Ukweli ni kwamba wapalestina hata wakiuwawa na waisrael pale sio kwao warudi walikotoka

Ukweli ni kwamba wapalestina hata wakiuwawa na waisrael pale sio kwao warudi walikotoka

Hatutafuti history ya nyuma tunachoangalia ni pale Ibrahim alipopewa ardhi Hiyo kuwa urithi wake huko mwanzo inawezekana kabisa ilikua yao lakini MUNGU wa Ibrahim alimpa Ibrahim tena kwa agano dhabiti lisilo wezwa kuvunjwa, Hivyo ndugu zenu wapelestina wanajisumbua tu.
Maluku
 
Jibu lako linazidi kuibua maswali zaidi mkuu!
Kwa kifupi tu hivi leo hii au kesho ikitokea Wayahudi wakaja hapa Tanzania wakiwa na ndege za kijeshi, vifaru, bunduki na kila aina ya silaha wakaanza kutushambulia kila kona wakisema, "JEHOVAH/MUNGU KATUPA NCHI YA TANZANIA TUITAWALE NA KUIMILIKI!" utawaelewa na kuwasaport kwa kuwa Mungu wao ndio amewapa Tanzania?
Kumbuka Mungu wao pia wakati ule aliwaamuru waue kila mtu watakaemkuta mule kanaan kuanzia watoto, wazee, kinamama, vijana, kukatakata na maashera yao na kuua mpaka na wanyama wafugwao! Sasa chukulia ndio tupewe taarifa leo kuwa asubuhi ya kesho tuwe tumeondoka nchini mwetu laa sivyo tutauawa wote na Wayahudi kwa kuwa Mungu amewapa nchi hii.

Nakuuliza tena! Utakuwa tayari kwa jambo hilo kwa kuwa Mungu ndio kasema?
Je, kwaweza kuwa na Mungu mpumbavu namna hii?

Mungu muweza wa yote, mwenye upendo, mjuzi wa yote, aliyeko kila mahali aweza kuyatenda hayo?

Unajua binadamu mwenye akili timamu akiyaamini haya, basi kuna haja hizi dini zipigwe marufuku maana zinadumaza akili za watoto wetu.
mjadala umefungwa rasmi hapa...sina la kuongeza
 
Hata mimi nabariki kwasababu ni haki yao na ni urithi wao na ni ardhi yao na wanacho kitaka ni mipaka yao halali waliyopewa na MUNGU wao ambae ni MUNGU wako pia, na hawataacha wapelestina watakapo achia aridhi yao waliyopewa urithi, na ukae ukiamini kwamba anguko la palestina limekalibia.
mwanangu akijakuwa na akili kama hii namkataa
 
Kwa utafiti wangu tu nimegundua wakanaan hawapo tena
Wafilisti hawapo tena
Waliopo pale ni waarabu wa kiislamu waliovamia tu
Warudi kwao wawaachie wayahudi eneo lao
Ww unawafahamu wakanaan na wafilisti walikuwa na sura gani na rangi gani? Je una hakika gani kuwa waliopo pale ndio wale wa Israel wa kale na sio wazungu ws ulaya?
 
Wafilisti walikuwa kabila la watu wa Ulaya ambao walivuka Bahari ya Kati na kisha kushindwa kuvamia Misri waliteka pwani ya Kanaani (1175 KK hivi) wakifaidika na silaha za chuma walizozitumia dhidi ya watu waliokuwa na zile za shaba tu, wakiwa wenyeji au Waisraeli.

Ingawa hawakuwa wengi, waliathiri sana nchi yao mpya, kiasi cha kuiachia jina la Palestina.

Habari nyingi juu yao zinapatikana katika Biblia.
Kwa mfano tukitumia vitabu vya kuaminika kama biblia ardhi ya wapalestina itakua eneo gani?
Bado hainiingii akilini
 
Kijana unapingana na biblia yako

Wagalatia 3
28 Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote mmekuwa mmoja katika Kristo Yesu.
29 Na kama ninyi ni wa Kristo, basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na warithi sawasawa na ahadi
.

