

In the meantime, in 1984, he had graduated from the university of Ljubljana in Yugoslavia.
 
ziara yake moja tu ya mkoa wa Morogoro imezua tafrani nchi nzima

Acha ushabiki wa kijinga changia hoja, unadhani hii ndiyo ziara yake ya kwanza? umesahau kuwa ziara yake ya kwanza alianzia Lindi na Mtwara, sasa nini kinachoendelea kwa sasa huko Lindi na Mtwara kuhusu CCM?
Kwa ujumla Kinana ni mzuri kutokana na hiyo historia, lakini kwa hapa tuliopfika hakuna mwenye shida na historia hiyo tuliyoandikiwa hapa kwenye huu uzi, leo hii hata kama Baba wa taifa angefufuka akawa ndiyo katibu mkuu wa CCM (kwanza sidhani kama angekubali) mambo yasingekuwa mteremko kama mnavyodhani. Kwa leo si habari ya CHADEMA, CCM au Kinana watu wanhitaji kuona raslimali zao zinawanufaisha vipi, sasa kama Kinana mwenyewe kampuni yake ni agent wa kuiba raslimali za nchi, atawaambia nini watanzania?
Je hiyo ziara aliyoifanya Morogoro, kama si kualika wanamziki pale moro kama Diamond, unadhani ule mkutano ingekuwaje?
Ndugu zangu, kazi nzuri iliyofanywa na CHADEMA ni kuwajengea uwezo watu namna ya kuhoji na kudai haki zao, haijali ni nani atakuwa madarakani hata kama ni CHADEMA wenyewe bado watabanwa, kwahiyo kwangui mimi Kinana si issue sana kihivyo, suala je ataweza kufumua mifumo ya hovyo ambayo iko ndani ya CCM ambayo yeyey mwenyewe ni mshirika wake?
 
Amefanya nini,kukishauri chama chake,kudeliver? Au ni mzuri kwa kuunda jisi ya kushinda chguzi tu.
 
DEBE tupu haliwachi makelele. Kinana, Nchimbi, megji, Mohd Seif Khatib, Nape na wengine wengi ni madebe matupu yanayopiga makelele. Mafisadi matupu na 2015 wawekwe pembeni maana wamechoka sana
 
it's easy to teach a blind person and understand but extremely tiring job to get a stupid eyed person understand!
 
Sina haja ya kupoteza muda kusoma majisifu ya jangili kinana,non sense!!!mleta mada ukome kutupotezea muda kuleta pumba za lumumba hapa..
 
Samahani sijaona ukweli wowote mchungu wa kubadili ccm Au jangiri na mafisadi kubadili tabia zaidi ya kuendelea kulindana na kuongeza shida kwa wanyama na maisha ya watu.
 
mtaangaika sana lakini huwezi mfananisha Comrade Kinana na hao MaDJ
 
Weka mbali na TEMBO wetu huyu mtu. Ila leo ni weekend nitapata KINANA moja ya baridi hapo baadaye ili kuwakumbuka tembo wetu waliouwawa na JANGILI kinana
 
Back
Top Bottom