1.
Mabaharia walifikia mahali hawakutakiwa kuleta magari, kama ilikuwa ni sheria au sio hilo sijui, kila aliyerudi na magari aliambiwa kuwa sheria hairuhusu kwa sababi magari ni mabovu yataleta polution, lakini wenye connection waliweza kuyatoa bila noma, sasa wasiokuwa na connections, ilibidi kuyasubiri magari yao wenyewe kwenye mnada wa serikali, ambako ndiko walikoenda kuyanunua tena kwa bei poa,
Hakuna baharia aliyerudi fresh ambaye hakuwa na hela za kulipia kodi ya gari lake, huo sio ukweli, maana hata hayo magari tulikuwa tukiyanunua Uholanzi kwa bei ndogo sana yakiwa katika process ya kuelekea kuyeyushwa, ndio maana mabaharia wengi walikuwa wakiyasubiri magari yao kwenye mnada wa serikali,
Mabaharia wenye connection, kama Timmy Toma, yeye alirudi na magari mawili, na vyombo vya bendi akaanzisha bendi ya Toma Toma na kina Kasaloo Kyanga, baadaye maa-agent wakaanza kumsumbua kuwa alitoaje magari na vyombo vyake ndipo alipoamua kukimbilia Zimababwe, btu kama unaaamini kuwa mabaharia waliorudi fresh walishindwa kukomboa magari kwa sababu ya kodi, labda unajua something I do not kuhusu mabaharia maana gari ilikuwa dola 300-500, kodi haikuwa zaidi ya dola 100, kwa waliokuwa nje kwa sughuli tofauti na ubaharia, sasa kweli baharia angeshinda kulipia hizo hela mbuzi mkuu? Hayo yako ni matusi kwa mabaharia!
2.
Mkuu ninamfahamu mshikaji wangu aliyekuwa na biashara moja tu mjini nayo ni passport, ambazo nyingi alikuwa akiwauzia wahindi na waarabu, ambao hawajawahi hata kufika bongo licha ya kuonyesha safari kama unavyosema, na huyo kijana na wakubwa wake aliokuwa akishirikiana nao, kupitia kwa Mbwana aliyekuwa mkuu wa uhamiaji then walitajirika sana na passport, kama hyajui mkuu dawa ni kuuliza tukufahamishe!
3.
Ili kuweza kupata passport kwa uhalali au kwa mizengwe, ilikuwa ni lazima uwe una uwezo kwa hiyo mkuu wale wote waliop[ata pass kwa uahalali hata siku moja hawakuzamia meli, isipokuwa aliondoka kwa halali, vijana kama kina Chelu Fundikira, Raja Kaka, Mlela, Omondi, Lengwe, na watoto wachache kutoka Migo Migo, na Chang'ombe waliokuwa na uwezo wa kupata passport kwa halali yaani kimizengwe waliondoka kihalali, moja ya sababu kubwa ya kuzamia ilikuwa ni kutokuwa na passport mkuu, no way baharia wa kweli akazamia meli huku akiwa na passport kibindoni, hiyo sio kweli!
4.
Hawa vijana wote nilikuwa nikipambana nao nikiwa MV Liemba, ambayo ndio waliyokuwa wakiitumia kwa biashara zao, 90% hawakuwa na passport, walikuwa na travelling documents, na pia walikuwa na ujanja mwingi wa kuweza kuingia Buja bila pass, wala karatasi yoyote, wengi walikuwa vijana kutoka Bukoba, wachache sana waliokuwa wakitoka Dar, na nia na madhumuni yao ilikuwa ni ku-raise funds ili waondoke bongo kihalali, hata Vijana Jazz wenyewe na Maneti walipokwenda Buja hawakuwa na passport isipokuwa travelling documents tu mkuu, that is how serious passport ilikuwa kuwa nayo!
5.
Mkuu ili usafiri ulitakiwa kuwa na passport, kibali cha kununua tiketi ya ndege, na kibali cha kununua dola kutoka benki kuu, vibali hivi vilikuwa vinatolewa na BOT tu, sasa niambie baharia wa kawaida angeweza vipi ku-satisfy masharti ya kuweza kupata hivyo vibali?
6.
Sasa muhuri huo vijana wangeupata wapi na wao kazi yao ilikuwa ni magendo tu ya mtaaani? Ni wabongo wangapi then waliokuwa wakilipa kodi mpaka kueza kupata huo mhuri, si ndio zilikuwa njia tu za kula hizo mkuu?
7.
Vile vita sheria za kimataifa zinasema kuwa aliyekuchokoza unamtoa kwenye ardhi yako tu, halafu unaachana naye na kuwaachia UN walete majeshi yao ya peacekeeping, sasa kilichotupeleka Kampala ni nini? Maaana ni kwenda huko ndiko kulikotu-cost tunalipa madeni mpaka leo! Maneno ya kufunga mkanda miezi 18 mbona yalikuwa hayawagusi wenye nguvu na the connected? Maaaan sikumbuki Mwalimu akisema kuwa itakuwa kwa wanyonge tu!
8.
Katika hii topic nzima sijaona mahali point, labda ni yako mkuu, wananchi wamesema Mwalimu hakupenda kuwa karibu na wananchi wenye elimu nzuri na uwezo mkubwa kufikiri, akaishia kuzungukwa na kina Mkapa, sasa haya yanayotukuta taifa letu si ndio matokeo yake, umeabiwa Mao, alizungukwa na wananchi wenye akili kama yeye matokeo yake yanaonekana kule China sasa.
9.
Kwenye hili sijakuelewa mkuu, una maana hiyo ilikuwa ni sera nzuri, kama ni kweli sasa kwa nini tumekwama na uchumi?
10.
Mkuu wangu tunajaribu kuangalia hizo sera na tulipo sasa hivi kitaifa, kwa sababu kulikuwa na vubali vya kuendesha gari jumapili, ambavyo wanaohusika walipewa tu njia ya kula, aliyeamua alikuwa ni Mwalimu sio wananchi wote wa bongo, maana faida yake kwa uchumi wetu sasa hivi ilikuwa ni nini? Ni wapi leo katika uchumi wetu unaweza kusema kuwa tumefanikiwa kutokana na the fact kwamba one time tulikuwa haturuhusiwi kuendesha magari jumapili?
11.
Mkuu hapa tunatoa heshima kwa Kambona, kwa sababu miaka 22 iliyopita alisema maneno yanayorudiwa leo na Chadema na kina Mwanakijiji kila siku hapa against serikali yetu, the man had a vision, lugha yako ndio hasa Mwalimu alitaka iongewe atakapookuwa hayupo, kwamba ni yeye tu peke yake ndiye aliyeleta mazuri kwa nchi.
__________________