Paulo alionya kuhusu kuwapo wanaonena kwa roho bila kutafsiri.
Mtu akinena kwa roho na atafsiri au awepo mtafsiri.
Ukiangalia walokole wengi wanaonena kwa roho hawajui hata wanasema nini.
hata kwenye kundi la wanaonena kwa roho hukuti hata mmoja anaetafsiri.
Angalieni msije mkawa mnapagawa na pepo na kunena maneno ya kufuru kwa mwenyezi Mungu.
Shetani ni mjanja sana
ilikuwa muhimu sana kujiuliza ni kwanini Paulo alisisitiza watu wanene kwa lugha, na akataka wawepo watafasiri. sheteni amewawekea upofu hapo tu, kawapiga chenga muamini kwamba kama mtafasiri hatakuwepo, hakuna kunena kwa lugha, na mmesahau kuwa kunena tunakosema sio kule mbele za watu tu, hata ukiwa chumbani kwako ukiwa unaomba unatakiwa kunena na kuomba kwa akili pia, kwasababu unapoomba unaongea na Mungu moja kwa moja, unapotumia akili yako mara nyingi unaomba kwa tamaa za mwili wako tu na mahitaji ya kidunia, ila Roho Mtakatifu akiwa anakusaidia kuomba yeye ni Mungu anajua yaliyopita na ya baadaye, anajua yepi ni mapenzi ya Mungu kwako unatakiwa kuomba. Paulo aliongea hivyo kwa waongofu wapya, kwasababu ilifika mahali kila mtu akawa ananena tu hawahubiri. watu wanaingia kanisani, wananena hadi mwisho wanaondoka wakiamini kuwa wameshaongea na Mungu inatosha, ndio sababu aliwaagiza sasa pamoja na kunena, wawe wanahutubu pia kwa faida ya wale wasionena. LAKINI HAKUKATAZA KWAMBA WATU WASINENE.
1 Wakorintho 14: 5 “Nami nataka ninyi nyote mnene kwa lugha, lakini zaidi sana mpate kuhutubu, maana yeye ahutubuye ni mkuu kuliko yeye anenaye kwa lugha, isipokuwa afasiri, ili kusudi kanisa lipate kujengwa”
kwanini hapo anasema anataka wote wanene kwa lugha? jiulize, na je, hapo aliongea watu wakiwa kanisani, what kwa maombi unayoomba peke yako nyumbani, huwa unanena? kunena kuna umuhimu? jibu ni NDIYO, unaponena kwa lugha Roho yako huomba, yaani Roho Mtakatifu ambaye ni nafsi ya Mungu yuleyule anakusaidia kupeleka maombi yote moja kwa moja, na maombi ya Roho ni uhakika kwamba yamefika. sio maombi yote unaomba yanafika kwa Mungu au anayasikiliza, mengine unaomba Mungu anayadharau. mfano, wewe ni masikini, unamwendea Mungu unaomba akupatie baiskeli, kumbe Mungu alipanga akupatie gari, nyumba na mtaji, unafikiri ombi lako la baiskeli atalisikiliza? au unaomba akupe cheo fulani, yeye anaona kabisa huyu akikaa pale juu ataniacha, atafungua milango ya mashetani itakayomfanya awe mbali nami na atauliwa au kupata madhara, unafikiri Mungu atakusikiliza? ndio maana Biblia inasema Roho mtakatifu anapoomba ndani yetu (unaponena), huomba sio kwa tamaa zako, yeye anajua nini unahitaji. sasa wewe ambaye hauna Roho, nani anakusaidia kuomba sawasawa na mapenzi ya Mungu?
1 Kor 14:15
Imekuwaje, basi? Nitaomba kwa roho, tena nitaomba kwa akili pia; mtaimba kwa roho, tena nitaimba kwa akili pia.