Ukweli mchungu: Tatizo sio watekaji, tatizo liko vichwani mwa wananchi

Ukweli mchungu: Tatizo sio watekaji, tatizo liko vichwani mwa wananchi

Samia atosha tukutane2030

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
17,728
Reaction score
49,762
Watanzania wengi kichwani . Ukipiga stori na Mtanzania mwenzako utagundua hili.

Ni wachache sana ukikaa nao mezani kupiga stori utaweza kuondoka na kitu. Wengi wataishia kuropokaropoka tu.

Hii hali ya miongoni mwa Watanzania Mimi sijui ni man made au ni genes.

Vyovyote vile iwe man made au asili ya uzao wetu tufahamu kuna watu wananufaika na huu utahira wa wananchi.

Na ikitokea mwananchi mmoja ana ufahamu, ana nuru huyo atachukiwa , atafanyiwa mambo ya hovyo ikiwemo na kutekwa pamoja na kuuwawa.

Mfano ni huyu kijana Mdude_Nyagali , kijana huyu sio mtu mwenye elimu kubwa ila ana ufahamu kuzidi watu wengi wenye shahada ya kwanza, pili na tatu.

Anaweza kuongea kwa dk 2 tu lakini akaongea kitu kikubwa.

Sasa team ya wala asali hawataki watu kama hawa.

Wanataka watu wajinga wajinga na wenye kautahira kidogo.

Watu ambao unaweza ukawapa elfu 10 tu wakasahau shida zao zote, watu ambao ukiwapa chips yai na mirinda orange kwisha habari yao.

NAKUAMBIA uchaguzi mkuu 2020, jamaa mmoja wa makamo around 55 yrs alisema haendi kupiga kura. Mara akapita diwani aliyekuwa madarakani ambaye pia aligombea udiwani. Akampa buku 5, ghafla akabadili mtazamo na kwenda kupiga kura ya ndiyo kwa mh. Diwani.

Watu wajinga kama yule brother ndio wanatakiwa.
Smart people kama Ben Saanane , Mdude, na wengine hatupendwi.

Wanatamani sote ambao hatuendwshi na njaa pamoja na ujinga watunyofoe miguu
Kama angalau Watanzania millioni 10 wamgekuwa smart wasingehangahika na mtu yeyote.
 
Back
Top Bottom