Ukweli ni upi kuhusu Oscar Kambona?

Ukweli ni upi kuhusu Oscar Kambona?

Mohamed Said unajua nilikuwa nikikutusi kulikopitiliza mpaka niliposoma kitabu chako August 2014.

You are a good Author, ila ulionesha kwa sehemu kubwa kuwa Waislam walinyanyaswa.

Na nikishakuuliza hili swali mara mbili na leo nitakuuliza tena kuwa:-

■ Kwanini unasema historia yao ilifutwa? Ilifutwa kwani ilikwishaandikwa?

■ Unafikiri ni nini kiliipa Ukristo nguvu ya kuweza kuwafanyia waislam hayo? Je ni Elimu tu au Urais wa Nyerere?
Usiku umekuwa mkubwa In Shaa Allah kesho tukiamka salama nitakueleza kisa cha kuandika historia ya TANU na matatizo yaliyotokea.
 
Safi sana Mkuu!

Huu uzi uliouweka unamambo ya kujifunza...binfasi Mimi niliupitia mwezi January upo vizuri sana tena sana.

Watu walichangia vyema kwa weledi wa hali ya Juu,kama Mtu anania ya kujua historia ya kambona na Nyerere namuomba aupitie utamusaidia sana.
Kuna watu walifanya kazi kubwa sana kutengeneza standard ya mijadala mingi sana hapa JF,huwa nasikitika sana hizi mada za siku hizi.Historia ya mambo mengi ya Tanzania ipo hapa JF,kuna mijadala mizuri sana kuanzia 2007-2012
 
Inshaa Allah, naingojea kwa hamu na shauku.
Azarel,
Dossa Aziz
anasema iko siku mara baada ya uhuru walikuwa wamekaa yeye
Dossa, Mwalimu Kihere, Nyerere na Abdul Sykes.

Mwalimu Kihere akaleta wazo la kuandika historia ya TANU na uhuru wa
Tanganyika.

Mwalimu Nyerere akalipenda wazo lile na akasema kati yao mtu anaeijua
TANU ni Abdul Sykes kwa hiyo kazi hiyo aichukue yeye.

Nyerere akampa Abdul Sykes mtu wa kumsaidia katika hiyo kazi na mtu
huyo alikuwa Dr. Wilbert Klerruu ndiyo kwanza karudi nchini baada ya
kumaliza Ph D yake Marekani.

Abdul Sykes akitegemea nyaraka za baba yake, Kleist na yale aliyoyaona
na kuyafanya yeye mwenyewe na aliokuwanao katika kuunda TANU alianza
hiyo kazi na alitumia ofisi yake ya TANU aliyokuwa akiitumia katika miaka ya
1950 alipokuwa Katibu wa TAA kisha kaimu Rais wake kati ya 1950 - 1953.

Lakini inaelekea kuwa yale aliyokuwa anaandika Abdul, labda kwa kuanza na
historia ya African Association na baba yake hayakuwa yanampendeza Nyerere.

Abdul
alipogundua tatizo hili akajitoa katika utafiti ule lakini Dr. Klerruu yeye
aliendelea na kukamilisha ile kazi.

Hata hivyo kitabu hakikuchapwa lakini mswada ukaibiwa ofisi ya TANU na huyo
mwizi akafanya mabadiliko katika ule mswada akachapa kitabu kilichotoka mwaka
wa 1971.

Kimya kimya TANU ikakemea kitendo hiki na kuamuru kuwa kitabu hicho
kisichapwe tena.

Kitabu hiki hakina tofauti na kitabu cha Historia ya TANU cha Chuo Cha Kivukoni
kilichochapwa 1981.

Kitu muhimu katika historia hii ni kuwa baada ya uhuru palijitokeza kauli ya
kuibeza TAA na viongozi wake kuwa hicho hakikuwa chama cha siasa bali cha
starehe.

