Ukweli ni upi kuhusu Oscar Kambona?

Naomba unielimishe ndugu Dr. Aggrey ni nani? Maana mie nafahamu yule aliyekuwa mghana sijui kama nipo sahihi.Muelezee kwa kina.
Ile Aggrey street Kariakoo na Mnazi mmoja yamepewa jina la huyu mtu?
Iliuaje hadi amepewa mitaa Tanzania? na anaingiaje kwenye hiyo historia ya Tanganyika?
I'm humbled.
 
Herikipaji,
Nakunyambulia habari za Dr. Aggrey kutoka katika kitabu cha Abdul Sykes:

''... alikuwa Dr James Kwegyir Aggrey, Mwafrika kutoka Ghana ndiye mtu aliyemtia Kleist hamu ya kuingia katika siasa. Dr Aggrey alikuja Tanganyika mwaka 1924. Dr Aggrey alikuwa katika Phelps-Stokes Commissions iliyokuwa imeundwa kuchunguza elimu ya Waafrika. Ilikuwa katika kipindi hiki akiwa ndani ya kamisheni hii ndipo alipokuja Tanganyika. Dr Aggrey alikataliwa kupanga New Africa Hotel kwa kuwa alikuwa mtu mweusi. Ikabidi Gavana Donald Cameron amtafutie chumba Government House ajisitiri kwa malazi. Ilikuwa wakati huu alipokuwa Dar es Salaam ndipo Dr Agrrey alipokutana na Kleist. Dr Aggrey alimtunukia Kleist moja ya vitabu vyake na akakitia sahihi yake. Hakuna hata mtoto mmoja wa Kleist ambae anakumbuka jina la kitabu hiki. Kleist alikithamini kitabu hiki na kilipamba shubaka lake la vitabu kwa miaka mingi. Mafanikio ya Dr Aggrey kama Mwafrika yalimtia moyo Kleist.



Mwaka wa 1929 Kleist na baadhi ya rafiki zake wa karibu kama Mzee bin Sudi, ambaye wazazi wake walikuwa Wamanyema kutoka Belgian Congo, Ibrahim Hamis - Mnubi ambaye baba yake alitoka Daffur nchini Sudan, Zibe Kidasi, Ali Said Mpima - Mzaramo, Suleiman Majisu, Raikes Kusi, Rawson Watts na Cecil Matola - Myao kutoka Masasi walianzisha African Association, Kleist akiwa katibu muasisi. Wakati ule Gavana wa Tanganyika alikuwa Sir Donald Cameron ambae alitawala Tanganyika kuanzia mwaka wa 1925 ñ 1929. Cameron alikuwa gavana mliberali na alikuwa akifahamiana na Kleist. Cameron ndiye aliyeanzisha Baraza la Kutunga Sheria la kwanza na mfumo wa Indirect Rule katika Tanganyika. Msimamo wake huu ndiyo hasa uliochangia katika kuwezesha kunzishwa kwa African Association. Lakini juu ya haya yote, chama hiki kiliaswa kisijiingize kabisa katika siasa. Wakati chama hiki kinaanza tayari kulikuwepo na chama cha Wazungu na Waasia. Lakini katika Baraza la Kutunga Sheria Waafrika walikuwa wakiwakilishwa na padri wa Kikatoliki, Father Gibbons, ambae hakuwa hata anaishi na Waafrika bali akikaa Minaki Misheni nje ya Dar es Salaam...''
 
Ibn Hazm Bookshop Msikiti wa Mtoro na Manyema bei shs. 10,000.00 kipo kwa Kiingereza na Kiswahili.
 
Huenda Mwl Nyerere atakuwa ni Mwenye heri Mwenye Roho Mbaya zaid kuwahi kutokea kwny Historia ya Kanisa Afrika Mashariki Kama utatumia Maisha ya Oscar Kambona na mateso na Manyanyaso waliopewa na Mwl Nyerere katika Miaka yote ya Utawala wake !
Najaribu kutafuta uhusiano wa hii post yako na mjadala unaondelea naona kama nafeli.
 
Najaribu kutafuta uhusiano wa hii post yako na mjadala unaondelea naona kama nafeli.

Umeshindwa kujua Mahusiano kwa kuwa Wewe ni Mtoto!

