Ukweli ni upi kuhusu Oscar Kambona?

Nyani,
Naona nimedandia mada. For what it is worth, ndugu zake Kambona waliwekwa detention baada na si KABLA ya Kambona kukimbilia London. Kilichompa hofu ni pale washirika wake katika jeshi na intelligence walipoanza kukamatwa mmoja mmoja, including the late Eli Anangisye. Hii ya kwamba tofauti baina ya Nyerere na Kambona zilianza baada ya mutiny ya 1964 siiafiki. Kufikia 1966 Kambona alikuwa very close na Mwalimu. Ni baada ya mabadiliko ya uongozi katika chama, pale Kawawa alipochukua nafasi ya Kambona kama katibu mkuu wa chama, na hasa baada ya mkutano wa Azimio la Arusha, ndipo tofauti zilipoanza kuibuka kati ya Nyerere na Kambona. Kambona aliona kunyang'anywa Ukatibu mkuu na kupewa kazi ya waziri wa local government kama ni demotion. Akajiuzulu na kumwambia Mwalimu afya yake si nzuri. Yaliyofuata ndiyo hayo ya kukimbilia London through Kenya.
 
OK, OK,

Kuna mtu kaongea hpo juu kama vile Economic hitmen walikuwa wanacheza "fair game".I am not advocating that position lakini ninachosema ni kuwa, lawama zangu kubwa ni kwa viongozi wetu walioshindwa kutetea maslahi yetu ya kiuchumi kwani katika dunia hii ya "social Darwinism" utakutana tu na situation za economic hitmen kama sio hao wa World Bank utakutana nao hata huko Paris Club.

Sasa Watanzania tukipata deals za ajabu tunaweza kulalamika kweli? Rais mwenyewe Kikwete Mainuna akienda Paris Club ana-sign mikataba hata kabla economic hitmen hawajaongea kutokana na psychology tu.

Bill Cosby huwa anaandamwa sana kwa kusema mambo mabaya ya African Americans, kuna wengine wanasema "mbona watu weupe wako kwenye welfare zaidi huwasemi unatusema sisi tu" ukweli ni kwamba ana uchungu na watu wake.I don't care about the hitmen, they were doing their job, my question how did our leadership protect us?
 
Ukweli ni kuwa Kawawa alikuwa kilaza hivyo Julius was easy to manuplite him ndiyo maana akampa uwaziri mkuu. Kambona alikuwa kipanga. alikuwa anamcricise Julius openly. Vipnga wawili hawakai zizi moja. na kwa vile Julius alikuwa juu ikabidi kambona aanze. Ila ukichambua masuala ya kisiasa za kupigania uhuru Jina la kambona inabidi litajwe tena apewe heshima yake kama muasisi as well. kutofautiana itikadi sio usaliti wa nchi. Kamboana still alikuwa mzalendo wa Tanganyika na itabakia hivyo.
 

Ubepari ni muundo wa jamii unaotambua haki za mtu binafsi, zikiwemo haki miliki, na mali zote zinakuwa mikononi mwa watu. Katika mfumo huu serikali inajiondoa katika masuala ya uchumi (uzalishaji na biashara) kama vile inavyojiondoa katika masuala ya kidini. Katika mfumo huu serikali haitakiwi kuingilia soko huria na kama inaingilia basi iwe inafanya hivyo ili soko huria liweze kufanya kazi kwa kutumia misingi yake ya uchumi.

Sidhani kwamba umasikini wa nchi unafanya nchi isiwe ya kibepari.
 

That's a very good question!

Nafurahi pia unakubaliana na Maswali kuwa kusema mabaya yaliyofanywa na western countries dhidi ya nchi za Afrika sio kutetea viongozi wa Afrika bali pia kuongeza something in the mix.

Kwa nini viongozi hawakulinda masilahi yetu hilo ni swali ambalo ninajiuliza kila siku nikikumbuka kilichotokea siku ile Karamagi anasaini mkataba wa Buzwagi au usiku ule mkataba wa Richmonduli ukisaininiwa.

Ninachojiuliza katika kujaribu kujibu swali lako ni kuwa? Kama huyu dikiteta Nyerere alikuwa na power kiasi hiki, kwa nini basi hakuchukua hii migodi yote iliyouzwa wakati wa Mkapa na Mwinyi na kuifanya ya kwake.? Nani angemuuliza kama haya yanayosemwa hapa kuwa aliyafanya hakuna alokuwepo wa kumzuia.

Hii ni sababu nyingine ya kumuadhibu dikiteta Nyerere kwa kutoruhusu watu wa kabila (wazanaki) kuchimba dhahabu ya buhemba na badala yake Mkapa na wenzake wamekomba dhahabu na kuacha mashimo matupu...

damn you Nyerere....... grrrrrrrrrr, kusambaza ujamaa duniani hadi unalalisha njaa ndugu zako?
 
Maarifa,
Kawawa hakuwa kilaza. Tizama historia yake katika trade unions.Ila for Julius, hasa baada ya kasheshe ya Chifu Fundikira, na waislamu kuja juu kuwa TANU inaongozwa na Wakristo, Kawawa, being a Muslim and a southerner, was very important to Julius.
 

Jasusi, karibu na umetupa kitu ambacho tumekuwa tukikitafuta sana, historia yetu ya nyuma hasa kwa wale wanaojua. Hapa umetupa kitu kingine makini sana cha kufikiria. Vipi kuhusu mutiny ya 1964, ni kitu gani ambacho Kambona alikifanya kilichokuwa nje ya majukumu yake kama waziri wa Mambo ya Nje au Waziri wa Ulinzi?
 

