1.
Kuna JF member moja kasema ati watu walizuiwa kuagiza magari madogo, hili sio kweli. Ukweli ni kwamba kodi ya magari madogo ilikuwa ni kubwa sana kiasi kwamba wenye uwezo wa kufanya hivyo walikuwa watanzania wachache sana. Mimi nawafahamu wachache ambao waliweza kulipia na kuwa na hayo magari. Mwenye hiyo sheria kama ilikuwepo atuwekee hapa.
Mabaharia walifikia mahali hawakutakiwa kuleta magari, kama ilikuwa ni sheria au sio hilo sijui, kila aliyerudi na magari aliambiwa kuwa sheria hairuhusu kwa sababi magari ni mabovu yataleta polution, lakini wenye connection waliweza kuyatoa bila noma, sasa wasiokuwa na connections, ilibidi kuyasubiri magari yao wenyewe kwenye mnada wa serikali, ambako ndiko walikoenda kuyanunua tena kwa bei poa,
Hakuna baharia aliyerudi fresh ambaye hakuwa na hela za kulipia kodi ya gari lake, huo sio ukweli, maana hata hayo magari tulikuwa tukiyanunua Uholanzi kwa bei ndogo sana yakiwa katika process ya kuelekea kuyeyushwa, ndio maana mabaharia wengi walikuwa wakiyasubiri magari yao kwenye mnada wa serikali,
Mabaharia wenye connection, kama Timmy Toma, yeye alirudi na magari mawili, na vyombo vya bendi akaanzisha bendi ya Toma Toma na kina Kasaloo Kyanga, baadaye maa-agent wakaanza kumsumbua kuwa alitoaje magari na vyombo vyake ndipo alipoamua kukimbilia Zimababwe, btu kama unaaamini kuwa mabaharia waliorudi fresh walishindwa kukomboa magari kwa sababu ya kodi, labda unajua something I do not kuhusu mabaharia maana gari ilikuwa dola 300-500, kodi haikuwa zaidi ya dola 100, kwa waliokuwa nje kwa sughuli tofauti na ubaharia, sasa kweli baharia angeshinda kulipia hizo hela mbuzi mkuu? Hayo yako ni matusi kwa mabaharia!
2.
Swala jingine ni la passport, kweli zilikuwa zinatolewa tu kama unasababu ya msingi ya kusafiri nje
Mkuu ninamfahamu mshikaji wangu aliyekuwa na biashara moja tu mjini nayo ni passport, ambazo nyingi alikuwa akiwauzia wahindi na waarabu, ambao hawajawahi hata kufika bongo licha ya kuonyesha safari kama unavyosema, na huyo kijana na wakubwa wake aliokuwa akishirikiana nao, kupitia kwa Mbwana aliyekuwa mkuu wa uhamiaji then walitajirika sana na passport, kama hyajui mkuu dawa ni kuuliza tukufahamishe!
3.
ya nchi na wengi walikuwa wanapata lakini ukija kuomba na ukaonekana huna sababu ya msingi ulikuwa hupati kutokana na vijana wengi hasa miaka chini ya 25 waliopoteza maisha yao kwa kuzamia meli. Wengi waliweza kupata kwa njia moja au nyingine,
Ili kuweza kupata passport kwa uhalali au kwa mizengwe, ilikuwa ni lazima uwe una uwezo kwa hiyo mkuu wale wote waliop[ata pass kwa uahalali hata siku moja hawakuzamia meli, isipokuwa aliondoka kwa halali, vijana kama kina Chelu Fundikira, Raja Kaka, Mlela, Omondi, Lengwe, na watoto wachache kutoka Migo Migo, na Chang'ombe waliokuwa na uwezo wa kupata passport kwa halali yaani kimizengwe waliondoka kihalali, moja ya sababu kubwa ya kuzamia ilikuwa ni kutokuwa na passport mkuu, no way baharia wa kweli akazamia meli huku akiwa na passport kibindoni, hiyo sio kweli!
4.
nakumbuka wakati ule vijana wengi walikuwa wanakwenda buja na kuleta mashati ya juliana n.k.
Hawa vijana wote nilikuwa nikipambana nao nikiwa MV Liemba, ambayo ndio waliyokuwa wakiitumia kwa biashara zao, 90% hawakuwa na passport, walikuwa na travelling documents, na pia walikuwa na ujanja mwingi wa kuweza kuingia Buja bila pass, wala karatasi yoyote, wengi walikuwa vijana kutoka Bukoba, wachache sana waliokuwa wakitoka Dar, na nia na madhumuni yao ilikuwa ni ku-raise funds ili waondoke bongo kihalali, hata Vijana Jazz wenyewe na Maneti walipokwenda Buja hawakuwa na passport isipokuwa travelling documents tu mkuu, that is how serious passport ilikuwa kuwa nayo!
5.
wakati ule kusafiri kwa ndege ilibidi utume maombi benki kuu ili uweze kupata foreign currency, hili lilikuwa kuanzia mwaka 1978 kama sikosei na sio kipindi chote ambacho mchonga alikuwa madarakani.
