herikipaji
JF-Expert Member
- Aug 23, 2016
- 1,198
- 1,369
Naomba unielimishe ndugu Dr. Aggrey ni nani? Maana mie nafahamu yule aliyekuwa mghana sijui kama nipo sahihi.Muelezee kwa kina.Pascal,
Wala mimi sishangai kwa wewe kusema hayo uliyosema kwani hao waliokuja
kuingia TANU 1954 hapo ndipo ulipo ukomo wao wa kujua mambo mtu hawezi
kuwalaumu kwani hawakuwapo na hawajui kilikuwapo nini kabla yao.
Lakini ukienda kwa waliokuwapo na wa miaka ya 1920 watakuambia kuwa
alikuwa Dr. Aggrey ndiyo aliyempa Kleist Sykes fikra ya kuanzisha African
Association alipokuja Tanganyika 1924.
Hii ni historia na kwa mtu mwenye ubongo uliokaa vyema atataka kumjua huyu
Aggrey ni nani, katoka nchi gani na vipi alikutana na Kleist na kumpa fikra hiyo
na huyi Kleist ni nani katika historia ya uhuru wa Tanganyika?
Ikiwa ubongo wako una maradhi basi utajilazimisha uridhike na TANU bila ya
kuifahamu African Association na waasisi wake wala kujiukiza imekuwaje ndugu
wawili Abdul na Ally Sykes wote wawe waasisi wa TANU na kadi zao za ziwe
zimefuatana na kadi ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere?
Kadi no. 1 Julius Nyerere, no. 2 Ally Sykes na no. 3 Abdul Sykes na kadi
zote hizo tatu ziwe na sahihi ya Ally Sykes?
Hakika haiwezekani kuwa haya yalikuja hivi hivi pasi ya kuwa na sababu.
Waarabu wana msemo: ''Ukiijua sababu huondoka ajabu.''
Sasa ukiwa haya yote huyataki nani mwenye hasara.
Mwenye hasara utakuwa wewe unaebakia na ujinga ilhali elimu ipo wazi na
kwa kuhitimisha nukta hii chembelecho Maalim Faiza, ''Elimu bila khiyana,''
elimu ipo na ukitaka utawezakuipata bure.
Hassan Upeka aliliambia jopo la Chuo Cha Kivukoni la waandishi wa historia
ya TANU kuwa haiwezekani mkamfikia Nyerere katika TANU bila ya kupita kwa
Abdul Sykes, hiyo haitakuwa historia ya TANU.
Lakini wewe unasema historia hii ya Kivukoni ndiyo iliyokupa alama ''A'' katika
mtihani.
Sawa wala mimi sistaajabu.
Leo tuaona nchi inavyohangaika na vyeti vya kughushi.
Haya ndiyo matokeo yake.
Vyuo vyenye kughushi na shule zake na vitabu vya kughushi vitatoa ''A'' kama hiyo
yako na wala mimi sikulaumu wewe.
Itatuchukua muda kukaa vyema.
Lakini Chuo Kikuu Cha Harvard na Oxford University Press baada ya kusoma historia
ya Kleist Sykes wamemtia katika Dictionary of African Biography (DAB).
Ukipenda unaweza kusoma hapo chini ukalinganisha na historia unayoijua wewe:
Mohamed Said: KLEIST SYKES (1894 - 1949) KATIKA DICTIONARY OF AFRICAN BIOGRAPHY (DAB) OXFORD UNIVERSITY PRESS, NEW YORK
![]()
Ile Aggrey street Kariakoo na Mnazi mmoja yamepewa jina la huyu mtu?
Iliuaje hadi amepewa mitaa Tanzania? na anaingiaje kwenye hiyo historia ya Tanganyika?
I'm humbled.