Lakini kubwa ikawa kila inapoelezwa kuwa Nyerere alichukua uongozi wa TAA
mwaka wa 1953 haisemwi huo uongozi aliuchukua mikononi kwa nani.

Ikawa kama vile inakwepwa kutajwa jina la Abdul Sykes na ikazuka dhana kuwa
Nyerere ndiye aliyeasisi TANU peke yake.

Dhana hii ilidumu kwa kipendi kirefu hadi mwaka wa 1988 nilipoandika makala
katika gezeti la African Events, ''In Praise of Ancestors,'' nikalitaja jina la Abdul
Sykes
na mchango wa Waislam katika uhuru wa Tanganyika.

Hili gazeti lilikuwa linachapwa London.

Toleo lote lilikusanywa likatolewa katika, ''circulation,'' na toleo lililofuatia Dr.
Mayanja Kiwanuka
wa CCM Dodoma akatoa karipio kali ndani ya gazeti hilo
dhidi ya mwandishi.

Mkasa mzima wa uandishi wa historia ya TANU nimeueleza kwa kirefu katika
kitabu cha Abdul Sykes.

Tusimame hapa kwa sasa.
Unaweza kuingia hapo chini kwa taarifa zaidi:
Mohamed Said: UTATANISHI KATIKA HISTORIA YA TANU
 
Mzee

Nchi yetu haiko katika sura ya udini kama unavotaka wewe iwe.Ndio maana wakapewa majina "neutral" infact nimesoma kitabuni mwako unakiri kua huyo chief wa Songea kuna wanazuoni wanapinga kua sio kama ulivyosema wewe ndiye,ila wewe ukaona fahari kusema Sultan Abdul Rauf Songea ndiye haswa Chief Songea Mbano.
Mzee Mohamed Said naomba unipe majibu [emoji121] [emoji121] [emoji121]
 
Azarel,
Dossa Aziz
anasema iko siku mara baada ya uhuru walikuwa wamekaa yeye
Dossa, Mwalimu Kihere, Nyerere na Abdul Sykes.

Mwalimu Kihere akaleta wazo la kuandika historia ya TANU na uhuru wa
Tanganyika.

Mwalimu Nyerere akalipenda wazo lile na akasema kati yao mtu anaeijua
TANU ni Abdul Sykes kwa hiyo kazi hiyo aichukue yeye.

Nyerere akampa Abdul Sykes mtu wa kumsaidia katika hiyo kazi na mtu
huyo alikuwa Dr. Wilbert Klerruu ndiyo kwanza karudi nchini baada ya
kumaliza Ph D yake Marekani.

Abdul Sykes akitegemea nyaraka za baba yake, Kleist na yale aliyoyaona
na kuyafanya yeye mwenyewe na aliokuwanao katika kuunda TANU alianza
hiyo kazi na alitumia ofisi yake ya TANU aliyokuwa akiitumia katika miaka ya
1950 alipokuwa Katibu wa TAA kisha kaimu Rais wake kati ya 1950 - 1953.

Lakini inaelekea kuwa yale aliyokuwa anaandika Abdul, labda kwa kuanza na
historia ya African Association na baba yake hayakuwa yanampendeza Nyerere.

Abdul
alipogundua tatizo hili akajitoa katika utafiti ule lakini Dr. Klerruu yeye
aliendelea na kukamilisha ile kazi.

Hata hivyo kitabu hakikuchapwa lakini mswada ukaibiwa katika pale ofisi ya
TANU na huyo mwizi akafanya mabadiliko katika ule mswada akachapa kitabu
kilichotoka mwaka wa 1971.

Kimya kimya TANU ikakemea kitendo hiki na kuamuru kuwa kitabu hicho
kisichapwe tena.

Kitabu hiki hakina tofauti na kitabu cha Historia ya TANU cha Chuo Cha Kivukoni
kilichochapwa 1981.

