Ukweli Mchungu kwa Wanasimba: Televisheni ya Yanga kuwa na Thamani kubwa kuliko Klabu ya Simba ni upumbavu

Ukweli Mchungu kwa Wanasimba: Televisheni ya Yanga kuwa na Thamani kubwa kuliko Klabu ya Simba ni upumbavu

Ujue pia Mo na Azam ni bitter rivals kwenye biashara, ni dhahiri dili nyingi za Azam kwa Mo zitapita kwa Mbinde.
Usije ukasikia Mo nae anaanzisha Media house yake, huyu Mo ni dizaini ya Diamond kimtazamo
 
Wewe ni chizi wanahisa hawagawani mtaji wanagawana faida tu

Umeandika nini.

Chizi ni Mimi au wewe ambaye hukuelewa.

Punguza Mhemko usome tene na uelewe kwanza ndo utukane kabla ya kuwahi kutukana
 
Umemsikia Ghalib? Anakwambia thamani ya yanga ni 60bn to 200bn, simba wabaki na nafasi yao ya 10 Afrika, na yanga ya 80, ila yanga inakuja huko kwenye 10 kwa kishindo, alijibu kijembe cha moo akiweka tu bn 20

Mashabiki wa timu ya Simba wao wanaangalia furaha ya matokeo ya Muda mfupi

Hawaangalii madhara ya huu mkataba .

Mo anapata wap nguvu ya kukataa mikataba mingine just kwa kuwa ni rivals wa Mo Kampuni. ?
 
Yanga wenye elimu wako wapi? Ikiwa kushiriki kimataifa hadi wabebwe.

Wewe unaminyana bure, yaani unajiona upo kwenye banda la mpira. Uzi unakiri kuwa Simba ndo ina Matokeo bora, Simba ni timu bora East Africa.

Uzi unaitambua Simba kuwa na Thamani kubwa sana. Thamani hii haipaswi kuwa kwenye Maneno bali kwenye Makaratasi pia.

Kipi hujaelewa hapo. ?

Timu top 10 kwa Ubora Africa then ina thamani ya B40?
 
Mwanzoni mlisema mbona haweki hizo billioni 20, sasa kaweka Mnaanza mbona ndogo. Hii nchi tabu sana..
 
Hivi nyie kwa nini mnatumika kuwapigania wanachama wachache wa juu ili wapige pesa? Sisi wanachama tunachokihitaji kwa club ni ushindi na mataji tu,mwekezaji kama amewekeza na amepata zaidi muache avune. Hao wanachama unaotaka wapate nusu wanachangia nini?
Eti wao hawataki mtu apate faida. Acha tu apate faida hata mara mbili lakini kikubwa timu ifanye vizuri uwanjani maana hiyo ndiyo furaha yetu mashabiki.
 
Na kinachonishangaza ni pale mtu anaposhangilia 38bn inayotoka kidogo kidogo na kidharau 20bn iliyotoka Cash.Hivi huyu mwenye 20bn akiiwekeza baada ya hiyo 10yrs itakuwaje? Hili Utopolo hawalifikirii kabisa.

Asante MO kuwagomea Azam,kama wanataka waweke pesa ya kueleweka.Next ni Sportpesa,naona na wao wakipewa masharti mazito,hakuna cha usawa hapa wa Simba na Yanga.Kila mtu atavuna alichopanda.
Mh. 38bn ni udhamini, 20bn ndio umiliki, tungoje ya hisa za yanga za mara moja
 
Wewe unaminyana bure, yaani unajiona upo kwenye banda la mpira. Uzi unakiri kuwa Simba ndo ina Matokeo bora, Simba ni timu bora East Africa.

Uzi unaitambua Simba kuwa na Thamani kubwa sana. Thamani hii haipaswi kuwa kwenye Maneno bali kwenye Makaratasi pia.

Kipi hujaelewa hapo. ?

