Ukweli mchungu: Zanzibar tunaishi kwa kudra za Tanganyika!

Mimi nimesema hivi.
Hicho unachosema ni misaada mara zote ni mikopo (utapaswa kulipa) na kina mtego (kuna masharti). Je, Zanzibar tunakopesheka kirahisi?
Na je tuna uwezo wa kulipa?

Wakopeshaji hawaji bure bure, wanaweza kuja kuikopesha SMZ ili mwisho wa siku Zanzibar ishindwe kulipa na visiwa vipigwe bei.

Mwisho kabisa, fahamu Serikali ya muungano ni moja ya taasisi inayoongoza kuikopesha pesa SMZ, na mara nyingi SMZ wanashindwa kulipa na serikali ya muungano inapotezea kisiasa kwa kusema ni ruzuku, pesa ya maendeleo au kuingizwa kwenye kasma ya bajeti ya mambo ya muungano.
 
Zanzibar ni nchi mpaka hapo , anakopa kwa uwezo wake atapata mikopo kutoka kwa nchi za Asia kulingana ukaribu wao ...Mega porject ila na nyie mjiandae kurudisha pesa ya uanzishwaji wa BOT.
Zenji wataheshimika zaidi watafika mbali , wana bandari lango la biashara haswa sisi ndugu zao wa kanda ya pwani tutafanya nao biashara sana.
Zanzibar ilikuwepo kabla ya TZ ikaporwa .
 
Hakuna mwarabu ht mmoja ataeitwa, watakuja wenyewe....infact watarudi kuja kuijenga zanzibar yao baada ya kuikimbia. Na waliikimbia baada ya mapinduzi na muungano uso tija kwa wazanzibari. Wanasubiri kwa hamu hio siku ifike
 
We unadhani bandari ipo mahututi kwa sababu gani we mzanzibari wa mchongo!!!?
 
Mapato kikodi ya Zanzibar,
Mwaka 2021/2022,bilioni 374.2
Mwaka 2022/2023 bilioni 579.5
Mwaka 2023/2024 bilioni 565.8
Katika Mwaka wa Fedha uliokwisha wa makusanyo ya bilioni 565.8 wastani wa makusanyo ni 47 bilioni kwa mwezi.

Katika Mwaka wa Fedha 2023/2024 bajeti ya Zanzibar ni 2.8 trilion: trilion 1.3 matumizi ya kawaida na 1.5 trilioni ni maendeleo.Una finance vipi bajeti ya 2.8 trilioni kwa makusanyo ya 565 bilioni kwa Mwaka?.Kama sio pesa zinahamishwa kutoka Tanzania bara kufanance bajeti ya Zanzibar?.au mnataka kuniambia mnakwenda kukopa 2.3 trilioni kila mwaka kwa makusanyo ya 565 bilioni??.

Kiuchumi huu muungano unaumiza sana upende wa Tanzania bara,ni basi tu Watanganyika wengi ni matahira tusio jitambua na kufatilia mambo.Zanzibar haiwezi ku survive bila Tanganyika watakufa vibaya sana.takwimu zinaongea.
 
jamani si mna wajomba zenu arabuni huko? au ndio mlisema ma hizbu chotara
 
Ungekuwa unaongea haya kama Tanganyika ndio wangekuwa wanalalamika.

Umewahi ona wapi kisiwa kikashindwa kujiendesha?

Mwisho aliyeandika hapa ni Mtangangika anajitoa ufahamu tuu
 
Tuna mambo 22 ya Muungano,maana yake ni kuwa tuna Wizara karibu 5 zinahusuka na Muungano moja kwa moja; ulinzi,sheri na katiba,Fedha,mambo ya ndani, utumushi, uchukuzu.

Kwa makusanyo ya Zanzibar ya Bilioni 565? isiyoweza kukidhikuu support bajeti yao wenyewe watatoa wapi hela za kuchangia katika bajeti za hizo Wizara za Muungano.

