Swali kwa Wakatoriki.
Mama wa Yesu ambaye aliolewa na Yusufu jina lake ni Mariam.
Mathayo (Mat) 1:16
Yakobo akamzaa Yusufu mumewe Mariamu aliyemzaa YESU aitwaye Kristo.
Luka (Luk) 1:30
Malaika akamwambia, Usiogope, Mariamu, kwa maana umepata neema kwa Mungu.
Katika kila Ibada ya Wakatoriki iwe ya mtu mmoja au wawili au watatu au Jumuiya au Kanisani ni lazima katika sala atajwe mwanamke anayeitwa Maria.
Tena inaenda mbali mpaka anaimbiwa nyimbo za kumtukuza atasikia.
" Salamu Maria eeh mamaa, salamu Maria eeeeeh"
Inaenda mbali hadi katika kila kanisa ni lazima iwekwe sanamu zaidi ya moja ya huyo mwanamke aitwae Maria.
Inaenda mbali mpaka sanamu hiyo inasujudiwa na waumini na kuwekwa mbele ya mimbari huku waumini wakisali kwa kuitizama na kuomba kusamehewa dhambi.
Nimeisoma Injiri Yesu kuanzia Mathayo hadi Ufunuo wa Yohana sijawahi kuliona jina la Maria, katika Biblia zote.
Nimesoma Qurani hakuna Aya inamtaja mwanamke aitwaye Maria Bali inamtaja Mariam tena imempa sura nzima ingawa inamtaja kwa makosa makosa ila inamaanisha Mariam Mama wa Yesu.
فَأَتَتْ بِهِ قَوْمَهَا تَحْمِلُهُ ۖ قَالُوا يَا مَرْيَمُ لَقَدْ جِئْتِ شَيْئًا فَرِيًّا
(MARYAM - 27)
Akenda naye (mwanawe) kwa jamaa zake amembeba. Wakasema: Ewe Maryamu! Hakika umeleta kitu cha ajabu!
Swali naliwauliza Wakatoriki.
Huyo Maria ni nani ?
Wakatoriki Naomba Jibu Tafadharini