Uchaguzi 2020 Ukweli mchungu kwa Lissu, sio kila mtu anaweza kuwa Rais wa JMT

Uchaguzi 2020 Ukweli mchungu kwa Lissu, sio kila mtu anaweza kuwa Rais wa JMT

Wakuu nawasalimu,
Naomba muelewe kitu kimoja kuwa sio kila mtu anaweza kuwa Rais wa JMT hili mliweke akilini. Kwa ufupi tuu hata kama Lissu akishinda uchaguzi na CCM kuamua kukubali kushindwa na ku backdown 'system haiwezi kumkubali Lissu abadani... vyovyote itavyokua. Hatuwezi kuongozwa na Rais mbeambea, Rais asieweza kusimama peke yake katika maamuzi.

Rais huandaliwa na kuchunguzwa uadilifu wake kwa nchi yake, nikimuangalia Lissu sioni akiwa na sifa hiyo hata robo
bora Membe, Maalim hata Mbowe. Hawa wana uadilifu kwa nchi yao kuliko Lissu

Kama nilivyosema huu ni ukweli mchungu kwa wafuasi wake ila ni bora mkajua mapema kabisa!!

Pia naomba mjifunze historia ya nchi hii nzuri, mjifunze misingi ya uendeshaji wa nchi hii nzuri pia mjifunze sera mbalimbali zinazotumika kitaifa na kimataifa za nchi hii nzuri.
Kwa hiyo unamaanisha Tundu Lissu atakuwa Maalim Seif wa Bara?
 
KAMA MTU MWENYE IQ NDOGO KAMA JIWE AMEWEZA KUWA RAISI WA TZ BASI KILA MTU ANAWEZA HATA KINGWENDU,GWAJIMA BASHITE.UKIWA NA UHAKIKA WA KUIBA KURA BASI UNASHINDA UCHAGUZI HIVI NDIVYO TUNAVYOPATA VIONGOZI WETU KARNE YA SAYANSI NA TECHNOLOGIA. FOMULA YA TANZANIA MWIZI WA KURA NDIO ANASHINDA URAISI ,WHAT A SHAME
Mkuu, tumia basi herufui ndogo ili kumvutia msomaji
 
Kwa maslahi mapana ya nchi BOX la kura is not essential, hata Marekani hawajawahi kulitegemea box la kura, huu ndiyo ukweli mchungu. Urais ni zaidi ya kushinda uchaguzi, hili nalo chungu
Good, inahitajika broader human potential and national discipline, huyo Jamaa Hana!
 
Ni kweli Magufuli anaweza kumshinda Lisu kukiwa na uwanja huru, ila itakuwa ni kwa margin ndogo sana. Wakati huo huo idadi ya wabunge wa upinzani itavuka 1/3, ambayo itakuwa ngumu wabunge wa ccm kupitisha jambo watakalo, na watakavyo kwa njia ya kura bungeni. Na ikitokea kuwe na tume huru ya uchaguzi, unahitaji chaguzi 2 tu ccm kuwa historia.
Margin ndogo? Lowasa ashindwe, sembuse huyo. Iyo CCM ya kuishinda within two years ni ile ya kikwete, sasa hivi mtangoja sana.
 
Kwa maslahi mapana ya nchi BOX la kura is not essential, hata Marekani hawajawahi kulitegemea box la kura, huu ndiyo ukweli mchungu. Urais ni zaidi ya kushinda uchaguzi, hili nalo chungu

Machafuko pekee ndio huleta heshima.
 
Margin ndogo? Lowasa ashindwe, sembuse huyo. Iyo CCM ya kuishinda within two years ni ile ya kikwete, sasa hivi mtangoja sana.

Ni kweli, maana ccm ya sasa imeamua kutumia vyombo vya dola waziwazi.
 