Wazanzibar kaeni kimya tu,maana mnaigharimu sana Serikali kuliko mnavyo dhania.
 
Mkuu ulichosema ni kweli kabisa, sababu za huu MUUNGANO zilikuwa zimeegemea katika siku moja kuiona THE UNITED STATES OF AFRICA (USA) na mpango wa Nyerere, Nkuruma na Gaddafi ilikuwa kuziona nchi zinazokaribiana kikanda zinaungana kwanza kurahisisha muunganiko wa Afrika nzima hapo baadae, ndiomana unaona baada ya lengo hilo kufa na kubaki nadharia tu miaka yote hii zaidi ya 60 hakuna maelewano mazuri ya kijumuiya EAC, ECOWAS, SADC's etc kila nchi inafanya kitu inachoona kina faida nacho.
Malengo ya wazee na vijana wa sasa ni tofauti, vijana hawaoni umuhimu wa huu muungano wa Tanganyika na Zanzibar ikiwa Zanzibar ni sovereign country while Tanganyika is not. Kama ni MUUNGANO bhasi kuwe na serikali 3 au moja tu itakayoiwakilisha TANZANIA.
 
Ungekuwa unaongea haya kama Tanganyika ndio wangekuwa wanalalamika.

Umewahi ona wapi kisiwa kikashindwa kujiendesha?

Mwisho aliyeandika hapa ni Mtangangika anajitoa ufahamu tuu
Usiongee kwa maneno,ongea kwa takwimu.zanzibar inafanana kwa vitu vingi na visiwa vya Seychelles & Comoro hali za kiuchumi za hizo nchi unazijua?.uchumi wa Zanzibar ni mdogo hawezi kujiendesha watakuwa maskini wa kutupwa.
 
Tangu 1964 mpaka sasa Zanzibar ni nchi, na hakuna nchi iliyozuiwa au inayozuiwa kuja kuwekeza mega projects Zanzibar hata sasa. Kwa kifupi suala la uwekezaji sio jambo la muungano. Sasa jiulize, kwanini hao unaosema hawajaja mpaka sasa, kwanini uamini kuwa muungano ukifa watakimbilia kuja kuwekeza Zanzibar?

Kuhusu pesa za mtaji wa uanzishwaji wa BOT zilizotolewa na Zanzibar tulishajibu humu JF. Labda turudie tu kusema.
Thamani ya zile pesa za mtaji ni kiasi gani kiasi cha kuamini ni pesa nyingi?
Mkataba ulitaka Zanzibar ilipwaje fidia?
Zanzibar ni lini tuliwahi kutoa hata senti tano ya uendeshwaji wa BOT?
Faida za kuanzishwa kwa BOT Zanzibar tutawezaje kuzirudisha ikiwa tutadai turudishiwe mtaji wetu?
Hasara ambayo mara kwa mara uliikumba BOT kiasi cha kuathiri mtaji wake wa awali zinafidiaje mtaji wa Zanzibar?
Zanzibar tulitoa lini tena kiasi kingine cha mtaji kuweza kuifufua BOT wakati ilipokuwa imedorora?

Kwa sasa ukanda wa Afrika mashariki Bandari zipo nyingi na zimeendelezwa. Zanzibar hatuna tena upekee wa bandari, tumedorora. Hata sasa bandari iko chini ya SMZ, haihitaji muungano uvunjike ili ipanuke, haina msaada mkubwa sana kama zamani.

Kuhusu undugu, biashara na ushirikiano wa Zanzibar na bara (sio pwani tu), umekuwepo kabla ya ukoloni, wakati wa ukoloni, wakati wa uhuru, kwenye huu muungano na hata baada ya huu muungano, haina issue yoyote kwenye hii hoja yangu. Hapa tunazungumzia jinsi muungano unavyotusitiri wazenji kupitia pesa za wavuja jasho wa kitanganyika.
 
