Ukweli ni upi kuhusu Oscar Kambona?

Ukweli ni upi kuhusu Oscar Kambona?

Now you are being very unreasonable!!! I'm amazed but at the same time I'm not!!
 
Nyerere aliua wangapi waliokuwa wanampinga? Tuwekee data na sisi tufaidike.
...may be kusema kuua nimekuwa extreme na sijui nani aliwahi kuuliwa na Kambarage ila nina uhakika kambona either angepigwa ndani mpaka tumsahau au angefanywa kama wenzake waliopelekwa vijijini(kasanga,tuntemeke etc) na kuambiwa wasitoke huko,all in ala JK alikuwa dikteta wa aina yake tuu hata mkimpamba vipi!
 
nyerere was a dictator at times......simlaumu kambona kukimbia, hasa ukizingatia kuwa watu walikuwa wanatoweka na wengine kufungwa bila sababu za msingi.

kumsema ni coward ni rahisi, tunapokuwa hatujawa in the same position.........lakini kuozea jela ambayo unaijua vizuri sana kwa huduma zake mbovu,...na ukikumbuka ni kuwa unawatia matatizoni ndugu zako ambao hawapo kwenye game yako unayoicheza, it make sense kutafuta asylum i think
 
Inawezekana kabisa kuwa mimi ni mpuuzi na sioni tatizo kuitwa hivyo. Kutofautiana nawewe kwa kuita suala la Kambona kukimbia nchi uoga na ubinafsi sidhani kama ni justification tosha ya kuniita mpuuzi.

Anyway, Upuuzi wangu unaonyesha kwamba Kambona alikuwa bonge la mwoga kama kitoto kichanga. Mambo yalipokuwa tough kidogo yeye huyoo kakimbia mbio na vilio vingi kama kitoto.

Ilikuwa haki kabisa kukataza wana-Dorm wenzangu kuwa waoga kama Kambona maana inaonekana kuna wengi sana wangekuwa wanakimbia kila mara mambo yakiwa magumu.

Kambona the coward! A man without bollz to stand the heat

Hiyo ndiyo title ya kitabu changu kuhusu Kambona.

....koba a man without bollz to stand the heat...done na Jk & Kambona na sirudi tena hii thread,sasa ngoja nikatafute umbeya wa BOT na report yao fake sasa nasikia iko tayari na this time majina ya mafisadi wote nahakikisha nayaforward dunia nzima mpaka kwa wajukuu zao ili waone aibu tuu
 
nyerere was a dictator at times......simlaumu kambona kukimbia, hasa ukizingatia kuwa watu walikuwa wanatoweka na wengine kufungwa bila sababu za msingi.

kumsema ni coward ni rahisi, tunapokuwa hatujawa in the same position.........lakini kuozea jela ambayo unaijua vizuri sana kwa huduma zake mbovu,...na ukikumbuka ni kuwa unawatia matatizoni ndugu zako ambao hawapo kwenye game yako unayoicheza, it make sense kutafuta asylum i think

Kuna mifano mingi tu ya watu waliokaa Tanzania wakati wa Nyerere, Mwinyi, na Mkapa ingawa muda wote kumekuwa na hizi story za watu kuuliwa au kupotea.

Kama Kambona alikuwa hero kama watu wanavyotaka sisi tuliozaliwa juzi tuamini hapa? Kwa nini alikimbia na hakusimamia kile alichoamini? Nimekupa mifano ya Kenya - Odinga, Mandela, na wengine wengi tu waliobakia nchini na kuweka gerezani hadi pale walichopata kile wanachoamini.

Kambona alikimbia na akawa Kimya, aliporudi alikuja na ahadi kibao za kusema maovu ya Mwalimu na akaishia kusema nothing.

This guy was flawed. Ni bonge la baby and coward.

I just have said it here on JF
 
nyerere was a dictator at times......simlaumu kambona kukimbia, hasa ukizingatia kuwa watu walikuwa wanatoweka na wengine kufungwa bila sababu za msingi.

kumsema ni coward ni rahisi, tunapokuwa hatujawa in the same position.........lakini kuozea jela ambayo unaijua vizuri sana kwa huduma zake mbovu,...na ukikumbuka ni kuwa unawatia matatizoni ndugu zako ambao hawapo kwenye game yako unayoicheza, it make sense kutafuta asylum i think

Unajua kumuita mtu coward ni rahisi sana. Vile vile mtu anaweza aka-argue kwamba humu jamboforum kuna ma-cowards kibao wanaotumia majina feki. Kama kweli wangekuwa na balls au viharage (sijui female version ya balls ni nini...ovaries?) si wangekuwa wanatoa maoni yao bila hofu wala uoga wowote kwa kutumia majina yao ya kweli? Ni kawaida ya binadamu kuona kasoro au mapungufu ya wengine....aliyesema Nyani (Mimi) haoni kundule hakukosea kabisa!!!
 
