Uchaguzi 2020 Ukweli mchungu kwa Lissu, sio kila mtu anaweza kuwa Rais wa JMT

Uchaguzi 2020 Ukweli mchungu kwa Lissu, sio kila mtu anaweza kuwa Rais wa JMT

H
Wakuu nawasalimu,
Naomba muelewe kitu kimoja kuwa sio kila mtu anaweza kuwa Rais wa JMT hili mliweke akilini. Kwa ufupi tuu hata kama Lissu akishinda uchaguzi na CCM kuamua kukubali kushindwa na ku backdown 'system haiwezi kumkubali Lissu abadani... vyovyote itavyokua. Hatuwezi kuongozwa na Rais mbeambea, Rais asieweza kusimama peke yake katika maamuzi.

Rais huandaliwa na kuchunguzwa uadilifu wake kwa nchi yake, nikimuangalia Lissu sioni akiwa na sifa hiyo hata robo
bora Membe, Maalim hata Mbowe. Hawa wana uadilifu kwa nchi yao kuliko Lissu

Kama nilivyosema huu ni ukweli mchungu kwa wafuasi wake ila ni bora mkajua mapema kabisa!!

Pia naomba mjifunze historia ya nchi hii nzuri, mjifunze misingi ya uendeshaji wa nchi hii nzuri pia mjifunze sera mbalimbali zinazotumika kitaifa na kimataifa za nchi hii nzuri.
Haki ingetendeka NCCR ingeshika dola 1995 na CDM ingeshika dola 2015. Hakika.
 
Nianze kwa kumpa Pole Nyingi Ndg Tundu Lissu kwa kwa madhira yote aliyoyapitia
Kwa Ndg Yetu Tundu Lissu huu sio wakati wake wa kugombea urais angalau angesubiri hata miaka 5 kwanza na ukiangalia bado ni Kijana mwenye nguvu kama sio Urais angeanza kwanza hata na Ubunge Jimboni kwake au hata Jimbo Moja kubwa pale Dar es Salaam kupima nguvu yake tena na upepo wa Kisiasa nchini
Kwa sasa Siasa za Tanzania zimebadilika more scientific na Sera Angavu,wananchi wamebadilika hawataki tena kelele Nyingi wanahitaji FACTS.
Hivyo basi kwa CHADEMA kumteua lissu kama Chaguo lao wanaenda kutupa Ushindi sisi kama CCM mapema mnoo na Ushindi Mkubwa wa kishindo angalau asilimia 95 kama sio 97,Chadema wangekua wajanja wangeweka mpira kwapani na kutuachia Uwanja CCM kuliko aibu watakayoenda kutana nayo hapo Octoba 28.
CHADEMA INAENDA KUFUTIKA RASMI TANZANIA OCTOBER 28
 
Mkuu, mbona unatesa hvyo leo tatizo nn.. Mara Lissu Mara chadema.. Shida iko wapi kwani, huyu Lissu mbona ametulia zake hana habari na watu kama ww.

2020, vijana wote twende na Lissu hakuna wa kutupangia maisha zaidi yetu wenyewe
 
Naona wale wote waliokuwa wanamsakama Mbowe sasa wamehamia kwa Lisu. Kweli hakuna kazi ngumu kama uchawi!
 
We unavyo vyote lakin hata familia yako haiwez kuchagua kwa lolote[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]Jichunguze mkuu....kila mtu anamadhaifu
Kinachoangaliwa n strength ziwe nyingi kuliko weakness
Basi na TL msimshambulie kama kila mtu ana madhaifu yake
 
Nianze kwa kumpa Pole Nyingi Ndg Tundu Lissu kwa kwa madhira yote aliyoyapitia
Kwa Ndg Yetu Tundu Lissu huu sio wakati wake wa kugombea urais angalau angesubiri hata miaka 5 kwanza na ukiangalia bado ni Kijana mwenye nguvu kama sio Urais angeanza kwanza hata na Ubunge Jimboni kwake au hata Jimbo Moja kubwa pale Dar es Salaam kupima nguvu yake tena na upepo wa Kisiasa nchini...
Hivi unavyosema siasa bingo zimebadilika watu wanataka facts twambie ni lini waliwahi mchagua mpinzani akawa raisi mpaka ulete porojo zako eti watanzania wamebadiluka kana kwamba waliwahi nadilika na kumchagua mpinzani.
 
Nianze kwa kumpa Pole Nyingi Ndg Tundu Lissu kwa kwa madhira yote aliyoyapitia Kwa Ndg Yetu Tundu Lissu huu sio wakati wake wa kugombea urais angalau angesubiri hata miaka 5 kwanza na ukiangalia bado ni Kijana mwenye nguvu kama sio Urais angeanza kwanza hata na Ubunge Jimboni kwake au hata Jimbo Moja kubwa pale Dar es Salaam kupima nguvu yake tena na upepo wa Kisiasa nchini..
Mbona huu ushauri unaonekaba kama vile unatoka kwa mtu ambaye ameshaogopa?
 