Kitu muhimu katika historia hii ni kuwa baada ya uhuru palijitokeza kauli ya
kuibeza TAA na viongozi wake kuwa hicho hakikuwa chama cha siasa bali cha
starehe.

Lakini kubwa ikawa kila inapoelezwa kuwa Nyerere alichukua uongozi wa TAA
mwaka wa 1953 haisemwi huo uongozi aliuchukua mikononi kwa nani.

Ikawa kama vile inakwepwa kutajwa jina la Abdul Sykes na ikazuka dhana kuwa
Nyerere ndiye aliyeasisi TANU peke yake.

Dhana hii ilidumu kwa kipendi kirefu hadi mwaka wa 1988 nilipoandika makala
katika gezeti la African Events, ''In Praise of Ancestors,'' nikalitaja jina la Abdul
Sykes
na mchango wa Waislam katika uhuru wa Tanganyika.

Hili gazeti lilikuwa linachapwa London.

Toleo lote lilikusanywa likatolewa katika, ''circulation,'' na toleo lililofuatia Dr.
Mayanja Kiwanuka
wa CCM Dodoma akatoa karipio kali ndani ya gazeti hilo
dhidi ya mwandishi.

Mkasa mzima wa uandishi wa historia ya TANU nimeueleza kwa kirefu katika
kitabu cha Abdul Sykes.

Tusimame hapa kwa sasa.
Unaweza kuingia hapo chini kwa taarifa zaidi:
Mohamed Said: UTATANISHI KATIKA HISTORIA YA TANU
Mzee Mohamed Said, shikamoo.
Nilipokuwa primary school 1970's mwishoni nilisoma kitabu cha Historia ya TANU, na ninacho hadi leo nyumbani kijijini, kiliandikwa na Ulotu Abubakar Ulotu. Je kitabu hiki kinahusikaje katika maelezo uliyotoa hapa na kwenye maandishi yako mengine?
 
Ralph sijaelewa unaposema kinahusikaje. Nifafanulie.
 
Historia imetulia, asante, mwenye historia nyingine aanzishe uzi wake hii ni kuhusu Oscar Kambona
 
YEYOTE AMBAE ALIKUWA NA MAWAZO TOFAUTI NA YALE YA MWALI ALIONEKANA NI HAINI WAKUTUPWA. ZIDUMU FIKRA ZA M/KITI NDO ZILIIPONZA NCHI TOKA ZAMANI HATA KAMA HAZIKO SAHIHI NA OLE WAKO UPINGE WE JAIL YOU. INAINGIAJE AKILINI ETI UMEFIKIA NYUMBANI KWANGU TUKAPANGA MIKAKATI YA KUPATA UHURU HADI TUKAUPATA KWA SHIDA ZOTE HALAFU ILE NYUMBA UNATAKA UITAIFISHE. YAANI ISIWE YANGU TENA , HIVI KUNA TAHIRA YEYOTE ATAKUBALI SUALA HILO NA KAM UKIPINGA WE NI HAINI WE JAIL U, KISA CHA BIBI TITI NA CHIEF SAID FUNDIKIRA KINASIKITISHA. NDO PALE NIKAJA KUAMN KAULI YA LISSU KUWA HUYU JAMAA ALIKUW DCTTA
 
Stori yako ni nzuri endelea kutupatia mwendelezo wa stori hizi.
 
Naomba unifahamishe kama kitabu hicho cha mzee Ulotu nacho umekirejea katika maandishi yako, na usahihi wa historia iliyomo mle
Kitabu cha Ulotu nitakueleza baadae nikiingia kwenye laptop hivi niko kwenye simu. Kuna nukuu zangu nataka usome.
 