Hapa ndipo sasa tunakubaliana na wewe. Kama ukiniona mimi nimeanzisha kampeni ya kutaka niitwe hero wakati hapa JF tu ninatumia jina ambalo si langu! basi inabidi uwe the first person kunichallenge.

So far, sijawahi na sitawahi kujiita hero kwa sababu I am not.
Tukianzisha thread ya kuniongelea mimi na kiharage changu, I will be the firt person kujiita coward hapa. I said it here.

Kwa sababu tunamuongelea Kambona na namna history itasema kuhusu yeye. Mimi nimetoa side yangu kuwa kambona ni bonge la baby na mwoga kama fisi - kupiga makelele na kukimbia mambo yakiwa tafu.

Kambona alikimbia nchi na fight ambayo alianzisha. Na alipoenda UK alijichimbia chini mpaka aliporudi baada ya wenzake wenye bollz kupigana nchini kwa ajili yake na akajifia kimya kimya.

What a coward!
 
Mwafrika wa Kike,

siyo wote waliokwenda uhamishoni ni waoga. wako wengi waliokimbia nchi zao na ninakutajia hawa hapa: Oliver Tambo, Eduardo Mondlane, Samora Machel,Augustino Neto,Robert Mugabe, Joshua Nkomo,Joaquim Chissano, Kanyama Chiume, etc etc.

Ninachoweza kusema ni kwamba Nyerere ana nafasi ya pekee kwa kutuongoza watanzania mpaka tukafika mahali tukawa na fahari kubwa mno kwa Utanzania wetu.

Lakini tangu Uhuru wetu hakuna kiongozi ambaye ameporomosha uchumi wa nchi ile kama alivyofanya Nyerere. Kuna uwezekano hali hiyo haikutokana na ufisadi, lakini something went drastically wrong.

Pamoja na kwamba nilikuwa mtoto mdogo lakini nikumbuka kushudia jinsi hali ya familia yetu ilivyobadilika na kuwa ya mashaka makubwa sana. Kile kitendo cha kutanga-tanga kutafuta mahitaji muhimu[mkate,mafuta ya taa,unga,sukari,majani ya chai] nilikishudia. Katika familia yetu mimi ndiyo nilikuwa nikitumwa kwenda duka la kaya.

Hali haikuishia kwenye uhaba wa mahitaji muhimu tu. Barabara za kwenda mikoani zilikuwa mbaya mno mno. Maeneo ambayo unachukua masaa 6 kusafiri, ilifika mahali ukatumia siku 2 barabarani--ukilazimika kuunganisha safari. Barabara zote kuu ziligeuka vumbi tupu.

Wako jamaa zetu walioamua ndugu yao akazikwe kijijini walilazimika kubeba jeneza kilimita zaidi ya 10. Lakini kwenda kuzika hauendi mikono mitupu, kwa hiyo msafara huo ulilazimika kubeba mahitaji muhimu kama mafuta na sukari etc etc.

Sasa Mwalimu kwa kweli alikuwa mwanasiasa mjanja na mahiri mno. Kwasababu mpaka sasa hivi sielewi ni jinsi gani aliweza KUWAPOOZA Watanzania ktk mazingira yale magumu.

Baada ya kuondoka madarakani Mwalimu alipewa zawadi nyingi ajabu na mashirika ya umma, idara za serikali,na kila mkoa aliokwenda kuaga. Kuna mikoa iliyotoa mifugo, magari, matreka, mashine nzito za kilimo,mashine za ujenzi, mbegu, chakula, fenicha, etc etc.

NB:
Hivi ni kwanini Kambona hakuendeleza mapambano yake toka nje ya nchi? Kwanini hatukumsikia hata wakati ule wa matatizo makubwa ya Uchumi? Watanzania wangemwelewa zaidi kipindi kile kuliko wakati wowote ule.
 
Ni kweli unaweza kwenda uhamishoni na kuendeleza mapigano ya nguvu ukiwa huko au ukajipanga kisha ukarudi na nguvu mpya.

Kambona hakufanya chochote cha hayo hapo juu, yeye alijiishia kimya kimya na akapiga makelele ziku za kwanza baadae alivyopata vipesa, akaingia mtini na kuwasahau watanzania aliodai kuwa anapigania haki zao.

