watawala huzaliwa
hata watawaliwa huzaliwa pia inategemea tuu ulzaliwa kwe kundi lipi
Zaidi sana inategemea wakati gani.
Na wakati umebadilika mkuu hata kama akili za wengi hazijabadilika.
Kipindi fulani kilichopita huko Marekani asingeweza kutokea raisi nje ya kundi la WASP(White Anglo Saxon Protestants) kwa matakwa ya system yao ya wakati huo.
Lakini bado walipatikana kina Theodore na Franklin Roosevelt, wazawa wa wahamiaji kutoka Neatherlands pamoja na ubabe wa hiyo system.
Baada ya hapo matakwa ya wakati yaliruhusu achaguliwe John Kennedy( mkatoliki) na hatimaye Barrack Obama(mweusi na mkatoliki pia) na Donald Trump(mzawa wa wahamiaji kutoka Ujerumani).
Obama, kwa zaidi sana ni mfano mzuri wa jinsi matakwa ya wakati yanavyohitaji kuzingatiwa zaidi na hiyo system yetu yenye mkono wake katika kumsimika kiongozi mkuu wa nchi, kuliko kuangalia makundi ya watawala na watawaliwa au matajiri na masikini.
Niamini mkuu. Sina haja ya kukunanga lakini kwa maoni yako niliyoyanukuu, ungeweza tu kufupisha mada yako kwa kusema Lissu hafai kuwa
raisi wa JMTZ kwasababu hajazaliwa kwenye kundi la watawala.
Angalizo: Trump ni zao la makundi zaidi kuliko mahitaji ya wakati. Ona alivyotokea kuwa raisi wa ovyo!
Linganisha na Obama: mweusi, mzawa wa mhamiaji kutoka Afrika Mashariki. Na bado amekuwa mmoja wa maraisi bora kuwahi kuiongoza Marekani.