Ukweli ni kwamba kama Nchi tunahitaji watu kama Tundu Lissu na Hayati Magufuli walioboreshwa

inchi gani hiyo?

yaan Tz ndio inahitaji vibaraka wa mabwenyenye ya magharibi 🙄🐒
 
Lissu anamudu tu taaluma yake ya sheria, ila JPM alikuwa mwanasiasa mzuri na mzalendo.
 
Naona tofauti kwamba Magufuli aliamini kuwa anajua kila kitu wakati Lissu ni kinyume chake.
Magufuli alipoambiwa achukue fomu kabla, alisema watu watalimia meno.
Hata hivyo Lissu ana mapungufu yake ambayo ni tofauti na Magufuli.
 
Binafsi sijawahi ona tofauti ya jpm na lissu zaidi ya Chama
Tofauti: Lissu kwake utawala wa sheria ndio kila kitu. Hakuna aliye juu ya sheria na hakuna huruma katika kutekeleza sheria. Hakuna mtu kusamehewa hata kama kakosea kwa “nia njema”. No flexibility, no leniency, no double standards. Ni adhabu tu. Hapo ndipo ulipo udikteta wa Tundu Lissu.

Bila kusahau msimamo wa Lissu kuwa akiingia madarakani kazi yake ya kwanza itakuwa kukamilisha mchakato wa katiba mpya itakayoleta demokrasia ya kweli nchini. Tumuamini au tusimuamini?

Magufuli kwake sheria hazikuwa na maana bali “uzalendo” na “maslahi ya taifa”. Kwenye hayo ikibidi kwake yeye ni “hatufungwi na sheria”, zinaweza kupindishwa hata kutupiliwa mbali kama akiona zinapishana na mtazamo wake kuhusu uzalendo na maslahi ya nchi. Kwake sheria zinachagua mahali na watu wa kushughulikiwa kulingana na “maslahi ya taifa” - kwa uwazi hata gizani.

Hizo ndizo tofauti za udikteta wa Magufuli na unaodhaniwa kuwa wa Lissu akiwa madarakani. Na katika mazingira ya katiba iliyopo.
 
Vivyo hivyo hakuna baya ambalo JPM alifanya TL hawezi fanya kama hatoboreshwa
Huu mstari hukutumia akili kabisa kuuandika. Utawezaje kulinganisha uchafu ule wa Magufuli na wa mtu mwingine yeyote? Hata huwezi kamwe kuulinganisha uchafu huo wa Maguful akiwa Rais, na Magufuli kabla ya kuukwa urais.

Ila ninakubaliana na wewe katika mlinganisho wako katika mistari hiyo ya mwanzo.
Ni dhahiri kabisa Tanzania ni nchi inayomhitaji sana kiongozi 'forceful' asiyechekacheka na wapuuzi toka ndani au nje ya nchi.

Siwalaumu kwa hilo hata kidogo, na ni matumaini yangu kwamba wataziona baadhi ya sifa hizo ndani ya Tundu Lissu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…