Ukweli ni upi kuhusu Oscar Kambona?

Paskali,
Kitabu toleo la Kiingereza tunakwenda toleo la tatu na cha Kiswahili
tunakwenda toleo la nne.

Kitabu kithaminiwe vipi?

Je. unajua kitabu cha Kivukoni kimechapwa mara ngapi baada ya 1981
kilipochapwa kwa mara ya kwanza?
Kiukweli sifahamu kwa sababu mimi nimekijibia mtihani wa CSEE mwaka 1985 baada ya hapo sijujua chochote. Wakati nikuwa skuli sikuwahi kusoma kitabu chochote cha mwandishi Muhammed Said kwa sababu maabdishi yake hayakupitishwa kwenye ithbati ya kufundisha shule yoyote ya Tanzania!. Muhammed Said tuliyemsoma sisi ni Mzee MSA, Mohemed Said Abdullah
1.Duniani kuna watu
2.Kisima cha Giningi
3.Mke Mmoja Watume Watatu
4.Siri ya sifuri
5.Mzimu wa watu wa kale
6.Kosa la bwana msa

Paskali
 
[emoji122][emoji122][emoji122]
 
Povuuuuuu !!!
 
Pascal Mayalla

Kwanini unaikwepa "TAA" ?
 
Nina mashaka na hiyo Alama "A" yako.. Ulikua unajibu maswali ya historia bila kui trace back history!?

Historian yeyote lazima tujue chimbuko lake, historia inaleta mvuto pale unapoi trace sio kuja juu juu tu.
Usiwe na mashaka nayo, ni ile historia ya kujibia mitihani, TANU ilianzishwa mwaka 1954 na musisi wake ni Mwallimu Julius Kambarage Nyerere pekee!. Uhuru wa Tanganyika ulipatikana December 9 mwaka 1961na shujaa wa Uhuru ni Mwallimu Julius Kambarage Nyerere pekee!. Jamhuri ilipatikana December 9 mwaka 1962 na shujaa wa Jamhuri ni Mwalimu Julius Kambarage Nyerere pekee. Muungano ni 1964 mashujaa ni Nyerere na Karume, etc etc.

Hao wengine sio mashujaa wanaotambulika rasmi ila kwa heshima yao wote wamepewa majina na mitaa na kwa bahati nzuri sasa, mimi naishi huku Cleist Sykes Close!.

Paskali
 
Nakubalian na wewe, sote tuanajua Hayati Mwaliimu Nyerere ndio shujaa Wa Taifa. Lakini kwa afya ya Taifa na vijana wetu, kwanini wasiwatambue na hawa waasisi Wa harakati za Uhuru akina Sykes nk?

Unadhani wataathiri heshima ya Baba Wa Taifa?
 
Pascal Mayalla
Kwanini unaikwepa "TAA" ?
Siikwepi TAA, tunapozungumzia historia ya kitu inaanzia kilipozaliwa!. Hata wewe historia yako huanzia ulipozaliwa na sio ulipotungwa!.

TANU ilizaliwa 1954 na historia hiyo safi imeandikwa kwa umahiri kabisa na Chuo cha Chama Kivukoni. Tusilazimishe historia ya wale walowezi wa Kizulu wa TAA kuwa ndio historia ya TANU, TANU ni TANU, TAA ni TAA na CCM ni CCM, kama somo ni chimbuko then ndipo tufukue makaburi ya TAA!.

Paskali
 
Nakubalian na wewe, sote tuanajua Hayati Mwaliimu Nyerere ndio shujaa Wa Taifa. Lakini kwa afya ya Taifa na vijana wetu, kwanini wasiwatambue na hawa waasisi Wa harakati za Uhuru akina Sykes nk?

Unadhani wataathiri heshima ya Baba Wa Taifa?
Wanaotambulika sana ndio maana wote wamepewa mitaa!.

Paskali
 
Paskali,
Mohamed Said: MEDALI YA ABDULWAHID SYKES: MWENGE WA UHURU 1961 - 2011
 
Duh!
 
Hata muda ungerudi nyuma msidhani ingekua tofauti. The code of conduct doesnt change
 
Asante sana....historia nzuri kuhusu Kambona...kumbe nyuma ya mafanikio ya Nyerere kulikua na watu majembe sana kama wakina Kambona na wengine..R.I.P
 
Ongezea na Mwana wa Yungi Hulewa
 
Mzee Mohamed Said
Unaona ufahari gani hao machief kuwa waislam?

Hakuna ajabu yeyote,wangeanza kuja wahindi Pwani yetu Mkwawa asingeitwa Abdallah angeitwa Vishal au Gunpreet.

Hakuna Mwafrika yeyote aliyekua Muislam/Mkristo by default, wote wamerithi tu dini za kuletewa.Waafrika tulikua na dini zetu wenyewe na kiuhalisia Misri(Kemet) ndio asili ya Ukristo hivyo basi ndio asili ya uislam pia.
 
Huenda Mwl Nyerere atakuwa ni Mwenye heri Mwenye Roho Mbaya zaid kuwahi kutokea kwny Historia ya Kanisa Afrika Mashariki Kama utatumia Maisha ya Oscar Kambona na mateso na Manyanyaso waliopewa na Mwl Nyerere katika Miaka yote ya Utawala wake !
 
Cynical and satirical
 
kifimbo cheza aisee wakati mwingine hakuwa na shukran. mambo mengine inaweza kuwa aliadhibiwa na Mungu tu ndio maana alikufa hakuwa na furaha maishani kwasababu ya yale aliyowafanyia watz wenzake. kambona hakuwa mtu wa kumgeuka namna hiyo. na kile kweli kilikuwa kichwa cha mwanasheria, alikuwa na akili sana aisee hata katika speech zake huwezi kabisa kulinganisha na za kifimbo. kifimbo aisee alipitwa mbali na huyu jamaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…