Naomba unifahamishe kama kitabu hicho cha mzee Ulotu nacho umekirejea katika maandishi yako, na usahihi wa historia iliyomo mle

Ralph...
Nukuu hii imetoka katika kitabu cha Abdul Sykes (1998).
Nadhani utaelewa na swali lako kuhusu kitabu ulichoniuliza litakuwa limejibiwa:

''Haukupita muda Abdulwahid akatambua kuwa viongozi wapya walioshika nafasi katika TANU kwa kweli hawakuwa na nia hasa ya kutafiti na kuandika historia ya Tanganyika bali nia na azma yao ilikuwa na kumjenga Nyerere na kumkuza kwa sifa ambazo hazikumstahili.

Abdulwahid alipong’amua hili haraka akajitoa katika kazi ile. Hata hivyo Dr. Kleruu aliendelea na utafiti na akaandika historia ya TANU. Historia hii inasemekana ilifuta mchango mzima wa akina Sykes katika kuunda African Association na baadae TANU.

Hata hivyo baada ya mswada kukamilika haikuchapishwa na ikabaki katika maktaba ya TANU, Mtaa wa Lumumba, Dar es Salaam.

Lakini baadae kazi ile ilitoweka na ikachapishwa baada ya ‘’mwandishi,’’ kufanya mabadiko kadhaa katika mswada ule ili usitambulike chanzo chake.

Hata hivyo TANU iligundua kuwa ile ilikuwa historia yao iliyoandikwa na Dr. Kleruu na wakafanya bidii kuzuia isichapishwe. Kimya kimya TANU ikafanya juhudi ya kuzuia kitabu hicho kisitoke toleo la pili.

Lakini hili halikuwezekana na kitabu hicho kimechapishwa sasa mara kadhaa. Uandishi wa kitabu kile haukutofautiana sana na kitabu cha TANU kilichotoka mwaka 1981 kilichoandikwa na Chuo cha TANU cha Kivukoni.

Hata hivyo kuna kasoro katika kitabu hicho ambacho ‘’mwandishi,‘’ alishindwa kugundua na kuweza kujikinga asijulikane kama kile kitabu hakikuandikwa na kalamu yake. ‘’Mwandishi’’ kama tunavyoweza kumwita, akiandika katika nafsi ya kwanza, anaeleza kuwa amekiandika kitabu kile mwaka wa 1964.

Katika maelezo hayo ‘’mwandishi,’’ anatoa habari ambazo msomaji makini anahisi kuwa ‘’mwandishi’’ alikuwa marika sawa na anawafahamu vyema wale wazalendo anaoandika habari zao. Lakini mwandishi anasahau kuwa mwaka 1964 wakati yeye anadai alikuwa akiandika habari hizo yeye alikuwa mvulana mdogo na asingeweza kuwajua vile wale wazalendo na habari zilizotokea miaka ya 1950 wala asingeweza kuwa na ubongo wa kutafakari mambo kama yale.

Sasa swali linakuja. Huyu aliyeandika habari zile ni nani hasa? Kutokana na maelezo ambayo kitabu hiki kimeeleza ni wazi aliyeandika habari zile hawezi kuwa Dr. Kleruu kwa sababu Kleruu katika kipindi kile, hakuwapo katika harakati zile za kuunda TANU.

Ni mtu mmoja tu ndiye anaeweza kuwa na habari zile na kuwa na ufahamu wa mambo yalivyokuwa miaka ile. Huyu atakuwa ni marehemu Abdulwahid akiandika mwaka 1964.

‘’Mwandishi,’’ kwa ujinga amenakili kutoka kwenye maandishi ya Abdulwahid ambayo yalikuwa yamehifadhiwa katika Maktaba ya TANU, Dar es Salaam.

Na huyu ‘’mwandishi,’’ wala hakunakili maandishi yale mwaka 1964, bali miaka mingi baada ya kifo cha Abdulwahid kutokea.''
 