Ni kweli, maana ccm ya sasa imeamua kutumia vyombo vya dola waziwazi.
nafkiri unalijua hili wazi...
ulinzi na usalama haupo chini ya ccm upo chini ya vyombo ya dola kwa mujib wa sheria

so kama kunaviashiria vya uvunjufu wa usalama lazima wavizuie kwa nguvu zote
ili mimi na wewe tuishi kwa furaha na amani nchini kwetu!
 
I do not know Why the truth brings violence?
Mtu akiambiwa ukweli, kazi yake ni ndogo tu, ni kuchukua hatua na kuyafanyia kazi anayoambiwa basi!
 
Kwa maslahi hayohayo ya taifa, Lissu hawezi kuwa rais hata kwa siku1
Ndio CCM ilishindwa kumnunua ila mabeberu waliweza tena kwa kujipeleka mwenyewe sokoni..
Ni vile tuu taasisi ya urais imeshuka heshma miongoni mwetu lakini trust me haijashuka heshma kwe mfumo hata chembe.
Wewe inasema kama nani bhana. Mbona mnajipa hati milki ya taifa hili. Lissu ana haki ya kugombea na anauwezo mkubwa kuliko hata huyo. Lissu ni mzalendo wa tangu enzi za mkapa. Tunalijua hilo. Tangu aingie magufuri mmeweka mkakati wa kusema anatumika na mabeberu. Lakini ukweli ni kwamba lissu ni mzalendo wa kweli. Pia mnashangaza sana. Hao mabeberu wakiwapa misaada mnashangilia sana. Cjui mpoje nyie

Sent from my SM-J250F using JamiiForums mobile app
 
Sisi Watanzania wazalendo ndyo tutakaomchagua Lissu tena kwa kura nyingi sana zitakazompa ushindi,huo ujinga wako peleka Lumumba wanakokupa buku saba!
Yaani hawa jamaa tangu jamaa jamaa aliposema anarudi nchini waliamini hakuna watu watakaokwenda kumpokea kwasababu watu wanampenda sana magufuri. Lakinj kitendo cha umati wa watu kujaaa pale uwanjani mpaka leo wamedata ndio maana wanakuja na thread za kumdiss lissu. But ukweli unajulikana 'lissu anapendwa na watu wengi sana'

Sent from my SM-J250F using JamiiForums mobile app
 
nafkiri unalijua hili wazi...
ulinzi na usalama haupo chini ya ccm upo chini ya vyombo ya dola kwa mujib wa sheria

so kama kunaviashiria vya uvunjufu wa usalama lazima wavizuie kwa nguvu zote
ili mimi na wewe tuishi kwa furaha na amani nchini kwetu!

Kama vyombo vya ulinzi na usalama hauko chini ya ccm, kipi kinafanya vyombo vya ulinzi na usalama kusimamia wizi wa kura? Viashiria vya uvunjifu wa usalama ni hiyo kulazimisha ccm kutangazwa washindi bila ridhaa ya wananchi.
 
Lisu akuna wakuweza kumzuia kugombea isipokua chama chake.
nani aljua ccm ingempitisha JPM na sio lowasa au membe?
tuelewane pale linapokuja swala la kiinchi lazima watu wenyeakili na walopewa mandates kusimama Ustawi wa nchi wafanye uhakiki hii aijalishi mgombea anatoka wapi.
Kwahiyo hao wenye akili wapo ccm?[emoji849]

Sent from my SM-J250F using JamiiForums mobile app
 
Uraisi mtu lazima afanyiwe vetting ya nguvu awe CCM au Upinzani .Sababu kugombea Ni kutaka vyombo vya dola viwe chini yake .Haviwezi kukubali kuwa chini ya mtu ambaye vetting ripoti yake mbaya .Vitaiba au kukimbia hata na masanduku ya kura au kumtangaza wanayemuona anafaa hata Kama hakushinda

Lisu vetting report yake ya vyombo vya dola bila Shaka hahitaji kuambiwa anaijua vizuri

Eeh mola wetu kama ilivyokuwa kwa Farao wa Misri, ukakisambaratishe kiburi chao. Ili mataifa yakaujue mkuu wako ulio mkuu sana.