Ninachoweza kusema ni kwamba Nyerere ana nafasi ya pekee kwa kutuongoza watanzania mpaka tukafika mahali tukawa na fahari kubwa mno kwa Utanzania wetu.

Lakini tangu Uhuru wetu hakuna kiongozi ambaye ameporomosha uchumi wa nchi ile kama alivyofanya Nyerere. Kuna uwezekano hali hiyo haikutokana na ufisadi, lakini something went drastically wrong.

Naona hapa unataka niongee kuhusu Nyerere na kwa sababu katika hii thread naongea kuhusu Kambona nitaacha hoja hii ipite.

Pamoja na kwamba nilikuwa mtoto mdogo lakini nikumbuka kushudia jinsi hali ya familia yetu ilivyobadilika na kuwa ya mashaka makubwa sana. Kile kitendo cha kutanga-tanga kutafuta mahitaji muhimu[mkate,mafuta ya taa,unga,sukari,majani ya chai] nilikishudia. Katika familia yetu mimi ndiyo nilikuwa nikitumwa kwenda duka la kaya.

It is always about you and your family au sio?

Hali haikuishia kwenye uhaba wa mahitaji muhimu tu. Barabara za kwenda mikoani zilikuwa mbaya mno mno. Maeneo ambayo unachukua masaa 6 kusafiri, ilifika mahali ukatumia siku 2 barabarani--ukilazimika kuunganisha safari. Barabara zote kuu ziligeuka vumbi tupu.

Wako jamaa zetu walioamua ndugu yao akazikwe kijijini walilazimika kubeba jeneza kilimita zaidi ya 10. Lakini kwenda kuzika hauendi mikono mitupu, kwa hiyo msafara huo ulilazimika kubeba mahitaji muhimu kama mafuta na sukari etc etc.

Sasa Mwalimu kwa kweli alikuwa mwanasiasa mjanja na mahiri mno. Kwasababu mpaka sasa hivi sielewi ni jinsi gani aliweza KUWAPOOZA Watanzania ktk mazingira yale magumu.

Haya unayoyasema yameendelea kuwepo hata leo miaka 23 baada ya mwalimu kustaafu. Mhh kuna mengi mabaya aliyofanya Nyerere ila kama hayo mabaya yanaendelea miaka 23 baada ya yeye kustaafu basi hiyo nchi imelaaniwa.

Baada ya kuondoka madarakani Mwalimu alipewa zawadi nyingi ajabu na mashirika ya umma, idara za serikali,na kila mkoa aliokwenda kuaga. Kuna mikoa iliyotoa mifugo, magari, matreka, mashine nzito za kilimo,mashine za ujenzi, mbegu, chakula, fenicha, etc etc.

Najaribu kujiuliza hili linahusiana vipi na ajenda ya Kambona

NB:
Hivi ni kwanini Kambona hakuendeleza mapambano yake toka nje ya nchi? Kwanini hatukumsikia hata wakati ule wa matatizo makubwa ya Uchumi? Watanzania wangemwelewa zaidi kipindi kile kuliko wakati wowote ule.

Haya ni mongoni mwa maswali yanayoulizwa hapa. JIBU fupi ni kuwa Kambona alikuwa bonge la mwoga like a baby. Hakuweza kuhimili joto la mapambano? Wanaomuita hero wanaitaji kuandika definition mpya ya HERO!
 
Hapa ndipo sasa tunakubaliana na wewe. Kama ukiniona mimi nimeanzisha kampeni ya kutaka niitwe hero wakati hapa JF tu ninatumia jina ambalo si langu! basi inabidi uwe the first person kunichallenge.

So far, sijawahi na sitawahi kujiita hero kwa sababu I am not.
Tukianzisha thread ya kuniongelea mimi na kiharage changu, I will be the firt person kujiita coward hapa. I said it here.

Kwa sababu tunamuongelea Kambona na namna history itasema kuhusu yeye. Mimi nimetoa side yangu kuwa kambona ni bonge la baby na mwoga kama fisi - kupiga makelele na kukimbia mambo yakiwa tafu.

Kambona alikimbia nchi na fight ambayo alianzisha. Na alipoenda UK alijichimbia chini mpaka aliporudi baada ya wenzake wenye bollz kupigana nchini kwa ajili yake na akajifia kimya kimya.

What a coward!

Hakuna mtu aliyeanzisha kampeni ya yeye kutaka aitwe shujaa hapa. Kinachojadiliwa ni historia. Sasa wengine kama wewe mmekuja na kuanza kuwaita subjects majina. Ohh coward...ooh hana ballz...na much more. Ni rahisi sana kuwaita watu majina. Na ni rahisi zaidi kujenga hoja za dhihaka na dharau kuliko zenye nguvu na akili.....we endelea tu mama cita
 
Huyu Baghdella najuana na washikaji zake kadhaa(kuna mmoja alikuwa na Celica kama ya Virani) huwa wananipa sana story zao za kuzunguka viwanja.