Mkuu ili usafiri ulitakiwa kuwa na passport, kibali cha kununua tiketi ya ndege, na kibali cha kununua dola kutoka benki kuu, vibali hivi vilikuwa vinatolewa na BOT tu, sasa niambie baharia wa kawaida angeweza vipi ku-satisfy masharti ya kuweza kupata hivyo vibali?
6.
Vile vile lazima kupata muhuri wa customs wakati ule kuomyesha kwamba unalipa kodi (matatizo mengi ya wakati huo ilikuwa ni pamoja na kuvunjika kwa jumuiya ya Afrika mashariki 1977,
Sasa muhuri huo vijana wangeupata wapi na wao kazi yao ilikuwa ni magendo tu ya mtaaani? Ni wabongo wangapi then waliokuwa wakilipa kodi mpaka kueza kupata huo mhuri, si ndio zilikuwa njia tu za kula hizo mkuu?
7.
vita ya Iddi Amin iliyokuwapo 1978 kama sikosei n.k) Nyerere alipohutuba taifa alisema tufunge mkanda kwa miezi 18. wengi walitafsiri alimaanisha miaka 18.
Vile vita sheria za kimataifa zinasema kuwa aliyekuchokoza unamtoa kwenye ardhi yako tu, halafu unaachana naye na kuwaachia UN walete majeshi yao ya peacekeeping, sasa kilichotupeleka Kampala ni nini? Maaana ni kwenda huko ndiko kulikotu-cost tunalipa madeni mpaka leo! Maneno ya kufunga mkanda miezi 18 mbona yalikuwa hayawagusi wenye nguvu na the connected? Maaaan sikumbuki Mwalimu akisema kuwa itakuwa kwa wanyonge tu!
8.
Mwalimu hakupenda watanzania wasome - Kama ni kweli wengi tu tusingeweza kuwa hapa tulipo, shule za dini zilitaifishwa ili WTZ wasiende shule - MAKUBWA HAYA. Siye yeye aliyeanzisha hata elimu ya ngumbaru?
Katika hii topic nzima sijaona mahali point, labda ni yako mkuu, wananchi wamesema Mwalimu hakupenda kuwa karibu na wananchi wenye elimu nzuri na uwezo mkubwa kufikiri, akaishia kuzungukwa na kina Mkapa, sasa haya yanayotukuta taifa letu si ndio matokeo yake, umeabiwa Mao, alizungukwa na wananchi wenye akili kama yeye matokeo yake yanaonekana kule China sasa.
9.
Njia kuu za uchumi kumilikiwa na serikali - Huu ndio ulikuwa msingi wakati ule na nakumbuka mabasi ya Kamata, Shirika la reli mabasi yake tuliyabatiza rab na mikoani kulikuwa na mabasi kama vile KAUDO kule Dodoma, UDA Dar es Salaam n.k.
Kwenye hili sijakuelewa mkuu, una maana hiyo ilikuwa ni sera nzuri, kama ni kweli sasa kwa nini tumekwama na uchumi?
10.
MAFUTA HAYAKUUZWA JUMAPILI - Wakati wa vita ya nduli utumiaji wa mafuta ulikuwa ni mkubwa na jambo lililokubaliwa ni kubana matumizi ya mafuta na kupunguza gharama, hivyo iliamuliwa magari yasitembee siku za jumapili kuanzia saa saba mchana isipokuwa teksi na kwa shughuli muhimu kama dharura imetokea, sasa nalo hili unapoamua kubana matumizi ni lazima ufikirie ufanye nini, Je lilifanikiwa? wenye takwimu watupatie. Mwalimu alikuwa kiongozi kwa miaka takriban 23 katika hiyo alipata mafanikio makubwa katika nyanja za nyumbani na ugenini. Jukumu lake lilikuwa kuongoza.
Mkuu wangu tunajaribu kuangalia hizo sera na tulipo sasa hivi kitaifa, kwa sababu kulikuwa na vubali vya kuendesha gari jumapili, ambavyo wanaohusika walipewa tu njia ya kula, aliyeamua alikuwa ni Mwalimu sio wananchi wote wa bongo, maana faida yake kwa uchumi wetu sasa hivi ilikuwa ni nini? Ni wapi leo katika uchumi wetu unaweza kusema kuwa tumefanikiwa kutokana na the fact kwamba one time tulikuwa haturuhusiwi kuendesha magari jumapili?
11.
Kambona sikuona mafanikio aliyoleta Tanzania, kama kuna vitabu ameandika wanaofahamu watujulishe huenda tukavisoma.
Mkuu hapa tunatoa heshima kwa Kambona, kwa sababu miaka 22 iliyopita alisema maneno yanayorudiwa leo na Chadema na kina Mwanakijiji kila siku hapa against serikali yetu, the man had a vision, lugha yako ndio hasa Mwalimu alitaka iongewe atakapookuwa hayupo, kwamba ni yeye tu peke yake ndiye aliyeleta mazuri kwa nchi.
__________________