Ukweli ni kwamba mkulima kijijini anaumia zaidi na Mfumuko wa Bei, tofauti na tunavyoaminishwa

Ukweli ni kwamba mkulima kijijini anaumia zaidi na Mfumuko wa Bei, tofauti na tunavyoaminishwa

Mbona wewe ukipokea mshahara wako na kwenda Bar kumwagilia moyo au kumhonga Mwajuma ndala ndefu mshahara wote na kuacha familia haina kitu hakuna mahala serikali inakuingilia? Yaani serikali ifunge mipaka ili mazao ya wakulima yaozee shambani? Haya ni mawazo gani wajameni? Badala ya kufurahia ili kilimo kivutie vijana wetu waache kubeti na kuchana mikeka , ambayo ni sawa na kuwachangia matajiri wachache, wakimbilie shambani wakalime wapate mapesa wanunue matrekta, mafuso nk ili kupanua kilimo nyie mna mawazo ya kuzuia?
Vijana hawawezi kuvutiwa na umasikini

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Serikali kila mwaka inawachukua viijana zaidi ya elfu kumi kuwapeleka kuwalimisha mashamba uko jkt kwa zaidi ya miaka miwili je umeshawai kuona jkt wakiwa matajiri ? Au vijana wanao maliza jkt wakirudi uraiani wanaenda kujitegemea kwa kilimo? Vijana wanao maliza kulimishwa kama misukule kule jkt wote hakuna anayekubali kurudi kwenye kilimo, Bora wanao waende kuomba kazi ya ulinzi walipwe mshahara laki na nusu kuliko kwenda shamba kulima ata mboga mboga,na walipo kuwa uko utumwani jkt walikuwa wanalimishwa wangeona faida ya kilimo kupitia kilimo uko jkt.

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Inafikirisha sana, mkulima anauza magunia ya mahindi apate pesa ya sukari na sabuni n.k halafu anakwenda kununua kilo moja ya sembe.
Mleta mada, the burning spear, yuko sahihi. Ni kwamba hakuna mkulima anayelima kila kitu hivyo hakuna anayejitosheleza kwa kila aina ya chakula. Atauza kwa mfano mahindi akanunue mahitaji na vyakula vingine ambavyo bei iko juu mara dufu!
 
Mbona wewe ukipokea mshahara wako na kwenda Bar kumwagilia moyo au kumhonga Mwajuma ndala ndefu mshahara wote na kuacha familia haina kitu hakuna mahala serikali inakuingilia? Yaani serikali ifunge mipaka ili mazao ya wakulima yaozee shambani? Haya ni mawazo gani wajameni? Badala ya kufurahia ili kilimo kivutie vijana wetu waache kubeti na kuchana mikeka , ambayo ni sawa na kuwachangia matajiri wachache, wakimbilie shambani wakalime wapate mapesa wanunue matrekta, mafuso nk ili kupanua kilimo nyie mna mawazo ya kuzuia?
Unataka kusema Miaka yote zaidi ya 70 Chakula kilikuwa hakitoki nje Tanzania.

Unataka kusema Miaka yote tumenunua mchele 1500 per kg mipaka ilikuwa imefungwa.

Tusijifiche nyuma ya serikali dhaifu amabayo haiwezi kudhibiti Mambo
 
Mkulima kutunza chakula ni ngumu kwasababu hawana pesa za kujikimu mahitaji ya kila siku kwaiyo lazima auze chakula ili apate kununua sukari, mafuta, uniform za watoto wa shule na kama ana mwanae yupo chuo mbali na nyumbani atamtumia pesa za kujikimu, familia kuumwa.

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
Watu hawajui haya wanakimbikia kusema mkulima anafaidi.