Huyu Spencer unayemzungumzia ni yule alikuwa anapenda kuhang out pale Chef Pride? Alafu huyo Msoffe ile issue yake na wachina pale sea cliff ilishaisha?

HAHAHAHAHAAA kumbe watoto wa mjini mpo eeeh? naona namba zingine lakini hujazistukia!

Ebwana yap MSOFE last time nilipata taarifa kuwa baada ya kule pesa za wajerumani kwa kuwaonyesha shaba za wazambia kule kilwa road wazee wakaamua kumpumulia kifuani mchizi akaingia mitini kuibuka ndio akaja na skendo la kuwala tena wajerumani wengine pesa za diamond ambalo noma lake lake lilikuwa si mchezo...maana wajerumani Dar walikuja juu ile kinoma yaani nazungumzia kuwanzia kule Ubalozini mpaka kwa wale GTZ ole naiko naye kule TIC naye alikuwa hakai ofisini ndipo JK akapata safari ya kwenda Ujerumani basi si manoma yaho huko Ujerumani...matokeo yake CID wakanyanganywa kesi na hao USLAMA WA TAIFA...mbona huyo msofe alijisalimisha mwenyewe! unajua jamaa wa UT waliamua kudeal na ndugiu zake wa karibu na walichofanywa siweki kukisema hapa hadharani lakini naweza kusema kuwa It worked na pesa MSOFE alizirudisha....hakuna cha PAPA MUSOFE wala lile hirizi lake linalopumua kwenye mkono wake

Hilo la wa china nalo nasikia bado halijaisha....na inshort MSOFE hakanyagi ulaya hata kwa mtutu wa Bunduki!

Akina Baghdella si unajua tena kuwa close na akina Kinje mambo yao yanaenda tuu hivyo kimungu mungu tuuu si unajua tena pesa za General supplies zilivyo? The same can be asaid about akina Fundikiara na akina Songambele...hapo ndipo utajua umuhimu wa shule wale watu baba zao walikuwa na nafasi lakini wapi!

Ebwana sijui kama sikuhizi Spencer anashinda pale chefs pride lakini zamani walikuwa na nyumba pale Mtaa wa sikukuuu jirani na BIG MAYAI pembeni ya SAIGON CLUB na nyumba yao ilinunuliwa na LYATONGA MREMA kisha akajenga ghorofa pale nasikia sikuhisi imekuwa hoteli

Vipi unamjua BABU MTAMA MCHUNGU wa pale Magomeni Mtaa wa MSANGA?nadhani unafahamu kama jamaa likuwa anatoa visa kuliko haop state dept (ubalozi wa USA Dar) mpaka wenyewe walipokuja kumtembelea

MWAKITWANGEEEE...du jamaa kahama..pale kariakoo tandamti nyumba namba 8..jirani na kwa capt tony..bado yupo na yule demu wake wa kipare..ile nyumba aliyokuwa amepanga imeuzwa na kubomolewa,,,..
 
Hakuna mtu aliyeanzisha kampeni ya yeye kutaka aitwe shujaa hapa. Kinachojadiliwa ni historia. Sasa wengine kama wewe mmekuja na kuanza kuwaita subjects majina. Ohh coward...ooh hana ballz...na much more. Ni rahisi sana kuwaita watu majina. Na ni rahisi zaidi kujenga hoja za dhihaka na dharau kuliko zenye nguvu na akili.....we endelea tu mama cita

Ohhh Nyani,

Jaribu kupitia some posts zilizowekwa hapa uone kampeni iliyosemwa kuwa Kambona was a hero or He should be considered one.

Wao wametoa mawazo yao na sababu zao za kwanini Kambona awe hero na wengine wakasema kuwa Kambona was hero kuliko Mwalimu etc. Mimi sina tatizo na hilo ndio maana sijachukua muda wangu hapa kuanza kubishana nao kuhusu mawazo yao.

Mimi nimetoa msimamo wangu kuwa this guy was never a hero na nikaanza kutoa sababu za kutetea msimamo wangu. Nadhani Nyani unajua vyema kabisa kuwa HERO is a name, the same thing should be on Coward.

Ukiita mtu a hero umetumia name kama vile ukiitwa mtu a coward.
I am just on the opposite side of your point of view.

Thanks Baba Cita!
 
HAHAHAHAHAAA kumbe watoto wa mjini mpo eeeh? naona namba zingine lakini hujazistukia!

