Dubai ipi uliyotokaa na hujaambatanisha picha😂🙌
Wadangaji wanaenda Dubai mbona. Anajifanya mfanyabiashara anaenda Dubai anakaa siku 28 anarudi na kabegi kamoja ka vinguo na vipafyumu. Costs zote hizo, nauli, VISA na kila kitu anavirudisha kwa kabegi kamoja na pafyumu za elfu 60 @ za kuzugia? Tafuta kijana yeyote anayeenda Dubai mara kwa mara akwambie uko wanaishije.
Ukiachana na Dubai, pia mtaani wapo, Kigamboni yupo mmoja nimemtoa Snapchat analipia mtoto private school, anapanga na anaishi vizuri ila hafanyi kazi yoyote kazi kujiuza ila yeye anasafiri kwenda Zanzibar.
Nilipokuwa chuo kuna demu mmoja agemate kabisa, sikujua anajiuza mpaka alipoomba nimuunganishe na OF akanipa na details zake za bank na mengine. Baadae tulipoteana sijui alienda wapi maana alipanda hadhi, last time tunaonana alikuwa amenunuliwa IST sijui na nani. Alikuwa ananikubali sana kuna vitu technical nilikuwa namsaidia, nilikuwa naenda kwake all the time ila mara zote kapanga nyumba tofauti.
Na kuna mmoja age kama 20 hivi namkadiria. Alidai anasoma Diploma ila nahisi uongo nimemfuatilia pattern sioni akikanyaga chuo. Huyo nimekutana nae supermarket nikamlipia bill yake ndogo sana haikufika 15k. Nikapewa namba ajabu akawa anaomba hela kila asubuhi na jioni, nikawa nampa sometime simpi siku nikamuita akakubali ila akataja dau nikasema sawa, aligoma kupima HIV nikamtimua sikumpa hela alikuwa ashakula hapo kabla.
Ila namba yake bado ninayo namuona anapishana kwenye mahoteli, last week katoka Arusha alikuwa hotelini.
So kwa mimi na washkaji zangu ambao tukikaa tukajadili yanayotusibu inaonekana Dar ni jiji gumu sana kwenye mahusiano. Wapenzi wa mikoani angalau tunadumu nao ila kwa hapa Dar hawajanyooka.