Aliyepo alichunguzwa na nani? hakuna chuo cha kufundisha uraisi. ila raisi bora utokana kwenye fani ya sheria,uchumi au diplomasia ya kimataifa.

mtu yeyeto anayo chance sawa ya kuwa raisi muhimu ajue kusoma na kuandika ili aweze kufuuta katiba
 
Baadhi ya wajasiriasiasa (wapinzani)wanadhani uraisi unapatikana kwa huruma(kuonewa huruma) kweli sonona mbaya pole sana lisu
 
Atagombea kama mgombea binafsi? Maana wamiliki wa CDM wanachaguo lao tayari, Nyalandu. Ni mtu ambaye wanaamini hatowasumbua kwenye kampeni financially
Bila shaka una kitambi kwa kuwa upo msitari wa mbele kula jasho la wengine ila kwa upande wa mgombea anayepeperusha bendera ya CDM wapiga kura wamesema hapana kwa Nyarandu (mwenye hela) bali wakasema ndio kwa Tundu asiye na hela.

Tukutane October 28 vitambi vyote vya wala rushwa vitatoweka wallah.

Uamuzi wa wananchi kumpa nchi Tundu hautahusiana na rushwa bali tumempenda haswaa na hatujahongwa chochote
 
Yehodaya you go to hell! Hizo kila siku tunazowashukuru wahisani unadhani zinatoka kwa mjomba wako? Lisu hili Lisu vile!
 
Inaonekana wajasiriamali wa ccm wameleta hasira sana kuna nini?Mpaka mnatafuta sanabu ya kutomtangaza Lisu?Kama kweli hakuna woga chama tawala ebu tuchague tume huru! Tuchukue tu wale waliokuwa katika tume ya Warioba ukiondoa walioingia kwenye vyama fulani fulani.
 
Nilichogundua mleta mada hana chuki na Lissu isipokuwa njaa inamsumbua anajua Magu akishindwa anarudi kijijini kwao Nanyamba kulima ufuta, pia si kwamba mleta mada anampenda Magu la hasha tumbo ndilo lililoharibu Central Nervous System.
Ukizungumzia vetting Magu angefanyiwa hiyo kitu wala asingekanyaga Ikulu labda kusalimia, utopolo kama akina bashite usingeweza kunajisi nafasi kama ya mkuu wa mkoa.

Kwa hiyo kama unahisi familia yako bado changa na kwamba Magu ataiacha ikiwa bado haina mwelekeo ndo maana unajilazimisha kumfagilia kama Lijualibaridi alivyojilipua akidhani dodo alilookota Nchemba chini ya mwarobaini nae ataliokota. Mbele ya Lissu mtapoteana hakuna cha Slowslow wala makomeo wa kusimisha move hii.

Pia usipende kulitaja Jina la Lissu vibaya unaweza shushiwa ngumi humu ukahisi tofali la block, waweza ongea aina nyingi za utopolo huko choo cha lumumba but not here.
 
Wakuu nawasalimu,
Naomba muelewe kitu kimoja kuwa sio kila mtu anaweza kuwa Rais wa JMT hili mliweke akilini. Kwa ufupi tuu hata kama Lissu akishinda uchaguzi na CCM kuamua kukubali kushindwa na ku backdown 'system haiwezi kumkubali Lissu abadani... vyovyote itavyokua. Hatuwezi kuongozwa na Rais mbeambea, Rais asieweza kusimama peke yake katika maamuzi.

Rais huandaliwa na kuchunguzwa uadilifu wake kwa nchi yake, nikimuangalia Lissu sioni akiwa na sifa hiyo hata robo
bora Membe, Maalim hata Mbowe. Hawa wana uadilifu kwa nchi yao kuliko Lissu

Kama nilivyosema huu ni ukweli mchungu kwa wafuasi wake ila ni bora mkajua mapema kabisa!!

Pia naomba mjifunze historia ya nchi hii nzuri, mjifunze misingi ya uendeshaji wa nchi hii nzuri pia mjifunze sera mbalimbali zinazotumika kitaifa na kimataifa za nchi hii nzuri.
Uadilifu wa magufuli uko wapi? Kutawala nchi kwa mkono wa chuma, kuvunja katiba waziwazi, kujilipa bilioni 1.2 kila mwezi wakati tayari anahudumiwa kila kitu huo ndio uadilifu muutakao huko Lumumba, eti?
 
Kosa lake kubwa lililo mwaribia lissu kuwa Rais wa Tanzania matamshi yake wakati wa mchanga wa dhahabu wa Makenikia , kuunga mkono wazungu wachukue Madini yetu na kusema tusipowapa tutanyolewa kwa chupa , ilo tu linatosha kufuta kwenye ramani ya urais ktk historia ya Maisha yake. kumpa ukuu wa wilaya na ubunge nikosa kubwa tunataka Rais atakae tetea raslimali za nchi yetu . kwa ili tu lissu hafai kuwa Rais wa Tanzania atauza raslimali zetu zote kwa wazungu.
 
Back
Top Bottom