Hakuna mkulima anayelima Kila kitu mengine Lazima anunue
 
Hakuna mkulima mdogo,ambao ndio 95% ya wakulima nchini,ambaye anauza sasa kwa bei kubwa.
Wanaouza ni wachuuzi ambao hawajui hata mpunga unavumwaje shambani.
Wakulima walushauza kitambo kwa bei ya njaa kwa sababu hata maghala ya kutunzia vyakula hawana

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
Hyo bei ya 100,000+ kwa gunia la mpunga iliwatosha kabisa na wameweza kufanya mambo makubwa tu

Sio kama kipindi cha Magufuri gunia la mpunga waliuza 50,000+
Mahindi yalioza kwa kukosa soko huko mbeya
 
Hyo bei ya 100,000+ kwa gunia la mpunga iliwatosha kabisa na wameweza kufanya mambo makubwa tu

Sio kama kipindi cha Magufuri gunia la mpunga waliuza 50,000+
Mahindi yalioza kwa kukosa soko huko mbeya
Hakuna siku mahindi yatakuja kukosa soko labda wafanyabiashara waache biashara ya mahindi na waafrika tuache kula, Serikali imeingia mkataba na Shirika la wakimbizi dunia kuwauzia mahindi kwaiyo mahindi haya kukosa soko sema vyakula vilikuwa bei chini wananchi tulikuwa tuna uhakika wa kula chakula cha m
Kutosha.

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Watanzania wenzangu ifike mahali tuwe tunafuatilia mambo Kwa kina na tusiwe benderea fuata upepo.

Leo hii kuna mfumuko wa bei ya vyakula tunaambiwa mkulima anafaidi.

Nasema hivi huu ni uongo Kwa asilimia 100. Mchana kweupe.

Mara zote wakulima huuza mazao Yao kipindi cha mavuno kipindi bei iko chini kabisaa.

Sasa leo hii tunapoongea haukuna mkulima anayeuza mazao Kwa 3000 kilo ya mchele.

Anayenufaika ni Dalali aliyenunua mazao bei ikiwa chini kabisaa.

Amini usiamini mkulima yuleyule sasa Analía njaa na kuhangaika kununua tena chakula.

Je, ushawahi kujiuliza serikali ikitoa chakula cha msaada huwa inapeleka mjini au kijijini?

Ukipata jibu hapo juu ndo utaelewa Nini kinaendelea.

MWISHO.

Serikali Makini lazima ilinde usalama wa chakula wa watu wake Lazima kucontrol inflation.

Ndo maana Mataifa yaliyoendelea watu kuingia barabarani Kisa mfumuko wa bei ni Jambo la kawaida sana..

Mfumuko wa bei kwa lugha ya kitaalamu ni kudorola Kwa Uchumi huo ndo ukweli wenyewe japo watu wanajificha nyumba ya kumsaidia mkulima.

Tukisema Kila mtu afe na chake huyo mkulima bidhaa Za viwandani vikipanda bei mara dufu na huduma nyingine Za kijamii atatoboa?

Nasema serikali Lazima i control inflation kulinda purchasing power ya Tanzania Shilings/ Thamani ya pesa Yetu.
Msikariri maisha na msidhani mkulima ndio wa kutafutia pointi za kisiasa
 
Dear members nawataarifu kuwa tuko wakulima ambao tumenufaika na bei hiz,binafsi Leo nmeuza gunia 100 za mpunga debe 7 kwa 170,000 namshukuru raid na waziri wa kilimo kwa msimamo wao.Hiiimenipa morale nmeongeza eneo LA kulima mpunga na mahindi nmelima mwaka huu.mahindi ntayawekea mbolea as nmepata mtaji kutoka kwenye mpunga.Kwa ujumla safari ya maendeleo ni step by step I hope mwakni wakulima zaidi watanufaika.bei zikiendelea hivi tutapata maendeleo tuvumilieni kidogo na sisi tunufaike.By the way huku sumbawanga ni mvua ndo kikwazo ila mahindi yameshakomaa likiwaka wiki Moja mahindi mapya yanatoka.
 
Msimu wa Mavuno Bado haujanza rasmi , mvua mwaka huu zilichelewa kuanza kunyesha kidogo, Mahindi Bado hayajakauka masjambani maeneo mengi wanategemea kuanza kuvuna may katika Maeneo ya Songwe -Tunduma, KITETO Bado hawajanza wanaovuna Mahindi wanakutana na changamoto ya Mvua, mfano. Nimevuna kidogo ila changamoto ya kuanika juani huku mvua,
 
Attachments

  • VID_20230429_131635.mp4
    3.9 MB
Back
Top Bottom