Ukweli ni upi katika kuvunjwa kwa EAMWS na kuundwa BAKWATA?


king joniva

Hakuna tatizo ndugu yangu mimi nimeandika historia ya wazee wangu unaiamini sawa la unaona haina umuhimu pia si ubaya.

Muhimu kwangu ni kuwa historia ya wazee wangu iliyokuwa imefutwa nimeirejesha na sasa inafahamika.

Unataka kubakia na historia ile iliyoandikwa na Chuo Cha CCM Kivukoni huo ni uamuzi wako sina uwezo wa kukuzuia.

Amini kile akili yako inakuelekeza.
 
Utaongea weee lakini watz hawana mpango na wewe wana ku ignore sana mkuu pole!!

Sema wewe, siyo Watanzania. Mimi simui-gnore.
Mzee Said anatufundisha mambo mengi sana. Binafsi nimeanza kuamini wanaoumia na anayoyasema mzee wetu ni Wakristo waliojimwambafai huko nyuma na sasa mzee anawaweka uchi.

I think we need a new revolution.
 

Sio kwamba siamini ndani ya historia hizi za wazee wetu, nikifanya hivyo means sintakuja kuamin hata historia kizazi changu pia. Tatizo unatusimulia historia Ambayo imekuwa "historia jumuishi" tangu ilipoanza kuzungumzia juu ya Taifa letu, katika hila sinashaka kukosolewa hakukwepeki maana kila mtu atamleta Mzee / wazee wake kuwa ndio wajenzi wakuu wa nguzo za nchi yetu kuliko Nyerere, Tewa Said Tewa, Kambona, Saadan Kandoro, familia ya Sykse n.k...hivyo kulinda mpasuko wa historia yetu ni afadhar tubaki kutumia Fact za historia zinazo kubarika, hzo nyingine zitakuwa ni sehem tu ya historia yetu.

Kuna post yako Moja nimeisoma kuwa historia yetu imepindishwa thus why najaribu ku-argue. Sorry kama nakosea M.S
 

King...
Mimi nimeandika historia baada ya kufanya utafiti ulionichukua muda mrefu sana na hapa achilia mbali kuwa nimelelewa ndani ya historia hii na kusikia mengi yakihadithiwa katika mazugumzo ya kila siku..

Nilipoanza utafiti kwanza nimesoma nyaraka zote zilizokuwa mikononi mwa Sykes family ambazo zinakwenda nyuma hadi miaka ya 1920s.

Ukimtoa John Iliffe hakuna mtafiti ambae amepata kuzisoma nyaraza hizi hadi hii leo.

Nimemsoma Herman von Wissman akiwa kijijini Kwa Likunyi, Imhambane Mozambique alipokwenda kutafuta askari mamluki aliokujanao hadi Pangani kuanza vita na Bushiri bin Salim Al Harith kisha na Mtwa Mkwawa.

Katika askari hawa Sykes Mbuwane akiwa mmoja katika hilo jeshi.

Anaeeleza historia hii ni Chief Mohosh ambae ndiye alikuwa kiongozi wa jeshi hili baadae baada ya vita vile akawa mkuu wa Germany Constabulary Tanganyika lakini sasa akiwa anafahamika kama Affande Plantan.

Historia hii Affande Plantan ndiyo aliyomweleza Kleist Sykes mtoto wake wa kulea baada ya kifo cha baba yake Sykes Mbuwane Mto Ruaha wakati wakirejea Bagamoyo baada ya vita na Mkwawa.

Historia hii Kleist Sykes akaiandika katika mswada wa kitabu kabla hajafa nwaka wa 1949 na ilichapwa kama ''seminar paper,'' (1968) na mjukuu wake Aisha ''Daisy'' Sykes na utaipata Maktaba ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, East Africana na pia ni sura katika kitabu alichohariri John Ikiffe, ''Modern Tanzanians,'' (1973).

Haya nimeyaeleza hapa mara nyingi.

Nimefika hadi Pangani na kuangalia bandari walikoshukia askari hao na kupiga picha sehemu nyingi za mji kusukuma fikra zangu.

Nimemsoma Kleist Sykes anavyoeleza kukutana kwake na Dr. Kwegyr Aggrey 1924 mtu aliyemshajiisha kuunda African Association.

Nimezungumza na baba yangu aliyekua katika mtaa wa Kipata na Abdul Sykes anihadithie yote anayokumbuka kuona katika 1950s wakati Abdul anaanza harakati za kuunda TANU nk.nk.

Baba yangu ndiye aliyenieleza kuwa yeye kamjulia Nyerere nyumbani kwa Abdul Sykes mwaka wa 1952 na akijua kuwa Abdul alikuwa na mpango wa kuunda chama cha siasa na hili kaelezwa na Abdul mwenyewe siku alipomtambulisha kwa Nyerere.

