Ukweli ni kwamba mkulima kijijini anaumia zaidi na Mfumuko wa Bei, tofauti na tunavyoaminishwa

Ukweli ni kwamba mkulima kijijini anaumia zaidi na Mfumuko wa Bei, tofauti na tunavyoaminishwa

Kwa asilimia kubwa huwa ni mipangilio isiyo mizuri ya familia. Lazima watu wajitahidi kuweka akiba ya chakula. Niliwahi kuishi Mwanza na kuliona hili, mkulima anavuna mazao mengi na kipindi cha mavuno ndiyo ngoma huwa zimeshamiri (sijui inaitwa gobogobo?). Pale chakula ndiyo kinapotea kwa wingi bila ya kujua kuwa kesho kutwa kitahitajika kwa ajili ya familia.
Wakipigwa na hii njaa kisawasawa watapata akili, msimu ujao watakuja makakini
 
Hakuna mkulima mdogo,ambao ndio 95% ya wakulima nchini,ambaye anauza sasa kwa bei kubwa.
Wanaouza ni wachuuzi ambao hawajui hata mpunga unavumwaje shambani.
Wakulima walushauza kitambo kwa bei ya njaa kwa sababu hata maghala ya kutunzia vyakula hawana

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
Kuhifadhi gunia 3 za mahindi au mchele unahitaji ghala?
 
Inafikirisha sana, mkulima anauza magunia ya mahindi apate pesa ya sukari na sabuni n.k halafu anakwenda kununua kilo moja ya sembe.
Mimi ni mkulima, hakuna mkulima lofa wa hivyooo... Wasukuma na wengine huko vijijini wana vihenge vya kutunzia mazao yao kwa ajili ya chakula cha familia yake. Ukiona mkulima kauza mazao yoooteee mpaka akiba ya chakula basi jua huyo ni sawa tuu na mfanyakazi ambaye anapata mshahara mwisho wa mwezi na wote anaenda kuumalizia bar... Ndani ya siku 3 mifuko mweupe.... Hata Babu yangu nilikuwa namuona tukijaza kihenge mahindi, maharage, mihogo mikavu halafu tunakisiriba juu chote ili kusubiri kipindi cha shida.
 
Ila waafrika huna ni watu tunao penda kudekezwa kama watoto.

Kwani hao wakulima huwa wanashikiwa bunduki kuuza hayo mazao yao kwa bei ndogo?

Je, hao wakulima ni watoto wadogo mpaka washinde kuweka akiba ya chakula mpaka wanauza chote?

Yaani mtu umeowa una mke na watoto unashindwa kujua kuwa ukivuna unatakiwa kuweka akiba ya chakula kwa ajili ya familia yako mpaka ukumbushwe na serikali? Mbona kuoa na kuzaa watoto haukiusubili serikali ukukumbushe?

Je, wafanya biashara unao waita madalali wao hawana haki ya kupata faida?
Mkuu hii ni pure exaggeration ya watu wa mijini eti wanawapangia wakulima namna ya kuendesha maisha yao. Hivi ingekuwa wazee wetu hawana elimu ya kuweka akiba ya mazao yao wanayovuna ili yawasaidie mpaka mavuno mengine huko vijijini watu wangeishije? Niambie ni mwaka gani serikali iliwahi kugawa unga mchele, maharage etc bure huko vijijini kote nchini wakati wa njaa au mavuno kidogo? Miaka na miaka wakulima wanajua wanalimaje na jinsi ya kutunza vyakula vyao. Leo mtu wa mjini eti anamuona mkulima hana akili [emoji23] [emoji23]
 
Lakin kuna wakulima ambao nawajua, mwaka jana wamenufaika sana kwa kuuza bei nzuri mpunga wao,wengine walijenga, wengine hyo pesa waliwekeza kwenye biashara zao zingine.
Nilikuwa Moshi, kule kwenye irrigation schemes za mpunga kuna wakulima wamevuna mpunga vizuri sana, wakapeleka mashine kuukoboa na kuwauzia wanunuzi kutoka Kenya, yaani ekari moja mkulima kapata mpaka milioni 6, wenye ekari 2, 3 na zaidi ndiyo usiseme yaani wakulima wamenunua bodaboda, bajaj, power tiler etc kila mkulima anafurahia kazi yake. Na hapa niseme kwamba hata wale walioamua kuuzia mazao yao shambani bei kwa gunia ilikuwa si chini ya laki moja na elfu 20 au 30. Lakini walio wengi walikuwa wanapeleka mipunga yao mashine wanakoboa na kuuza mchele, tena kwa kilo. Huko mashine wanakuja wanunuzi wengi na wabashindana bei.
 