Ila bado mnaamini waisraeli wana ahadi zao wakati biblia imeshahitimisha hapa kuwa wote ni sawa na uzao wa Abraham ni wakristo wote sasa kwanni muamini ile nchi ni ya wayahudi pekeee?? Kwanni mnaipinga biblia yenu wenyewe!!??
Nilijua wewe ni tapeli tu uliposema ni mkristo.
 
Shida husomi biblia kijana nchi ya ahadi ipo misri hadi iraq ila mmeng'ang'ania tu palestina ya watu

Mwanzo 15
18 Siku ile BWANA akafanya agano na Abramu, akasema, Uzao wako nimewapa nchi hii, kutoka mto wa Misri mpaka huo mto mkubwa, mto Frati,

Kwanni hamuendi misri au iraq mnagombania nchi na wapalestina?? Why wakati nchi ya ahadi hipo hadi huko if at all NCHI YA AHADI ndio hoja yenu??
Uko yalipewa makabila mengine ya israel, ila kwa hapo israel kabila la Yuda lilipewa hilo eneo
 
Na hii ndio shida ya wafia dini hivi hujui kuna wapalestina wakristo na wayahudi pia?? Na je unafaham kuna raia wa israel ambao ni waislam kabisa ingawa sio waarabu??? Je ina maana hao waislam wakiisrael nao ni wajinga na wale wapalestina wakristo/wayahudi ndio sio wajinga???
Najua wapo sana ulishasikia wakiipinga Israel ni kwasababu wanaelewa wao huishi kwa amani kabisa bila vurugu
 
Sasa nitajie nchi yeyote sahivi ambayo wakazi wa hapo walikuwepo miaka 2000 nyuma ntajie hata sehem moja...... Tanzania wote tulitoka pande zingine za afrika vivo hivyo hata ulaya sasa kwanni kwa palestina kuhamia ardhi nyingine kama tu ulimwengu mzima ulivyofanya iwe nongwa??

Anyway nasubiri unitajie hiyo nchi
Israel
Hao waarabu wangebaki huko kwao tu
Mfano hapa kwetu tanzania wenyeji hasa walikuwa mbilikimo wenyewe tu wakaona hawawezi kujichanganya na watu wa Jamii zingine wakasepa sehemu nyingine
 
Ndio zimeishia hapo naomba uniambie kwanni wayahudi wanakaa kwenye 10% ya nchi ya ahadi ilihali mipaka ya kibiblia ya nchi ya ahadi ni kubwa zaidi?? Kwanni wasiende misri au syria ambayo kibiblia ndimo nchi ya ahadi kwanni walazimishe kugombanka ardhi na wapalestina?? Kwanni hawafuati mipaka ya kibiblia wanajiamulia wenyewe alafu wakristo mnashabikia tu bila kuhoji??

Embu jibu hili ndio mada yako iwe na uhalali
We tatizo lako unaikurupukia Biblia
Biblia inasema Mungu alimwambia abraham hivi nitalithibitisha agano langu nawe, wazawa wako na vizazi vyao vyote milele
Tena nitakuwa Mungu wako na Mungu wa wazawa wako milele
Nitakupa wewe na wazawa wako nchi hii ambapo unaishi kama mgeni, yaani nchi yote ya kanaan iwe Mali yenu milele nami nitakuwa Mungu wao
Mwanzo 17/7-8
 
Wote ni wakuja pale, wageni tu wote!
Hamna original that’s all
 
We tatizo lako unaikurupukia Biblia
Biblia inasema Mungu alimwambia abraham hivi nitalithibitisha agano langu nawe, wazawa wako na vizazi vyao vyote milele
Tena nitakuwa Mungu wako na Mungu wa wazawa wako milele
Nitakupa wewe na wazawa wako nchi hii ambapo unaishi kama mgeni, yaani nchi yote ya kanaan iwe Mali yenu milele nami nitakuwa Mungu wao
Mwanzo 17/7-8
Hiyo ni ahadi ya nchi yetu Tanzania, that’s all!
 