Historia Ya Kambona haikamiliki bila ya kukumbusha Unyama aliofanyiwa na Nyerere ikiwa ni Pamoja na uzushi mwingi na Propaganda chafu alizosambaza dhidi ya Oscar na kumweka Kizuizini Mdogo wake Oscar Kambona kwa zaid ya Muongo mmoja Gerezani kisa ni Ndugu wa Mtu anaemchukia Pamoja na kutaifisha/ ku pora Mali zote ikiwa ni Pamoja na Nyumba za Kambona na za Familia yake!

Wasifu tunaozungumzia hapa Great thinkers tofautisha na vile vi CV vya page mbili vya kuombea Kazi!
 
Acha uongo,Tunapogusa historia basi iwe historia kweli sio kupapasa juu tu.Lakini nikwambie shule ya msingi inafundisha historia ya TAA isipokuwa kwa uchache
 
Duuuuh..!
 


Kupata Alama A si lazima iwe ni uthibitisho wa Weledi wako inawezekana pia Ikawa Majibu yako yalifanana sana na Marking scheme ya Mitihani uliyofanya, Kama Marking scheme ilikuwa na Makosa lakin bado Majibu yako yakafanana na Marking scheme lazima upate Alama A.


Kusema Historia ya TANU ilianzia 1954 pale ilipozaliwa imenifanya kutafakari Kama baada ya zoezi la uhakiki wa Vyeti feki inawezekana kuanza na uhakiki wa Elimu feki?

Kama Historia ya kitu inaanza pale kilipopatikana Mf TANU ianzie 1954 kwanini Histria ya Uhuru wa Tanganyika isianzie 1961?
 
TANU ilizaliwa mwaka 1954 Lakini haikuwa mwanzo wa TANU.TAA ndo ilizaaa TANU yaani hii ni sawa na mtoto kuzaliwa alafu hataki kujuwa historia ya wazazi wake
 
Nakufuatilia kwa karibu sana wewe na Pascal Mayalla
Mvaa...
Ahsante sana.

Faraja wa mwandishi yeyote yule ni kupata mrejesho kwa wasomaji wake
kuwa wanamsoma kama ulivyofanya wewe hapa.

Kabla ya kuandika kitabu cha Abdul Sykes hakuna mtu aliyenijua katika
duru ambazo unaweza kuziita za ''kisomi,'' ukipenda.

Baada ya kitabu kutoka London na kufanyiwa ''reviews,'' yaani mapitio
ya kitabu na wasomi mbalimbali ghafla nikaona nimekuwa nikitajwa na
kupata mialiko kwingi ndani na nje ya nchi.

Furaha yangu ilizidi siku nilipopekea email kutoka kwa Prof. Ali Mazrui
na siku nilipoona kitabu changu kimeandikiwa, ''review,'' na John Iliffe
katika Cambridge Journal of African History.

Yaliyobakia sasa ni historia.
 
TANU ilizaliwa mwaka 1954 Lakini haikuwa mwanzo wa TANU.TAA ndo ilizaaa TANU yaani hii ni sawa na mtoto kuzaliwa alafu hataki kujuwa historia ya wazazi wake
Forum...
Marehemu Abdul Sykes anasema yeye kumbukumbu yake ya awali kabisa ya TAA
ni kuchukuliwa na baba yake, Mzee Kleist pale New Street wakati inajengwa hiyo
ofisi ambayo ilikuja kuwa ofisi ya African Association kwa mtindo wa kujitolea kwa
wanachama wote kukusanyika pale kila Jumapili kusaidiana na mafundi katika ujenzi.

Wakati ule Abdul Sykes labda alikuwa mtoto wa umri wa miaka 9 hivi au chini ya
hapo.

Hii ilikuwa miaka ya mwanzoni 1930 na ofisi ikafunguliwa rasmi 1933.

Ukimtoa mdogo wake Ally na Tewa Said Tewa katia wale waasisi 17 wa TANU
1954 hakuna mwingine mwenye historia na kumbukumbu kama hii.
 
Ok, ni kweli watu wengi wamekua wakifanya mambo mengi mazuri au mabaya lakini hawafahamiki, anaweza akabahatika jambo moja tu maishani mwake likamfanya jamii imfahamu na aweze kua maarufu, kwa mfano kiongozi wa Alshabab hakuna ambaye angemfaham angeendelea na shughuli zake za awali, lakini alipoanza kumwaga damu kwa jina la Allah hata mimi nikataka kujua chimbuko lake.
 
Mvaa...
Umetoa mfano ambao mimi sijaupenda hata punje.