Sasa kusema ati atakuja mtu kusema kuwa na yeye wazee wake waliunda chama cha siasa sawa hakuna wa kumkataza lakini chama hicho hakitakuwa TANU kwani muasisi wa TANU anafahamika kwa ushahidi.

Ndiyo hapo nilipokuwa nalichangamsha darasa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam na kuwashangaza hadi walimu wangu kwa yale niliyokuwa nayajua na hii ndiyo sababu kitabu cha maisha ya Abdul Sykes kimeweza kubadili historia nzima ya Mwalimu Nyerere na historia ya uhuru wa Tanganyika.

Bahati mbaya sana historia hii hamuipendi inawachoma moyo mnapenda tubaki na historia inayomtaja Nyerere peke yake kuwa ndiye muasisi wa TANU na harakati za kudai uhuru 1954.

Katika picha hiyo hapo chini yuko Kleist Sykes na Ramadhani Mashado Plantan wa pili kushoto katika hao waliokaa chini na hapo ndipo ilipokuja kuzaliwa TANU na Mashado Plantan akiwa mmoja wa wazalendo waliohudhuria mkutano wa kwanza wa TANU August 1954.

 
Kama umefanya research na ukaguzi rasmi wa kihistoria juu ya taarifa na vyanzo hivyo, Mimi naikubali hiyo historia, na nina uhakika Tanzania tuna historia kubwa isiyo fahamika, NI VYEMA IKAWA WAZI kwa umma wa Watanzania. Asante mkuu kwa kunielewesha!!!!!!
 
King...
Historia ya Kleist Sykes na wanae ipo katika Dictionary of African Biography mradi wa Harvard na Oxford University Press New York.

Hizi ni vol. VI za tawasifu fupi za watu mashuhuri Afrika.

Nilishirikishwa kama mmoja wa waandishi 500 kutoka sehemu mbalimbali ulimwenguni.
 
Sasa mkuu kuna shida Gani kuziweka taarifa hizo kuwa rasmi katika Historia ya nchi, ni nin kinachokwamisha jambo hili....? Maana ni muhimu kwa mustakabari wa vizazi vyetu na vijavyo......
 
Najaribu kufikiria, huyu Kleist Sykes alipata wapi ujasiri wa kuanzisha chama cha kupinga ukoloni, wakati alikuwa anaishi kwa fadhila za wakoloni, na watoto wake Abdul na Ally aliwatoa kwa wazungu wakawasaidie vita huko Burma. inawezekana hiki chama cha AA kilianzishwa na wazungu ili kupunguza nguvu za wapinga ukoloni wa ukweli akina Bushiri, Mkwawa , n k
 
Huwa nasoma sana maandiko yako Mzee Mohamed Said. Mara nyingi huwa marefu na ambayo huwa hayaleti muungano wa kitaifa. Mtu akimaliza kusoma hujengewa chuki tu, na ndio maana kwenye maandiko yako huwa na majibizano yasiyojenga.

Shida yako kuu ni hiyo mistari hapa chini ambayo hujirudiarudia kwenye uandishi wako kila unapokosolewa. Huwa wajificha chini ya mwamvuli wa kuwa na uhusiano wa kidugu au kuwahi kuishi na kusimuliwa na hao wapigania Uhuru wako na pia kujidai umefanya utafiti ambao kwa mtazamo wako utafiti wako ndio pekee huwa sahihi. Kwa hiyo kusikia historia zitolewazo na vinywa vya wengine kwako huwa ni uongo, na unataka tuamini usemacho wewe tu.

Wote tuna historia toka viunoni mwa wazazi wetu; mojawapo ya historia anayopewa kila mtu ni wazazi kutwambia walipokuwa shule walikuwa wazuri sana kimasomo. Kumbe wazazi hujifagilia tu.

Kuna reference za vitabu vichache ambazo wewe hudai zinatoka upande wa pili ambazo huzitumia pale zinapoungana na mtazamo wako wa Waislamu kuonewa na tawala za kikoloni na baada ya Uhuru.

Historia yako yoyote unapoitoa huegemea upande mmoja ambao ulishauchagua tangu utotoni. Huwezi ukawa mwanahistoria uliyechagua upande. Labda tukuite mtetezi.

Lakini sawa, labda kwa siku ya leo tukubali kwamba Waislam walionewa wakati na baada ya ukoloni. Sasa utalalamika hadi lini? Hata muuza sumu ya panya, huzima kipaza sauti baada ya kukamilisha mauzo ya siku na usiku kuingia. Shauri Waislam wafanye nini toka hapa walipo? Toa mashauri ambayo yataleta amani na si kutujengea chuki kila siku kwa kufuata historia zako ambazo hutaki zikosolewe. Hivi Muislam wa sasa itamjenga historia au maamuzi ya kutoka hapa alipo sasa?