Usiongee kwa maneno,ongea kwa takwimu.zanzibar inafanana kwa vitu vingi na visiwa vya Seychelles & Comoro hali za kiuchumi za hizo nchi unazijua?.uchumi wa Zanzibar ni mdogo hawezi kujiendesha watakuwa maskini wa kutupwa.
Punguani mmja wewe, unadhani Seychelles ni LDC kama Tanzania?

Takwimu zipi? Kama sio Bara kuiba pesa ya Zanzibar,Wanaweza kuwa na Bajeti ya Trilioni 2 Kwa mwaka ,Kitu gani watashindwa kugharania hapo?
 
Hakuna mwarabu ht mmoja ataeitwa, watakuja wenyewe....infact watarudi kuja kuijenga zanzibar yao baada ya kuikimbia. Na waliikimbia baada ya mapinduzi na muungano uso tija kwa wazanzibari. Wanasubiri kwa hamu hio siku ifike
Kwani Zanzibar tulishaacha kuimba mapinduziiiii, daima!
Unadhani tunaimba vile ili kujifurahisha eeeeh?

Tunamaanisha, mwarabu tulimuondoa milele, hatutaki arudi tena pale, na akirudi tutampindua tena. Hiyo ndio dhana kamili ya mapinduzi matukufu ya Zanzibar.
 
Tatizo linalowasumbua Wazanzibar ni kutaka watengane na Bara ili wajiuze kwa Mwarabu.
Wanafikiri Mwarabu atawapa kila kitu bure!
 
umeandika vitu vingi na kuchanganya mambo. Tuchambue.
Ndio. Ni kwa sababu kuna haja ya kufanya hivyo ili kujenga hoja. Hapa ndo sikubaliani kwani hakuna hoja. Hivi Wazanzibari tunaishi kirahisi kwa mgongo wa Watanganyika ? Weka ushahidi wa hili. Huenda hujui kinachoendelea na unasikia maneno yasiyo na ushahidi. Hakuna siku, mimi nasema, Wazanzibari wameishi kwa mgongo wa Watanganyika, na haitotokea. Sababu kubwa ni kwamba Watanganyika hawana moyo huo. Unapozungumza haya ni kama hujui yaliyotokea hata Tanganyka na kwengineko. Hivi wakoloni walipokuja walikuja kugawa pesa au kutawala? Hivi Nyerere na Karume walikuja kugawa pesa au kutawala?

Hili la mapinduzi naomba nikukumbushe, kama umesahau, kwamba Zanzibar ilidai uhuru kutoka kwa Mwingereza, kwani Wazanzibari (Waafrika na Waarabu) walitawaliwa na Mwingereza, na ndo maana wote- Waafrika na Waarabu- walidai uhuru kwa Mwingereza. Na ni Mwingereza aliyekabdhi bendera ya uhuru tarehe 10 Disemba, 1963. Mara nyingi ukweli huu hausemwi. Unajua ni kwanini? Jiulize halafu huenda utapata jibu.

Nimeyaweka niliyoyaweka kukunesha kwamba Zanzibar inaweza kujiendesha yenyewe, tofauti na unavyotaka watu tuamini.
Kwa sasa ukanda wa Afrika mashariki Bandari zipo nyingi na zimeendelezwa. Zanzibar hatuna tena upekee wa bandari, tumedorora. Hata sasa bandari iko chini ya SMZ, haihitaji muungano uvunjike ili ipanuke, haina msaada mkubwa sana kama zamani.
Hili la bandari ungeliwacha, limekupita kimo. Hivi unajua kwanini Tanganyika inataka kujenga bandari Bagamoyo, sehemu iliyo pua na mdomo na Zanzibar? Jitahidi kufunika kombe ili mwanaharamu apite. Kuna mambo huyajui kwani wewe si mjuzi. Mkuu sasa nimejiridhisha kwamba hujui kuchambua kilichoandikwa. Nilipozungumzia biashara nlkuwa najibu hoja yako uliyodai Zanzibar haina kazi za maana na hata biashara haina, hivyo inaishi kwa mgongo wa Tanganyika.

Zawadini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…