Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Usiku umekuwa mkubwa In Shaa Allah kesho tukiamka salama nitakueleza kisa cha kuandika historia ya TANU na matatizo yaliyotokea.Mohamed Said unajua nilikuwa nikikutusi kulikopitiliza mpaka niliposoma kitabu chako August 2014.
You are a good Author, ila ulionesha kwa sehemu kubwa kuwa Waislam walinyanyaswa.
Na nikishakuuliza hili swali mara mbili na leo nitakuuliza tena kuwa:-
■ Kwanini unasema historia yao ilifutwa? Ilifutwa kwani ilikwishaandikwa?
■ Unafikiri ni nini kiliipa Ukristo nguvu ya kuweza kuwafanyia waislam hayo? Je ni Elimu tu au Urais wa Nyerere?
Inshaa Allah, naingojea kwa hamu na shauku.Usiku umekuwa mkubwa In Shaa Allah kesho tukiamka salama nitakueleza kisa cha kuandika historia ya TANU na matatizo yaliyotokea.
Kuna watu walifanya kazi kubwa sana kutengeneza standard ya mijadala mingi sana hapa JF,huwa nasikitika sana hizi mada za siku hizi.Historia ya mambo mengi ya Tanzania ipo hapa JF,kuna mijadala mizuri sana kuanzia 2007-2012Safi sana Mkuu!
Huu uzi uliouweka unamambo ya kujifunza...binfasi Mimi niliupitia mwezi January upo vizuri sana tena sana.
Watu walichangia vyema kwa weledi wa hali ya Juu,kama Mtu anania ya kujua historia ya kambona na Nyerere namuomba aupitie utamusaidia sana.
Azarel,Inshaa Allah, naingojea kwa hamu na shauku.
Mzee Mohamed Said naomba unipe majibu [emoji121] [emoji121] [emoji121]Mzee
Nchi yetu haiko katika sura ya udini kama unavotaka wewe iwe.Ndio maana wakapewa majina "neutral" infact nimesoma kitabuni mwako unakiri kua huyo chief wa Songea kuna wanazuoni wanapinga kua sio kama ulivyosema wewe ndiye,ila wewe ukaona fahari kusema Sultan Abdul Rauf Songea ndiye haswa Chief Songea Mbano.
Mzee Mohamed Said, shikamoo.Azarel,
Dossa Aziz anasema iko siku mara baada ya uhuru walikuwa wamekaa yeye
Dossa, Mwalimu Kihere, Nyerere na Abdul Sykes.
Mwalimu Kihere akaleta wazo la kuandika historia ya TANU na uhuru wa
Tanganyika.
Mwalimu Nyerere akalipenda wazo lile na akasema kati yao mtu anaeijua
TANU ni Abdul Sykes kwa hiyo kazi hiyo aichukue yeye.
Nyerere akampa Abdul Sykes mtu wa kumsaidia katika hiyo kazi na mtu
huyo alikuwa Dr. Wilbert Klerruu ndiyo kwanza karudi nchini baada ya
kumaliza Ph D yake Marekani.
Abdul Sykes akitegemea nyaraka za baba yake, Kleist na yale aliyoyaona
na kuyafanya yeye mwenyewe na aliokuwanao katika kuunda TANU alianza
hiyo kazi na alitumia ofisi yake ya TANU aliyokuwa akiitumia katika miaka ya
1950 alipokuwa Katibu wa TAA kisha kaimu Rais wake kati ya 1950 - 1953.
Lakini inaelekea kuwa yale aliyokuwa anaandika Abdul, labda kwa kuanza na
historia ya African Association na baba yake hayakuwa yanampendeza Nyerere.
Abdul alipogundua tatizo hili akajitoa katika utafiti ule lakini Dr. Klerruu yeye
aliendelea na kukamilisha ile kazi.
Hata hivyo kitabu hakikuchapwa lakini mswada ukaibiwa katika pale ofisi ya
TANU na huyo mwizi akafanya mabadiliko katika ule mswada akachapa kitabu
kilichotoka mwaka wa 1971.
Kimya kimya TANU ikakemea kitendo hiki na kuamuru kuwa kitabu hicho
kisichapwe tena.
Kitabu hiki hakina tofauti na kitabu cha Historia ya TANU cha Chuo Cha Kivukoni
kilichochapwa 1981.
Kitu muhimu katika historia hii ni kuwa baada ya uhuru palijitokeza kauli ya
kuibeza TAA na viongozi wake kuwa hicho hakikuwa chama cha siasa bali cha
starehe.