Mkuu Maalim Mohamed Said
mtaka nyingi nasaba hupata mwingi msiba, kama lengo ni kuzungumzia historia ya TANU, ilianzishwa mwaka 1954 na Mwalimu Nyerere. Hatutafuti nyingi nasaba za historia ya TAA kwa sababu hatutaki mwingi msiba!. Kama lengo ni historia ya TANU kwa ajili ya Watanzania, then ni historia ya TANU ya Kivukoni ya kupatia A kwenye macheti, halafu hiyo ya Oxford na Cambridge yenye TAA, iwafae wasomi wa Oxford na Cambridge na sio Watanzania wa UDSM. Siku ukiitwa kutoa mhadhara pale Nkrumah Hall nijulishe nije nikisikize, lakini ukiitwa Oxford na Cambridge wala usihangaike kunijulisha, bali ukirejea ndipo unihadithie!.

Nabii wa kweli ni yule anayethaminiwa nyumbani na sii ugenini!. Historia ya kweli ya TANU ni ile ya Kivukoni na sio hiyo ya DAB!.

Paskali
Paskali,

Leo asubuhi mmoja wa marafiki zangu aliyekuwa akifuatilia mjadala wangu
na wewe ameniandikia maneno hayo hapo chini ambayo sijathubutu hata
kubadili nukta.

Nimekuwa na ujasiri tu wa kuondoa jina lake kwa kuwa sina uhakika kama
angependa jin lake lionekane na nimeogopa kumuomba ruhusa yake asije
kunikatalia.

Naamini maneno haya anakulenga wewe na mfano wa wewe:

''... nakusifu sana kwa jinsi unavyoweza kuwa "cool" with extreme level ya controlled anger unapoongea na ving'ang'anizi wa ubishi usio na hoja. Uvumilivu wako naamini ni kipaji na si exercise pekee ya academic au intellectual tolerance. Maana wengi hawana hiyo.

Tabu ya baadhi ya Nyerereists ni tabia yao ya kwenda "overboard" ktk fikra zao za kumpamba mwalimu. Nimesikitishwa sana kuona student wa Kivukoni school anathubutu kumuita Abd/Kleist mtu wa "kuja" kwa juhudi za kutaka asipewe haki yake ya kizalendo ktk ukombozi wa nchi hii kwa hofu ya kum- eclipse/obscure Nyerere anaemtaka atambulike peke yake.

Hawa wanafunzi na waalimu wao wanajua wazi kwamba uwananchi wa Abd/Sykes hauwezi kufifishwa kwa namna yoyote ile kutokana na ukweli wa historia ya Africa na watu wake ilivyokuwa. Its only the mind infested with primitive ideas of tribalism ndo inaweza isielewe. Sijui huyu anawatizamaje Wangoni (Wazulu) walioondoka Zululand kutokana na janga la "Mfecane" 1815/1840 na kuingia huku, wengi wakipitia Rukwa, Tabora, Iringa na kutua Ruvuma. Ipo mifano mingi kwa makabila mengine ya nchini yenye historia ya aina hiyo. Pamoja na hayo, A/Kleist bibi yake mzaa baba hakutoka Zululand. Katoka hapa ktk nchi aliyoipigania na kuikomboa toka kwa Waingereza.

Ama kuhusu akina Budohi, Okoch, Fiah, Phombea; inasikitisha kuwa inabidi wewe Uncle uchukue dhima ya kuwa elimisha graduates wa Kivukoni school kuhusu "early anti - Colonial African solidarity." Leo sisi tunajisifu kusaidia ukombozi wa nchi za kusini mwa Afrika na kutoa dhana kwamba "tulifikiri, tukaamua, tukafanya jambo la hisani kuliko wengine." Wakati ukweli ni kwamba akina Budohi waliisha tutangulia. Na wala hatutaki kuonesha kuwa spirit hii alikuwa nayo pia Bi Titi aliekubali na kwenda kuhamasisha anti -Colonial struggle ya Wakenya kuanzia Mombasa hadi Kisumu.