Timu top 10 kwa Ubora Africa then ina thamani ya B40?
Mkuu mbona unaumia sana? toa huo mwiko huko nyuma labda akili zitakukaa sawa, siku zote adui muombee njaa sasa hiyo yanga mnayoisifia ina nini cha maana? hata uwanja wa mazoezi tu upo kwenye makaratasi miaka nenda miaka rudi, kwa wakati tuliopo Mo ni mtu sahihi kwa simba
 
Wewe unavyoona ina thamani ya shillingi ngapi?.
Wewe unaminyana bure, yaani unajiona upo kwenye banda la mpira. Uzi unakiri kuwa Simba ndo ina Matokeo bora, Simba ni timu bora East Africa.

Uzi unaitambua Simba kuwa na Thamani kubwa sana. Thamani hii haipaswi kuwa kwenye Maneno bali kwenye Makaratasi pia.

Kipi hujaelewa hapo. ?

Timu top 10 kwa Ubora Africa then ina thamani ya B40?
 
Umeandika nini.

Chizi ni Mimi au wewe ambaye hukuelewa.

Punguza Mhemko usome tene na uelewe kwanza ndo utukane kabla ya kuwahi kutukana
Wewe ndio chizi haiwezekani useme kila mpunga utakaoingia kwa simba Mo anachukua 49%, Simba na Mo watakuwa wanagawana faida au hasara itakayopatikana tu, halafu waache simba walingie walichonacho sasa haya ya mbeleni yatajulikana hukohuko
 
Wewe ndio chizi haiwezekani useme kila mpunga utakaoingia kwa simba Mo anachukua 49%, Simba na Mo watakuwa wanagawana faida au hasara itakayopatikana tu, halafu waache simba walingie walichonacho sasa haya ya mbeleni yatajulikana hukohuko
Sasa faida wanagawanaje?..

Faida inayopatikana wanagawana kulingana na kiwango cha uwekezaji wewe.. katika kila 100 inayopatikana Mo anachukua 49.

nenda shule
 
Sasa faida wanagawanaje?..

Faida inayopatikana wanagawana kulingana na kiwango cha uwekezaji wewe.. katika kila 100 inayopatikana Mo anachukua 49.

nenda shule
Ila kumbuka ni kwenye faida, sasa wewe na mazuzu wenzako mnajua simba akipata udhamini wa bilioni moja basi mo ana fungu lake, kumbuka hadi faida ipatikane ndio mo atapata chochote, hii simba kuchukua ubingwa mara4 mfurulizo ndio inakufanya uweweseke
 
Ila kumbuka ni kwenye faida, sasa wewe na mazuzu wenzako mnajua simba akipata udhamini wa bilioni moja basi mo ana fungu lake, kumbuka hadi faida ipatikane ndio mo atapata chochote, hii simba kuchukua ubingwa mara4 mfurulizo ndio inakufanya uweweseke
Tatizo simba wanajiona level moja na alhly ndio shida, hiyo hela mo aliyonunulia timu ndio inasjili mtu kule
 
Naam kuweka uelewa sawa ni vyema nikafupisha mada. Lakini sitakuwa sawa kama sitowapongeza wanamsimbazi kwa ubingwa na hatua kubwa waliyopiga kwenye soka kwa miaka hii minne. Lakin pia niwapongeze kwa wapenzi wa timu ya Simba kwa support yao isiyokatika kwa timu yao.

Tumekuwa tukifuatilia mijadala mingi inayohusu mkataba wa mabadiliko ya Klabu hizi mbili kongwe Tanzania bi maana Simba na Yanga. Mijadala ilianza muda mpaka tumefika pahali mabapo tunaenda pazuri. Hongera kwa Simba kwani wameenda haraka sana. Lakini pia niwapongeze wanayanga kwa kulifanya jambo hili polepole na kwa Umakini sana.

Wakati huu ambao wanasimba ni kama wako hatua za mwisho za kuhitimisha jambo lao kuna maswali kadahaa yameanza kutrend mitandaoni na mabarazani hasa baada ya watani zao wa jadi kuingia mkataba na kampuni ya Azam. Kiuhalisia mjadala mkubwa ni thamani halisi ya klabu ya Simba , lakini pia inaibuka hoja nyingine hapo kwa ndani ya thamani halisi ya Klabu ya Yanga in relatin to the Simba-Mo Deal . Ugumu wa hili suala ni kama vile Siasa zetu za vyama vingi hapa nchini kwamba kila mmoja anaona upande wake uko sawa lakini hakuna anayetaka kubase kwenye fACTS HALISI.

