Ukweli ni kwamba mkulima kijijini anaumia zaidi na Mfumuko wa Bei, tofauti na tunavyoaminishwa

Wakipigwa na hii njaa kisawasawa watapata akili, msimu ujao watakuja makakini
 
Kuhifadhi gunia 3 za mahindi au mchele unahitaji ghala?
 
Inafikirisha sana, mkulima anauza magunia ya mahindi apate pesa ya sukari na sabuni n.k halafu anakwenda kununua kilo moja ya sembe.
Mimi ni mkulima, hakuna mkulima lofa wa hivyooo... Wasukuma na wengine huko vijijini wana vihenge vya kutunzia mazao yao kwa ajili ya chakula cha familia yake. Ukiona mkulima kauza mazao yoooteee mpaka akiba ya chakula basi jua huyo ni sawa tuu na mfanyakazi ambaye anapata mshahara mwisho wa mwezi na wote anaenda kuumalizia bar... Ndani ya siku 3 mifuko mweupe.... Hata Babu yangu nilikuwa namuona tukijaza kihenge mahindi, maharage, mihogo mikavu halafu tunakisiriba juu chote ili kusubiri kipindi cha shida.
 
Mkuu hii ni pure exaggeration ya watu wa mijini eti wanawapangia wakulima namna ya kuendesha maisha yao. Hivi ingekuwa wazee wetu hawana elimu ya kuweka akiba ya mazao yao wanayovuna ili yawasaidie mpaka mavuno mengine huko vijijini watu wangeishije? Niambie ni mwaka gani serikali iliwahi kugawa unga mchele, maharage etc bure huko vijijini kote nchini wakati wa njaa au mavuno kidogo? Miaka na miaka wakulima wanajua wanalimaje na jinsi ya kutunza vyakula vyao. Leo mtu wa mjini eti anamuona mkulima hana akili [emoji23] [emoji23]
 
Lakin kuna wakulima ambao nawajua, mwaka jana wamenufaika sana kwa kuuza bei nzuri mpunga wao,wengine walijenga, wengine hyo pesa waliwekeza kwenye biashara zao zingine.
Nilikuwa Moshi, kule kwenye irrigation schemes za mpunga kuna wakulima wamevuna mpunga vizuri sana, wakapeleka mashine kuukoboa na kuwauzia wanunuzi kutoka Kenya, yaani ekari moja mkulima kapata mpaka milioni 6, wenye ekari 2, 3 na zaidi ndiyo usiseme yaani wakulima wamenunua bodaboda, bajaj, power tiler etc kila mkulima anafurahia kazi yake. Na hapa niseme kwamba hata wale walioamua kuuzia mazao yao shambani bei kwa gunia ilikuwa si chini ya laki moja na elfu 20 au 30. Lakini walio wengi walikuwa wanapeleka mipunga yao mashine wanakoboa na kuuza mchele, tena kwa kilo. Huko mashine wanakuja wanunuzi wengi na wabashindana bei.
 
Hasira za nini kwangu?
Sie tunachojua huu mfumko wa bei za vyakula unawafaidisha wachache.
Hakuna mkulima anayefaidika.Usitumie nguvu nyingi kutetea uongo.
Mbona mambo yako wazi sana?

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
 
Tatizo la kusoma madesa unadhani hata kwenye maisha ni kama kujibu mtihani wa desa.

Hivi hao unaowaita wakulima wa irrigation scheme ndio kama akina Mbowe na matajiri wanaolima kwa starehe?

Ni irrigation scheme ngapi zipo nchini?

Sisi ndio tunataka serikali iwekeze huko ili watu wa chini pia wapate nafasi ya kujiinua kiuchumi wafaidi ruzuku za pembejeo kutoka serikalini.
Kwa sasa pembejeo zinatolewa kwa kodi ya umma,wanaofaidi ni watu wachache ambao ni madalali wa mazao.

Kibaya zaidi kuna waganda wakati wa mavuno wananunua mzigo ukiwa bado shambani na hivyo wanafaidika sana na hiyo ruzuku inayotolewa na serikali.
Usimamizi mbaya wa Sera za fedha ni tatizo nchi hii

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
 
Tumepiga mayowe humu kuwa Bashe analiingiza chaka hili taifa kwa upatikanaji wa chakula cha bei himilivu. Sasa hivi tuna mlaumu aliye mteua kwani ilibidi amkemee huko huko kwenye vikao vyao.
 
