Hardwaycomes
JF-Expert Member
- Dec 26, 2018
- 370
- 492
Hapa tu, pamekushusha hadhi yako, nilijua una hoja katika uzi wako huu, hivi huu wimbo wa kwamba "LISSU AMENUNULIWA" ni nani ameuasisi, na wanunuzi wake ni akina nani? (Dhana ya kununuliwa na mabeberu ni mfu kwani hata majina ya hao mabeberu hayajawahi kutajwa)Kwa maslahi hayohayo ya taifa, Lissu hawezi kuwa rais hata kwa siku1
Ndio CCM ilishindwa kumnunua ila mabeberu waliweza tena kwa kujipeleka mwenyewe sokoni..
Ni vile tuu taasisi ya urais imeshuka heshma miongoni mwetu lakini trust me haijashuka heshma kwe mfumo hata chembe.
Kama watu wanataka kusema makampuni ya madini yanayofanya uchimbaji hapa nchini ndiyo "mabeberu" swali la msingi ni je, nani aliwaleta nchini kwetu? Nani aliwapa vitalu vya uchimbaji madini? Ni miaka ipi? Waliopo leo madarakani walikuwa wapi wakati madini yetu yakiuzwa kwa "mabeberu"?
Wanaoimba wimbo wa kwamba LISSU AMENUNULIWA kimsingi ndiyo wenye Chama kilichouza rasirimali zetu kwa bei ya kutupa,(hatujawahi kuongozwa na chama chochote zaidi ya kilichopo madarakani) hivyo dhambi zote za uuzaji wa rasirimali zetu kiholela,haziwezi kwenda kwa mtu yeyote isipokuwa chama hicho na washirika wake!
Kwa wasiofahamu, mkitaka kumjua Lissu na utetezi wa madini yetu, tafuteni historia yake, imeandikwa vizuri kabisa kabla hata hajawa mbunge,Kuna kitu mtafahamu kuhusu watafunaji na watetezi halisi wa rasirimali zetu.