Azarel,
Dossa Aziz anasema iko siku mara baada ya uhuru walikuwa wamekaa yeye
Dossa, Mwalimu Kihere, Nyerere na
Abdul Sykes.
Mwalimu Kihere akaleta wazo la kuandika historia ya TANU na uhuru wa
Tanganyika.
Mwalimu Nyerere akalipenda wazo lile na akasema kati yao mtu anaeijua
TANU ni
Abdul Sykes kwa hiyo kazi hiyo aichukue yeye.
Nyerere akampa
Abdul Sykes mtu wa kumsaidia katika hiyo kazi na mtu
huyo alikuwa
Dr. Wilbert Klerruu ndiyo kwanza karudi nchini baada ya
kumaliza Ph D yake Marekani.
Abdul Sykes akitegemea nyaraka za baba yake,
Kleist na yale aliyoyaona
na kuyafanya yeye mwenyewe na aliokuwanao katika kuunda TANU alianza
hiyo kazi na alitumia ofisi yake ya TANU aliyokuwa akiitumia katika miaka ya
1950 alipokuwa Katibu wa TAA kisha kaimu Rais wake kati ya 1950 - 1953.
Lakini inaelekea kuwa yale aliyokuwa anaandika
Abdul, labda kwa kuanza na
historia ya African Association na baba yake hayakuwa yanampendeza
Nyerere.
Abdul alipogundua tatizo hili akajitoa katika utafiti ule lakini
Dr. Klerruu yeye
aliendelea na kukamilisha ile kazi.
Hata hivyo kitabu hakikuchapwa lakini mswada ukaibiwa katika pale ofisi ya
TANU na huyo mwizi akafanya mabadiliko katika ule mswada akachapa kitabu
kilichotoka mwaka wa 1971.
Kimya kimya TANU ikakemea kitendo hiki na kuamuru kuwa kitabu hicho
kisichapwe tena.
Kitabu hiki hakina tofauti na kitabu cha Historia ya TANU cha Chuo Cha Kivukoni
kilichochapwa 1981.
Kitu muhimu katika historia hii ni kuwa baada ya uhuru palijitokeza kauli ya
kuibeza TAA na viongozi wake kuwa hicho hakikuwa chama cha siasa bali cha
starehe.
Lakini kubwa ikawa kila inapoelezwa kuwa
Nyerere alichukua uongozi wa TAA
mwaka wa 1953 haisemwi huo uongozi aliuchukua mikononi kwa nani.
Ikawa kama vile inakwepwa kutajwa jina la
Abdul Sykes na ikazuka dhana kuwa
Nyerere ndiye aliyeasisi TANU peke yake.
Dhana hii ilidumu kwa kipendi kirefu hadi mwaka wa 1988 nilipoandika makala
katika gezeti la African Events, ''In Praise of Ancestors,'' nikalitaja jina la
Abdul
Sykes na mchango wa Waislam katika uhuru wa Tanganyika.
Hili gazeti lilikuwa linachapwa London.
Toleo lote lilikusanywa likatolewa katika, ''circulation,'' na toleo lililofuatia
Dr.
Mayanja Kiwanuka wa CCM Dodoma akatoa karipio kali ndani ya gazeti hilo
dhidi ya mwandishi.
Mkasa mzima wa uandishi wa historia ya TANU nimeueleza kwa kirefu katika
kitabu cha
Abdul Sykes.
Tusimame hapa kwa sasa.
Unaweza kuingia hapo chini kwa taarifa zaidi:
Mohamed Said: UTATANISHI KATIKA HISTORIA YA TANU