Ukweli Mchungu sana: Ndugu yenu akiwa kwenye " naturally life threatening situation" msimuombe Mungu amuepushe na kifo bali mapenzi yake yatimie

Ukweli Mchungu sana: Ndugu yenu akiwa kwenye " naturally life threatening situation" msimuombe Mungu amuepushe na kifo bali mapenzi yake yatimie

LIKUD

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
18,037
Reaction score
33,681
Kwa sababu most of the time inakuwaga ni Mungu mwenyewe ndio anataka kumtoa mhusika kwenye maisha yenu.

Hata yule mtu wa kwenye biblia ambae siku zake za kufa zilikuwa zimefika ila akamuomba Mungu amuongezee miaka ya kuishi Mungu akamuongezea miaka 15 alifanya mambo mengi maovu ndani ya hiyo miaka 15 ya ziada kuliko miaka yake aliyo ishi.

Ishu hii haiwahusu ndugu tu bali pia jamaa, wenza( spouses) na watu wa karibu( ikiwemo viongozi)

Haihusu vifo tu bali na mambo mengine pia kama vile mahusiano n.k(kama kuna mtu yoyote yule anataka kuondoka kwenye maisha yako usijaribu kumshawishi au kumlazimisha abaki...muache aende. Haijalishi ni nani kwakk awe mpenzi,mwanandoa,rafiki, mtoto etc).

Case study:
Ina muhusu rafiki yangu wa utotoni.

Kwao wamezaliwa wanane. Wanaume watatu. Wanawake wa5. Wa kwanza kuzaliwa ni mwanamke wa pili mwanaume then wanafuatana wanawake halafu mwisho kabisa wanakuja wavulana wawili, rafiki yangu akiwa kitinda mimba.

Mwaka 1997
Kaka wa kwanza kwenye familia ambae ni mtoto wa pili kwenye familia akiwa anasoma udsm mwaka wa mwisho ( jina la kozi kapuni) aliugua nusu ya kufa.

Ilifikia hatua madaktari wakasema huyu arudishwe kwao tu akatibiwe kiswahili.

Personally nilikuwa darasa la Sita mwaka huo nakumbuka jinsi familia ya rafiki yangu ilivyo kuwa imetawaliwa na giza jeusi.

Majirani walikuwa wanasema huyu ni wa leo au wa kesho.

Itaendelea
 
SEHEMU YA PILI:
Ni katika kipindi hiki cheusi " dark moment " ndani ya familia ya huyu rafiki yangu ndo niligundua kumbe dini ya kweli ya mwafrika sio uislam wala ukristo. Kwa sababu hiyo familia walihangaika kwa wachungaji na mashekhe bila kupata suluhisho lolote mwisho wakahamia kwa masangoma ambako ndipo walipopata suluhisho la ndugu yao. Jamaa aliuguzwa for almost one year akaja kupona kwa waganga. Alitapishwa vitu vingi sana kwenye mwili wake.

Baada ya afya yake kukaa sawa jamaa alirejea chuo na kuanza upya mwaka wake wa mwisho. Hiyo ilikuwa mwaka 99/2000.

MWAKA 2001: SAFARI YA DIZONGA

Mwaka 2001 jamaa alienda South Africa kutafuta majani ya kijani zaidi.
Ni hivi, ali disco mwaka wa mwisho so akaona kuliko kupoteza muda wa kuendelea kusoma akaamua kwenda DIZONGA.

ANAJIUNGA NA MAKANISA YA KISHETANI.( Cult oriented churches)

Kwa wale ndugu zangu mnaoishi SA mtakubaliana na mimi kwamba S.A. kuna makanisa mengi sana ya kishetani. Makanisa haya huongozwa na wacongo na wanaijeria.

Haya ni makanisa yanayo fundisha na ku practice kwa siri doctrines zinazo tofautiana na generally accepted Christianity teachings .

Kwa mfano mchungaji( mara nyingi hujiita mtume na nabii au mwonaji) anaweza kutangaza ibada maalumu kwa wafanyabiashara akagawa dawa maalumu " annointed products" kwa wafanya biashara wote walio hudhuria ibada halafu akawaambia kama wiki hii usipo ingiza kiasi hiki cha pesa basi book an appointment with me uje tuonane ofisini.

Ukienda ofisini atakwambia wewe ili ufanikiwe inakubidi umtoe kafara mtoto wako wa kwanza. Ukihoji how comes? Anakwambia hata Ibrahim aliambiwa na Mungu amtoe mtoto wake wa kiume Isaka( Ishmael?).


Utamjibu lakini mwisho wa siku Ibrahim hakumtoa kafara mtoto wake kwa sababu Mungu alimshusha mwanakondoo as a substitute.

Atakwambia unajuaje na wewe kama Mungu hatomshusha mwanakondoo?

Experience huwa hivi:
Siku ya kwanza mhusika atasema ngoja akajifikirie au atasema hayupo tayari ila baada ya wiki chache mhusika atarejea na kujisubmit mwenyewe kwa huyo " mtume na nabii"

Mtume atamwambia kwa kumsimanga " Hata Mungu mwenyewe ilimlazimu kumtoa kafara/dhabihu mtoto wake aliye mpenda ili kuirejesha dunia kwenye mikono yake baada ya dunia kuwa imeanguka kwenye mikono ya shetani ,u nani wewe hata usitoe kafara ili kuirejesha destiny yako ambayo sasa hivi ipo chini ya shetani?"

LITAANZA ZOEZI LA KAFARA

Baada ya hapo kitakacho fuata ni zoezi la kafara.

Kafara za South Africa ni tofauti na kafara za kibongo....

Itaendelea
 
Back
Top Bottom