Ukweli mchungu na sababu za kusimamishwa kwa Chama jr

Chama ambaye awali alitaka kuvunja mkataba mwenyewe akajua viongozi watambembeleza...wakamtolea nje,kaona ngoma ishakuwa nzito anafanya vituko ili Simba imvunjie mkataba
Hapa chama amefanya Mchezo wa kitoto Kula nyama kwa jirani alafu kafuta mdomo kwa mkono

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
This makes a lot of sense . Inawezekana ndio sababu hasa. Yeye alitaka wambembeleze ili wamuongezee mkwanja?
 
Hasaa na alitaka aaminishwe namba Kwanza maana Simba sasa wanahangaika kupata mbadala wa chama. insha'Allah kikao cha kamati ya nidhamu kitatupa majibu sahihi

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
 
Tulisema mapema benchika hataki goigoi kamwe
Unajua Benchika alipoingia Simba alisema maneno haya
Hakuna mchezaji mkongwe katika timu yangu

Hakuna mchezaji ambaye atakuwa na uhakika na namba katika timu yangu

Wachezaji wote ni Sawa juhudi yako ndio itakufanya upate nafasi

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
 
Miaka ya nyuma sana kombe la Afrca Mashariki lilifanyika hapa dar. Simba siku hiyo ilicheza na Gor Mahia. Kabla ya hio mechi Simba walikuwa wanasumbuliwa na mchezaji Frank Kassanga (Bwalya) kwa ulevi uliopindukia. Viongozi wakijaribu kumsihi lakn wapi nakuachia.

Mtangaziji alikuwa Ahmed jongo.
Nikiwa mwanafunzi mdogo tuliingia kwa kupenya chini ya geti mojawapo dogo upande wa Mashariki. Akiwa anatangaza list alisema ... "namb nne ni jamuhuri kiwelu na centre half ni method mogella. Method mogella fundi leo ni centre half..." uwanjani mzima uliguna.

Kweli method alikuwa bonge la mchezaji, lakn alikuwa alicheza kiuongo na mara nyingi namba nane ambaye hamis gaga ndie ilikuwa namba yake. Siku moja mechi ya Simba na Sigara, yeye method akianza kama namba nane na gaga alikaa nje. Kipindi cha pili kimeenda dk kadhaa uwanja unashangilia, mtangazaji anasema hizo kelele sio kuwa Simba imepata goli ila gaga anapasha Misuli. Kwahiyo walizoea kumwona fundi akicheza dimba la juu sio beki.

Method alikiwasha sio mchezo kiasi kwamba Simba hawakuona tena umuhimu wa Kasssangq. Na kuanzia hapo Kasanga alipumzushwa na msimu ulipoisha akatemwa. Najua Simba itampata mtu wa kuziba nafasi ya Chama soon or later.

Yanga nayo kombe hilohilo sijui kabunda au nani akizingua wakiwa Uganda, Said Mwamba Kizota akamaliza centre half, na alidumu sana kwny hio nafasi. Sijui kwann inakuwaga hivi maana hata Okwi naye akianza kuleta kama hizi
Method Mogella "fundi" alikuwa anacheza 6 mkuu,Said Mwamba baada ya kucheza straiker kwa muda mrefu baadae sana mwaka 1998 ndio alicheza 5 kwenye mashindano ya Afrika Mashariki na Kati kule Uganda,hata Hussein Marsha naye baada kucheza kiungo kwa muda mrefu aliishia kucheza 5 tena kwa kiwango cha juu mno
 
Haya madini muwe mnayaweka wazi daah thanks san

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
 
Haya madini muwe mnayaweka wazi daah thanks san

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
Jamaa yuko sahihi, Frank Kasanga "Bwalya" alikuwa beki mahiri but mwenye changamoto,mwaka 1991 kwenye fainali ya kombe la Afrika Mashariki na Kati kati ya Simba na SC Villa,aliibuka Jamhuri Kiwhelo akicheza vema sana akimzuia straiker hatari sana East Africa wakati huo Majidu Musisi,Bwalya ndio akapotea jumla kwani baadae Simba wakamsajili George Masatu kutoka Pamba,moja kati ya mabeki mahiri wa kati kuwahi kutokea Tanzania.
 
Safi Sana mkuu unaanza kunipa mwaka sisi wa 95 kuja juu shida sana

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
 
Yote kwa yote kama ni Kweli basi Chama atakuwa mjinga sana hajui wengi wazuri wamepita hapo na yeye atapita tu
 
Nimeandika mwaka mkuu,ni 1991 ndio Bwalya alipotea,mwaka 1992 Simba walisajili wachezaji mahiri sana kama kipa Mohammed Mwameja kutoka Coastal Union, George Masatu (beki wa kati) na Hussein Marsha (kiungo no 8) kutoka Pamba, Godwin Aswile na Thomas Kipese kutoka Yanga,Hawa ndio waliipeleka Simba Fainali ya kombe la CAF mwaka 1993
 
Kwanza hii wameitaka viongozi wenyewe mwaka Jana wakati WA usajiri alitingisha kiberiti viongozi watambembeleza kama Mungu mtu ili abaki na mashabiki wakawaka bila chama hatuji uwanjani viongozi wakaona ohooo maji tushayavulia nguo wacha tuyaoge madhala yake ndio haya

Nakumbuka kuna kipindi kibu dennis alipitia magumu ila hakuchoka kuwa na subra sasa hivi huyoo Kila mwalimu anaingia kwenye mfumo wake

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
 
Nimeandika mwaka mkuu,ni 1991 ndio Bwalya alipotea,mwaka 1992 Simba walisajili wachezaji mahiri sana kama kipa Mohammed Mwameja kutoka Coastal Union, George Masatu (beki wa kati) na Hussein Marsha (kiungo no 8) kutoka Pamba, Godwin Aswile na Thomas Kipese kutoka Yanga,Hawa ndio waliipeleka Simba Fainali ya kombe la CAF mwaka 1993
umeniwlewesha vzr Sana

Saved

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
 
Chama ana dharau sana, Hana LA maana halafu anajiona Iniesta.

Mbona Kuna wachezaji wakubwa walipita kwa heshima zao?

Waachane naye!
 
Back
Top Bottom