Hivi nyinyi mbona mna akili za kipumbavu? wananyonywa kwani hao mnao waita madalali walienda kwa wakulima na bunduki na kuwarazimisha wawauzie hayo mazao yao kwa hiyo bei inayo itwa ndogo?

Alafu kingine huyo mfanya biashara yeye hana haki ya kupata faida kiasi kwamba yeye akienda akanunua kwa mkulima aje akuuzie bei unayo taka ww hata kama hailipi.

Mna mawazo ya kimasikini sana.
Hasira za nini kwangu?
Sie tunachojua huu mfumko wa bei za vyakula unawafaidisha wachache.
Hakuna mkulima anayefaidika.Usitumie nguvu nyingi kutetea uongo.
Mbona mambo yako wazi sana?

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
 
Nilikuwa Moshi, kule kwenye irrigation schemes za mpunga kuna wakulima wamevuna mpunga vizuri sana, wakapeleka mashine kuukoboa na kuwauzia wanunuzi kutoka Kenya, yaani ekari moja mkulima kapata mpaka milioni 6, wenye ekari 2, 3 na zaidi ndiyo usiseme yaani wakulima wamenunua bodaboda, bajaj, power tiler etc kila mkulima anafurahia kazi yake. Na hapa niseme kwamba hata wale walioamua kuuzia mazao yao shambani bei kwa gunia ilikuwa si chini ya laki moja na elfu 20 au 30. Lakini walio wengi walikuwa wanapeleka mipunga yao mashine wanakoboa na kuuza mchele, tena kwa kilo. Huko mashine wanakuja wanunuzi wengi na wabashindana bei.
Tatizo la kusoma madesa unadhani hata kwenye maisha ni kama kujibu mtihani wa desa.

Hivi hao unaowaita wakulima wa irrigation scheme ndio kama akina Mbowe na matajiri wanaolima kwa starehe?

Ni irrigation scheme ngapi zipo nchini?

Sisi ndio tunataka serikali iwekeze huko ili watu wa chini pia wapate nafasi ya kujiinua kiuchumi wafaidi ruzuku za pembejeo kutoka serikalini.
Kwa sasa pembejeo zinatolewa kwa kodi ya umma,wanaofaidi ni watu wachache ambao ni madalali wa mazao.

Kibaya zaidi kuna waganda wakati wa mavuno wananunua mzigo ukiwa bado shambani na hivyo wanafaidika sana na hiyo ruzuku inayotolewa na serikali.
Usimamizi mbaya wa Sera za fedha ni tatizo nchi hii

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
 
Watanzania wenzangu ifike mahali tuwe tunafuatilia mambo Kwa kina na tusiwe benderea fuata upepo.

Leo hii kuna mfumuko wa bei ya vyakula tunaambiwa mkulima anafaidi.

Nasema hivi huu ni uongo Kwa asilimia 100. Mchana kweupe.

Mara zote wakulima huuza mazao Yao kipindi cha mavuno kipindi bei iko chini kabisaa.

Sasa leo hii tunapoongea haukuna mkulima anayeuza mazao Kwa 3000 kilo ya mchele.

Anayenufaika ni Dalali aliyenunua mazao bei ikiwa chini kabisaa.

Amini usiamini mkulima yuleyule sasa Analía njaa na kuhangaika kununua tena chakula.

Je, ushawahi kujiuliza serikali ikitoa chakula cha msaada huwa inapeleka mjini au kijijini?

Ukipata jibu hapo juu ndo utaelewa Nini kinaendelea.

MWISHO.

Serikali Makini lazima ilinde usalama wa chakula wa watu wake Lazima kucontrol inflation.

Ndo maana Mataifa yaliyoendelea watu kuingia barabarani Kisa mfumuko wa bei ni Jambo la kawaida sana..

Mfumuko wa bei kwa lugha ya kitaalamu ni kudorola Kwa Uchumi huo ndo ukweli wenyewe japo watu wanajificha nyumba ya kumsaidia mkulima.

Tukisema Kila mtu afe na chake huyo mkulima bidhaa Za viwandani vikipanda bei mara dufu na huduma nyingine Za kijamii atatoboa?

Nasema serikali Lazima i control inflation kulinda purchasing power ya Tanzania Shilings/ Thamani ya pesa Yetu.
Tumepiga mayowe humu kuwa Bashe analiingiza chaka hili taifa kwa upatikanaji wa chakula cha bei himilivu. Sasa hivi tuna mlaumu aliye mteua kwani ilibidi amkemee huko huko kwenye vikao vyao.
 