Bila kusema valuation ya Simba SC imefanyikaje, wapi na ni taasisi gani zimefanya hiyo Valuation nakwenda moja kwa moja kwenye thamani iliyopatikana ambapo imegawanywa kwenye vipande 100 kama shares (100%). Mohammed Dewji "Mo" yeye amewekeza hapo na kuchukua 49% yote ambayo mwekezaji anatakiwa kuichukua kwa Shilingi Bilioni 20 za kitanzania. Kiuhalisia wengine wanapinga kuwa sehemu ya Simba haijanunuliwa lakini ukweli nikwamba takribani nusu ya klabu ya Simba imenunuliwa na "Mohammed Dewji" na wanachama wamebaki na nusu iliyobaki.

HII INATHIBITISHWA HAPA:

"A stock is an investment. When you purchase a company's stock, you're purchasing a small piece of that company, called a share.
Investors purchase stocks in companies they think will go up in value. If that happens, the company's stock increases in value as well. The stock can then be sold for a profit.

Definition: What are stocks?

Stocks are securities that represent an ownership share in a company. For companies, issuing stock is a way to raise money to grow and invest in their business. For investors, stocks are a way to grow their money and outpace inflation over time.

When you own stock in a company, you are called a shareholder because you share in the company's profits."

Kwa hiyo tukubaliane kuwa takribani nusu ya Klabu ya Simba imeuzwa. Swali vipi thamani ya Simba: Hii ni Hesabu nyepesi ya 51% iliyobaki ukijumlisha na ile ile ya 49% utapata Bilioni 40.8 kwa Brand, Assets na klabu yote kwa ujumla.

Kinachogonga vichwa sasa ni ukweli huu mchungu kukubalika sasa na isiwe baadae ambapo utaleta mgogoro ikitokea kuna mgongano wa Maslahi kati ya Wanachama na Mwenye 49%.

Yanga wameingia Mkataba wa miaka 10 wa Shilingi Bilioni 41 pamoja na VAT .Kwa ajili ya Televisheni yake tu "Yanga TV" . Yaani huu Mkataba hauhusu Mambo mengine ya Klabu.

Kwa akili za viongozi wetu kufanana, huu mkataba wa Simba na Mo utaakisi mktaba ambao Yanga wanaweza kuingia na Mwekezaji wake atakayekuja. Wanaweza kufanya kuiga wa Simba halafu waweke Value kubwa kidogo ili waseme wamewazidi wenzao lakini pia nao Thamani halisi ya Yanga itakuwa haijatizamwa. Nao wanapaswa kuwa makini sana. Ni heri hii mikataba iwe na ukomo ili kuziba makosa yatakayofanyika.

Upumbavu unapokuja Sasa mkereketwa wa Simba bila kufikiria mwaka 2035 timu itakuwa na hali gani wakati 20B zimeisha na Mo & Family wakiendelea kula matunda ya 49% ya Klabu kwa uwekezaji mdogo sana. Huyuhuyu Mkereketwa atakwambia Simba ina thamani kubwa kuliko Yanga, Nami nakubaliana naye kuwa Simba ina thamani kubwa sana kuliko Klabu yeyote si Tanzania tu balia Afrika Mashariki. Lakini hii thamni Mbona haijaheshimiwa wakati wa kuuza Nusu ya hii klabu. Mbona imeuzwa kwa hela ya Mboga?. Bilioni 40 kumiliki klabu kubwa Tanzania kama Simba , assure you kuwa ni Ndogo sana. Maana wengi sana wangeweza kumiliki hizi timu zenye uwekezaji wa Miaka zaidi ya 60 huko nyuma.

Kutokana na Mkataba wa Yanga Tv na Azam tena ni wa miaka 10 tu kuwa mkubwa zaidi ya Simba, huu ni ukweli mchungu kuwa Thamani ya ya Yanga TV ni kubwa kuliko Simba na inaweza pia kuweka kwenye Rekodi za Kibiashara kuwa Yanga ina thamani kubwa kuliko Simba kwa sasa kwani kama Tv yao tu imewaingizia hicho kiasi, vip kuhusu klabu?, pia vipi kuhusu mkataba wa Tv ukiisha? Maana wanaweza kuongeza tena mwingine wenye thamani zaidi.