Ebwana yap MSOFE last time nilipata taarifa kuwa baada ya kule pesa za wajerumani kwa kuwaonyesha shaba za wazambia kule kilwa road wazee wakaamua kumpumulia kifuani mchizi akaingia mitini kuibuka ndio akaja na skendo la kuwala tena wajerumani wengine pesa za diamond ambalo noma lake lake lilikuwa si mchezo...maana wajerumani Dar walikuja juu ile kinoma yaani nazungumzia kuwanzia kule Ubalozini mpaka kwa wale GTZ ole naiko naye kule TIC naye alikuwa hakai ofisini ndipo JK akapata safari ya kwenda Ujerumani basi si manoma yaho huko Ujerumani...matokeo yake CID wakanyanganywa kesi na hao USLAMA WA TAIFA...mbona huyo msofe alijisalimisha mwenyewe! unajua jamaa wa UT waliamua kudeal na ndugiu zake wa karibu na walichofanywa siweki kukisema hapa hadharani lakini naweza kusema kuwa It worked na pesa MSOFE alizirudisha....hakuna cha PAPA MUSOFE wala lile hirizi lake linalopumua kwenye mkono wake

Hilo la wa china nalo nasikia bado halijaisha....na inshort MSOFE hakanyagi ulaya hata kwa mtutu wa Bunduki!

Akina Baghdella si unajua tena kuwa close na akina Kinje mambo yao yanaenda tuu hivyo kimungu mungu tuuu si unajua tena pesa za General supplies zilivyo? The same can be asaid about akina Fundikiara na akina Songambele...hapo ndipo utajua umuhimu wa shule wale watu baba zao walikuwa na nafasi lakini wapi!

Ebwana sijui kama sikuhizi Spencer anashinda pale chefs pride lakini zamani walikuwa na nyumba pale Mtaa wa sikukuuu jirani na BIG MAYAI pembeni ya SAIGON CLUB na nyumba yao ilinunuliwa na LYATONGA MREMA kisha akajenga ghorofa pale nasikia sikuhisi imekuwa hoteli

Vipi unamjua BABU MTAMA MCHUNGU wa pale Magomeni Mtaa wa MSANGA?nadhani unafahamu kama jamaa likuwa anatoa visa kuliko haop state dept (ubalozi wa USA Dar) mpaka wenyewe walipokuja kumtembelea

Nilisikia jamaa wa UT walimtumia ujumbe, ndio maana nilisema serikali yetu wakitaka kumshika Vithlani basi "wamtumie ujumbe" kupitia kwa ndugu zake hapo West London
Eh!! Bwana we..Ngoja tusiwaaribie wenyewe mada yao

Ila kukimbia kwa Kambona nadhani alijua nini kingemtokea maana naye si alikuwa mmoja wao wa wanaotunga sheria. Lakini swali kwa nini akuendeleza mapambano akiwa Uingereza?
 
Ohhh Nyani,

Jaribu kupitia some posts zilizowekwa hapa uone kampeni iliyosemwa kuwa Kambona was a hero or He should be considered one.

Wao wametoa mawazo yao na sababu zao za kwanini Kambona awe hero na wengine wakasema kuwa Kambona was hero kuliko Mwalimu etc. Mimi sina tatizo na hilo ndio maana sijachukua muda wangu hapa kuanza kubishana nao kuhusu mawazo yao.

Mimi nimetoa msimamo wangu kuwa this guy was never a hero na nikaanza kutoa sababu za kutetea msimamo wangu. Nadhani Nyani unajua vyema kabisa kuwa HERO is a name, the same thing should be on Coward.

Ukiita mtu a hero umetumia name kama vile ukiitwa mtu a coward.
I am just on the opposite side of your point of view.

Thanks Baba Cita!

Sawa...unapomuita mtu hero haumalizii na kibwagizo cha "jamaa alikuwa na ballz kweli kweli"....hicho kibwagizo kwako wewe kinaendana na "cowardice"....sasa jilo sio tusi?
 
Sawa...unapomuita mtu hero haumalizii na kibwagizo cha "jamaa alikuwa na ballz kweli kweli"....hicho kibwagizo kwako wewe kinaendana na "cowardice"....sasa jilo sio tusi?

Nyani kusema mtu hana bollz sio tusi as far as I am concerned. Huu ni usemi tu wa kumtambulisha mtu mwoga na ambaye anashindwa kusimamia mitazamo au kazi zake.