Eeh mola wetu ukayasikie maombi yetu.
 
Kama vyombo vya ulinzi na usalama hauko chini ya ccm, kipi kinafanya vyombo vya ulinzi na usalama kusimamia wizi wa kura? Viashiria vya uvunjifu wa usalama ni hiyo kulazimisha ccm kutangazwa washindi bila ridhaa ya wananchi.
jaribu kuwaza nje ya box mkuu
mifumo ipo si kuna mahakama broh
*kinacho matter mahakamani ni sheria!!
 
ukishaaminiwa na system amna shida hata usipo amini wewe na wenzako

embu soma izo para 2za mwisho kwe bandiko langu

Hapo kwenye red ungeandika "utopolo" badala yake ungeeleweka tu mkuu.
 
Eeh mola wetu kama ilivyokuwa kwa Farao wa Misri, ukakisambaratishe kiburi chao. Ili mataifa yakaujue mkuu wako ulio mkuu sana.

Eeh mola wetu ukayasikie maombi yetu.
Naona baada ya kuona corona haina ishu sasa umeanza kunena kwa lugha
 
Watanzania wataamua nani awe Rais katika sanduku la kura na si wewe na ukoo wako, hilo ni moja. Lakini mbaya zaidi umeandika haya " Pia naomba mjifunze historia ya nchi hii nzuri, mjifunze misingi ya uendeshaji wa nchi hii nzuri pia mjifunze sera mbalimbali zinazotumika kitaifa na kimataifa za nchi hii nzuri."

Tunapoimba mabadiliko tunataka sera nyingine na kuzifuta hizo ulizoainisha. Kwasababu hizo ndizo zilizotuweka katika umasikini wa kutupwa mpaka leo, hata nchi zilizokuwa na vita ndani ya nchi zao zinatupita kiuchumi.

Tunataka mawazo mapya!
 
jaribu kuwaza nje ya box mkuu
mifumo ipo si kuna mahakama broh
*kinacho matter mahakamani ni sheria!!

Hakuna mahakama hapa nchini itakayotoa haki kwa wapinzani yasiyomfurahisha rais.
 
Kila Mtanzania anayekidhi vigezo vya Katiba yetu anaweza kuwa Rais wa JMT akichaguliwa na wananchi. PhD siyo moja ya vigezo vya Katiba yetu ndo maana Marais wa Awamu zote nne za kwanza hawakuwa nazo na waliongoza nchi yetu kwa umahili mkubwa na kutufikisha tulipo. Wajinga wa CCM wanafikiri kwa kuwa wametawala miaka 60 basi ni wao tu ndo wenye haki ya kuongoza nchi bila kutathimini au kujiuliza hapa walipotufikisha ndo tunapotakiwa tuwe baada ya muda huo?

Ukanda huu toka Kenya mpaka Afrika ya Kusini nchi yetu ilikuwa ya kwanza kupata Uhuru na nchi zote za Mashariki ya Mbali ukiacha Japan zilikuwa Kama sisi kabla ya Uhuru. Je katika uongozi wa CCM wa hiyo miaka 60 ya Uhuru tunajilinganishaje na nchi za Kanda hizo? Kwa hiyo kiongozi bora hatokani na kuwa na PhD Bali kuwa na uwezo na kufuata Katiba na taratibu zilizopo.

Kama Kibajaji ndo mtunga Sheria wa nchi hii mleta mada hii na wote wa aina hiyo wataonekana wajinga kupindukia kuamini msomi wa Sheria hawezi kuongoza nchi inayofuata Utawala wa Sheria. Lissu ana uwezo wa kuongoza nchi hii bila wasiwasi kwa sababu watangulizi wake wamefanya makosa mengi bila kujua. Mwenye akili hujifunza kutokana na makosa yake na ya wengine.
 
Back
Top Bottom