Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kweli kabisa mkuu! Nafikri baada ya Oyster bay na Mikocheni inayofuata kwa uzuri wa mitaa sasa ni Kijichi! Kunduchi beach haoni ndani! Atakazidi maghorofa tu lakini siyo uzuri wa mitaa! Aliyeipanga Kijichi apewe sifa yake!Kijichi ndio Oysterbay ya Temeke
Duh, hata mimi nilikuwa sijawahi kuvutiwa na Temeke tangu nafika mara ya kwanza Dar miaka ya 80's lakini juzi nimeingia ndani ndani huko ndipo nakutana na Kijichi, looh! Pazuri bwana!Temeke ukiiondoa Kijichi, kwingine naona pagumu sana kuishi. Sijawahi kupapenda
Kuanzia Chanika, Mvuti, Mbagala Wilaya yote ya Mkuranga, Mkoa wa Lindi, Mtwara na Zanzibar ni mwendo wa futi 50x40 ambazo ni sawa na mita 17x13.Hili la kupima viwanja futi 30 si lilipigwa marufuku na Lukuvi? Limerudi tena? Hii wizara haina akili sawasawa!
Ni aibu sana! Unajenga nyumba halafu huna hata kipande cha kuweka mboga mboga! Ukitaka kufuga kuku wa kitoweo labda uishi nao ndani! Hovyo kabisa!Kuanzia Chanika, Mvuti, Mbagala Wilaya yote ya Mkuranga, Mkoa wa Lindi, Mtwara na Zanzibar ni mwendo wa futi 50x40 ambazo ni sawa na mita 17x13.
Ajabu ni kwamba kuna kampuni mbili ninazifahamu ambazo zina sites Kibaha na Bagamoyo ambapo huko hupima kwa mita, ila sites zao za Homboza, Mvuti, Chanika na Mkuranga hupima kwa futi.
Ninadhani ni utamaduni wa huko!
Mkondo wa maji ndio tatizo hapa, sio uzuri au ubaya wa ardhi.Bei ya Viwanja huko Tegeta, Bunju na Boko ni kubwa mno ukilinganisha na Mbagala, lakini linapokuja suala la Mvua Mbagala haina mafuriko kabisa kulinganisha na Tegeta, Bunju na Boko.
Sasa kinachowafanya wengi kukimbilia huko ni nini?