Kwa asilimia kubwa huwa ni mipangilio isiyo mizuri ya familia. Lazima watu wajitahidi kuweka akiba ya chakula. Niliwahi kuishi Mwanza na kuliona hili, mkulima anavuna mazao mengi na kipindi cha mavuno ndiyo ngoma huwa zimeshamiri (sijui inaitwa gobogobo?). Pale chakula ndiyo kinapotea kwa wingi bila ya kujua kuwa kesho kutwa kitahitajika kwa ajili ya familia.
Mkulima kutunza chakula ni ngumu kwasababu hawana pesa za kujikimu mahitaji ya kila siku kwaiyo lazima auze chakula ili apate kununua sukari, mafuta, uniform za watoto wa shule na kama ana mwanae yupo chuo mbali na nyumbani atamtumia pesa za kujikimu, familia kuumwa.

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Hivi duniani kuna biashara isiyo kuwa dalali?
Inaonekana ww ni mweupe kwenye biashara bidhaa yeyote ile mpaka inafika kwa mtumiaji huwa imepitia kwenye cheni ndefu.
Hata wakifanya hivyo unavyo sema ww bado hao unao waita madalali hawa epukiki maana sio kila mtu ataweza kusafirisha mazao yake kupeleka kiwandani.

Alafu kingine biashara ya mazao sio kama biashara ya simu au gari ya kwamba yana kuwa na bei moja miaka yote.

Bei ya mazao huwa haitulii kwenye bei moja kwa sababu bei ya mazao huamuliwa na musimu husika ina maana msimu ukiwa na mazao mengi basi bei ya mazao hushuka na msimu ukiwa na mazao ukiwa na mazao machache bei ya mazao upanda.
Serikali inanunua chakula na muifadhi kwenye maghala yake, mfano kwenye mazao ya korosho wakulima wanamfumo wa stakabadhi ghalani uwezi kusika mkulima wa korosho kauza korosho zake zote shambani kabla ya kuzivuna

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Ila waafrika huna ni watu tunao penda kudekezwa kama watoto.

Kwani hao wakulima huwa wanashikiwa bunduki kuuza hayo mazao yao kwa bei ndogo?

Je, hao wakulima ni watoto wadogo mpaka washinde kuweka akiba ya chakula mpaka wanauza chote?

Yaani mtu umeowa una mke na watoto unashindwa kujua kuwa ukivuna unatakiwa kuweka akiba ya chakula kwa ajili ya familia yako mpaka ukumbushwe na serikali? Mbona kuoa na kuzaa watoto haukiusubili serikali ukukumbushe?

Je, wafanya biashara unao waita madalali wao hawana haki ya kupata faida?
Hujui maisha unalelewa bado kaa kimya. Unadhani wanauza Kwa kupenda?
 
Tatizo la kusoma madesa unadhani hata kwenye maisha ni kama kujibu mtihani wa desa.

Hivi hao unaowaita wakulima wa irrigation scheme ndio kama akina Mbowe na matajiri wanaolima kwa starehe?

Ni irrigation scheme ngapi zipo nchini?

Sisi ndio tunataka serikali iwekeze huko ili watu wa chini pia wapate nafasi ya kujiinua kiuchumi wafaidi ruzuku za pembejeo kutoka serikalini.
Kwa sasa pembejeo zinatolewa kwa kodi ya umma,wanaofaidi ni watu wachache ambao ni madalali wa mazao.

Kibaya zaidi kuna waganda wakati wa mavuno wananunua mzigo ukiwa bado shambani na hivyo wanafaidika sana na hiyo ruzuku inayotolewa na serikali.
Usimamizi mbaya wa Sera za fedha ni tatizo nchi hii