Post iliyopita nimeeleza vipi Abdul Sykes alivyokuwa anaijua TAA na TANU kiasi
alishuhudia kwa macho yake wakati ofisi ile ikijengwa katika miaka ya 1933.

Taarifa kama hizi na nyinginezo ambazo hakuna mtafiti yeyote kabla yangu alau
alizigusia kwa mbali ndizo zilizofanya watu wanisikilize.

Ndugu yangu katika historia kama hii unakuja na wauaji AlShabab.
Bahati mbaya iliyoje kwangu.
 
Kusema Historia ya TANU ilianzia 1954
Kama Historia ya kitu inaanza pale kilipopatikana Mf TANU ianzie 1954 kwanini Histria ya Uhuru wa Tanganyika isianzie 1961?
Mkuu Pohamba, historia ya kitu huanzia pale kilivyo anza. Historia ya uhuru inaanzia harakati za kudai uhuru. Historia ya TANU imeanzia 1964. Historia ya CCM imeanzia 1977. Historia ya Muungano imeanzia 1964. Historia ya Pohamba imeanzia siku alipozaliwa na sio alipotungwa.

Lakini kama unazungumzia chimbuko ndipo utarudi nyuma kwa chimbuko la, TANU ni TAA, Chimbuko la CCM ni Muungano wa TANU na ASP. Chimbuko la Pohamba ni Baba Pohamba na Mama Pohamba etc.

Historia ni mwanzo wa kitu not necessarily chanzo.

Paskali
 
Acha uongo,Tunapogusa historia basi iwe historia kweli sio kupapasa juu tu.Lakini nikwambie shule ya msingi inafundisha historia ya TAA isipokuwa kwa uchache
Historia ya TAA ni historia ya TAA. Historia ya TANU ni historia ya TANU na Historia ya CCM ni historia ya CCM. Labda kama unazungumzia Chimbuko, hapo utakuwa sawa kuwa chimbuko la TANU ni TAA, Chimbuko la CCM ni TANU na ASP.

Ukiuliza swali kwenye mtihani TANU ilianza lini, utajibu Tarehe 7/7/1954. Not a word more, not a word less na utapata 100% kama mimi nilivyopata.

Ukianza kuandika kikapanda kikashuka, utapata maksi kama za Bashite.

Paskali
 

Historia ya Kitu ni Pamoja na chimbuko la hicho kitu aliekufundisha kuwa Historia ya kitu na chimbuko lake ni vitu Tofauti kakuhadaa Hata Kama alikupa A kwny Mitihani!

Ukiambiwa Utaje Historia ya Vita ya kwanza ya Dunia ukaanza kueleza kuanzia Siku ya kwanza Risasi kurushwa badala ya kuanza na Matukio yaliyopelekea hiyo vita utakuwa unajiabisha!

akikwambia umueleze History ya CCM usipotaja chimbuko lake la kutokana na ASP na TANU utakuwa umetaja Historia Pungufu!
 
Paskali,
Ukisoma Nyaraka za Sykes kichwaa kitakuuma na utapigwa na bumbuzi kubwa
wakati mwingine kujiuliza hivi haya ninayosoma ni kweli?

Lakini ni kweli kwa kuwa ndiyo hizo nyaraka unazo mkononi unaziona, umezishika
na unazisoma.

Abdul anasema yeye kamuona baba yake na rafiki zake wakijenga ofisi ya African
Association New Street na Kariakoo Street akiwa mtoto mdogo.

Abdul anaongeza anasema baba yake alimwambia kuwa aliyekuwa anawawakilisha
Waafrika katika Legico miaka ya 1920 alikuwa Padri kutoka Misheni ya Minaki akiitwa
Father Gibbons.

Father Gibbons ndiye huyo hapo chini kwenye picha wa kwanza kushoto wa pili kulia
ni Chief Thomas Marealle na huyo mama wa kwanza waliokaa ni mke wa Chief
Marealle
:



Unaendelea kupitia hizi nyaraka unakutana na barua ''handwriiten,'' za Chief Marealle
anaandikiana na Ally Sykes kuhusu harakati na uongozi wa Tanganyika itakapokuwa
huru.

Chief Marealle anaeleza fikra zake kuhusu Mwalimu Nyerere kama kiongozi na TANU
kama chama.

Ikiwa mtu hataki kuisikia historia hii basi lazima atakuwa ana lake jambo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…