Kabila ya yuda ndio ashkenazi??? Umesoma wapi hayo unayosema..... Wayahudi walishachangamana na hao waliorudi 90% ni ashkenazi jews na asili yao ni ukooo wa japhet sio shem hivyo hawana damu yeyote na wayahudi halisi..... Biblia iko wazi wayahudi halisi bado wako utumwani na watarudi nchi yao kipindi cha mpinga kristo na messiah Yesu akirudi ssa hao ashkenasizi toka lini wametoka ukoo wa shem ambao ndio Abraham alitokea humo? Hao walishachangamana na wazungu so sio wayahudi tena ni kitu kingine kabisa

Ashkenazi Jews - Wikipedia
Sikulaumu ni uelewa wako umefikia hapo
 
Nilijua wewe ni tapeli tu uliposema ni mkristo.
Ni vizuri tupende kujibu hoja kuliko kushambuliana kwa matusi..... Nmeuliza kama wapalestina na waisrael wote ni watoto wa abraham je ni kwanni mtoa mada anadai hyo nchi ni ya waisrael pekee ilihali alipewa Abraham ambaye hakuwa Musiraeli??

2. Kibiblia ardhi waliyopewa israel mbona kuna maeneo wanaishi ambayo hayapo kwenye ramani ya kibiblia ya nchi ya ahadi?? Kwanni wasiishi ndani ya mipaka ile ya kibiblia??

3. Kibiblia nchi ya ahadi inaanzia mto nile hadi huko Iraq je ni kwanni waisrael wasiende huko wadai hyo ardhi ila wamekazana kuwapora palestina nchi yao??

4. Kibiblia wakristo wote ni warithi wa AHADI ZOTE ZA ABRAHAM ambayo moja yao ni NCHI YA AHADI sasa kwanni bado mnalazimisha nchi ile ni ya wayahudi tu wakati biblia ilishasema wakristo wote tumekuwa taifa teule na warithi wa abraham kama wanawe why bado mnaitenga israel kama ina baraka za kitofauti kiasi wana entitlements kwa ardhi ya palestina.....unaweza ukanipa mstari wa biblia baada ya wagalatia inaohalalisha hilo??

Mimi tapeli zitto junior nasubiri majibu
 
Wakanaan na walerisi sasa hivi wanaishi wapi?
Wakanaan hawapo
Waperisi hawapo
Wapalestina halisi hawapo
Waliopo eneo hilo ni wavamizi wa kiislamu wa kiarabu wanaojiita wapalestina wakati sio wapalestina halisi
Mi nawashauri warudi kwao la sivyo watakufa wote au wakubali masharti ya Wenye ardhi israel
 
We tatizo lako unaikurupukia Biblia
Biblia inasema Mungu alimwambia abraham hivi nitalithibitisha agano langu nawe, wazawa wako na vizazi vyao vyote milele
Tena nitakuwa Mungu wako na Mungu wa wazawa wako milele
Nitakupa wewe na wazawa wako nchi hii ambapo unaishi kama mgeni, yaani nchi yote ya kanaan iwe Mali yenu milele nami nitakuwa Mungu wao
Mwanzo 17/7-8

Mwanzo 15:18
18 Siku ile BWANA akafanya agano na Abramu, akasema, Uzao wako nimewapa nchi hii, kutoka mto wa Misri mpaka huo mto mkubwa, mto Frati,

Huu ndio mstari niliokuambia usome na ndio oroginal mpaka wa nchi ya ahadi ila sijasikia wayahudi wakidai misri ama syria na iraq ila wanadai palestina pekee je unaweza nisaidia ni kwanni wanafanya hivo alafu nyie bado mnatoka mapovu humu kuwatetea..... Why palestina sio misri iraq na syria???

Nasubiri majibu
 
Wafilisti walikuwa kabila la watu wa Ulaya ambao walivuka Bahari ya Kati na kisha kushindwa kuvamia Misri waliteka pwani ya Kanaani (1175 KK hivi) wakifaidika na silaha za chuma walizozitumia dhidi ya watu waliokuwa na zile za shaba tu, wakiwa wenyeji au Waisraeli.

Ingawa hawakuwa wengi, waliathiri sana nchi yao mpya, kiasi cha kuiachia jina la Palestina.

Habari nyingi juu yao zinapatikana katika Biblia.
Hebu waza kama great thinker,wewe kwenu wapi? je urudishwe kwenu??
 
Back
Top Bottom