I tend to favor Demokrats over Republicans kwenye siasa za Marekani ila kila wakati nikiingia kwenye liberal blogs na kuweka comments (Yes I am very active kwenye liberal blogs za hapa US - ukizifuatilia utagundua comments zangu) huwa wengi wetu tunawaita viongozi wa demokrats kwenye congress kuwa hawana bollz (ingawa Nancy Pelosi is a woman).

Kama umechukulia neno bollz kama tusi, basi from now on umejua kuwa sio tusi (kutoka kwangu) bali msemo...
 
Jukwaa la Historia

Kambona anapewa sifa nyingi za ushujaa ambao hakuwa nao isipokuwa nafasi yake ya kihistoria na mchango wake katika uhuru wa Tanganyika. Ushujaa ambao Kambona anadaiwa kuwa nao haukuwa wa bahati mbaya bali ni tukio lililomkuta kihistoria na kama mzalendo yoyote alitimiza wajibu wake na kiapo chake.

Ni kweli kabisa kuwa kati ya viongozi wa mwanzo wa nchi yetu wawili hawa walifuatana; Nyerere na Kambona na kuna baadhi ya watu waliohisi kuwa kama kuna mtu ambaye angekuja kumrithi Mwalimu alikuwa ni Oscar Kambona. Hata hivyo, hakuna wakati wowote (aidha kabla ya Uhuru au baada ya uhuru) ambapo Kambona alimzidi Mwalimu kwa hoja, kwa ushawishi, au kwa mvuto. Mara zote ilionekana kuwa Nyerere namba moja, Kambona namba mbili.

Maasi ya 1964.

Maasi ya wanajeshi wa Afrika ya Mashariki ya 1964 yalikuwa ni jaribio la kwanza kwa uongozi wa Tanganyika Huru. Kama ilivyo mahali popote duniani kama target ya maasi ni viongozi wa juu wa nchi basi Rais na Makamu wake hulindwa. Hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa Mwalimu Nyerere na Makamu wake Rashid Mfaume Kawawa. Kupelekwa kwao Kigamboni kwa wengine inaonekana ni kujificha lakini kwa wale wanaofahamu siasa na utawala uamuzi huo ulikuwa ni muhimu na wa lazima. Wakati wa Enzi za vita ya pili ya Dunia wakati Wajerumani wanajaribu kuichukua Roma, Papa alifichwa na wakati wajerumani wanalipua London Churchill hakukaa Namba 10 kusubiri waje wamberbecue! Mfano mzuri wa karibuni ni wakati wa mashambulizi ya Septemba 11 ambapo wakati tukio hilo limetokea Rais George Bush na Makamu wake wa Rais walichukuliwa na kupelekwa kule kunakoitwa "undisclosed location". Sera hii ya kuwaficha viongozi wa nchi wakati wa hatari siyo ya kina Nyerere na Kawawa tu bali ipo sehemu nyingi duniani na Ikulu nyingi duniani zinazo utaratibu wa kuwatorosha viongozi wakuu endapo kuna hatari inayowakabili.

Hivyo kitendo cha Nyerere na Kawawa kwenda kufichwa Kigamboni kilikuwa ni kitendo cha lazima hasa kwa kutojua lengo la maasi ya wanajeshi ni nini. Nani sasa ambaye angeweza kuzungumza na waasi? Hakuwa mwingine bali Oscar Kambona ambayo kutokana na nafasi yake ya kiserikali (akiwa waziri wa Mambo ya Nje na pia Waziri wa Ulinzi) alielekezwa na Mwalimu kwenda kukutana na waasi hao na kwa ujasiri na utii kwa Rais wake na Amiri Jeshi Mkuu alikwenda na kukutana na waasi hao. Hakwenda bila rungu. Kambona aliwawekea wazi msimamo uliokubaliwa kuwa endapo hawatavunja uasi huo serikali itakuwa haina jinsi isipokuwa kuomba msaada wa wakoloni wetu.

Kitendo cha Mwalimu kumtuma waziri kuzungumza na waasi hakikuwa cha ajabu kwani Obote kwenye maasi ya kwake alimtuma Waziri wa Mambo ya Ndani kuzungumza na wanajeshi waasi. Kule Kenya hawakupata hata nafasi ya kujadiliana na waasi, Kenyatta yeye aliomba wapiganaji wa Uingereza kuingilia kati na katika mapambano ya muda mfupi wakarudisha utawala kambini huku askari wa jeshi muasi akiuawa.

