Uchaguzi 2020 Ukweli mchungu kwa Lissu, sio kila mtu anaweza kuwa Rais wa JMT

Hapa tu, pamekushusha hadhi yako, nilijua una hoja katika uzi wako huu, hivi huu wimbo wa kwamba "LISSU AMENUNULIWA" ni nani ameuasisi, na wanunuzi wake ni akina nani? (Dhana ya kununuliwa na mabeberu ni mfu kwani hata majina ya hao mabeberu hayajawahi kutajwa)

Kama watu wanataka kusema makampuni ya madini yanayofanya uchimbaji hapa nchini ndiyo "mabeberu" swali la msingi ni je, nani aliwaleta nchini kwetu? Nani aliwapa vitalu vya uchimbaji madini? Ni miaka ipi? Waliopo leo madarakani walikuwa wapi wakati madini yetu yakiuzwa kwa "mabeberu"?

Wanaoimba wimbo wa kwamba LISSU AMENUNULIWA kimsingi ndiyo wenye Chama kilichouza rasirimali zetu kwa bei ya kutupa,(hatujawahi kuongozwa na chama chochote zaidi ya kilichopo madarakani) hivyo dhambi zote za uuzaji wa rasirimali zetu kiholela,haziwezi kwenda kwa mtu yeyote isipokuwa chama hicho na washirika wake!

Kwa wasiofahamu, mkitaka kumjua Lissu na utetezi wa madini yetu, tafuteni historia yake, imeandikwa vizuri kabisa kabla hata hajawa mbunge,Kuna kitu mtafahamu kuhusu watafunaji na watetezi halisi wa rasirimali zetu.
 
Hii ingekuwa "clearly observed" hii nchi ingekuwa mbali sanaaa, leo hii watu wanamtukana rais Kikwete (wapinzani walimnanga akiwa rais, CCM wanamtukana baada ya kutoka madarakani) kwamba alilea ufisadi na hata kuona sasa chama kimepata malaika!

Kama kweli tumeibiwa miaka yote kwa usaliti wa Viongozi wetu,vyombo vyetu hivyo vilibariki? Havikufanya vetting kabla ya kupata hao viongozi? au vinafanya vetting kwa wale wa upinzani tu?
 
Unaweza kuwa na hoja lakini hujatuwekea wazi udhaifu wa Lissu uko wapi? Mbona ni mzalendo tuu?
CCM wametaka kumnunua mara nyingi ili kumnyamzisha lakini alibaki kuwa mpinzani kwa maslahi mapana ya Taifa hili ili aliondolee ndwele ya maumivu ya CCM
Wewe unadhani mabeberu wanachukua miaka miwili au mitatu kuandaa vibaraka wao!? Mabeberu huchukua muda mrefu kuandaa vibaraka wao kadri wanavyo amua kwa kila nchi. Hapa kwetu Lissu na wenzake wameandaliwa miaka mingi na sasa wanadhani ndio wakati muafaka wa kuwaweka madarakani ili waendelee kuinyonya nchi hii baada ya kupigwa BITI kuanzia Magufuli alipochukua nchi. Hakuna Mtanzania Mzalendo atakaye kubali kuingizwa CHAKA na hawa vibaraka kwa maneno yasiyokuwa na AKILI huko kwenye majukwaa ya siasa. Nchi hii italindwa na Watanzania Wazalendo wote kwa UMOJA WAO, iwe wa vijijini au wa mijini. Mabeberu na vibaraka wao hawana nafasi katika nchi hii, COME RAIN COME SUN PERIOD.
 
mwenye maskio na askie hata mwenye macho na aone...
ndugu yenu makammwenyekiti anazidi kuharibu tuu!!

Mtaendelea kulalama mitandaoni 30yrs to come
 
zikiwa zimebakia siku2 tuu
je niliyoyasema yanakwenda kutokea?
 
by the way kwa utafiti ulofanywa unaonesha upinzani wa safari umekua zaifu sababu
1.hawana cha kusimamia
2.ushiriki wao na watu toka nje ya nchi
3.swala la corona
4.wabunge wao kususasusa bunge
5.magu kuwambia wananchi ukweli kua wana/watajichelewesha kwa kuchagua upinzani
6.wapinzani kuchochea vurugu.