Lakini kubwa ikawa kila inapoelezwa kuwa Nyerere alichukua uongozi wa TAA
mwaka wa 1953 haisemwi huo uongozi aliuchukua mikononi kwa nani.
Ikawa kama vile inakwepwa kutajwa jina la Abdul Sykes na ikazuka dhana kuwa
Nyerere ndiye aliyeasisi TANU peke yake.
Dhana hii ilidumu kwa kipendi kirefu hadi mwaka wa 1988 nilipoandika makala
katika gezeti la African Events, ''In Praise of Ancestors,'' nikalitaja jina la Abdul
Sykes na mchango wa Waislam katika uhuru wa Tanganyika.
Hili gazeti lilikuwa linachapwa London.
Toleo lote lilikusanywa likatolewa katika, ''circulation,'' na toleo lililofuatia Dr.
Mayanja Kiwanuka wa CCM Dodoma akatoa karipio kali ndani ya gazeti hilo
dhidi ya mwandishi.
Mkasa mzima wa uandishi wa historia ya TANU nimeueleza kwa kirefu katika
kitabu cha Abdul Sykes.
Tusimame hapa kwa sasa.
Unaweza kuingia hapo chini kwa taarifa zaidi:
Mohamed Said: UTATANISHI KATIKA HISTORIA YA TANU
Bukoba...jibu kuhusu udini sitatoa mimi. Jibu atakupa Bergen (1981) na Sivalon (1992). Soma hizo rejea.Mzee Mohamed Said naomba unipe majibu [emoji121] [emoji121] [emoji121]
Ralph sijaelewa unaposema kinahusikaje. Nifafanulie.Mzee Mohamed Said, shikamoo.
Nilipokuwa primary school 1970's mwishoni nilisoma kitabu cha Historia ya TANU, na ninacho hadi leo nyumbani kijijini, kiliandikwa na Ulotu Abubakar Ulotu. Je kitabu hiki kinahusikaje katika maelezo uliyotoa hapa na kwenye maandishi yako mengine?
Naomba unifahamishe kama kitabu hicho cha mzee Ulotu nacho umekirejea katika maandishi yako, na usahihi wa historia iliyomo mleRalph sijaelewa unaposema kinahusikaje. Nifafanulie.
Kitabu cha Ulotu nitakueleza baadae nikiingia kwenye laptop hivi niko kwenye simu. Kuna nukuu zangu nataka usome.Naomba unifahamishe kama kitabu hicho cha mzee Ulotu nacho umekirejea katika maandishi yako, na usahihi wa historia iliyomo mle
Naomba unifahamishe kama kitabu hicho cha mzee Ulotu nacho umekirejea katika maandishi yako, na usahihi wa historia iliyomo mle
Paskali,Mkuu Maalim Mohamed Said
mtaka nyingi nasaba hupata mwingi msiba, kama lengo ni kuzungumzia historia ya TANU, ilianzishwa mwaka 1954 na Mwalimu Nyerere. Hatutafuti nyingi nasaba za historia ya TAA kwa sababu hatutaki mwingi msiba!. Kama lengo ni historia ya TANU kwa ajili ya Watanzania, then ni historia ya TANU ya Kivukoni ya kupatia A kwenye macheti, halafu hiyo ya Oxford na Cambridge yenye TAA, iwafae wasomi wa Oxford na Cambridge na sio Watanzania wa UDSM. Siku ukiitwa kutoa mhadhara pale Nkrumah Hall nijulishe nije nikisikize, lakini ukiitwa Oxford na Cambridge wala usihangaike kunijulisha, bali ukirejea ndipo unihadithie!.
Nabii wa kweli ni yule anayethaminiwa nyumbani na sii ugenini!. Historia ya kweli ya TANU ni ile ya Kivukoni na sio hiyo ya DAB!.
Paskali
Paskali,Mkuu Maalimhttps://www.jamiiforums.com/members/mohamed-said.12431/
naomba nisiongeze not a word more, not a word less ili nisiharibu.
Kiukweli nakiri kuwa mimi nina tatizo langu kubwa ni la kusoma baadhi maandishi sio kwa kuzingatia kilichoandikwa bali the motive behind mwandishi alipokuwa akiandika, na kiukweli natatizwa na kuwa mkali sana pale hadi urongo kuongezwa ili kukidhi the ill motive behind!.
Paskali