Uasi ule haukuzimwa kwa ushawishi wa Kambona bali kwa kuingiliwa na Jeshi la Uingereza na katika nchi zote tatu na kuuzima uasi huo. Hapa hapakuwa na ushujaa bali utekelezaji wa wajibu wa mtu kwa taifa lake. Nigeria nayo ilitoa askari wake kuweka ulinzi. Ni kweli hata hivyo kuwa kuwa mtu wa pili baada ya Nyerere na kuwa karibu sana na Nyerere Kambona aliheshimika, kupendwa na kusikilizwa na waasi kuliko kiongozi mwingine yoyote kwani walijua kabisa kama kuna mtu ambaye angeweza kuzungumza kwa jina la Rais alikuwa ni Kambona. Kwa hilo, Mwalimu mwenyewe alimshukuru hadharani baada ya kutoka mafichoni.

Na siyo ushawishi tu bali matumizi ya nguvu. Wakiongozwa na Brigeria Patric Douglas wa Afisa wa kizungu RF aliyetimuliwa makomandoo wa Uingereza waliingia kambini kwa mkwara mzito na baada ya kuwataka waasi wasalimu amri zilipikwa roketi kwenye kambi na kulazimisha wasalimu amri kwa nguvu. Askari watatu waliuawa na utulivu ukarudishwa.

Mgongano wa Kifikra.

Kati ya vitu vinavyosemwa kuhusu Kambona ni kuwa alipinga Ujamaa na Azimio la Arusha. Taarifa zote za awali toka wakati ule zinaonesha jinsi mgongano wa kifikra kati yake na Mwalimu ulivyoanza. Kwanza Kambona hakushabikia kubadilishwa kwa nchi kuwa ya chama kimoja zaidi na kuondoa vyama vingine. Kwenye hili aliona kuwa hakukuwa na utaratibu mzuri wa kuziwekea mipaka nguvu hizi mpya za serikali. Hofu yake ni kuwa Taifa lingegeuka kuwa la Kidikteta zaidi. Hata hivyo kama mmoja aliyekubali kushindwa kwa hoja, alikubaliana na mabadiliko yale ya 1965. Bila ya shaka aliamua kuishi ndani ya mfumo huo.

Mgongano mkubwa ulitokea baada ya kutangazwa kwa Azimio la Arusha na hasa uamuzi wa wazi wa kujenga Taifa la kijamaa. Kambona alikuwa ni shabiki wa mfumo wa kibepari wakati Mwalimu alikuwa amevutiwa na mfumo wa kijamaa hasa dhana nzima ya usawa wa watu. Kambona hakukataa Azimio zima la Arusha bali kimsingi alitaka tufanye majaribio kwanza kwenye maeneo fulani (pilot project) lakini Mwalimu kwa mara nyingine alimshinda kwa hoja. Azimio likatangazwa na Taifa la kijamaa likaanza kujengwa. Kambona alishindwa.

Kwenda Uhamishoni
Kambona aliamua kukimbia Tanzania baada ya kuona kuwa hana nafasi tena ya kumshinda Mwalimu kwa hoja, kwa mvuto na kwa ushawishi. Na kwa hakika ule ujio ambao inadaiwa alikuwa nao kwenye vyombo vya usalama hakuwa nao tena kwani maafisa Usalama walishikilia kiapo chao sawasawa kuwa utii wao ni kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano. Kambona licha ya kuwa ni kiongozi aliyependwa hakuwa ameliwa kiapo cha utii na afisa yoyote yule.

Ni baada ya kufarakana kifikra na Mwalimu na ujasiri wa Kambona aliouonesha wa kupingana na Mwalimu waziwazi ndiyo uliomfanya ajihisi kuwa hana nafasi katika siasa za Tanzania kwa kadiri ya kwamba Mwalimu yuko Madarakani. Kuondoka kwake hakukuwa kwa kificho kama wengi wanavyoamini na serikali kama ingetaka kumzuia ingemzuia. Hawakumzuia na walimwacha aende zake yeye na familia yake.

Kama Mwalimu alitaka kumdhuru au kumfanyia vibaya angeweza kufanya hivyo wakati Kambona yupo nchini lakini Kambona aliachiliwa kwenda na kufanya analotaka huko London. Na kufanya alilotaka alifanya. Wote wawili Mwalimu na Kambona walitoa madai dhidi ya mwenzake. Tarehe 12 Januari 1968 miezi michache baada ya Kambona kukimbia Rais Nyerere alimpa changamoto Kambona arudi nyumbani kuja kujisafisha jina lake na kuelezea kama hajaingiza fedha kwenye akaunti yake kiasi ambacho kilizidi kwa kiasi kikubwa kipato chake. Kwa upande wake Kambona akiambia serikali ichunguze utajiri wake na iweke hadharani watakachogundua. Hakuna aliyetekeleza changamoto ya mwenzake.