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
Uzuri ni kwamba serikali imeshafanya maamuzi, hakuna kufunga mipaka na wakulima ruksa kuuza mazao yao kokote. Sasa wewe endelea kulia lia hapo na visababu vyako vya kuokoteza. Hizo irrigation schemes nilizokupa mfano ni wakulima wenyewe wamejiongeza na kuzitengeneza, wakulima wa kawaida kabisa, ukiwa na muda nenda ukajionee mwenyewe hakuna cha matajiri wala nini. Wakati wewe unalia lia hapo mimi mwenzio nimewahi huku Mvomero nalima mahindi, mpunga, mbaazi nk mbolea za ruzuku, hata wakileta figisu tutanunua tuu kwa bei hata laki moja kwa sababu gunia zilizoko stoo bei ni laki mbili gunia moja. Wakulima wengi sana wamepanua mashamba yao, watumishi na wafanya biashara wako huku wamekodi mashamba, ekari moja kwa msimu ni elfu 50. Mvua zinanyesha vizuri mazao yanaenda vizuri, tukutane Juni/July kwenye mavuno huku wewe ukiendelea kulalamika badala ya kutumia hiyo fursa. Wewe endelea kubeti na kuchana mikeka [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Kwanza mfumuko wa bei na kudorora kwa uchumi ni mambo mawili tofauti kabisa. Pili, kuonea wakulima ndiyo kumezaa hao madalali na walanguzi. Wakianza kuja watu kutoka Kenya , Uganda, SS, SA nk, hutaona hao madalali wana nguvu waliyonayo. Leo mkulima anaonewa na dalali kwa sababu hana pengine kwa kuuza.
Umeongea vizuri, nimetoa mfano hapa kule Moshi wakulima wa mpunga wakivuna wanapeleka mpunga wao kuukoboa mashine ili wauze mchele kwa bei nzuri. Wananunua huo mchele siyo madalali bali ni wafanya biashara kutoka Kenya. Hata kama mkulima hana pesa ya kuvuna ekari zake mbili au 4 za mpunga anaenda tuu kumuona mwenye mashine ya kukoboa anamkopesha pesa ya kuvunia na usafiri kwa masharti kwamba mzigo utakobolewa kwenye mashine zake ili mashine zipate kazi. Wanunuzi wa mchele kutoka Kenya na kwingineko wao huja kununua mchele kwenye hizo mashine kwa kushindana. Mkulima akiona bei ya mchele imeshuka anaweza kuacha hapo mashine mzigo wake hata miezi 4 mpaka 6. Hapo hakuna cha dalali wala nani.
 
Huna uelewa japo kiduchu wa uchumi na fedha, inflation ipo tu Bali tunapima rate,Kuna rate mbaya na Kuna rate za kawaida,chakula tz kupanda inatokana na kuuza nje ya nchi,ukiuza nje ya nchi kiuchumi pesa yako itahitajika Sana,hivyo itapanda thamani,ndiyo maana Sasa shilingi yetu imepanda kiasi tunabadilishana kwa sh 18 kwa shilingi moja ya Kenya badala ya 20 Kama ilivyokuwa huko nyuma,jifunze kabla ya kubwabwaja ewe beberu mwenye maziwa
Huyo ni mchumi wa mchongo si Kwa shudu Hilo!
 
Wewe ni mkulima?tuache sisi wakulima hasa wa mpunga tupate faida tufidie hasara tuliyoipata kwa zaidi ya miaka 7,kwa kuuza mazao yetu kwa hasara huku pembejeo zikiwa juu
Ewaaaaa [emoji1666][emoji1666][emoji1666]
 
Ningumu mkuu wakulima wengi ni maskini wa kipato wengi wanauza mazao kabla ya kukomaa, wanauza mazao kabla ya kuvuna wanakuwa wameshachukua pesa siku ya kuvuna mazao yanakuwa siyo mazao yao tena.

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
Sasa huwa wanaishije miaka yote? Kuna mtu huwa anawapa chakula wakiuza mazao yao yote?
 
Ni kuwa ruhusu raia kutoka nchi jirani kwenda kununua chakula kwa madalali, Serikali ingeweka mkakati wa kujenga viwanda ili tuweze kuzalisha unga na kupaki nafaka kwenye vifunga shio, kuliko kuuza mazao kiolela, mfano Bakhressa akijenga viwanda vya kuzalisha unga, mchele, maharage hii itamsaidia mkulima kuuza bidhaa za shambani kwake moja kwa moja kiwandani kuliko kupitia kwa walanguzi .

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
Mbona wewe ukipokea mshahara wako na kwenda Bar kumwagilia moyo au kumhonga Mwajuma ndala ndefu mshahara wote na kuacha familia haina kitu hakuna mahala serikali inakuingilia? Yaani serikali ifunge mipaka ili mazao ya wakulima yaozee shambani? Haya ni mawazo gani wajameni? Badala ya kufurahia ili kilimo kivutie vijana wetu waache kubeti na kuchana mikeka , ambayo ni sawa na kuwachangia matajiri wachache, wakimbilie shambani wakalime wapate mapesa wanunue matrekta, mafuso nk ili kupanua kilimo nyie mna mawazo ya kuzuia?
 
Back
Top Bottom