Miaka ya nyuma sana kombe la Afrca Mashariki lilifanyika hapa dar. Simba siku hiyo ilicheza na Gor Mahia. Kabla ya hio mechi Simba walikuwa wanasumbuliwa na mchezaji Frank Kassanga (Bwalya) kwa ulevi uliopindukia. Viongozi wakijaribu kumsihi lakn wapi nakuachia.
Mtangaziji alikuwa Ahmed jongo.
Nikiwa mwanafunzi mdogo tuliingia kwa kupenya chini ya geti mojawapo dogo upande wa Mashariki. Akiwa anatangaza list alisema ... "namb nne ni jamuhuri kiwelu na centre half ni method mogella. Method mogella fundi leo ni centre half..." uwanjani mzima uliguna.
Kweli method alikuwa bonge la mchezaji, lakn alikuwa alicheza kiuongo na mara nyingi namba nane ambaye hamis gaga ndie ilikuwa namba yake. Siku moja mechi ya Simba na Sigara, yeye method akianza kama namba nane na gaga alikaa nje. Kipindi cha pili kimeenda dk kadhaa uwanja unashangilia, mtangazaji anasema hizo kelele sio kuwa Simba imepata goli ila gaga anapasha Misuli. Kwahiyo walizoea kumwona fundi akicheza dimba la juu sio beki.
Method alikiwasha sio mchezo kiasi kwamba Simba hawakuona tena umuhimu wa Kasssangq. Na kuanzia hapo Kasanga alipumzushwa na msimu ulipoisha akatemwa. Najua Simba itampata mtu wa kuziba nafasi ya Chama soon or later.
Yanga nayo kombe hilohilo sijui kabunda au nani akizingua wakiwa Uganda, Said Mwamba Kizota akamaliza centre half, na alidumu sana kwny hio nafasi. Sijui kwann inakuwaga hivi maana hata Okwi naye akianza kuleta kama hizi