Na mimi nimetafuta kweli kwenye research yangu nimekosa nchi hata moja ambayo serikali zimejiondoa katika uzalishaji na biashara! Inaonekana uzee umeanza kuniingia hapa tayari.
 

Sasa wewe unataka kuleta ukabila 🙂

Na akikwambia kuwa alikuwa anasubiri deal la kueleweka? Kwamba ma-deal yote aliyoyaona yalikuwa kama ya Richmond na Buzwagi, watu walitaka kumshikisha kitu kidogo halafu awaachie wavune kwa chee at the expense of Tanzanians.

Kuna wakati tulikuwa tunamsema sana Nyerere kutokana na kutotumia natural resources lakini nikiangalia mambo ya sasa naona labda mzee alikuwa na pointi.
 

Kwi kwi kwi,

Naona umeshaanza kumtetea Nyerere sasa! hujasoma hapa kuwa hakuna chochote chema alichofanya huyu baba na pia kuwa Nyerere ndiye chanzo cha ujamaa na umasikini wote wa Tanzania.

Na pia kuwa Nyerere ndiye mpaka sasa ameshikilia nchi ile isiendelee kutokana na sera zake za ujamaa? Mkuu utaitwa mjamaa kama Mwanakijiji! shauri yako
 

Mzee nilisema fair game. Mara ya kwanza unafanya makosa na kusamehewa. Lakini makosa ya kujirudia rudia ni Fair Game katika mambo ya Financials.
 
Mwanakijiji,
Kuhusu mutiny ya 1964 natamani mtu kama Kawawa angeandika memoirs zake kuhusu Kasheshe hilo. Niliwahi kumwuliza Mzee Bomani yeye alikuwa wapi wakati wa mutiny akaniambia alikuwa mmoja wa mawaziri waliopigwa makofi na 'afande', wakati wanamtafuta Nyerere. Wakati huo Mzee Bomani akiishi katika nyumba ile ya waziri karibu na Ikulu.Sasa ilikuwaje Kambona peke yake aliweza kuwasiliana na mutineers bila kupigwa makofi, sijui. Lakini ninachoamini, kama wangejua Nyerere alipokuwa, tungekuwa na kiongozi mwingine hapo 1964.
 
mwafrika wa kike mimi siogopi labels, hasa kama si za kweli.

Na mimi sipo hapa kuwa anti-Nyerere au anti-Kambona.Mimi nipo anti certain ideas or for certain ideas, kwa hiyo kuna ideas Nyerere alichemsha nitamblast (uchumi wa kujidai "kujitegemea" wakati hatuna viwanda wala mashamba makubwa, turning Tanzania into a police state etc) na kuna idea nitamsifu (hakuwa mroho kama Mobutu, ingawa angetaka kuiba mabilioni angeweza, kajitahidi kujenga national unity)

Hata Kambona naye kuna vitu alikuwa na vision (alitaka political plurality iendelee, hakutaka Azimio la Arusha) lakini kuna vitu alichemsha (hakuwa na organization formidable enough to launch opposition from within, which would have been more effective, alikuwa coward akakimbia)

Kwa hiyo you will see I tend not to fit into these labels too easily.
 
Pundit, Kambona hakukataa Azimio la Arusha, ambacho alikitaka yeye ni majaribio kwanza kabla ya kwenda full fledged.. alitaka kama ni vijiji vya ujamaa basi tuwe na vya mfano kwanza n.k
 

Ndio maana nasema childish, hiyo post unayonikariri nimekopi inasema wazi kuwa si maandishi yangu!!!. Nimeandika "paragraph hizi mbili toka kwenye article flani"...........maandishi yangu mimi ni kwa kiswahili na ya Scott kwa kizungu. Wallahi kila mtu alosoma ile post hata kama ni darasa la pili atajua kuwa maneno ktk paragraphs zile si yangu na hakuna sehemu nilosema ni yangu!!!!!!!!!. Jamaa bwana, kweli mkiishiwa hoja huleta vioja.........jaribu tena!!!!. Wakopie basi post nzima hapa watu waisome tena, waamue kama wewe umenikamata au umejikamata mwenyewe!!!!.
 

Hivyo ndivyo nilivyosema na kukopi hizo passages mbili za scott........................wapi nimesema haya ni maneno yangu YNIM!!!!????. Nimesema, "mfano mzuri ni huo hapo chini toka kwenye article flani hivi................." tatizo liwapi???. Watu bwana!!!
 
MKJJ,
Nakusubiri.............sema tatizo liwapi!!???
 

That is ok Pundit,

As longer as haya ni mawazo yako binafsi inabidi uyasimamie kwa nguvu zote. Good job, shule hiyo endelea kutoa maana hii ni JF baby! ambayo kila siku vichwa vipya vyenye nondo kama wewe na wengine wengi hapa vinaingia.

Thanks!
 
MKJJ,
Nakusubiri.............sema tatizo liwapi!!???

tatizo, hamna tatizo kwani SASA najua kuwa "article flani hivi" ilimaanisha siyo article yako. Maana hata mimi naweza kunukuu mojawapo ya article zangu (za kiingereza au kiswahili) na kuweka hapa na watu wakapata impression labda namnukuu mtu mwingine. Ila nikisema "article flani hivi" ina maana siyo ya kwangu. Sawa mkuu! Hii lugha ya Kiswahili inashida kidogo kwa sisi wengine. Kumbe uliposema "kutoka article flani hivi" ulikuwa unamaanisha hii ya Scott ambayo ina jina lake. Haya tuendelee kukata issue nimekuelewa sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…