 

Laki...
Ungesoma kitabu cha Abdul Sykes ungekuwa umejifunza mengi na usingeuliza maswali kama haya. Kuanzisha associations ikiruhusiwa na Waingereza kwani kulikuwa na European, Asian na Arab Association na Waafrika waliwakilishwa na Mzungu jina lake Father Gibbons kutoka Pugu Mission.

Hapakuwa na suala la ujasiri.

Ukitaka kuujua ujasiri wa Kleist itakubidi usome War Diaries zake katika WW I Kleist na nduguye Schneider Plantan wakipigana chini ya Paul von Lettow Vorbeck katikajeshi la Wajerumani dhidi ya Waingereza.

Abdul Sykes aliingizwa katika KAR kupigana Burma kwa mujibu wa sheria na Ally yeye alitoroka nyumbani kujiunga na jeshi na akapokelewa ingawa alikuwa hajafikia umri.

Sijui hizi lugha za "fadhila,"unakusudia kitu gani.
 
Ozzanne,
Kwako wewe kuandika historia ya kweli ni kuvunja udugu ila kupotosha historia ni kuunga udugu na kuleta umoja wa kitaifa.

Wala wewe huna haja ya kuniamini ninapoeleza kuwa babu yangu Salum Abdallah ni muasisi wa TANU Tabora na ni muasisi wa Tanganyika Railways African Union (TRAU) akiwa rais 1955 na aliongoza migomo mikubwa mitatu ya wafanyakazi wa reli, 1947, 1949 na 1960.

Ukipenda amini kuwa wala watu hawa hawakupata kuwepo Tanganyika.

Wala sina sababu ya kujidai.

Hawa ni wazee wangu na wala sikuwachagua.

Nimezaliwa wakati wao kwa uchaguzi wa Mungu.

Wala hawa wazee hawakupanga kuwa Nyerere atatoka kwao atakuja Dar es Salaam atamtafuta Abdul Sykes na wataungana na wazalendo wengine kupigania uhuru wa Tanganyika.

Historia hii ndiyo historia ya wazee wangu ambayo ilipotea nami nikaiandika ili isipotee na iwepo hadi siku ya kiama.

Bora wasingeandika kabisa kuliko kuandika historia iliyopotoshwa.

Ikiwa unayo historia ya TANU mfano wa hii yangu iandike isomwe kama dunia inavyosoma yangu.

Nimekusoma ahsante sana.
 
Sheikh dhulma imefanywa sana,hakika yana mwisho...Inshaalah

 
Nini kiliifanya EAMWS kuhamisha makao yake makuu kutoka Mombasa hadi Dar?

Kama ni Nyerere ndiye aliyeua EAMWS na kuanzisha BAKWATA, je ni yeye mwenyewe aliua EAMWS kule KENYA? Aliwaanzishia baraza gani kule?
 
Mzee said naisi kama nimewahi kukuona masjid idrisa kariakoo mwaka 2009 baada ya swala ya ijumaa, nakumbuka siku hiyo ulisimama na kusema leo ninawaletea historia ya tanganyika kabla ya uhuru nakumbuka siku hiyo waislam wengi walitulia sehem zao wakisubiri kusikia kile ulichowaandalia, sina kumbukumbu vzr ulisema kua miongoni wa wapigania uhuru waliokua hai hadi leo (2009) ni wawili tu ambao wazee sn na hali yao si nzr, nakumbuka ulisema uchunguzi wako ulikuchukua miaka mingi sn kukamilika, historia iliishia kwa Waislam wengi sn msikitini pale kulitokwa na machozi sn nami nikiwemo hii ni baada ya kugundua tumedhulumiwa sn na mbaya zaidi kwenye history babu zetu hawawamo, mzee said kama ni ww kweli basi allah akuifadhi mzee wangu. nakumbuka ilikuwa ndo mara ya kwanza report ile inatolewa na kulikua na wapiga picha wengi na video shooting kibao ulivaa kanzu Nyeupe na kofia yako Nyeupe, Allah kareem mzee wangu ipo siku haqq itajienga na batili in sha Allah na tupo vijana allahmdulilah
 
Haya unachosoma huelewi, nani kaandika hujasoma? Kanisome tena.
 
Mohamed Said, inawezekana chuki zako zimetokana na familia ya Sykes kufilisiwa mali zao kipindi Nyerere alipoanza kampeni zake za ujamaa kuanzia mwaka 1964,familia ya sykes ilikumbwa na kimbunga kilichowakumba akina kambona, titi mohamed, kaselabantu etc
 
Hiyo mihadhara na research unazoenda kuzifanya huko vyuo vya ulaya, UK, German zinafadhiliwa na nani? ni taasisi au mtu binafsi anaekufadhili?
 
Nyerere kafariki, mmeshindwa nini kujenga Chuo Kikuu mpaka sasa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…