Tutakazania kufurahia kwenye Mataji na current form ya klabu. Tukumbuke form siyo Parmanent, Ndo maana Recently Chelsea FC amechukua makombe kadhaa kuliko Man Utd lakini Thamani ya Man utd ni kubwa kuliko Chelsea based on Market value. Tukubali kuwa hii dili ya Simba imekosewa Sana. Ni heri ingepelekwa kwa namna yeyote ile kwnye soko la hisa kwa bei ya juu.

Ni jambo la furaha sana upande Mashabiki lakini vikombe na ushindi havidefine hali ya uchumi ya klabu kwa ukanda wetu huu. Lakin hatujui pia huo upande wa furaha ya vikombe miaka 3 ijayo watani nao watakuwa na Nguvu gani kwenye vikombe. Tusiwabeze kwani wanaonekana wanaboresha kikosi kila uchwao na ndani ya miaka hii mitatu watakuwa na ushindani mgumu sana na SIMBA. Na wanaweza pia kutakeover ufalme wa soka. Furaha ya ushindi itaondoka, itakuja hali ya kiuchumi ya klabu na kibiashara sasa, Hapo ndo failure itaonekana kuwa Thamani halisi ya Simba SC haikuheshimiwa.

Mashabiki na wapenzi wataanza movement zao. This time haitakuwa kumvua mwenyewkiti madaraka bali kuvunja mkataba wa kisheria. Ngumu sana Time will tell

Kazi na iendelee!
Zile bill 41 zinazolipwa kila mwezi?..nadhani thaman yake ningekuwa kubwa zaidi ya simba kama wamelipa kwa mkupuo lakini kwa malipo ya kila mwezi sioni la maana nahisi Adam ndio watanufaika zaidi..simba bil 20 zimeshawekwa haya Yanga watuoneshe 41 zao, ndio hapo utaona tofauti ya hizo mbili kaka.
 
Wewe unaminyana bure, yaani unajiona upo kwenye banda la mpira. Uzi unakiri kuwa Simba ndo ina Matokeo bora, Simba ni timu bora East Africa.

Uzi unaitambua Simba kuwa na Thamani kubwa sana. Thamani hii haipaswi kuwa kwenye Maneno bali kwenye Makaratasi pia.

Kipi hujaelewa hapo. ?

Timu top 10 kwa Ubora Africa then ina thamani ya B40?
Valuation ilifanyika 2016 wakati huo Simba ilikuwa na misimu minne bila ubingwa na haikuwa na Assets zozote zaidi ya jengo la pale Msimbazi centre ungekuwa wewe mwekezaji kipindi hicho ungeweka thamani ya Simba kwa value ya sasa ?
 
Ukiitaka ya Yanga Sc bado haijulikani. Wakitangaza kuwa wanauza Shea kwa 200B basi wao ndo wana Thamani kubwa kama klabu.
Sasa naona umejirekebisha kwa kusema thamani ya Yanga haijulikani, ila pale mwanzo ulitaka watu waamini kuwa hela za udhamini ndio thamani ya timu. Kwa sasa thamani ya Yanga haijulikani, na hiyo 200B ikitokea amepatikana mwekezaji akakubali kuweka 200B (kama yupo atakayekubali), hapo ndipo utakapoanza kusema Yanga ina thamani ya 200B. Kwa sasa inatosha kusema thamani ya Yanga haijulikani.

Tena sio suala la wao kutaka kuuza shea kwa bei hiyo, ni hadi ajitokeze atakayekubali kununua shea kwa bei hiyo. Unaweza ukataka kuuza koti kwa sh. laki tatu, lakini mwenzako mnunuaji anaona kabisa halina tofauti na koti la sh, elfu tatu pale Kariakoo. Thamani ya kitu inaamuliwa na mnunuaji, muuzaji ukikomaa utaendelea kubaki nacho
 
Back
Top Bottom