Kujipa Ujiko akiwa Uhamishoni
Kambona akiwa uhamishoni alianza ziara za kutoa mihadhara kuelezea ubaya wa Mwalimu. Ukumbi wa kwanza alioupata ulikuwa ni Nigeria. Tukumbuke kuwa Mwalimu alikosana na serikali ya shirikisho la Nigeria baada ya kutambua kujitenga kwa Biafra. Serikali ya Nigeria kulipiza kisasi ikatoa mwaliko kwa Kambona kutoa lecture zake kule. Huo ndio ulikuwa mwanzo wa Kambona kujitengenezea ujiko.

Alianza kwa kudai kuwa ni Mwalimu ambaye alikuwa anatoa msaada wa kijeshi kwa waliojitenga wa Biafra na alidai pia kuwa misaada iliyokuwa iende kwenye nchi za ukombozi kama alivyofanya tarehe 14 Juni 1968 akiwa Lagos. Katika mhadhara wake Kambona alidai kuwa silaha zilizokuwa zipelekwe Zimbabwe kwa ajili ya harakati za ukombozi zilikuwa zimepelekwa Biafra. Na alidai kuwa Serikali ya Nyerere kuitambua Biafra ilikuwa ni kitendo kilichoipunguzia heshima serikali yetu; kitu ambacho hakukijua ni kuwa msimamo ule wa Mwalimu ulitujengea heshima ya kuweza kuamua nani ni rafiki zetu na ulikuwa ni msingi wa harakati nzima za ukombozi na kusudio la kusimama upande wa wanyonge. Kambona akiwa mgeni wa serikali ya shirikisho la Nigeria hakuwa na njia nyingine isipokuwa kumkandia Mwalimu.

Kurasa hazijafungwa bado

Historia bado haijatoa hukumu ya mwisho kuhusu Kambona na nafasi yake katika historia yetu. Ni kweli alikuwa na nafasi ya pekee na ni lazima itambulikane hivyo. Pamoja na mapungufu mengine Kambona ni lazima akumbukwe kwa mema aliyoifanyia nchi yetu. Hatuwezi kujua kwa hakika Tanzania ingekuwaje kama Kambona angekuwa Rais, kutetea sera za kibepari peke yake siyo kigezo cha kuwa Rais Mzuri, tunafahamu ya Mobutu na ya Kenyatta. Na tunafahamu jinsi madaraka yanavyomharibu mtu.

Kuna mtu anaweza kutuambia kuhusu Kambona, mtu huyo bado yupo hai na aliwahi kuwa msaidizi wa karibu wa Mwalimu Nyerere na Kambona; mtu huyo aliwahi kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kama Mwalimu alikuwa na nafasi yoyote ya kumlipa Kambona na kumpa Urais hata wa heshima ni kumchagua mmoja wa wasaidizi wake Kambona na kumpa nafasi kubwa. Mwalimu alitoa nafasi hiyo kwa mmoja wa wasaidizi wake Kambona kuwa Rais wa Tanzania, msaidizi huyo wa Kambona ambaye alikuwa ni mwandishi wake wa hotuba na baadaye mhariri wa magazeti na msaidizi wa Rais ... yes you guessed it!! it is him.

NB:

Makala hii nitaiendeleza ninapoandika makala yangu mpya kutokana na Kambona.
 
Nyani kusema mtu hana bollz sio tusi as far as I am concerned. Huu ni usemi tu wa kumtambulisha mtu mwoga na ambaye anashindwa kusimamia mitazamo au kazi zake.

I tend to favor Demokrats over Republicans kwenye siasa za Marekani ila kila wakati nikiingia kwenye liberal blogs na kuweka comments (Yes I am very active kwenye liberal blogs za hapa US - ukizifuatilia utagundua comments zangu) huwa wengi wetu tunawaita viongozi wa demokrats kwenye congress kuwa hawana bollz (ingawa Nancy Pelosi is a woman).

Kama umechukulia neno bollz kama tusi, basi from now on umejua kuwa sio tusi (kutoka kwangu) bali msemo...

Ni tusi la kistaarabu. Lakini bado ni tusi. Yaani mimi kwa mfano, mimi ni mwanamume rijali. Sasa wewe ukiniambia mimi sina bilinganya utakuwa umenitusi vibaya sana. Utakuwa umetusi na kudharau uanamume wangu....we cheki kwa mfano, mara nyingi hilo neno hutumiwa kwa wanaume na si wanawake. Huwezi kusema eti Mama Clinton hana bollz unless una agenda nyingine....
 
Hii Euphemism kali sana, lazima nitaitumia siku moja...eti agenda nyingine sasa kwa mwanamama tunasema nini?
 
Back
Top Bottom