Umeandika sana kuwaelimisha Watanzania na wengineo jinsi political activists wa TAA; Ally Sykes alivyoingia na kutoka clandestinely Southern Rhodesia alikoenda ku strategise ukombozi na ma activists wenzake wa Central and Southern Africa; na jinsi akina Dosa na Abdu walivyofanya hivyo Kenya, in contacts with Kenyatta and other MauMau leaders ktk solidarity ya African liberation of East, Central and Southern Africa - kabla ya mwalimu kushiriki ktk kuasisi PAFMECA/PAFMECSA. Kipindi hicho cha African solidarity na internationalism cha akina Sykes ni kipindi ambacho hata political activists maaruf wa ANC J. B. Marx, Moses Kotane, Oliver Tambo na Nelson Mandela hawajafika kwetu. Hiyo ndiyo TAA na wanasiasa wake walioikomboa Tanganyika, ambao leo baadhi ya watu wanataka kushawishi historia yao isitambulike.

Cha kusikitisha zaidi ni historia ya Kivukoni school kuwa na ukaribu na 'Fabian Society' with its orientation towards the working class. Ni vipi mtu apitie hapo na atoke pasipo kumjua Rosa Luxemburg (1871 - 1919) na spirit yake ya international proletarians na namna alivyokuwa aki debate na Ilyich Lenin kuhusu theories za ukombozi. Au hata ile historia ya French Revolution (1789) na jinsi ilivyokuwa hijacked na bourgeois politics; ambapo kuna fursa kubwa ktk historia hiyo ya kumjua Marquis de Lafayette (1757 - 1834) ambae ni maaruf ktk historia ya dunia kuwa ni "hero of two worlds;" Kwa kushiriki French Revolution na kuendelea; na pia kushiriki kikamilifu ktk American War of Independence from British Empire (1775 - 1783) kiasi cha kupewa urai wa Marekani, zawadi za kila aina zikiwemo pesa taslim, minara na majina ya miji kadhaa iliyoweka kumbukumbu yake.

Kwa Afrika, hatua inayofanana na hiyo ni ile ya Rais wa Guinea, Ahmed Sekou Toure aliyempa Kwame Nkrumah Urais mwenza wa Guinea.

Historia hiyo ya dunia na Afrika inatarajiwa iwe maaruf hapa kwetu ktk vyuo vilivyofundisha siasa na itikadi za ukombozi. Ni jambo la kushangaza kuona mhitimu wa vyuo vya aina hiyo muelekeo wake hauendani na athari za msingi wa mafunzo ya historia hiyo. Labda iwe haikufundishwa; au tuseme mwanafunzi hakuwa makini ktk masomo yake?

Ni muhimu ku note kuwa licha ya yote hayo aliyofanyiwa na Wamarekani, Lafayette aliamua kubaki kuwa Mfaransa na kufia huko. Aliwaridhisha Wamarekani kwa kuruhusu kiasi cha udongo kutoka nchini Marekani utumbukizwe kwenye kaburi lake umauti utakapomfika. Na ilikuwa hivyo.''
 
Mkuu Maalimhttps://www.jamiiforums.com/members/mohamed-said.12431/
naomba nisiongeze not a word more, not a word less ili nisiharibu.

Kiukweli nakiri kuwa mimi nina tatizo langu kubwa ni la kusoma baadhi maandishi sio kwa kuzingatia kilichoandikwa bali the motive behind mwandishi alipokuwa akiandika, na kiukweli natatizwa na kuwa mkali sana pale hadi urongo kuongezwa ili kukidhi the ill motive behind!.

Huna elimu ya kujadili historia hii.
Wengi wanaiogopa.

Ndiyo uje si bure kuwa iliwatisha miaka 1960 na inaendelea kuwatisha
hadi leo zaidi ya nusu karne imepita.

Lipi la uongo katika historia hii?
Eleza nikupe jibu vinginevyo kaa kimya usizungumze kitu usichokijua.
 
Back
Top Bottom