Ukweli ni kwamba kama Nchi tunahitaji watu kama Tundu Lissu na Hayati Magufuli walioboreshwa

Ukweli ni kwamba kama Nchi tunahitaji watu kama Tundu Lissu na Hayati Magufuli walioboreshwa

Habari JF , TL na JPM personality zao zinafanana sana ukiachana tofauti zilizopo za kisiasa na ni wazalendo kweli kweli

Hivyo Kiuhalisia hakuna zuri ambalo JPM alifanya Tundu lissu asingefanya ukiachana na matamshi ya TL kulingana na kuwa nje box .

Vivyo hivyo hakuna baya ambalo JPM alifanya TL hawezi fanya kama hatoboreshwa .

JPM pamoja kuwa Rais bora alihitaji maboresho yafuatayo ambayo hata TL anahitaji
1. Kupokea ushauri ,kuutafakari kama mzuri kuufanyia kazi .

2.Kukubari kukosolewa , yaani sio mtu akikosoa anakuwa adui

3.Kama binadamu huwezi kuwa sahihi muda wote ,hivyo ni vizuri kufikiri zaidi kabla ya kutenda au kusema .

Bado naamini TL ni presidential material aandaliwa .
View attachment 2985467
Yaliyosemwa hapa hata TL angekuwa CCM kwa nafasi ya JPM yasingekuwa na Tofauti .

Ni mtazamo tu wana CDM na CCM muelewe .​
inchi gani hiyo?

yaan Tz ndio inahitaji vibaraka wa mabwenyenye ya magharibi 🙄🐒
 
Lissu anamudu tu taaluma yake ya sheria, ila JPM alikuwa mwanasiasa mzuri na mzalendo.
 
Habari JF , TL na JPM personality zao zinafanana sana ukiachana tofauti zilizopo za kisiasa na ni wazalendo kweli kweli

Hivyo Kiuhalisia hakuna zuri ambalo JPM alifanya Tundu lissu asingefanya ukiachana na matamshi ya TL kulingana na kuwa nje box .

Vivyo hivyo hakuna baya ambalo JPM alifanya TL hawezi fanya kama hatoboreshwa .

JPM pamoja kuwa Rais bora alihitaji maboresho yafuatayo ambayo hata TL anahitaji
1. Kupokea ushauri ,kuutafakari kama mzuri kuufanyia kazi .

2.Kukubari kukosolewa , yaani sio mtu akikosoa anakuwa adui

3.Kama binadamu huwezi kuwa sahihi muda wote ,hivyo ni vizuri kufikiri zaidi kabla ya kutenda au kusema .

Bado naamini TL ni presidential material aandaliwa .
View attachment 2985467
Yaliyosemwa hapa hata TL angekuwa CCM kwa nafasi ya JPM yasingekuwa na Tofauti .

Ni mtazamo tu wana CDM na CCM muelewe .​
Naona tofauti kwamba Magufuli aliamini kuwa anajua kila kitu wakati Lissu ni kinyume chake.
Magufuli alipoambiwa achukue fomu kabla, alisema watu watalimia meno.
Hata hivyo Lissu ana mapungufu yake ambayo ni tofauti na Magufuli.
 
Binafsi sijawahi ona tofauti ya jpm na lissu zaidi ya Chama
Tofauti: Lissu kwake utawala wa sheria ndio kila kitu. Hakuna aliye juu ya sheria na hakuna huruma katika kutekeleza sheria. Hakuna mtu kusamehewa hata kama kakosea kwa “nia njema”. No flexibility, no leniency, no double standards. Ni adhabu tu. Hapo ndipo ulipo udikteta wa Tundu Lissu.

Bila kusahau msimamo wa Lissu kuwa akiingia madarakani kazi yake ya kwanza itakuwa kukamilisha mchakato wa katiba mpya itakayoleta demokrasia ya kweli nchini. Tumuamini au tusimuamini?

Magufuli kwake sheria hazikuwa na maana bali “uzalendo” na “maslahi ya taifa”. Kwenye hayo ikibidi kwake yeye ni “hatufungwi na sheria”, zinaweza kupindishwa hata kutupiliwa mbali kama akiona zinapishana na mtazamo wake kuhusu uzalendo na maslahi ya nchi. Kwake sheria zinachagua mahali na watu wa kushughulikiwa kulingana na “maslahi ya taifa” - kwa uwazi hata gizani.

Hizo ndizo tofauti za udikteta wa Magufuli na unaodhaniwa kuwa wa Lissu akiwa madarakani. Na katika mazingira ya katiba iliyopo.
 
Vivyo hivyo hakuna baya ambalo JPM alifanya TL hawezi fanya kama hatoboreshwa
Huu mstari hukutumia akili kabisa kuuandika. Utawezaje kulinganisha uchafu ule wa Magufuli na wa mtu mwingine yeyote? Hata huwezi kamwe kuulinganisha uchafu huo wa Maguful akiwa Rais, na Magufuli kabla ya kuukwa urais.

Ila ninakubaliana na wewe katika mlinganisho wako katika mistari hiyo ya mwanzo.
Ni dhahiri kabisa Tanzania ni nchi inayomhitaji sana kiongozi 'forceful' asiyechekacheka na wapuuzi toka ndani au nje ya nchi.

Siwalaumu kwa hilo hata kidogo, na ni matumaini yangu kwamba wataziona baadhi ya sifa hizo ndani ya Tundu Lissu.
 
Back
Top Bottom