☆so nahitimisha kwa kufuta yale nloandika post#1 ya uzi huu maana kile nilichokiwaza hakita totea na badala yake ushindi kwa ccm ni sa2 asbuhi na mapema

kazi kwenu
 
Lissu ameshiandaa kurudi ubeligiji, tayari ana tikit mkononi
 
Lissu ni Mtanzania and he has every right to contest the highest office without any problem. He hass impeccable.track records of mp and is a prove .politician...acheni ujinga maccccm...wanafiki wakuba.nyinyi
 
Upambavu nikitu kijinga aaaa nanai anaanamfanyie vwtring mwenzake....yaani.ccm.imefanyia chadema vetting .. stop being stupid you are better than this
 
Sio kwamba Chadema ilikufa? Si Chadema chama cha Wachaga? Sacoss ya Mbowe? Hahahhahah dadeeeekk
Mku Wachagaa sio Watanzania kwani au hawadtshili kuwa kwenye Tasisi hapa Tanzania.

Hili suala tunalichukulia kawaida sana lakini linazidi kukitafuna chama kumbuka kuna wachaga wako vyama mbalimbali na Tasisi mbalimbali na kila wasomapo maneno kama haya wanazidi kumwaga sumu ktk hizo tasisi.

Na kumbuka kutoa elimu ya uraia sio kazi ngumu kwani ni kitu ninachokijua.Wanaccm wenzangu tuheshi Makabila ya Watu lasivyo tutazidi kukiumiza chama.

Kuna kauli zilivuma kutoka kwa baadhi ya viongozi zile za kuitana wazalendo na wasio wazalendo, na tuliwahi kujiuliza kama wasiowazalendo wanazidi kuongezeka au wanapungua.

Kama wanazidi kuongezeka jibu lake ni nini kwani hoja hujibiwa kwa hoja kwani siokugawanana kwani haya yote tunatakiwa kujiuliza haya yalitokana na nini zaidi ya ndimi zetu.
 
Kila mtu anaweza kuwa yeyote chini ya jua hakuna alie zaliwa kuwa fulanii
 
Labda utusaidie wewe uadilifu Kwa nchi unaupimaje?? Kama JPM kaweza kuwa Rais Kwa nini sio TL naomba ufafanuzi pls.

Unapaswa uelewe pia Urais sio Mtu, ni Taasisi. Unachotueleza wewe kuwa Urais ni Mtu. Ungekuwa hivyo Trump asingeweza ongoza Marekani.

Katiba yetu inatambua wananchi kupitia Kura zao ndio wenye uwezo wa kuamua Nani awe Rais na si vinginevyo.
 
Hiyo Katiba ya Kikoloni itafumuliwa kupunguza hizo powers.
nani ataifumua? ilhali upinzani ushajifia soma post #330 apo juu
 
Unaongea haya kwakuwa una maslahi binafsi na madaraka ya Magufuli, na ccm kwa ujumla. Hivyo unajua iwapo itaondoka madarakani utarudia umasikini uliotoka nao kijijini. Ww ni mwanaume mtu mzima, jifunze kujitegemea badala ya kutegemea wanaume wenzio.
Nakubaliana na wewe 100%. Ukiona mtu hashuki kwenye gari bovu basi jua humo ana mzigo wake.

Watu wengi wanaoishupalia CCM iendelee kututawala ukidig down unakuta nao ni wanufaika wa mfumo wa kinyonyaji.

Yani haiingii akilini, mtu Mwenye akili Huru na timamu unawezaje kujitia upofu na kisupport Mambo ya hovyo?

Vita ya CCM na CDM kwa asilimia kubwa ni vita ya wanyonyaji (+ wanufaika wa mfumo wa kinyonyaji) na wanyonywaji. Ukiona mnyonywaji kaamua ku-side na wanyonyaji wake basi jua huyo Saa Mbovu. Hajielewi.
 
Mpe Kura TL akubadilishie mfumo Ili uwe Huru kifikra
siwezi mpa chizi(mate kujaa pembeni ya mdomo wakat wa kuongea ni dalili ya uchizi)

siwezi mpa kura mtu asie jua maana ya uhuru tulopata
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…