Mkulima kutunza chakula ni ngumu kwasababu hawana pesa za kujikimu mahitaji ya kila siku kwaiyo lazima auze chakula ili apate kununua sukari, mafuta, uniform za watoto wa shule na kama ana mwanae yupo chuo mbali na nyumbani atamtumia pesa za kujikimu, familia kuumwa.

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Serikali inanunua chakula na muifadhi kwenye maghala yake, mfano kwenye mazao ya korosho wakulima wanamfumo wa stakabadhi ghalani uwezi kusika mkulima wa korosho kauza korosho zake zote shambani kabla ya kuzivuna

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Hujui maisha unalelewa bado kaa kimya. Unadhani wanauza Kwa kupenda?
 
Uzuri ni kwamba serikali imeshafanya maamuzi, hakuna kufunga mipaka na wakulima ruksa kuuza mazao yao kokote. Sasa wewe endelea kulia lia hapo na visababu vyako vya kuokoteza. Hizo irrigation schemes nilizokupa mfano ni wakulima wenyewe wamejiongeza na kuzitengeneza, wakulima wa kawaida kabisa, ukiwa na muda nenda ukajionee mwenyewe hakuna cha matajiri wala nini. Wakati wewe unalia lia hapo mimi mwenzio nimewahi huku Mvomero nalima mahindi, mpunga, mbaazi nk mbolea za ruzuku, hata wakileta figisu tutanunua tuu kwa bei hata laki moja kwa sababu gunia zilizoko stoo bei ni laki mbili gunia moja. Wakulima wengi sana wamepanua mashamba yao, watumishi na wafanya biashara wako huku wamekodi mashamba, ekari moja kwa msimu ni elfu 50. Mvua zinanyesha vizuri mazao yanaenda vizuri, tukutane Juni/July kwenye mavuno huku wewe ukiendelea kulalamika badala ya kutumia hiyo fursa. Wewe endelea kubeti na kuchana mikeka [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Umeongea vizuri, nimetoa mfano hapa kule Moshi wakulima wa mpunga wakivuna wanapeleka mpunga wao kuukoboa mashine ili wauze mchele kwa bei nzuri. Wananunua huo mchele siyo madalali bali ni wafanya biashara kutoka Kenya. Hata kama mkulima hana pesa ya kuvuna ekari zake mbili au 4 za mpunga anaenda tuu kumuona mwenye mashine ya kukoboa anamkopesha pesa ya kuvunia na usafiri kwa masharti kwamba mzigo utakobolewa kwenye mashine zake ili mashine zipate kazi. Wanunuzi wa mchele kutoka Kenya na kwingineko wao huja kununua mchele kwenye hizo mashine kwa kushindana. Mkulima akiona bei ya mchele imeshuka anaweza kuacha hapo mashine mzigo wake hata miezi 4 mpaka 6. Hapo hakuna cha dalali wala nani.
 
Huyo ni mchumi wa mchongo si Kwa shudu Hilo!
 
Wewe ni mkulima?tuache sisi wakulima hasa wa mpunga tupate faida tufidie hasara tuliyoipata kwa zaidi ya miaka 7,kwa kuuza mazao yetu kwa hasara huku pembejeo zikiwa juu
Ewaaaaa [emoji1666][emoji1666][emoji1666]
 
Ningumu mkuu wakulima wengi ni maskini wa kipato wengi wanauza mazao kabla ya kukomaa, wanauza mazao kabla ya kuvuna wanakuwa wameshachukua pesa siku ya kuvuna mazao yanakuwa siyo mazao yao tena.

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
Sasa huwa wanaishije miaka yote? Kuna mtu huwa anawapa chakula wakiuza mazao yao yote?
 
Mbona wewe ukipokea mshahara wako na kwenda Bar kumwagilia moyo au kumhonga Mwajuma ndala ndefu mshahara wote na kuacha familia haina kitu hakuna mahala serikali inakuingilia? Yaani serikali ifunge mipaka ili mazao ya wakulima yaozee shambani? Haya ni mawazo gani wajameni? Badala ya kufurahia ili kilimo kivutie vijana wetu waache kubeti na kuchana mikeka , ambayo ni sawa na kuwachangia matajiri wachache, wakimbilie shambani wakalime wapate mapesa wanunue matrekta, mafuso nk ili kupanua kilimo nyie mna mawazo ya kuzuia?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…